Ijumaa, 28 Februari 2014
BASI LA BUNDA EXPRESS LAGONGA TRENI MANYONI LAUWA WANNE
Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi hii limegonga Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.
Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi hii limegonga Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.
Treni iliyogongwa na basi hilo
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukiokinasema kuwa watu wanne wamefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa.Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.
SERIKALI YAWATOLEA UVIVU MAJANGILI, YANUNUA BUNDIKI 5,000 AINA YA AK47 KUKABILIANA NAYO.
DAR ES SALAAM.
SIKU moja baada ya Tanzania kutajwa na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kuwa kinara wa biashara ya meno ya tembo Afrika Mashariki, Serikali imelipia kodi na kukabidhiwa bunduki 500 aina ya AK47 ili kukabiliana na ujangili katika hifadhi na mapori ya akiba nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa silaha hizo zilizokuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tangu Novemba 2012 kutokana na kutokulipiwa kodi, zitasambazwa Ngorongoro, Selous, pamoja na Hifadhi za Taifa za Tanapa.
Kati ya silaha hizo, 250 zitapelekwa Idara ya Wanyamapori, 200 Tanapa na 50 Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.
“Silaha hizi jumla ya Sh427 milioni kuzinunua lakini zilikwama TRA kwa sababu ya kutolipiwa kodi na ushuru mbalimbali, hivyo wizara yangu leo inatoa Sh212 milioni kwa ajili ya malipo hayo,” alisema Waziri Nyalandu.
Alisema silaha hizo zimekombolewa ikiwa sehemu ya kutekeleza maazimio ya Bunge na ahadi ya Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira.
Akizungumzia sababu za kuchelewa TRA, Nyalandu alisema kulikuwa na ubishi wa ama zilipaswa kulipiwa kodi au la, lakini mamlaka hiyo ilifafanua kuwa hayo ndiyo matakwa ya sheria, hivyo akaamua kutoa fedha hizo.
Alipoulizwa ni jinsi gani Serikali itadhibiti silaha hizo, Nyalandu alisema wizara yake inaandaa miiko ya matumizi yake ikiwamo kufuatilia makabidhiano yake na askari wanaokabidhiwa.
“Kumbuka hizi si silaha za kwanza kuwa nazo, tunazo nyingine za AK47 na hizo zimetuwezesha kukamata silaha haramu zaidi ya 2,000 zinazotumiwa na majangili,” alisema.
Silaha hizo zimepatikana ikiwa ni takriban wiki mbili tangu Rais Jakaya Kikwete abanwe na vyombo vya habari vya kimataifa akitakiwa kueleza mikakati iliyopo kupambana na ujangili ambao umeharibu sura ya Tanzania nje ya nchi.
Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kupangua Baraza la Mawaziri na kuwatimua mawaziri wanne kutokana na vitendo vya kinyama vilivyobainishwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Majangili papa 40
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Nyalandu alisema majina ya majangili papa 40 ambayo Rais Kikwete alisema anayo, ‘yatabandikwa’ hivi karibuni. MWANANCHI
BANDARI YA DSM KUTOA HUDUMA MASAA 24 KUANZIA KESHO
Dar es Salaam. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikishirikiana na wadau wake kuanzia kesho wanatarajia kuanza kutoa huduma kwa saa 24, siku saba za wiki, mwaka mzima bila kupumzika.
Ofisa Uhusiano wa TPA, Janeth Zurangi alisema uamuzi huo ambao unakusudia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo, umefikiwa baada ya wadau mbalimbali kutia saini mikataba ya utekelezaji kazi hiyi
Zurangi alisema ingawa kulikuwapo mabishano kuhusu vipengele kadhaa ndani ya mkataba huo, wadau wote walikubali kuanza kutoa huduma kila siku kwa saa 24 kuanzia Machi Mosi.
"Mwezi ujao utaratibu huo utaanza na tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa. Hivi sasa mteja anaweza kuchelewa kuchukua mzigo kwa sababu baadhi ya wadau hawajasaini vibali husika," alisema.
Oktoba 14 mwaka jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwataka wadau wengine wanaofanya kazi na TPA kuanzisha utaratibu wa kufanya kazi kila siku, kwa kile alichoeleza kutofanya hivyo kunakwamisha kasi ya uondoaji mizigo bandarini.
