Jumapili, 27 Aprili 2014

PAPA FRANCIS AWATANGAZA WATAKATIFU WAPYA WAWILI

Mahujaji wakifuatilia tukio la kuwatangaza watakatifu Papa John Paul II na John XXIII jijini Vatican
Papa Francis akiongoza ibada kabla ya kuwatangaza watakatifu.
Mapaparazi wakiwa kazini wakati wa zoezi hilo.
Papa Benedict XVI akisalimiana na Rais wa Italia, Giorgio Napolitano jijini Vatican.

KIVUKO CHA KILOMBERO CHAFUNGWA

Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh, Fransisi Miti amesitisha huduma ya kivuko kati ya ulanga na kilombero kwa kutumia pantoni ya kivuko MV. KILOMBERO hadi hapo maji yatakapo pungua kutokana na kivuko hicho kuzidiwa na nguvu ya maji.

Amewaomba wananchi wa wilaya zote mbili kuto kusafiri kwa muda kwa safari zisizo za lazima hadi hapo maji yatakapo pungua huku kwa wale wanao lazimika kusafiri sasa kutumia boti ndogo zilizopo na kuacha kutumia mitumbwi ambayo si salama.
hatariii

Wakati huo huo maji hapo juzi jioni yalikata mawasiliano ya barabara kati ya Ulanga na Kilombero kwa kuzoa moja ya kalavati upande wa Ifakara ambapo moja ya gari lilisombwa na maji huku nayo pantoni ilisitisha huduma kwa muda baada ya kusombwa na maji na kupelekwa upande wa bondeni.
Mitumbwi na boti ndogo zilionekana zikivusha watu hapojuzi huku nauli katika boti na mtumbwi wa kawaida kwa mtu mmoja ikipanda kutoka shilingi 200 ya kawaida hadi 1000 kwa mtu mmoja huku pikipiki zikisafirishwa kwa kati ya shilingi 3000 hadi 8000.

Jumatano, 23 Aprili 2014

SASA WATU BINAFSI KUENDESHA RELI YA KATI

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajiwa kupata ushindani baada ya Serikali kuamua kuruhusu wawekezaji wa sekta binafsi kutumia Reli ya Kati.
Uamuzi huo wa Serikali huenda ukaongeza ufanisi kwa shirika hilo ambalo kwa miaka mingi limekuwa likikumbwa na matatizo ya kiuendeshaji.
Baada ya kuanzishwa upya mwaka 2007, TRL ilikumbwa na misukosuko baada ya mwekezaji Rites kutoka India kushindwa kulisimamia kikamilifu na kusababisha hasara ya mabilioni. Kabla ya TRL reli ya kati ilikuwa chini ya Shirika la Reli (TRC) ambalo nalo halikuwa na ufanisi.
Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kuijengea uwezo TRL iliyofanyika Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka alisema kampuni binafsi zitaruhusiwa kuingiza treni zitakazotumia reli hiyo kwa kulipa ushuru kwa Serikali.
Kutokana na mabadiliko hayo, Dk Mwinjaka alisema Serikali imeanza kuiandaa TRL kupambana na ushindani utakaotolewa na kampuni hizo binafsi.
"Katika hii warsha tunawaandaa kujua kwamba utafikia wakati wanahitaji kujitegemea. Kwa misingi hiyo basi, tumepata wataalamu kutoka ndani na nje kuweka mawazo yao pamoja kujua ni namna gani mabadiliko hayo yatafanyika," alisema Dkt Mwinjaka.
Alipoulizwa kuwa uamuzi huo utaanza kutekelezwa lini, Dkt Mwinjaka alisema ni baada ya TRL kujengewa uwezo wa kuwa na mabehewa, injini na watumishi wa kutosha ili kuweka uwanja mzuri wa ushindani.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL, Severin Kaombwe alisema mpango huo huenda ukaanza baada ya mwaka 2015 kutokana na mkakati uliopo kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
"Kwa sasa tumeshaagiza vichwa (injini) 21 na takriban mabehewa 200 ambayo yanatarajiwa kufika mwezi Agosti mwaka huu," alisema Dkt Mwinjaka huku akisisitiza kwamba mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa BRN.
Alisema injini na mabehewa hayo yana uwezo wa kurekebishwa kupita kwenye reli zote; za kawaida (ya kati) na ile ya kisasa inayotarajiwa kujengwa.
"Serikali imeamua kununua aina hiyo ya vifaa ili shughuli za usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kati ziendelee bila kuathiriwa wakati wa kujenga reli hiyo mpya na baada ya kukamilika tutarekebisha ili kupita njia mpya."
Reli mpya ya kisasa inatarajiwa kugharimu takriban Dola za Marekani 6 bilioni (Sh9.6 trilioni) zinazofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
CHANZO MWANANCHI

