Ijumaa, 31 Januari 2014

WAZIRI MKUU MHE MIZENGO PINDA AZINDUA MAPITIO YA MFUMO WA UWEKEZAJI TANZANIA

1(5)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika katika masuala ya uwekezaji nchini endapo itatekeleza kikamilifu Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji yaliyowasilishwa na Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 31, 2014), wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kitabu cha Mapitio ya Mfumo wa Uwekezaji kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa malengo ya mapitio ya mfumo huo ni kuboresha hali ya uwekezaji na biashara nchini ambayo matokeo yake yatasaidia kuongeza wawekezaji katika maeneo mengi.
“Kuna maeneo ya uwekezaji yanayopata uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi (Foreign Direct Investment -FDI) ambayo ni umeme, mafuta, gesi, madini, viwanda, ujenzi na huduma za jamii.
Amesema kuwa matokeo ya jitihada hizi ni makubwa na yameonekana ndani ya miaka miwili tu. Akitoa mfano, alisema: “Kilimo kimeweza kukua kutoka dola za marekani milioni 304.5 mwaka 2010 hadi dola za marekani milioni 355.4 katika mwaka 2011. Vilevile kwenye sekta ya Umeme na Gesi imekua kutoka dola za kimarekani milioni 328.6 hadi dola za kimarekani 539.8 mwaka 2011.”
Kutokana na matokeo hayo, Waziri Mkuu ameeleza kuwa Tanzania ina fursa nyingi zikiwemo rasilimali, nafasi yake kijiografia na historia ya siasa safi ambazo zinaifanya iwe kivutio kikubwa cha uwekezaji. Hali hiyo Waziri Mkuu alisema, imesaidia Pato la Taifa kuendelea kukua kwa asilimia sita kwa miaka 10 mfululizo na mwaka jana ilikua kwa asilimia saba na sasa inatarajiwa kufika asilimia 7.2 kwa mwaka huu.
Miongoni mwa maeneo yanayohusishwa na mfumo huu wa mapitio ya Uwekezaji ni yale yaliyoainishwa katika Matokeo makubwa sasa ambayo ni Kilimo, Maji, Uchukuzi, Elimu na Nishati.
“Ili kufanikisha maeneo hayo ni muhimu tukajenga mazingira bora ya uwekezaji, hivyo Serikali inawataka wadau wote kwa kushirikiana na Sekta binafsi kuchambua kwa makini mapendekezo ya mapitio ya mfumo huo ambayo yanatumika pia kuharakisha mafanikio ya Matokeo makubwa sasa”, alisisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema Serikali ya Tanzania inashukuru sana Taasisi ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) kwa kuweka sura maalum kwenye kitabu hicho inayozungumzia changamoto za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo.
“Ninatumaini kuwa utekelezaji wa mapendekezo haya utaongeza ufanisi wa mchakato huu na kuhakikisha kuwa tunazitumia fursa zilizopo na nyingine zaidi katika kuboresha uwekezaji katika kilimo nchini. Na kwenye kilimo ninamaanisha kilimo mazao, mifugo, uvuvi na nyuki,” aliongeza.
Mapema, Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya OECD, Bw. Rintaro Tamaki, alisema mazingira ya uwekezaji nchini yanabadilika kila mara kutokana na kuvumbuliwa kwa rasilimali mpya kama vile gesi, makaa ya mawe ambazo zinasababisha watu wavutive kuwekeza nchini.
Kutokana na kugunduliwa na sekta hizo, Serikali isizipuuzie sekta za zamani hususan Sekta ya kilimo, cha msingi ni kuboresha sekta hii kwa kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yenu”.

WAZIRI WA FEDHA AMJIBU pROFESA lIPUMBA KUHUSU ELIMU YAKE

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.
Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.
Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

lisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

WAZIRI AJIBU

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,”

German Chancellor Angela Merkel breaks hip while cross-country skiing in Swiss mountains... but only realises days later

  • Doctors told Angela Merkel the injury was an 'incomplete' bone fracture
  • She fell at 'low speed' while holidaying near St Moritz, Switzerland
  • German Chancellor has cancelled some official meetings while recovering
German leader Angela Merkel has returned from a Christmas and New Year break with a broken pelvis that she didn't know about.

The chancellor was on a skiing trip in Engadin in Switzerland when she fell.
She thought she suffered only bruises but a medical examination when she returned to the German capital Berlin showed she had actually broken a bone.
Mishap: Chancellor Merkel, pictured while skiiing at the resort in the Engadine valley of Switzerland on December 22, broke her hip during a fall
Mishap: Chancellor Merkel, pictured while skiiing at the resort in the Engadine valley of Switzerland on December 22, broke her hip during a fall
Doctors told her she will have to rest for the next three weeks while the injury heals.
Government spokesman Steffen Seibert said said: 'She suffered serious bruising in connection with a partial fracture on her left posterior pelvic ring.
 'We understand she was going at slow speed on a cross-country ski course when the accident occurred.'
Although she can walk unaided she has been instructed she cannot travel by plane and must lie down as much as possible for the next three weeks.
She will have to cancel a planned visit to Poland and a meeting with the Luxembourg Prime Minister in Berlin.
German Chancellor Angela Merkel breaks hip while cross-country skiing in Swiss mountains
Angela Merkel seen on a skiing holiday in St. Moritz on December 22
Out of action: Angela Merkel, pictured during her skiing trip to St Moritz on December 22, fell at 'low speed' according to her spokesman who said will spend the next few weeks recovering
On holiday: The 59-year-old politician, pictured during her trip to St Moritz before Christmas accompanied by two bodyguards, suffered a pelvis injury during a fall
On holiday: The 59-year-old politician, pictured during her trip to St Moritz before Christmas accompanied by two bodyguards, suffered a pelvis injury during a fall
But she will be able to attend the first cabinet meeting of the new coalition government she leads on Wednesday.
'It goes without saying that as chancellor, she is capable of acting as well as communicating fully,' added Seibert (TK).