Dk Mwakyembe alinukuliwa akisema: "Bandari wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki bila kupumzika, lakini wenzetu wa TRA wao sikukuu na siku za mwisho wa juma wanalala hali hii inaturudisha nyuma kimapato." Baadhi ya wadao waliosaini mkataba huo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa).(TK)
Alhamisi, 27 Februari 2014
50 CENT AKIONYESHA JEURI YA PESA
Mwanamuziki maarufu nchini Marekani 50 Cents ameonesha jeuri ya fedha pale alipoonekana akichezea manoti ya dola za kimarekani kama inavyoonekana hapa chini
Hapa anatengeneza picha ya ua ikimaanisha alama ya upendo.
Hapa anaonekana akiweka kitita cha noti mdomoni
Posted by TK
Jumanne, 25 Februari 2014
SERIKALI YASEMA ITABADILI MFUMO WA KILIMO ILI KULETA TIJA ZAIDI
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mikakati mbalimbali ya wizara yake katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Raphael Daluti na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
PICHA NA FATMA SALUM
Na Georgina Misama- MAELEZO.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kubadili mfumo wa uzalishaji ili kuleta tija katika sekta ya kilimo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Chiza alisema kuwa katika mfumo huo maeneo makuu matatu ya kipaumbele, ambayo ni kuwepo kwa mashamba makubwa ya uwekezaji yapatayo 25 kwa ajili ya kilimo cha mpunga na Miwa, kuwa na skimu za umwagiliaji 78 kwa ajili ya kilimo cha mpunga na maghala 275 ya mahindi kwa kutumia mfumo wa pamoja.
“Ili kuendana na kasi ya mfumo wa matokeo makubwa sasa, Serikali imeajapanga kuondokana na kilimo cha mazoea na kujikita kwenye kilio cha kisasa hasa kwenye mazao ya kipaumbele ambayo ni mpunga, miwa na mahindi” alisema Waziri Chiza.
Waziri Chiza alifanunua kuwa Serikali imejikita kwenye uzalishaji wa mazao hayo ili kukabiliana na changamoto zilizo kwenye sekta hiyo ikiwemo mfumuko wa bei.
Ili kukabiliana na upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini Waziri Chiza alisema kuwa Serikali imeidhinisha tani 23,312 za chakula cha msaada ili kisambazwe kwa waathirika 828,063 ambao walionekana kuwa na upungufu wa chakula katika wilaya 54 za mikoa 16.
Hifadhi ya Taifa ya Chakula hivi sasa ina tani 226,769.544 ambapo tani 226,270.862 ni za mahindi na tani 498.682 ni za mtama, ambapo kiasi hicho kinajumuisha tani 25,452.644 za mahindi kutoka msimu uliopita
SERIKALI YATANGAZA TAREHE YA USAILI KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KILIMO NA MIFUGO
Serikali inapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi kwa tangazo la tarehe 27 Novemba, 2013 wa kada za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Udereva kuwa usaili utaanza tarehe 4 Machi, 2014 takriban katika mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea kwa lengo la kufahamu masuala mbalimbali ya uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini.
Amesema usaili huo unaoanza tarehe 4 Machi katika mikoa takribani yote nchini utahusisha jumla ya wasailiwa 6,087 wa fani za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na udereva kwa kada ambazo sio za Maofisa. Amefafanua kuwa vigezo vya kupanga mikoa ya usaili vimetokana na anwani ambazo waombaji waliwasilisha katika barua zao za maombi husika ya kazi.
Daudi alibainisha kuwa kila mwombaji aliyekidhi vigezo na kuchaguliwa kwa ajili ya usaili anapaswa kwenda kufanyia usaili katika mkoa aliopangiwa kama anwani yake inavyoonyesha katika tangazo kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, isipokuwa kwa waombaji wa mkoa wa Katavi wao wataenda kufanyia usaili mkoa wa Rukwa na waombaji waliotumia anwani za mkoa wa Singida wao watafanyia usaili mkoa wa Manyara kutokana na sababu zisizozuilika.
Aliongeza kuwa kwa mwombaji ambae hatazingatia anwani, siku na muda aliopangiwa na kuamua kwenda mkoa mwingine tofauti na utaratibu uliopangwa ajue wazi hatasailiwa kwa kuwa ratiba na idadi ya majopo ilishapangwa kwa kila mkoa na haitabadilishwa ili kuweza kurahisisha kazi hiyo kukamilika kwa ufanisi.