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMUAGA DC CHANG'A



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang'a, nyumbani kwa marehemu Mbagala Kibonde Maji jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mkewe Tunu.Picha:Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaongoza baadhi ya viongozi na wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a.

Chang'a alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Shughuli za kuuga mwili wa marehemu Chang’a, zilifanyika nyumbani kwake Kibonde Maji Mbagala Wilaya ya Temeke jana na kusafirishwa kwenda Kihesa mkoani Iringa kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika leo.

Akizungumza kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili huo, Pinda alielezea alivyomfahamu Chang’a kwa muda mrefu kwa sababu sehemu kubwa ya utumishi wake amefanya akiwa serikalini.
 
“Ninyi mlimfahamu Chang’a kivingine, lakini mimi nilimfahamu kwa namna ya tofauti kutokana na jinsi alivyokuwa msaada mkubwa kwa serikali kila tulipokuwa tukipata shida ama migogoro ya kiuongozi,” alisema Pinda na kuongeza:

“Kama Tamisemi (Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), tumemtumia sana kusawazisha mambo kwa sababu Mungu alimjalia kipaji cha pekee ambacho ni ucheshi... hata jambo lingekuwa gumu vipi, huyu bwana alijua kufikisha ujumbe bila kumuudhi mhusika kutokana na maneno yake.”

Pinda alifikisha salamu za rambirambi kwa wafiwa kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye alisema yuko safarini kikazi.

Vile vile, aliwataka wanafamilia ambao wamebaki bila mama wala baba, wawe na umoja na mshikamano na kuahidi serikali itawasaidia watoto wake wakamilishe malengo ya elimu yao kama ambavyo baba yao alikuwa amepanga.

Marehemu Chang'a ameacha watoto watano, wa kike watatu na wa kiume wawili.

Katika maziko ya marehemu Chang'a, serikali itawasilishwa na Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Hawa Ghasia.
CHANZO: NIPASHE

GABI ACHUKIZWA NA CHELSEA `KUPAKI BASI`, TERRY, CECH WAUMIA!!

389319_heroa
BAADA ya suluhu pacha ya bila kufungana ( 0-0) na Chelsea, nahodha wa Atletioc Madrid, Gabi amekerwa na mbinu ya `kupaki basi` waliyotumia wapinzani wao katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Atletico wanaosifiwa kujilinda katika ligi ya Hispania, La Liga wamekutana na timu ya Chelsea ambayo ina uwezo mkubwa wa `Kupaki basi` kwenye ligi ya England.
Katika nusu fainali hiyo ambayo haitasahaulika kwa Atletico, vinara hao wa La Liga walimiliki mpira kwa asilima 62 na kupiga mashuti 26 golini, wakati Chelsea walipiga mashuti matano tu.
Matokeo ya leo yanaonekana kuwa mazuri kuelekea mechi ya marudiano darajani Stamford, ambapo washambiliaji wawili wa Chelsea Eden Hazard na Samuel Eto`o watarejea uwanjani.
Gabi amekiri kuwa matokeo ya leo yamewaacha katika hatari kubwa.
“Hatujaridhika, lakini mechi bado. Atletico walihitaji kushinda kutoka mwanzo wa mchezo hadi mwisho”.
“ Tulijua Chelsea wasingekubali kufungwa kirahisi na mwisho wa siku tumetoka kapa”. Gabi amewaambia waandishi wa habari.
Atletico hawajafungwa katika michuano ya kimataifa mwaka huu, lakini matokeo ya leo yamewafanya washindwe kupata ushindi kwa mara ya kwanza katika michuano ya ulaya msimu huu wa 2013/2014.
Katika mechi ya jana usiku, Chelsea wamepatwa na majanga baada ya nahodha wake, John Terry na mlinda mlango namba moja, Petr Cech kupata majeraha.
 