GARI DOGO AINA YA TOTOTA COROLLA T 379 AGL LAPATA AJALI WATATU WAJERUHIWA


Gari ndogo aina ya Toyota Corolla lenye nambari za Usajili T 379 AGL, likiwa ndani ya mtaro mara baada ya kupoteza mwelekeo wakati likiwa kwenye Mwendo mkali.
Tukio hili limetokea mchana huu katika Barabara ya Migombani kama unaelekea Makao Makuu ya Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel. Ndani ya Gari hii kulikuwa na watu watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika kwa haraka kutokana hali iliyokuwa, watu wawili kati yao wameumia vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
 Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa, gari hiyo ilionekana ikiwa kwenye mwendo kasi hali iliyopelekea kushindwa maarifa kwa dereva wakati akipishana na Bajaj.
Wasamaria wema wakihangaika namna ya kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo, ambaye alikuwa amenasa kutokana na kubanwa na sehemu ya gari hilo.
Huu ndio mwonekano wa gari hiyo baada ya kuingia kwenye mtaro huo.
Mdau akionyesha kibao cha namba cha Gari hiyo ambacho kiling'oka na kuingia mtaroni.
Wasamalia wakiengelea kuhakikisha kama kuna mtu mwingine ndani ya Gari hiyo.
Majeruhi wakipakiwa kwenye Gari tayari kwa kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Gari iliyowapakia Majeruhi hao ikiondoka eneo la tukio. (TK)

TANZANIA YAIJIBU RWANDA

kikwete_7921e.jpg
Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda umeeleza kusikitishwa na taarifa za blog ya Rwanda "News of Rwanda" ambayo inaunga mkono serikali ya nchi hiyo iliyotolewa mwishoni mwa juma zikimtuhumu rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuunga mkono na kufanya mikutano na wanachama wa makundi ya waasi yanayopingana na serikali ya Rwanda.
 
Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania Salva Rweyemamu amesema wao wameshangazwa kwa sababu mwaka jana kulikuwa na matatizo na marais wa nchi hizo wameshazungumza vizuri wakakubaliana na kuonyesha kwamba sasa mambo yameisha na kwamba wanaendeleza urafiki wao, udugu wao na ujirani mwema wa miaka mingi kati yao na kuongeza kwamba hilo ni jambo la kusikitisha sana kwa upande wa Tanzania .
 
Ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini humo visaidie kujenga uhusiano mwema na visiwe mwanzo wa choko choko ya kugombanisha watu akiuliza kuwa "Tanzania wakigombana na Rwanda magazeti yatauzwa?" au mkiwa kwenye hali ya vurugu kama ilivyo nchi zingine ambapo watu wanapigana kila siku kuna watu wananunua magazeti pale? CHANZO, SAUTI YA AMERIKA

JAJI MKUU AISHUKIA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NCHINI


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza kwenye mkutano na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mtendaji Mkuu  wa Mahakama, Hussein Kattanga. Picha na Venance Nestory.

JAJI Mkuu Mohamed Othman Chande ameitaka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kuharakisha mchakato wake wa kuandaa ripoti inayohusu migogoro ya ardhi nchini ili kutoa nafasi ya kufanyiwa marekebisho Sheria ya Ardhi.

Jaji Chande ametoa kauli hiyo wakati ambao maeneo mbalimbali nchini yamekumbwa na migogoro mikubwa ya ardhi na kusababisha wananchi kupoteza mali,mifugo,makazi na wengine kuuawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu sherehe ya Siku ya Sheria Nchini itakayofanyika Februari 3, mwaka huu, Jaji Chande amesema, “Ukiondoa idadi kubwa ya kesi za jinai, zinazofuata wa wingi ni kesi za migogoro ya ardhi, hasa za madai, mfano Mahakama Kuu ya Tanzania pekee kuna kesi za ardhi zaidi ya 6,000.”

Alisema asilimia 60 ya kesi hizo zinatoka kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya.“Mfumo wa kutatua kesi za ardhi uko chini ya mamlaka tatu. Ngazi ya chini kabisa ni Baraza la Ardhi la Kijiji ambalo lipo chini ya Serikali za Mitaa na Halmashauri. Pili, ni Baraza la Kata,” alisema na kuongeza.

“Na tatu ni Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ambalo mamlaka yake ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Baada ya hapo ndiyo kinafuata Kitengo cha Ardhi cha Mahakama Kuu” alisema.

Alisema tatizo lililopo sasa ni kwamba ili uweze kutatua migogoro ya ardhi ni lazima uangalie kesi husika ipo katika ngazi gani na kusisitiza kuwa migogoro mingi ipo katika ngazi za chini ambazo zipo katika mamlaka nyingine.

“Hivi sasa mfumo wa migogoro ya ardhi na mashauri ya ardhi unaangaliwa upya na Tume ya Kurekebisha Sheria ambayo imetembelea mikoa yote nchini na kukutana na wadau wote ikiwamo, mahakama, Wizara ya Ardhi, wananchi na wanasheria hivyo ripoti hiyo ikitolewa itasaidia kuboresha sheria,” alisema.


Mahakama za mwanzo


Akizungumzia mahakama za mwanzo, Jaji Chande alisema, “Tanzania tuna mahakama za mwanzo 960 lakini zinazofanya kazi ni 803, kati ya hizo zinazofanya kazi mahakama 487 ndiyo zina mahakimu wa kudumu na nyingine 316 hutoa huduma kwa kutembelewa na mahakimu mara moja au mbili kwa wiki kutokana na mahakimu kutoishi maeneo hayo.”


Alisema kwa sasa kuna uhaba wa majengo zaidi ya 296 ya mahakama za mwanzo, kwamba kuna majengo 157 ya mahakama za mwanzo ambayo hayafanyi kazi kwa sababu ya uchakavu.


Alisema mahakama hizo zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuwapo katika majengo chakavu na nyingine zikiwa ndani ya majengo yanayomilikiwa na taasisi mbalimbali na Serikali, jambo ambalo alisema linazifanya mahakama hizo kuonekana kutokuwa huru

AIBA MTOTO WA KIKE DAR


Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya kipolisi ya Dar Suleiman Kova akisisitiza jambo.