Aidha, amewataka waombaji wote wa tangazo hilo kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni http://www.ajira.go.tz/ wao wenyewe ili kuweza kujua kiundani endapo wamechaguliwa kufanya usaili, kufahamu tarehe, mahali na muda wa kuanza usaili ili kuepuka usumbufu usiokuwa na lazima.
Daudi aliendelea kufafanua kuwa kwa waombaji waliotumia anuani za mkoa wa Dar es Salaam kwa nafasi ambazo sio za maofisa usaili utafanyika tarehe 11 Machi, 2014.
Aidha, kwa nafasi za Maofisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wote usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, 2014.
Katibu amewataka waombaji wote kuhakikisha pindi wanapoenda kwenye usaili wawe wamejiandaa vya kutosha ikiwemo kubeba nyaraka muhimu hususani vyeti halisi vya taaluma zao maana vitahitajika kwa ajili ya uhakiki siku ya usaili. Aidha, amewasihi waombaji wa matangazo mengine ya nafasi za kazi kuwa na subira wakati uchambuzi ukiendelea na pindi utakapokamilika wahusika watataarifiwa.
Alimaliza kwa kuwasisitiza wadau wa Sekretarieti ya Ajira kuwa pindi wanapoona matangazo ya kazi, ikiwemo kuitwa kwenye usaili au kupangiwa vituo vya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hususani baadhi ya mitandao ya kijamii wajiridhishe kwanza kwa kuangalia taarifa hizo katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira, ili kuepuka taarifa zisizokuwa za kweli ambazo zimekuwa zikitolewa nyakati nyingine na baadhi ya watu wasio waaminifu kwa lengo la kupotosha Umma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 21 Machi, 2014
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (TK)
Jumamosi, 22 Februari 2014
UGANDA: MSWADA DHIDI YA PICHA ZA NGONO WATIWA SAINI
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda atia saini muswada wa sheria dhidi ya picha za ngono.
Ikiwa unaishi Uganda na unapenda kuvaa nguo fupi, zinazobana au zinazoonyesha sehemu za mwili ambazo zaweza kuwafanya watu wa jinsi nyingine kusisimkwa na kutamani kushiriki ngono nawe, basi jua uko taabuni.
Hii ni kwa sababu rais Yoweri Museveni ametia saini mswada dhidi ya picha za ngono ambao unapinga mavazi yasiyo ya heshima haswa yanayovaliwa na wanamuziki na picha za watu wakiwa uchi. (TK)
MWANAFUNZI AJICHOMA KISU BAADA YA KUFELI MITIHANI KIDATO CHA NNE
Kufuatia matokeo ya kidato cha nne kutangazwa rasmi jana Mwanafunzi mmoja alijipiga kisu akitaka kujiua.
Kijana ambae jina lake halijafamika mpaka sasa, anayeishi Mwananyamala Dar es Salaam anayesemekana kuwa ni mwanafunzi ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka jana yaani 2013 alikutwa amejichoma kisu shingoni na kuwahishwa hospital, huku chanzo kikisemekana kuwa ni matokeo yako ya kidato cha nne, matokeo yake hayakuwa mazuri maana amefeli kwa kupata ziro
MUGABE ATIMIZA MIAKA 90, SHEREHE YAKE KUFANYIKA UWANJANI JUMAPILI, ITATUMIA DOLA MIL 1
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza umri wa miaka 90. Hata hivyo sherehe yake imegubikwa na wasiwasi juu ya afya yake.
Wakati ambapo wasaidizi wake wanasema afya yake iko vizuri, wiki hii alienda tena nchini Singapore kwaajili ya upasuaji wa macho na hivyo kuamsha tena wasiwasi. Bado yupo nchini humo na sherehe yake ya kuzaliwa itafanyika uwanjani siku ya Jumapili na inadaiwa kugharimu dola milioni 1.
Mugabe alizaliwa tarehe 21 February 1924. Sherehe yake itahudhuriwa na maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa Marondera, mji uliopo kilomita 75 mashariki mwa mjini mkuu, Harare.
Kutakuwepo na muziki, michezo na chakula (TK).
Jumatano, 19 Februari 2014
NAFASI ZA KAZI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi
517 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
BENKI YA NIC TANZANIA KUTUMIA BILIONI 8.5 KWA WAJASIRIAMALI NCHINI
NIC Bank Tanzania watapata kiasi cha shiling bilioni 8.5/- kama nyongeza ya mtaji kutoka kwa wanahisa ili kuongeza ufanisi katika shughuli za kibenki kama vile utoaji mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati (SMEs).