Leo nusu fainali ya pili itashuhudiwa katika dimba la Santiago Bernabeu ambapo Real Madrid watawakaribisha mabingwa watetezi, Bayern Munich mechi ambayo ni kama fainali kutokana na timu zote  mbili kuwa ni timu kubwa na zenye wachezaji mahiri (TK).

Jumanne, 22 Aprili 2014

NAHODHA WA FERI ILIYOZAMA KOREA KUSINI AKAMATWA



Nahodha wa kivuko cha Korea Kusini kilichozama na kusababisha watu zaidi ya 300 kutojulikana walipo amekamatwa Jumamosi (19.04.2014) kwa tuhuma za uzembe na kuwatelekeza watu waliokuwa kwenye shida ya kuhitaji msaada. Wapelelezi wamemkamata Lee Joon -Seok na wafanyakazi wenzake wawili mapema leo asubuhi na wote watatu wameshutumiwa kwa kuwatelekeza mamia ya abiria waliokuwa wamenasa ndani ya chombo hicho na kuhangaika wenyewe kujiokowa. Mahakama imesema imeamuru kukamatwa kwao ili kuzuwiya watuhumiwa hao kukimbia au kuharibu ushahidi.
Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 68 yuko chini ya uchunguzi kwa kuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuitelekeza meli hiyo wakati abiria wake wakiwa bado wako hatarini.Lee amefunguliwa mashtaka ya uzembe na kushindwa kuhakikisha usalama wa abiria kinyume na sheria za bahari.Abiria waliambiwa kupitia vipaza sauti kwamba wabakie hapo walipo licha ya kuwa meli hiyo ilikuwa ikizama upande mmoja.
Nahodha atetea uamuzi wake
Watu 32 imethibitishwa kuwa wamekufa katika janga hilo na wengine 270 hawajulikani walipo wengi wao ni watoto wakiwa katikasafari ya shule ya sekondari.

AJALI YA BASI LA LUHUYE YAUA 12 SIMIYU


Watu 11 wamepoteza maisha papo hapo na mwingine mmoja kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.
Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa basi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na
kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na maiti 11.
Amesema kati ya majeruhi hao 25 hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

BREAKING NEWS : KOCHA DAVID MOYES AMTIMULIWA MAN U



Moyes amekuwa na Man U kwa miezi kumi pakee
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26. Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia  magazeti ya udaku kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.Writing on the wall: Moyes has seen United fail to qualify for the Champions League this season
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.

Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter United inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini (TK)

AUAWA KWA KISU NA MWANAMKE ALIYETAKA KUMBAKA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 katika eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 20, mwaka huu saa tisa usiku.
Amesema siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani ,akafariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi (TK).

POLICE IN KENYA WARNS OF RENEWED RADICALIZATION OF YOUTHS IN MOMBASA

Mombasa County Commissioner Nelson Marwa addressing the Press at the County Commander Robert Kitur’s (right) office Monday. Marwa has said the ongoing operation of hunting illegal aliens in the country will go on. 