MKAZI wa Bunju B, Grace Chapanga(34), anashikiliwa na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga wa kike mwenye umri wa mwezi mmoja.


Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova alisema Chapanga alimuiba mtoto huyo, Veis Venus Desemba 27 mwaka jana katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.

Alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo baada ya kumhadaa mama wa mtoto aitwae Salma Frank (29), mkazi wa Kawe Mji Mpya kwa kumuomba ambebee huku wote wakiwa abiria wa daladala, wakitokea Hospitali ya Mwananyamala.

Kova alisema walipofika kituo cha daladala Mwenge, mtuhumiwa aliteremka upesi na kutoweka na mtoto, wakati mwenye mtoto akikusanya vitu vingine alivyokuwa navyo.

“Chapanga alitenda kosa hilo kwa kushirikiana na Halima Alabi (46), mkazi wa Boko Maliasili ambaye naye alikamatwa Januari 4 mwaka huu,” alisema.

Alisema watuhumiwa wote baada ya kutenda kosa hilo, waliondoka kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo Chapanga alimdanganya mumewe kuwa yeye ni mjamzito na angependa kwenda kujifungulia nyumbani kwao Sumbawanga.

“Upelelezi wa tukio hilo ulifanikisha kumkamata mume wa Chapanga aitwaye Daniel Mwaikambo (38), mkazi wa Bunju B, ambaye pia ni mfanyakazi wa Uhamiaji Makao Makuu Dar es Salaam na kwenda naye Sumbawanga, ambapo walimkuta mtuhumiwa na kumkamata” alisema.

Inasemekana kwamba tangu Chapanga na Mwaikambo wafunge ndoa mwaka 2010 hadi sasa, wanandoa hao hawajabahatika kupata mtoto.

Aidha, Kova alisema mwaka 2012 Chapanga alifanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni na daktari alimwambia hatoweza kushika mimba tena, jambo ambalo mwanamke huyo hakumueleza ukweli mume wake wala ndugu yake yeyote hadi alipopanga njama na hatimaye kufanikiwa kumuiba mtoto huyo.

Alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa kufuatilia uchunguzi wa vinasaba (DNA) vya mama mzazi, mtuhumiwa na mtoto aliyeibwa. Pia alisema mtoto huyo amekabidhiwa

MOROGORO WATEKETEZA NYAMA YA NG'OMBE NA SAMAKI


Picha ya nyama iliyoharibika baada ya kukamatwa mjini Morogoro.
 
Watumishi wa afya Manispaa ya Morogoro wamekamata nyama na samaki waliooza kilo 80 katika maduka ya bidhaa hiyo baada ya operesheni ya kushtukiza ya ukaguzi na ukamataji wa vyakula maeneo mbalimbali Morogoro.
 
Zoezi kama hili ni muhimu kuwa endelevu kwa manufaa ya afya za wana Morogoro kwa sababu watu wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka watatufikisha pabaya. Tunawahongeresha sana mabwana afys Morogoro. (TK)

SERIKALI WILAYANI MVOMERO YAFUNGA KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA

http://www.timesfm.co.tz/content/uploads/2013/8/15/cache/DC%20MVOMERO%20ANTHONY%20MTAKA_full.jpgANTHONY MTAKA Mkuu wa wilaya ya Mvomero akiongea na waandishi.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka amekifungia kwa muda usiojulika shughuli za uzalishaji, Kiwanada cha Sukari cha Mtibwa mpaka kiwanda hicho kitakapolipa madeni ya wafanyakazi na wakulima wa miwa.
Akitoa msimamo wa Serikali ya wilaya hiyo juu ya kukifungia kiwanda hicho mbele ya wafanyakzi na wakulima hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi za mtendaji wa kata ya Mtibwa wilayani hapa, Mhe. Mtaka alisema kuwa  wamechukua uamuzi huo baada ya mabishano ya muda mrefu baina ya pande zote  mbili kutofikia muafaka.
Mkuu huyo wa wilaya katika mabishano hayo ya muda mrefu juu ya madai ya wakulima na wafanyakazi alisema wanakidai Kiwanda cha Mtibwa zaidi ya Sh1.9 bilioni ambazo ni za mauzo ya miwa na mishahara ya wafanyakazi.
Mtaka alisema shughuli nyingine kiwandani hapo zitaendelea kama huduma ya afya, ulinzi na idara ya fedha ili kuwezesha makundi hayo kupata mafao yao mwishoni mwa wiki hii kama ilivyoahidiwa na uongozi wa kiwanda hicho.
Meneja mkuu Hamad Juma alisema, kiwanda hicho kilikwama kulipa madeni hayo kutokana na uingizwaji mwingi wa sukari nchini kutoka nje ya nchi uliosababisha wao kukosa soko ingawa waliahidi kuanza kulipa mwezi huu. (TK)

Alhamisi, 30 Januari 2014

VIBAKA WACHOMWA MOTO BAADA YA KUKAMATWA WAKIIBA HUKO KAHAMA

Watu wawili ambao hawajafahamika majina yao wameuwawa kwa kuchomwa moto na wananchi wanaozaniwa kuwa na hasira kali katika kijiji cha Kagongwa wilayani Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kudaiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwemo Komputa.
 
Tukio hilo limetokea jana  majira ya saa tano asubuhi baada ya watuhumiwa hao kujaribu kuwakimbia viongozi wa Sungusungu waliokuwa wanawashikilia baada ya kuwakamata.

Kwa mujibu wa Mashuhuda wamesema vijana hao walikuwa ni tishio katika mji huo kutokana na kutuhumiwa kufanya vitendo wa wizi mara kwa mara. 
Wananchi wenye hasira kali baada ya kuwakamata wameamua kuwachoma moto kwa madai kuwa iwe ni fundisho kwa wengine.
 
Wamesema Awali watuhumiwa walikamatwa na sungusungu ya kijiji cha Iponya wilayani humo kabla ya kuamriwa wakaoneshe vitu hivyo ndipo wakapata mwanya wa kukimbia.
 