Ongezeko hilo la bilioni 8.5/- litatolewa kwa awamu mbili kutoka kwa wanahisa wa NIC Bank Kenya na tayari bilioni 5.8/- zimeshatolewa toka mwezi desemba 2013.
Vile vile kuna ongezeko la shilingi bilioni 2.7 kutoka kwa kundi la wanahisa kutoka NIC Tanzania ambapo kabla ya Juni 2014 watakuwa wameshamaliza kutoa kiasi chote kitachotakiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Pankaj Kansara alisema kuwa wameamua kuongeza mtaji ikiwa ni katika mikakati ya kuboresha huduma za kibenki na vile vile kuweza kutoa mikopo kwa ufanisi kwa wajasiliamali wadogo na wa kati.
Kansara alisema kuwa benki ya NIC Tanzania ni benki yenye kutoa fursa katika kukuza biashara, miundombinu ya miradi mbali mbali na kuboresha mifumo ya biashara ambapo imeweza kusaidia kuvutia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja na kuchochea ukuaji wa wajasiliamali wa kati na wadogo.
“Mpango huu wa kuongeza mtaji wetu ni sahihi sana kwani utaweza kutuwezesha kuongeza mikopo kwa soko Tanzania katika kuongeza ufanisi na utowaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati na vile vile katika makundi, ” alisema
NIC Bank Tanzania imeongeza mtaji wake baada ya kutoka shilingi bilioni 30 kwa mwaka 2009 hadi bilioni 180 / – mwaka 2013, ambapo ni asilimia 43 ya pato la ukuaji wa mtaji.
NIC Bank Tanzania imeongeza mtaji wake baada ya kutoka shilingi bilioni 30 kwa mwaka 2009 hadi bilioni 180 / – mwaka 2013, ambapo ni asilimia 43 ya pato la ukuaji wa mtaji.
“Kwa kuangalia mafanikio ya benki yetu mama, tuna matumaini ya kuongeza nguvu na juhudi katika kuhakikisha kuwa tunatumia rasilimali zilizopo katika benki mama ya NIC Kenya kuendeleza na kukuza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini Tanzania”
Aliongeza: ” NIC Bank Tanzania kwa sasa ina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam , Arusha, Mwanza na Kahama ambapo kwa matawi haya tutaweza kusambaza huduma nyingi za kibenki na kuweza kuwafikia watu wengi ambao ni wahitaji”
NIC Bank Tanzania ni kampuni tanzu ya Nairobi Securities Exchange (NSE) ambao wapo na NIC Bank ambao wanamiliki hisa kubwa toka mwaka 2009
Jumanne, 18 Februari 2014
MWANAFUNZI AFUNGWA MNYORORO ASHIDWA KWENDA SHULE, ASIMULIA MATESO YAKE
Mtuhumiwa Dorah Joseph (34). |
Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda, kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika harakati zake za kutaka kumtumia mtoto huyo kishirikina ili aweze kujipatia mali.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Eleray alisema shangazi yake huyo amekuwa akimfanyia ukatili wa kutisha akishirikiana na jirani yake ambaye jina lake linahifadhiwa.
Happy alisema wazazi wake wote walishafariki, hivyo kumfanya yeye na dada yake kuishi kwa shangazi yake huyo, aliyemwelezea kama amekuwa akimtesa kwa kumnyima chakula, kumpiga, kumfunga mnyororo na kumfungia ndani kama mbwa.ANGALIA PICHA ZAIDI
Mtoto Happy Joseph (13).
‘’Shangazi ananitesa sana, ananifunga mnyororo kama mbwa na kunifungia chumbani, hanipi chakula wala kunipeleka shule, nina zaidi ya mwaka sasa sijaenda,” alidai Happy.
Aliongeza kuwa tofauti na dada yake, yeye ndiye amekuwa akiteswa huku ndugu zake wakizuiwa kumuona.
Akizungumzia tukio hilo, Askari wa Dawati la Jinsia, Deborah alisema ukatili uliofanywa na dada huyo kwa mwanafunzi huyo hauelezeki na kwamba wanakamilisha mashtaka ili kumfikisha mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye hadi anafikishwa polisi, alikuwa bado na mnyororo mguuni kutokana na kukosekekana kwa ufunguo wa kufungua kufuli kubwa mguuni kwake.
Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alisema alilazimika kumfunga mnyororo binti huyo baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kuzurura ovyo, kwani muda mwingi anatoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
Alisema mara kadhaa mtoto huyo amekuwa akitoweka nyumbani hapo wakati mwingine kwa wiki nzima bila kujulikana alikoelekea, ikiwa ni pamoja na kutoroka shuleni
Jumatatu, 17 Februari 2014
MGOMO WA DALADALA MWANZA...WANANCHI WAPANDA MALORI KUWAHI KAZINI.
BORA KUFIKA
CAMERA YETU ILIMURIKA MAANEO HAYA NA KUONA DALADALA ZIKIWA ZIMEPAKI
MSEMO WA KUFA KUFAANA ULITIMIA,BODABODA WALIKULA VICHWA KWA BEI WATAKAZO
MKUU WA (W) NYAMAGANA BARAKA KONISAGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, MDA MFUPI BAADA YA KUKUTANA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI, MADEREVA, NA WADAU WOTE WA USAFIRISHAKI JUU YA MGOMO WA DALADALA JIJINI MWANZA.
ZAIDI KIKAO KIMETOA WITO KWA MADEREVA KUSITISHA MGOMO MARA MOJA, AMBAPO AMESEMA KUWA AMEWAAGIZA WAHUSIKA WA JAMBO HILI KUFUATILIA SUALA HILI MARA MOJA IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA NINI MALALAMIKO YA MADEREVA ILI YASHUGHULIKIWE HARAKA IWEZEKANAVYO
UKATILI WA KUTISHA!! WATOTO DAR WAFUNGIWA NDANI MIEZI 6..
TUNAJUA shangazi anatutesa kwa sababu baba na mama wapo mbali, kama wangekuwepo hapa tusingeteswa hivi.
Tunamuomba baba, tunamuomba mama kama watasoma habari hii waje watuchukue turudi nyumbani, shangazi anatutesa sana, wala hatukutegemea,” ndivyo alivyoanza kusema mtoto Hassan Yusuf (5) ambaye ni mkubwa kwa wenzake, Hussein Yusuf (5) na Rehema Said (5).
Ikifika mahali mtoto mdogo anasema anawakumbuka wazazi wake kwa sababu ya mateso anayoyapata ugenini ujue ni zaidi ya ukatili, tena ni ukatili wa kutisha.
Watoto hao, kwa sasa wanaishi Nzasa ‘A’, Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na ndiko walikopatia mateso yote.MAMBO YALIPOANZA KUTIBUKA
Wiki iliyopita, watoto hao waliokolewa na majirani katika kifungo cha miezi sita ndani huku afya zao zikiwa zimedhoofu kwa kukosa chakula.
Ilidaiwa kwamba, watoto hao Hassan na Hussein ambao ni mapacha na Rehema, walifungiwa katika banda la shangazi yao aitwaye Asia Bora ambalo ujenzi wake haujakamilika. Wamekuwa wakiishi humo kwa kula mabaki ya vyakula jalalani.
USHUHUDA WA MAJIRANI
Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni, majirani wa nyumba hiyo walimweleza mwandishi wetu kuwa watoto hao wamekuwa wakionekana nje ya nyumba hiyo mara chache sana wakiwa wanagombania mabaki ya vyakula kwenye jalala.
“Tumekuwa tukiwaona nje mara chache kwenye jalala. Unajua, Asia (shangazi yao) aliwachukua kwa kaka yake, Kijiji cha Namakongoro Kata ya Lihimalyao huko Kilwa mkoani Lindi.
“Tukasikia lengo lake aje kuishi nao kwa vile yeye Mungu hamkujalia kupata watoto. Lakini maisha hapo kwake yakawa siyo mazuri kwa kipato kwa mama huyo.
Jumamosi, 15 Februari 2014
WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO NANYUMBU
RAIS KIKWETE ASEMA KUWA KUNA MAJANGILI PAPA 40 NCHINI
Wakati kuna joto la vyombo vya habari vya kimataifa kuituhumu Tanzania kuwa haipambani na ujangili, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imeubaini mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha. Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi mtupu.“Gazeti hilo limezungumza na nani, ndiyo maana sitaki kupoteza muda kujadili upuuzi, achana na mambo hayo. Ndiyo maana tunasema, akutukanaye hakuchagulii tusi,” alisema Rais Kikwete.Alisema inashangaza kuona watu wanaozusha taarifa hizo hawaoni jinsi tulivyofanya jitihada za kutokomeza ujangili, kama operesheni za tokomeza ujangili na operesheni kipepeo.Kuhusu majangili 40 ambao wametambuliwa, Rais Kikwete alisema wameutambua mtandao mkubwa wa majangili unaoongozwa na mfanyabiashara mkubwa wa Arusha Mjini.“Kuna majangili 40 waliotambuliwa na tumetambua mtandao mzima, pale Arusha kuna mtu mkubwa alikuwa anaendesha biashara. Kazi ilikuwa ni kutambua mtandano wote, ule mtandao ni mpana sana,” alisema Rais Kikwete.