MOMBASA COUNTY: Security officials have disclosed that three Muslim clerics in Mombasa are radicalising youth and fanning religious fundamentalism.
This comes after an alert over renewed militancy in mosques in Majengo, Bondeni and Mwembe Tayari was issued.
The warning follows the emergence of a Kiswahili language Al Shabaab propaganda video on the Internet, which praises the September 21, 2013 terrorist attack on Westgate Shopping Mall in Nairobi.
It also follows an Easter anti-terror swoop in Mombasa in which 660 suspects including aliens were arrested. Mombasa Police Commander Robert Kitur said 188 suspects have since been set free after vetting while 472 will be charged in court this morning.
Counter-terrorism sources told The Standard that the ten-minute video was, most likely sanctioned by Kenyan fugitive jihadist Ali Ahmed Iman in February to entrench ties with Al Shabaab’s supreme leader in Somalia Ahmed Godane alias Mukhtar Abu al-Zubayr.
The video urges Kenyan Muslims to “leave and emigrate to Somalia” to fight jihad against Kenya, which is described as a land filled with “polytheism and disbelief”.
Although the faces of two armed militants in the video are covered, the man who reads the statement, justifying the Westgate massacre and warning of more violence, speaks in impetuous Kiswahili with a clear coastal Kenya accent and the man seated on the video’s extreme left is believed to be an Iman.
VIDEO RECORDING
And about 10 of the youths in the video, armed with AK47 riffles and a Rocket Propelled Grenade (RPG) against a desert background are believed to be Nairobi and Mombasa natives.
According to analysts who spoke to The Standard, the purpose of the video is to not only recruit more Kiswahili speaking militants from Mombasa and other Kenyan towns but also reconcile Kenya foreign jihadists in Somalia with Godane who has lately killed many foreign jihadists after accusing them of spying.
Iman is the commander of Kenya’s foreign fighters in Somalia, who were recruited through Al Hijra, Kenya’s Al Shabaab affiliate, which was led by recently slain radical islamist Sheikh Sharif Abubakar alias Makaburi

Car Bursts Into Flames, Nearly Feeding a Family to Lions

A mother her young children faced an agonizing choice on a recent visit to a safari park in England, when their car burst into flames in the middle of a lion habitat.
Helen Clements and her two young kids, visiting the Longleat Safari Park in Wiltshire, England, Friday, had to make a split-second decision whether to take the chance that the flames didn't reach them before help arrived, or trust themselves to the mercy of the lions outside.
"You're stuck and you can't control and you can't do anything about it," Clements said.
Other tourists in the safari park couldn't believe what they were seeing.
Bad day for someone! And we were in the lion enclosure

Clements said she tried to get out and her son tried to run off, but the park rangers stopped them.
"They were shouting at us get back in the car, do not get out the car and it's a situation - what do you do?" Clements said.
Fortunately for her and her children, the rangers rushed in and got her out just in the nick of time.
"Literally as he opened the door we just jumped into his vehicle," she said.
"(There's) always a ranger with their eye on the animals and a ranger there to assist the family," Longleat Safari Park marketing director Alex Lloyd said. "That training kicked into action and all worked well, so the first ranger stayed close by the lions whilst the second ranger was able to relatively freely get the family out of the vehicle."
Everyone was scared but they were all safe, Clements said.
"Why couldn't it be in the flamingos or the camels?" she said. "But no, it had to be in the lion enclosure."

Alhamisi, 17 Aprili 2014

KIKAO CHA 25 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAFANYIKA LEO JIJINI ARUSHA

image (2)Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akichangia mjadala wakati wa kupitia mapendekezo ya Wafungwa wanaopendekezwa kuachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi Kikao cha 25 cha Bodi hiyo leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo akifuatilia mjadala huo.image (3)Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia makabrasha yenye mapendekezo ya Wafungwa watakaoachiliwa na mpango wa Parole kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao hicho leo Aprili 17, 2014 katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha.image (4)Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo (katikati) mapema leo kabla ya kufungwa rasmi kwa Kikao kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity, Jijini Arusha (kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.image (5)Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo(katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha 25 cha Bodi hiyo kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Charity iliyopo Jijini Arusha (kulia aliyeketi) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto aliyeketi) ni Mjumbe wa Bodi, Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YASEMA MVUA KUBWA INAKUJA



Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam siku wakichimba udongo chini ya Daraja la Mto Msimbazi lililopo Tabata Matumbi jana kutafuta miili ya ndugu zao waliozolewa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji. Picha na Venance Nestory.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa kunyesha tena kuanzia leo na kesho katika ukanda wa Pwani.

Katika taarifa yake kwa umma jana jioni, TMA imesema maeneo ambayo yataathiriwa na mvua hizo za kuanzia leo ni Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.

Huo ni mwendelezo wa mvua zilizosababisha maafa makubwa ambazo zilianza kunyesha Aprili 10, mwaka huu katika ukanda huo wa pwani. Maeneo yaliyokuwa yameathiriwa zaidi ni Dar es Salaam na Morogoro ambako zaidi ya watu 25 walifariki dunia.

Mbali ya vifo hivyo, mvua hizo zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara hasa madaraja.