Diwani wa kata ya Kagongwa Hamis Kashantole ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo amekataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai kwamba hana muda wa kuongea.
 
Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na  uchunguzi unaendelea

GHANA NA LIBYA HAOOO FAINALI ZA CHAN KUPITIA MATUTA

Timu ya Taifa ya Ghana kwa wachezaji wa ndani imeitoa Nigeria kwenye mashindano ya CHA mwaka huu baada ya kuitoa kwa mikwaju ya penalti ambapo Ghan walipata penalti 4 kwa moja ya Nigeria.
CHAN 2014 Results: Scores, Analysis from African Nations Championship Semifinals
 Aidha Libya nayo imetinga fainali baada ya kuitoa Zimbabwe pia kwa matuta ambapo Libya ilipata penalti 5 kwa 4 za Zimbabwe katika fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani inayoendelea nchini Afrika Kusini.




UBALOZI WA CHINA NCHINI WASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO WA MOROGORO

Ubalozi China 02Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Youqin. akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi misaada hiyo.Ubalozi China 01
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali kutoka kwa Balozi wa Mhe. Lu Youqin.
Na Eliphace Marwa-Maelezo
Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya watu wa China nchini wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko mkoani Morogoro toka kwa Mhe. Lu Youqing ,vyenye thamani ya sh. milioni 30.
Msaada huo umetolewa na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing na ulikabidhiwa kwaMkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali amesema kuwa anaishukuru Serikali ya China kwani imekuwa mstari wa mbele pale Tanzania inapopata maafa mbalimbali.
Aidha Luteni Jenerali Rioba aliongeza kuwa mafuriko hayo ya aina yake hayajawi kutokea yalianzia milima ya Kilosa na Mvomero na kupelekea kufurika kwa mto Mkundi.
“Mheshimiwa Balozi mvua hizi zilikuwa kubwa ambazo hazijawahi kutokea wilayani Mvomero na kupelekea kuharibu daraja la Dumila ambalo ndiyo kiunganishi cha Mkoa wa Morogoro na Dodoma,” alisema Luteni Jenerali Rioba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Antony Mtaka akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema kuwa mamia ya nyumba ikijumuisha madarasa, majengo ya mahakama ya mwanzo, mashamba na barabara zimeharibiwa vibaya na mafuriko hayo.
“Kwa niaba ya Serikali napenda kushukuru Serikali ya China kupitia Mhe. Balozi Lu kwa msaada huu na ningependa kuahidi kuwa msaada huu utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa, ”alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wake Balozi wa china ametoa pole kwa waathirika wa mafuriko na kusema kuwa watu wa Jamhuri ya China wako pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.
“China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu hivyo kampuni ya ujenzi ya CCECC ilichukua hatua za haraka katika kushiriki ujenzi wa daraja hilo kwa kushirikiana bega kwa bega na ndugu zao Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana na kumaliza ujenzi huo kwa muda wa siku mbili,” alisema Balozi Youqing.
Ubalozi wa China kwa kushirikiana na makampuni ya China nchini umetoa vitu mbalimbali ikiwemo Chakula, mashuka, madawa na maturubahi ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa waathirika hao wa mafuriko mkoani Morogoro.

ZIMBABWEANS TO USE 9 DIFFERENET CURRENCIES

Acting Zimbabwe central bank governor Charity Dhliway addresses a conference in Harare on January 29, 2014. Zimbabwe has approved domestic trading in the Chinese yuan, Indian rupee, Japanese yen and Australian dollar, in a move that will effectively make those currencies legal tender. PHOTO | JEKESAI NJIKIZANA

Acting Zimbabwe central bank governor Charity Dhliway addresses a conference in Harare on January 29, 2014. Zimbabwe has approved domestic trading in the Chinese yuan, Indian rupee, Japanese yen and Australian dollar, in a move that will effectively make those currencies legal tender. PHOTO | JEKESAI NJIKIZANA AFP
HARARE
The Reserve Bank of Zimbabwe (RBZ) has announced the adoption of four more currencies in an attempt to address cash shortages in the economy.
The currencies of China, India, Japan and Australia are set to be legal tender and will be used alongside the US Dollar, South African Rand, Botswana Pula, British Pound and the Euro.
Zimbabwe introduced the multi-currency system in 2009 in response to runaway inflation.
“Trade and investment ties between Zimbabwe, China, India, Japan and Australia have grown appreciably,” said RBZ acting governor Charity Dhliwayo. “It is against this background of growth in trade and investment ties that in the 2014 national budget, the minister of finance and economic development underscored the importance of including other currencies in the basket of already circulating currencies.”
She said exporters and the general public could open accounts in the various currencies in the basket.
The adoption of multiple currencies helped Zimbabwe stem hyperinflation, which peaked at 500 billion percent in 2008.
President Robert Mugabe’s government was forced to dump the Zimbabwe dollar in 2009.
Zimbabwe has been trying to promote trade and investment with Asian countries after the veteran ruler’s inner circle was slapped with sanctions by western countries for alleged human rights violations.
Dr Dhliwayo also said the RBZ would assume its role of banker to government on March 31.
The bank would resume its lender of last resort function after government agreed to inherit its $1.35 billion debt and recapitalise it to the tune of $200 million.

SHILINGI ELFU KUMI ZAMTOA ROHO MFANYABIASHARA KENYA

Mfanyabiashara mmoja nchini Kenya amekutwa amekufa wilayani Nyamira kaskazni mwa Kenya..
Marehemu huyo James Keongo Ndubi, alisemekana kuwa ameenda kumdai mdeni wake sh 10,000 za Kenya sawa na sh 180,000 za Tanzania siku ya Jumanne lakini akaripotiwa kuwa hajulikani aliko siku hiyo hiyo.
Baada ya siku moja mwili wake ulionekana ukining'inia kwenye mti eneo la Boisanga.
Ndugu zake wanadai kuwa kuna mchezo mchafu umefanyika kwani alikuwa na majeraha kweny kichwa, miguuni na mikononi.
POST MORTEM
Taarifa kutoka kwa mpwa wa marehemu Bw Benard Momanyi, watafanya post mortem ili kubaini chanzo zha kifo hicho.
Mkuu wa Police huko Nyamira Shadrack Maithyaamethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa:
“Mwanzoni tulichukulia kifo hicho kuwa ni cha kujinyonga lakini baada ya hizi taarifa mpya tutafanya uchunguzi wa kina.”
Aliwaomba wananchi wenye taarifa zozote waisaidie polisi.