PROFESA TIBAIJUKA ATOA UTETEZI WA ZIWA NYASA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameweka wazi utetezi wa Tanzania katika mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Malawi.
Akizungumza na wahariri wa habari katika semina ya ardhi Dar es Salaam jana, Profesa Tibaijuka alisema tayari Rais Jakaya Kikwete ametoa ushahidi wa mpaka huo katika Kamati ya Marais Wastaafu, Festus Mogae wa Botswana, Joachim Chisano wa Msumbiji na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini.
Katika ushahidi huo, kwa mujibu wa Profesa Tibaijuka, Tanzania ilitumia zaidi historia ya ugawaji mipaka ilivyokuwa na kutumia ushahidi wa nyaraka za serikali za kikoloni, zilizoshiriki kugawa mipaka ya Afrika.
Profesa Tibaijuka alisema mipaka ya nchi iliwekwa mwaka 1890 katika Mkataba wa Wajerumani waliokuwa wakitawala Tanganyika kwa kutumia hadithi za wagunduzi waliotangulia Afrika, kabla ya Wakoloni kuanza kugawana bara hilo.
Wakati huo kwa mujibu wa Profesa Tibaijuka, mpaka kati ya Tanganyika na Kongo na hata Malawi, ulikuwa Mashariki ya Ziwa na hivyo hata Ziwa Tanganyika, lilipaswa kuwa Kongo.
Alifafanua kuwa katika upimaji, baada ya kufanya uamuzi huo wa watawala, hatua ya pili ilikuwa kuunda tume kwenda kuhakiki mpaka huo kwa kuzungumza na wenyeji, na kuurekebisha kwa kufuata taarifa za wenyeji.
Mwaka 1898 tume hizo zikaundwa, na matokeo yake mipaka ya Ziwa Tanganyika, Mto Songwe na hata Ziwa Victoria ikawekwa katikati.
Kwa bahati mbaya, mwaka 1914 Vita ya Kwanza ya Dunia iliibuka na kusababisha tume hizo kusimama kazi kabla ya kupita na kuthibitisha mpaka katika Ziwa Nyasa.
Profesa Tibaijuka aliendelea kuanika ushahidi huo, kwamba baada ya vita ya dunia, Ujerumani ilishindwa na kupoteza makoloni yake ambayo yalichukuliwa na League of Nations ikiwamo Tanganyika ambayo ilitolewa kwa Uingereza kama mwangalizi.
Tanzania imethibitisha katika ushahidi wake kuwa, kitendo cha Uingereza kupewa Tanganyika kuwa mwangalizi huku Malawi ikiwa koloni lake, kilisababisha tume hiyo kutoendelea na kazi, kwa kuwa hakukuwa na umuhimu wa mpaka, wakati mtawala wa Malawi na Tanganyika akiwa mmoja.
Kwa mujibu wa Profesa Tibaijuka, Uingereza ilikuwa ikipeleka taarifa za uangalizi mara kwa mara League of Nations na kabla ya uhuru miaka ya 1950, Gavana wa Tanganyika alipeleka taarifa kutaka tume ifanye kazi yake kuhusu mpaka.
Profesa Tibaijuka alisema taarifa hizo ziko Geneva, Umoja wa Mataifa, na ujumbe wa Tanzania ulilazimika kwenda kupekua katika maktaba ya Umoja huo kupata vielelezo vya taarifa za Uingereza kuhusu mpaka, ambazo zimetumika katika ushahidi.
Ushahidi mwingine ambao Profesa Tibaijuka alisema utaisaidia Tanzania ni makubaliano ya kimataifa yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa kuhusu kugawana eneo la maji.
Alisema kwa kufuata makubaliano hayo, haiwezekani watu wa Mbamba Bay, waombe kunywa maji ya Ziwa Nyasa kutoka Malawi.(TK)
Ijumaa, 14 Februari 2014
ADHA YA WAATHIRIKA MAFURIKO WA MAGOLE-DUMILA NAMNA WALIVYOJIOKOA KWA VITI NA MEZA KWA KUSIMAMA ZAIDI YA MASAA MATATU KUNUSURI KIFO NA MAJI YA MAFURIKO MOROGORO.