Mawasiliano ya barabara kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na mingine nchini yalikatika kwa siku mbili baada ya barabara zake zote zinazouunganisha na maeneo hayo ama kuharibiwa vibaya na mafuriko au kujaa maji na kushindwa kupitika.

Taarifa hiyo ya TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwani zitazidi milimita 50 katika saa 24.

“Wakazi wa maeneo ya hatari, watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki,” ilisema taarifa hiyo.MWANANCHI

WANAFUNZI WALIOZAMA KOREA KUSINI WALIANDIKA SMS

Screen Shot 2014-04-17 at 4.07.50 PM
Meli ya Korea Kusini iliyokuwa imebeba zaidi ya abiria 460 wengi wakiwa ni Wanafunzi, ilizama kusini mwa pwani ya nchi hiyo siku ya Jumatano asubuhi ambapo mpaka sasa wengi hawajapatikana huko Korea Kusini ilikozama na ni siku moja tu baada ya ajali ripoti zimeanza kutoka za msg zilizotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo.

140417120950_ujumbe_wanafunzi_512x288_bbc_nocredit
Msg ya mwanafunzi mmoja kwa mamake wakati meli ikizama.

Mwanafunzi:’huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama: ”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.
Screen Shot 2014-04-17 at 4.07.24 PM
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake, yalinukuliwa na shirika la habari la AFP ni haya hapa chini
Mwanafunzi: “baba usijali, nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”
Baba: Najua msaada uko njiani, lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.”
Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama”
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafunzi mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini’
Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.’ baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano mengine yaliyoendelea.
melii
BBC

CHUNGULIA NAFASI MPYA ZA KAZI KUTOKA SERIKALINI


PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT
Ref. Na EA.7/96/01/G/12 16stApril, 2014
VACANCIES ANNOUNCEMENT


On behalf of the Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology (CAMARTEC), The Small Industries Development Organization (SIDO), The Capital Markets and Securities Authority (CMSA) and The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA), Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 51 vacant posts in the above Public Institutions.

NB: GENERAL CONDITIONS

i. All applicants must be Citizens of Tanzania and not above 45 years old, however, should also observe the age limit for each position where indicated.

ii. Applicants must attach an up-to-date current Curriculum Vitae (CV) having reliable contact, postal address, e-mail and telephone numbers.

iii. Applicants should apply on the strength of the information given in this advertisement.

iv. The title of the position and institution applied for should be written in the subject of the application letter and marked on the envelope; short of which will make the application invalid.

v. Applicants must attach their detailed relevant certified copies of academic certificates:

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma transcripts.

- Form IV and Form VI National Examination Certificates.

- Computer Certificate

- Professional certificates from respective boards

- One recent passport size picture and birth certificate.

vi. FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS ARE STRICTLY NOT ACCEPTED

vii. Testimonials, Partial transcripts and results slips will not be accepted.

viii. Presentation of forged academic certificates and other information in the CV will necessitate to legal action

ix. Applicants for senior positions currently employed in the public service should route their application letters through their respective employers.

x. Applicants for entry levels currently employed in the Public Service should not apply, they have to adhere to Government Circular Na. CAC. 45/257/01/D/140 dated 30th November, 2010.

xi. Applicants who have/were retired from the Public Service for whatever reason should not apply.

xii. Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts.

xiii. Certificates from foreign examination bodies for ordinary or advanced level education should be certified by The National Examination Council of Tanzania (NECTA)

xiv. Certificates from foreign Universities should be verified by The Tanzania Commission for Universities (TCU)

xv. Deadline for application is 30th April, 2014 at 3:30 p.m.

xvi. Applicants with special needs/case (disability) are supposed to indicate

xvii. Women are highly encouraged to apply

xviii. Only short listed candidates will be informed on a date for interview

xix. Application letters should be written in Swahili or English

APPLICATION LETTERS SHOULD BE POSTED TO THE FOLLOWING ADDRESS. HAND DELIVERY IS NOT ACCEPTABLE:

Secretary

Public Service Recruitment Secretariat


P. O. Box 63100

DAR ES SALAAM

OR

Katibu


Sekretarieti ya Ajira katika UtumishiwaUmma

S. L. P 63100,

DAR ES SALAAM.