WATANZANIA WANA UHABA MKUBWA SANA WA MAJI.


MAJJJJJJJ_093d2.jpg
Sehemu za ndani ya mikoa ya Tanzania zikiwa kame.
Watanzania wanalaani hali ya hewa na kuongezeka kwa joto wakati usambazaji wa maji mijini ukidorora na huku mabishano yakizidi kuwa makali baina ya wakulima na wafugaji kuhusu matumizi ya vijito katika maeneo yao.
(MM)
Taarifa nyingi za kitaalam siku za nyuma zilionya kuhusu uongezekaji wa mahitaji ya maji na viwango vya maji yanayopatikana lakini tahadhari hizo ama zilipuuzwa au hazikutiliwa maanani ipasavyo.
Mara nyingi wanasiasa walibeza tahadhari hizo bila kufikiri pale walipowapotosha wananchi wao kuvamia mazingira yaliyohifadhiwa ili wakate miti, kuanzisha makazi au kulima mashamba karibu na vyanzo vya mito.
Miji ambayo imepanuka kwa haraka katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa na vijito vingi, kama vila Morogoro na Tanga katika ukanda wa mashariki, sasa inapata adha nyingi kuanzia mazingira machafu mpaka uhaba wa shughuli za kiuchumi kutokana na ukosefu wa maji.
Jiji kuu la biashara na viwanda, Dar es Salaam, pia limekumbwa na adha hizo. Mamia ya wakazi wa jiji hili hutumia saa nyingi kila siku wakitafuta maji. Matatizo yao huenda yasikomee hapo kadiri gharama za upatikanaji maji zinavyozidi kupanda siku hadi siku.
Mameneja wa rasilimali hii pia wanasumbuka kuziba mabomba yanayovuja huku wakipambana na wizi wa maji pale ambapo watu hujifungia mabomba isivyo halali, wakati viwango vya maji vikishuka kule yanakotoka kabla ya kuingizwa katika mifumo ya usambazaji.
"Uhai wetu, ustawi wetu, afya zetu na maendeleo yetu vyote hutegemea upatikanaji maji safi na salama pale tunapoishi. Wakati umefika tuone kila anayeharibu chanzo cha maji ni adui," amesema Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji wakati wa kuzindua mradi wa maji katika manispaa ya Moshi.

RWANDA YAZIDI KUMCHOKOZA JK



Kagame-na-Kikwete 4744f
BUSARA ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kuitaka Serikali ya Rwanda kukaa kwenye meza ya mazungumzo na waasi wa FDLR, imeendelea kutafsiriwa vibaya na baadhi ya wakubwa wa nchi hiyo, ambapo sasa wameanza kumchokonoa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, kwa kudai kuwa amekutana kwa siri jijini Dar es Salaam na waasi hao. (HM)

Gazeti la News of Rwanda ambalo linatajwa kuwa mshirika mkubwa wa Serikali ya nchi hiyo, katika toleo lake la Jumapili iliyopita, liliandika kuwa Rais Kikwete amekutana na waanzilishi wa chama cha upinzani nchini humo cha Rwanda National Congress (RNC) na makamanda waandamizi wa waasi wa FDLR.
Habari iliyoandikwa na gazeti hilo, imebainisha kuwa kikao hicho cha Rais Kikwete na watu hao kilifanyika kwenye makazi binafsi ya Rais Kikwete.
Gazeti hilo lilidai kuwa limepata taarifa hizo kutoka kwenye vyanzo vyake vya habari vilivyopo nchini Tanzania, ambapo viliwaeleza kuwa ujumbe huo uliwasili, jijini Dar es Salaam Alhamisi ya wiki iliyopita.
Wameandika kuwa viongozi wa RNC waliokutana na Rais Kikwete ni Mratibu wa chama hicho, Dk. Theogene Rudasingwa na mshauri wake, Condo Gervais.
Katika kikao hicho, News of Rwanda lilidai kuwa kundi la waasi wa FDLR, liliwakilishwa na Katibu Mtendaji wake, Luteni Kanali Wilson Irategeka na Kanali Hamadi ambaye ni kamanda wa operesheni.
IMG_0417Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za DAWASA. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry na Kulia ni Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa.Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry.IMG_0480Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akizungumza katika mkutano alipotembelea DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala jana alitembelea DAWASA na DAWASCO kuzungumza na uongozi wa taasisi hizo nchini zenye dhamana ya kusimamia huduma za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na miji midogo ya Kibaha na Bagamoyo.Mhe. Makala ametembelea taasisi hizo na kuzungumza na menejimenti na bodi za taasisi hizo ili kufahamu maendeleo na utendaji wa taasisi hizo katika kuleta matumaini ya huduma bora za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na mji midogo wa Kibaha na Bagamoyo.
“Tuna chanagamoto ya upatikanaji wa maji, lakini kama Serikali ni jukumu letu kuhakikisha tunalipatia ufumbuzi ”, alisema Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala.“Hatuna budi kuweka mikakati sahihi na kutekeleza kwa kasi miradi inayoendelea ili wananchi wapate maji na waliopewa dhamana ya usimamiaji watekeleze kwa wakati”, alisema Naibu Waziri.Pia, Mhe. Makala amedhamiria kutatua tatizo sugu la wizi wa maji na kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na akasisitiza wahusika lazima wachukuliwe hatua kali.Aliongeza suala la upotevu wa maji liwe ni ajenda ya kudumu ili kuhakikisha linakwisha na kuziasa DAWASA na DAWASCO zisiwe chanzo cha matatizo, bali watafute ufumbuzi wa tatizo la maji.Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa alisema DAWASA imeweka mikakati ya upanuzi wa mitambo na mifumo ya maji, ujenzi wa bwawa la Kidunda na kuthibiti maji yanayopotea kuhakikisha inaboresha huduma zake.Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala alisema mikakati waliyojiwekea ni kupunguza madeni wanayodai wateja wake, kufunga mita kwa wateja wote na kuongeza uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa mamlaka hiyo.
Hii ni mara ya kwanza tangu Mhe. Makala ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea taasisi hizo zinazotoa huduma ya maji jijini Dar miji midogo wa Kibaha na Bagamoyos.
Ziara hiyo itaendelea kwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea miradi ya maji ya Ruvu Chini na Juu na maeneo ya Segerea na Ubungo
IMG_0464IMG_0587
IMG_0560
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.