Mwalimu Kongera.
Haya ndiyo sehemu ya makochi yaliyogeuka kuwa mwokozi kwa watu zaidi ya 20 kunusuru maisha yao ikiwemo na viti kwa kusimama zaidi ya masaa 3.
Na Mtanda Blog, Morogoro.
TULISIMAMA juu ya makochi zaidi ya watu 25 kwa muda wa masaa manne tukiwa na watoto wadogo wa miaka mitano hadi saba waliosimama juu ya mabega ya mama zao katika chumba kilichojaa maji ya mafuriko na ilifikia wakati tukawa tumechoka.
Lakini, tunashukuru mungu maji yalipungua taratibu kwa masaa mawili yakitoka urefu wa futi nane na yalipongua kwa urefu wa futi nne kulipata afueni maana tayari tulikuwa tumechoka na ingezidi saa moja mbele yetu, pale ndani hakuna angekuwa mzima.
Ilikuwa siku yenye mateso makubwa na uchungu wa kupotelewa na mali mbalimbali hasa kwa wale wananchi wa kijiji cha Magole ambao walizingirwa na maji ya mafuriko, licha ya kupotelewa na kila kitu, kwanza kila mtu alikuwa na aina yake ya kujiokoa kwani wapo niliowaona wapo juu ya miti ilimradi tu ni namna gani ya kutafuta njia ya kujinusuru na roho yake isipotee katika janga la maji ya mafuriko yaliyoambatana na kila aina ya uchafu.
Mwalimu wa shule ya msingi kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro, Marthin Kongera (42) anaeleza mkasa mzima uliyoikumba familia yake pamoja na yeye mwenyewe na majirani waliokimbilia katika nyumba yake iliyojengwa na matofali ya saruji yenye vyumba viwili na ukumbi mmoja ili kuweza kujihifadhi na mafuriko yaliyoikumba tarafa ya Magole januari 22 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi.
Haya ndiyo sehemu ya makochi yaliyogeuka kuwa mwokozi kwa watu zaidi ya 20 kunusuru maisha yao ikiwemo na viti kwa kusimama zaidi ya masaa 3.
Na Mtanda Blog, Morogoro.
TULISIMAMA juu ya makochi zaidi ya watu 25 kwa muda wa masaa manne tukiwa na watoto wadogo wa miaka mitano hadi saba waliosimama juu ya mabega ya mama zao katika chumba kilichojaa maji ya mafuriko na ilifikia wakati tukawa tumechoka.
Lakini, tunashukuru mungu maji yalipungua taratibu kwa masaa mawili yakitoka urefu wa futi nane na yalipongua kwa urefu wa futi nne kulipata afueni maana tayari tulikuwa tumechoka na ingezidi saa moja mbele yetu, pale ndani hakuna angekuwa mzima.
Ilikuwa siku yenye mateso makubwa na uchungu wa kupotelewa na mali mbalimbali hasa kwa wale wananchi wa kijiji cha Magole ambao walizingirwa na maji ya mafuriko, licha ya kupotelewa na kila kitu, kwanza kila mtu alikuwa na aina yake ya kujiokoa kwani wapo niliowaona wapo juu ya miti ilimradi tu ni namna gani ya kutafuta njia ya kujinusuru na roho yake isipotee katika janga la maji ya mafuriko yaliyoambatana na kila aina ya uchafu.
Mwalimu wa shule ya msingi kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro, Marthin Kongera (42) anaeleza mkasa mzima uliyoikumba familia yake pamoja na yeye mwenyewe na majirani waliokimbilia katika nyumba yake iliyojengwa na matofali ya saruji yenye vyumba viwili na ukumbi mmoja ili kuweza kujihifadhi na mafuriko yaliyoikumba tarafa ya Magole januari 22 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi.
Alhamisi, 13 Februari 2014
IMAMU AMWAGIWA INAYODAIWA TINDI KALI ARUSHA
BABA AMUUA MWANAE KINYAMA KWA KUMBAMIZA BARABARANI
ONESTORY Mgaya (31) mkazi wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Nesta Mgaya mwenye umri wa miezi saba kwa kumbamiza chini kwenye barabara ya lami.
Kamamnda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimenke amesema,tukio hilo limetokea Februari 9 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi eneo la kijiji cha Lilondo wilayani humo.