1.0 CENTRE FOR AGRICULTURAL MECHANIZATION AND RURAL TECHNOLOGY – CAMARTEC.

REAL MADRID BINGWA KOMBE LA MFALME

Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kushoto akishangilia na Alonso kulia
Mfungaji wa bao la ushindi la Real, Gareth Bale kulia akipiga shuti pembeni ya Dani Alves
REAL Madrid imetwaa Kombe la Mfalme baada ya kuichapa Barcelona mabao 2-1 usiku huu Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, Hispania.
Real walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11, mfungaji Angel di Maria akimalizia pasi ya Karim Benzema, lakini Bartra akaisawazishia Barca dakika ya 68 kwa pasi ya Xavi.


Shujaa wa Real  alikuwa na nyota wa Wales, Gareth Bale aliyefunga bao la ushindi dakika ya 85 kwa pasi ya Fabio Coentrao. Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo alikuwa nje leo akiendelea kuugulia maumivu yake na aliungana na wenzake kuwapongeza baada ya mechi kwa ushindi huo.


Baada ya kunyakua taji la kwanza msimu huu, Real sasa inaelekeza nguvu zake katika mataji mengine mawili, La Liga na Ligi ya Mabingwa ambako imefika hatua ya Nusu Fainali na itamenyana na mabingwa watetezi, Bayern Munich.
Kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, Real inachuana na Atletico Madrid walio kileleni na Barca walio nafasi ya tatu.




Campeones: Real Madrid supporters celebrate as their team wins the Copa del Rey at the Mestalla stadium
Mashabiki wa Real Madrid wakisherehekea taji la Copa del Rey Uwanja wa Mestalla
Frustrations: Lionel Messi reacts as Barcelona suffer defeat to rivals Real Madrid in Valencia
Lionel Messi akilalamika baada ya kipigo cha Barcelona kwa wapinzani wao, Real Madrid mjini Valencia
Ronaldo akitazama mechi leo Mestalla
Thumb on: Real Madrid's Argentinian midfielder Angel di Maria celebrates after scoring the opening goal

Angel di Maria akishangilia baada ya kuifungia bao la kuongoza Real

Get in: Bartra celebrates after pulling Barcelona level with Real Madrid in the 68th minute
Bartra akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona
Effort: Real Madrid's Gareth Bale shoots towards goal under a challenge by Javier Mascherano
Gareth Bale akipiga shuti mbele ya Javier Mascherano

Jumatano, 16 Aprili 2014

ANASWA AKIMNYANYASA MTOTO MDOGO



Mama mmoja maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salaam aliyenaswa kwa kosa la kumtumikisha mwanaye wa miaka 13 kazi nzito.


MAMA mmoja maarufu kwa jina la mama Mpare (pichani), mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salaam amenaswa kwa kosa la kumfanyisha mwanaye kazi nzito zisizoendana na umri wake wa miaka 13 (picha ndogo). Majirani wa mama huyo walitoa taarifa kwa waandishi wetu wakidai kuwa, mwanamke huyo humfanyisha kazi nzito mtoto wake huyo kama mfanyakazi wa ndani akiwatunza wadogo zake huku akiuza genge lililopo karibu na nyumbani kwao.

Mtoto Saumu Shaban (13).


Ilidaiwa kuwa pamoja na kazi hizo ngumu, mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Saumu Shaban (13) hukaanga chipsi kuanzia mishale ya jioni mpaka usiku wa saa 5 ambapo hufunga shughuli zake kabla ya siku inayofuata kurudia utaratibu huo.

Baada ya kupata taarifa hizo waandishi wetu walifika na kujionea hali halisi ambapo mtoto Saumu alionekana akiuza genge huku vikaango vya chipsi vikionekana tayari kwa ajili ya kupikia mara baada ya jua kuzama.

WATU WAWILI (PICHANI HAPA CHINI) WANATAFUTWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA DEREVA BODA BODA


Mmoja wa anayetuhumiwa
Mtuhumiwa wa pili
Mamia ya wananchi na Polisi wakiwa katika harakati za kuwatafuta vijana wawili hapo juu aliyechuchumaa na anayecheza mziki kwa tuhuma za kumuua Dereva bodaboda Kiteto.