ZABUNI ZA VITALU KUFUNGWA MEI-WAZIRI

muhongo 7fc90
Serikali imesema zabuni ya vitalu vya utafiti wa mafuta na gesi asilia vilivyo bahari kuu na ziwa Tanganyika Kaskazini, itafungwa Mei 15, mwaka huu.
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo alisema hayo alipofanya mazungumzo na Waziri Mstaafu wa Nishati na Viwanda kutoka Ufaransa, Erick Besson aliyemtembelea ili kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika Sekta za Nishati na Madini akiiwakilisha Kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa.
"Kampuni unayoiwakilisha ni kubwa, yenye teknolojia ya kisasa na inafanya uwekezaji mkubwa duniani,"alisema Profesa Muhongo.
Waziri Muhongo alimweleza Besson kwamba Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), linamiliki vitalu viwili vya gesi karibu na mpaka wa Msumbiji lakini linahitaji mbia mwenye nia ya dhati watakayeshirikiana naye katika hatua zote za uendelezaji wa vitalu, kwa sababu TPDC bado inakua, alitoa changamoto kwa kampuni hiyo ya GDF Suez kuingia katika ushindani huo.

Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa Muhongo alimweleza Besson kuwa TPDC pia itahitaji kupata uzoefu na pengine mbia aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini.
Profesa Muhongo alisema Serikali itasambaza gesi katika makazi ya watu ili kupunguza uharibifu wa mazingira huku akitoa mfano kuwa Dar es Salaam pekee inatumia si chini ya magunia 50 ya mkaa kwa siku hivyo gesi itapunguza uharibifu wa mazingira.
Naye Waziri huyo mstaafu kutoka Ufaransa,Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa taarifa nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC,Stamico na Tanesco ili kuona jinsi kampuni yake itakavyoshirikiana na mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.
Ugunduzi wa mafuta na gesi umeleta habari njema kwa taifa na wawekezaji. Chanzo: mwananchi

HELKOPTA YA CHADEMA YAPOTEA ANGANI



HELIKOPTA ya Chadema maarufu kama Chopa, juzi ilipotea angani na kusababisha viongozi wa chama hicho kushindwa kufanya mkutano katika Kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino, kama ilivyokuwa imepangwa kwenye ratiba.
Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imepangwa, viongozi wa kitaifa ambao ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (BAVICHA), walikuwa wafanye mkutano katika kijiji hicho saa 4 asubuhi.
Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Steven Massawe alikiri kupotea kwa helikopta hiyo na kukanusha kwamba hakuna njama zozote zilizofanywa na CCM kutokana na kupotea kwa helikopta hiyo.
Kijiji cha Mpwayungu kipo katika Kata ya Mpwayungu, ambayo nafasi ya udiwani ipo wazi na vyama vya Chadema na CCM vyote vimesimamisha wagombea.
“Sababu kubwa ya kupotea kwa helikopta ni tatizo la mawasiliano kama mnavyojua Kijiji cha Mpwayungu hakina mawasiliano. Helikopta ilikuwa ifike katika Kijiji cha Mpwayungu saa nne asubuhi, lakini Kapteni alipotea na kusababisha kukaa angani kwa saa moja na dakika arobaini na akatua Kijiji cha Chipogolo.
“Alipofika Chipogolo akaambiwa sio kijiji hicho chenye mkutano na akatakiwa kurudi nyuma kwa upande wa magharibi kwa kilometa 40, hata hivyo hakufanikiwa ikabidi arudi mjini kujaza mafuta,” alisema Massawe.

Alisema baada ya kujaza mafuta, viongozi hao hawakwenda tena kufanya mkutano Mpwayungu badala yake wakaenda Mpwapwa ambapo kulikuwa na mkutano mwingine saa 7 mchana kwa mujibu wa ratiba.

“Leo (jana) hii viongozi hao kwa kutumia helikopta wamekwenda tena Mpwayungu na kufanikiwa kufanya mkutano majira ya saa nne asubuni na baada ya hapo waliekea Kijiji cha Segala Wilaya ya Chamwino, baadaye wataenda Kiteto na Moshi,” alisema.

Alisema sio kweli kwamba CCM walifanya njama helikopta ya Chadema ipotee ili isifanye mkutano katika kijiji hicho na kwamba Chadema na CCM vyote vilishafanya uzinduzi wa kapteni katika kata hiyo.

“Chadema ilifanya uzinduzi wake wa kampeni katika Kata ya Mwayungu, Januari 26 mwaka huu na CCM walifanya uzinduzi wao Januari 20,” alisema Massawe.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema iwapo Serikali ya CCM haitaweka mazingira ya haki kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kwa ajili ya amani ya kudumu, migogoro ya ardhi italitumbukiza taifa katika sintofahamu na hatari kubwa nchini.

Dk. Slaa aliyasema hayo kwenye mikutano ya M4C Pamoja Daima, jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Iselamagazi, Kishapu, Mhunze, Itilima, Lugulu na Bariadi.