Amesema, inadaiwa siku ya tukio mtuhumiwa na mkewe Blesila Mponda (30) pamoja na mtoto wao Nesta walifunga safari kutoka Madaba kwenda Lilondo kumsalimia mama wa mtuhumiwa ambapo wakati wakiwa njiani kutoka nyumbani kwa mtuhumiwa wakielekea kituo cha mabasi Blesila aligundua kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao hivyo alilazimika kumwachia mtoto mtuhumiwa ili kwenda kuchukua kadi hiyo.
Amesema, mtuhumiwa akiwa amembeba mwanae kuelekea kituoni ghafla alianza kumbamiza huyo mtoto chini kwenye barabara ya lami akiwa amemshika miguu na kumpigiza kichwa chini ambapo wakati akiendelea kufanya unyama huo watu waliokuwa jirani walifika na kwenda kutoa msaada ambapo mtuhumiwa alikimbilia porini na kumwacha mtoto chini.
Hata hivyo Kamanda Nsimenke ameeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku hiyohiyo ya tukio na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili ili aweze kufunguliwa mashitaka. (TK)
Kamamnda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimenke amesema,tukio hilo limetokea Februari 9 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi eneo la kijiji cha Lilondo wilayani humo.
Amesema, inadaiwa siku ya tukio mtuhumiwa na mkewe Blesila Mponda (30) pamoja na mtoto wao Nesta walifunga safari kutoka Madaba kwenda Lilondo kumsalimia mama wa mtuhumiwa ambapo wakati wakiwa njiani kutoka nyumbani kwa mtuhumiwa wakielekea kituo cha mabasi Blesila aligundua kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao hivyo alilazimika kumwachia mtoto mtuhumiwa ili kwenda kuchukua kadi hiyo.
Amesema, mtuhumiwa akiwa amembeba mwanae kuelekea kituoni ghafla alianza kumbamiza huyo mtoto chini kwenye barabara ya lami akiwa amemshika miguu na kumpigiza kichwa chini ambapo wakati akiendelea kufanya unyama huo watu waliokuwa jirani walifika na kwenda kutoa msaada ambapo mtuhumiwa alikimbilia porini na kumwacha mtoto chini.
Amefafanua zaidi kuwa, inadaiwa wananchi walilazimika kumkimbiza mtoto huyo kwenye kituo cha afya cha Madaba na kutokana na kuumizwa vibaya kichwani alihamishiwa hospitali ya serikali ya Rufaa Songea ambapo alilazwa wodi ya majeruhi kwa matibabu na siku iliyofuata aliaga dunia.
Hata hivyo Kamanda Nsimenke ameeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku hiyohiyo ya tukio na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili ili aweze kufunguliwa mashitaka. (TK)
Jumanne, 11 Februari 2014
MAFURIKO YALETA KIZAZAA UINGEREZA
Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron,amesema kuwa pesa sio hoja wakati huu ambapo watu wanahitaji msaada wa dharura huku baadhi ya sehemu za nchi hiyo zikikumbwa na mafuriko.
Baada ya kuzuru eneo la Kusini mwa England, ambako mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa, bwana Cameron amesema kuwa atafutilia mbali ziara yake ya Mashariki ya kati wiki ijayo ili ahakikishe kuwa hali inashughulikiwa vilivyo.
Alilaumu kile alichotaja, msimu mbaya wa baridi ambao umekuja na mvua kubwa kuwahi kushudiwa katika kipindi cha miaka 250.
Alionya kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi.
Mafuriko haya yamesababisha uharibifu wa zaidi nya nyumba elfu moja huku maelfu wakilazimika kuhama makwao.
Usafiri pia umetatizika.
SUMAYE APOKELEWA NA MABANGO YANAYOMSIFU LOWASSA JIJINI MWANZA
Hapa vijana waliamua kuonyesha waziwazi mahaba yao kwa mh.Lowasa na kutuma salamu kwake kama unavyoona bango hili
IMEANDIKWA NA Shadrack Mgaya
Hapa ni baadhi ya washiriki kwenye kongamano lilofanyika katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza washiriki walikuwa wanafunzi wa vyuo jijini Mwanza
Mh. Sumaye akizungumza katika kongamano hilo
waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma katika kongamano hiliwalikuwepo na walifuatilia kwa makini pia
Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa
Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa
Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa
Viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa wanafuatilia suala hili kwa makini kabisa
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)