Alisema ni haki kwa wananchi kuwa na matumaini, kwani ndiyo misingi wa amani ya kweli ambayo haihitaji kuhubiriwa jukwaani

NAFASI ZA KAZI OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA

THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA

VACANCY ADVERTISEMENT
The Open University of Tanzania (OUT) is a public University, established by the Act of
Parliament No 17 of 1992. Since 1st January, 2007, the University has been operating under
the OUT Charter Inc. of 2007, which is in line with the Universities Act No. 7 of 2005. Its
stated mission is to continuously provide open and distance education, research, and public
services for sustainable and equitable socio-economic development of Tanzania in particular,
and the rest of Africa. The Open University of Tanzania operates through its temporary
headquarters in Kinondoni, Dar es Salaam and its 27 regional centres in each region of
Tanzania Mainland and two coordination centres in Zanzibar and Pemba Islands.
The University hereby invites applications from competent and suitably qualified candidates,
to enhance its human resource capacity needed to fulfill its mission, as follows:
A. ASSISTANT LECTURER (PUTS 3)
Qualifications:
Possession of a good Master’s Degree (B+ or above, GPA 3.8 - 3.6) in the relevant discipline
or equivalent with a GPA of 3.8 and above at undergraduate level.
Duties:
As for Tutorial Assistant plus:
- Prepare new study materials, scripts for radio broadcast, video and audio cassettes,
various reports and papers,
- Adopt and/or supplement existing materials,
- Liaise with course writers, editors, reviewers, producers, artists, coordinators and
other members of the course team,
- Revise course materials and audio programmes,
- Conduct public lecture, tutor and lead academic discussions,
- Set and mark course assignments and/or tests, examinations supervise field work,
practicals and all other related academic activities,
- Encourage and motivate students to improve academic performance,
- Identify and set up local study groups,
- Conduct research and disseminate research findings.
NB. Age limit: Not above 45 years.
B. LECTURER (PUTS 4 - 5)
Qualifications: Candidates should have a PhD degree in the relevant field or equivalent
professional qualifications for non PhD applicants, relevant publications will be considered.
Duties:
As for Assistant Lecturer/Research Fellow with added responsibilities, he/she will be
required to:
- Teach face to face course and lead seminars;
- Undertake individual research and participate in bigger multi-disciplinary research
projects;
- Prepare manuals and case studies for training;
- Offer close supervision and guidance to students;
- Manage undergraduate programmes
- Undertake consultancy projects.
NB. Age limit: Not above 45 years
C. PROFESSOR (PUTS 10)
Qualifications: The Candidate should have at least three years of professional work as
Associate Professor with extensive teaching and research experience. In addition one must
have published study materials whose weighing totals eight points (for course units) on one
good book with one course unit. For Associate Research Professor, Candidates should have
eight course units or sixteen points or two books and two course units since last promotion.
Duties:
As the Associate Professor plus the following:
- Conduct formal training in specific multidisciplinary projects conducted by the
University.
- Provide personal guidance and advice to client in the field; undertake large
consultancy projects
- Provide guidance to members of staff;
- Prepare and publish manuals or textbooks in related fields. A Professor is also
expected to deliver a Professional Inaugural lecture within two years of promotion.
He /she should demonstrate the ability to provide the highest leadership in the
discipline at large, in research, or supervision.
D. SENIOR HUMAN RESOURCES MANAGEMENT OFFICER (PGSS 15-16)
Qualifications: The Candidate should have attained Masters Degree in Human Resources
Management, Public Administration, Business Administration, Sociology, Law or any other
relevant field with at least five years working experience in a similar position. Must be
computer literate.
Duties:
- Participates in preparation of policies.
- Counsels employees who present problems of attitude and or performance.
- Recommends disciplinary action for staff.
- Recommends changes in classification of job positions.
- Prepares personal emoluments budget for the University.
- Prepares training needs and budgets.
- Prepares quarterly, half year, and annual training reports for the Directorate and the
University.
- Deals with staff allocation.
- Participates in performance appraisals of staff
- Organizes and supervises support staff services including confirmation and promotion
- Performs any other related duties as be assigned by his/her supervisor
NB. Age limit: Not above 45 years.
E. SENIOR LEGAL OFFICER (PGSS 15- 16)
Qualifications:
Possession of LLM Degree plus one year attendance of Intern-ship /the Law School and must
be admitted as an Advocate of the High Court. Must be computer literate, with at least five
years of relevant working experience in a similar position.
Duties:
- Scrutinizes and effects registration of leases and transfer of properties in liaison with
the Estates Manager.
- Participates in negotiations for writing general contracts pertaining to such leases and
transfer of properties.
- Represents the University in more complex legal issues.
- Liaises with retained external legal agencies.
- Interprets laws and other legal technicalities.
- Appearing in court on behalf of the University.
- Prepares legal briefs and provides legal advice to Management.
- Compiles evidence relevant for court cases involving the University.
- Performs any other duties as may be assigned by his/her supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
F. SENIOR ACCOUNTANT (PGSS 15-16)
Qualifications: The Candidate should be a holder of CPA (T), ACCA, ACA, ICMA, /RIA or
equivalent qualifications with 5 years working experience in a similar position. Must be
computer literate.
Duties:
- Prepares monthly trial balances and bank reconciliation statements
- Maintains debtors and creditors records.
- Prepares financial statements.
- Checks accuracy of payment vouchers
- Prepares various payment reports, schedules and lists of various expenditures.
- Maintains vote book and various registers (e.g. debtors, imprest, creditors), etc.
- Prepares salaries and wages and submits statutory and voluntary staff deductions as
required by the relevant legislation and /or contractual agreements.
- Maintains students’ fees subsidiary ledger.
- Performs any other related duties as may be assigned by his/her supervisor
NB. Age limit: Not above 45 years.
G. ACCOUNTANT II (PGSS 11-12)
Qualifications: The Candidate should be holder of a First Degree/Advanced Diploma in
Accountancy e.g. B.Com (Accountancy), BBA (Accountancy), BA (Accountancy) or
professional Module C and D and must be computer literate.
Duties:
- Prepares reports of various payments, schedules and lists of various expenditures.
- Maintains vote book and various registers (e.g. debtors, imprest, creditors), etc.
- Prepares salaries, and wages, and submits statutory and voluntary staff deduction as
required by the relevant legislation and /or contractual agreements.
- Maintains students’ fees subsidiary ledger.
- Maintains full and accurate accounts records.
- Maintains imprest retirement journal.
- Prepares monthly staff imprest account balances.
- Performs any other related duties as may be assigned by his/her supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
H. ACCOUNTS ASSISTANT II (PGSS 7-8)
Qualifications: The candidate should be a holder of Form VI Certificate with NABE
III/ATEC II/Diploma in Accountancy/Module A and B plus ICT skills.
Duties:
- Receives and keeps in proper custody all incoming bills and claims.
- Maintains primary books of accounts.
- Prepares payment requisitions, vouchers and cheques.
- Prepares journals voucher/batches for various activities.
- Maintaining accounting records.
- Performs any other related duties as assigned by his/her supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
I. PERSONAL SECRETARY II (PGSS 10-11) - TWO (2) POSITIONS
Qualifications: The candidate should be a holder of National Form IV/VI Certificate with
credit passes in English and Kiswahili or foundation course certificate plus Diploma in
secretarial studies from Tanzania Public Service College or any recognized Institutions with
at least four years working experience in the relevant field and Shorthand/Hatimkato 100/120
w.p.m and 50 w.p.m typing, tabulation and manuscript stage III. Must be computer literate in
the following programmes: Microsoft office, Internet, E-mail and Publisher.
Duties:
- Types confidential and non confidential documents.
- Ensures expedient, accurate and clean execution of duties
- Organizes travel arrangement for senior officers and other officers within the Unit
- Prepares meeting and records Proceedings.
- Supervises and guides junior secretaries
- Attends telephone calls and keeps appointment.
- Types all general correspondence and non-confidential matters.
- Types letters, minutes, notices, bulletins, circulars, certificates, charts and stencils.
- Performs any other related duties as may be assigned by supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
J. TITLE: RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT III PGSS 7-8
Qualifications: Possession of Form IV/VI Certificate with two Principal Passes in Arts
subjects and must have a credit pass in English at “O” level plus a Certificate in Records
Management from a recognized institution. Must be computer literate.
Duties
- Opens new files and indexes cards.
- Maintains an up-to-date register of office files.
- Files correspondences into the appropriate files and cross references.
- Copies correspondence to relevant files.
- Gives searchers numbers of files which are required for filing.
- Ensures proper file Management.
- Returns files to the cabinets and arranges them in proper order.
- Maintains up-to-date file index books.
- Performs any other related duties as may be assigned by his/her supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
K: COMPUTER PROGRAMMER I - PUSS 9
Qualifications The Candidate should be a holder of First Degree in Computer Science/
Information Systems/ Telecommunication/Electrical Engineering/Information
Technology/GIS or any related computer studies with at least three years relevant working
experience in a similar position.
Duties;
- Advises and assists computer users.
- Analyses, designs and programmes medium size applications.
- Installs standard software and server operating systems.
- Installs modems and dial-up networking
- Solves complex hardware/software problems
- Assists in designing and coding small system jobs for users
- Assists both students and staff in debugging programmes and programming systems
- Performs any other related duties as be assigned by his/her supervisor.
NB. Age limit: Not above 45 years.
MODE OF APPLICATION
• Applicants should clearly specify the Vacancy Number and Position they are applying
for, from the list above. Applications bearing no such information shall not be
considered.
• Applications should be accompanied with a detailed curriculum vitae, certified copies
of relevant certificates, one colored passport size photograph of the applicant, names
and full contact details of three referees
• The applicants should be willing to work in any of the regions in Tanzania Mainland’s
and Zanzibar, as specified in the vacancy list above. No change of work station is
possible after being appointed.
• All applicants who are currently employed in the Public Service should route their
application letter through their respective employers.
• All applicants with certificates from foreign Universities should have the certificates
verified by the Tanzania Commission for Universities (TCU).
For Academic Posts, interested applicants should submit the applications to the undersigned;
The Deputy Vice-Chancellor (Academics)
Open University of Tanzania
Kawaka Road, Kinondoni
P.O. Box 23409, Dar es Salaam, TANZANIA
Tel. +255 22 2668820
Fax: +255 22 2668759
Email: dvc-ac@out.ac.tz
For Administrative Posts, interested applicants should submit the applications to the
undersigned;
A. ACADEMIC POSTS
VACANCY
NUMBER POSITION FACULTY SPECIALIZATION NUMBER OF POSTS WORK STATIONS
OUT2014/01 Professor FSTES ANY 1 HQ
OUT2014/02 Professor FSTES ANY 1 HQ
OUT2014/03 Lecturer FASS ANY 1 HQ
OUT2014/04 Assistant
Lecturer
FASS LINGUISTIC 1 HQ
B. ADMINISTRATIVE POSTS
VACANCY
NUMBER
POSITION NUMBER OF
POSTS
WORK STATION
OUT2014/05 Senior Human Resources
Officer
1 Dar-es-Salaam
OUT2014/06 Senior Legal Officer 1 HQ
OUT2014/07 Senior Accountant 1 HQ
OUT2014/08 Accountant II 1 HQ
OUT2014/09 Assistant Accountant II 1 Kinondoni
OUT2014/10 Personal Secretary II 1 HQ
OUT2014/11 Personal Secretary II 1 HQ
OUT2014/12 Records Management Assistant
III
1 HQ OUT2014/13 Computer Programmer I 1 HQ
KEY:
FASS – Faculty of Arts and Social Sciences
FSTES – Faculty of Science, Technology and Environmental Studies
The qualifications and duties for each of the positions above are described below
The Deputy Vice-Chancellor (Resources)
Open University of Tanzania
Kawaka Road, Kinondoni
P.O. Box 23409, Dar es Salaam, TANZANIA
Tel. +255 22 2666752
Email: dvc-rm@out.ac.tz
The deadline for receiving applications is TWO WEEKS from the date of the first
appearance of this advertisement in the news paper.
Only short-listed candidates will be contacted