Mtu yeyote anayewafahamu atoe taarifa kituo cha Polisi kilichopo karibu nae.



(TK)















MAJAMBAZI YAPORA MAMILIONI BARCLAYS DAR



DAR ES SALAAM.

Watu watatu wamepora kiasi kikubwa cha fedha katika Benki ya Barclays, Tawi la Kinondoni, Dar es Salaam katika tukio linaloweza kufananishwa na sinema. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana saa tatu asubuhi, watu hao wakiwa kwenye pikipiki moja walifika katika benki hiyo na kuiegesha nje ya uzio, kisha wawili kati yao wakiwa na silaha waliingia ndani.


Muda mfupi baadaye, walitoka nje wakiwa na mfuko mkubwa wenye fedha na lakini walipokuwa wakitaka kukimbia, mfuko huo ulianguka. Hata hivyo, waliuokota na kutokomea kusikojulikana.


Mmoja wa mashuhuda, Ali Lunde alisema: “Walitoka bila wasiwasi tena hawakupiga risasi wala kumtisha mtu yeyote. Walikuwa na mfuko mkubwa wa ‘kisalfeti’. Walipopanda pikipiki jamaa aliyebeba mfuko aliukumbatia kama amepakata mtoto.”


Lunde alisema wakati watu hao wakiondoka na pikipiki, baadhi ya wafanyakazi wa benki walitoka nje huku wakipiga kelele kuwa wamevamiwa na majambazi.


“Walitoka nje wakipiga kelele, ndipo kila mtu akajua walikuwa ni majambazi, kama watu wangekuwa na silaha wangeweza kuwadhibiti maana wote tuliokuwa hapa tumewaona wanavyoondoka,” alisema.


Dereva teksi anayeegesha gari lake karibu na benki hiyo, Herode Munyi alisema aliwashuhudia majambazi hao wakiingia kwenye benki wakiwa na silaha mkononi, jambo lililomfanya kuwapa taarifa watu wengine huku akitafuta namba za polisi.


“Baadaye nilifanikiwa kuwaona polisi hawa wanaotembea na pikipiki nikawaambia lakini kama vile walipitiliza, hawakwenda moja kwa moja benki,” alisema Munyi.


Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo walionekana kushangazwa na mazingira ya wizi huo, kwani walisema mlinzi wa benki hiyo hakuwa na bunduki wala kirungu chochote wakati majambazi walipovamia.


Mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema wakati majambazi wanavamia benki hiyo, hakukuwa na watu wengi waliokuwamo ndani, jambo lililowapa urahisi wa kutekeleza dhamira yao.


Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alisema tawi hilo la benki halina polisi wanaolinda baada ya benki hiyo kuwaondoa hofu kwa madai kuwa halina biashara kubwa.


“Mwaka 2012/2013 waliondoa polisi katika benki ambazo hazina biashara kubwa ikiwamo hii, lakini kuna haja ya kurudisha ulinzi wa askari polisi,” alisema Wambura. MWANANCHI

THREE SHOT WHEN BANDITS ATTACK MATATU

Maralal, Kenya: Three people have been seriously wounded after bandits attacked a matatu at Muguri in Maralal. Among the injured is an Administration Police Officer who was shot in the left leg and a student.

The officer was headed to Wamba Hospital for orthopedic review for his right leg. The three are undergoing treatment at Wamba mission hospital.

James Maina, the matatu driver, told The Standard that bandit attacks are on the rise in the area.

"We will stop plying this route if the government will not intervene”, Maina threatened.

Other passengers were rescued by Kenya wildlife service officers who were traveling from Wamba towards Maralal.

Samburu County Senior Game Warden Dominic Wambua said that his officer are pursuing the suspects who are believed have escaped towards Lodungokwe in Samburu East.

Waisilamu hawatapelelezwa tena New York

Kamishna wa polisi New York William Bratton alikutana na wakereketwa wa mpango huo

Marekani imefunga kitengo chake maalum cha ujasusi ambacho huwapepeleza waisilamu ili kuchunguza kama kuna tisho lolote la ugaidi.

Kitengo hicho kilikuwa kinatumia polisi waliokuwa wanavalia nguo za kiraia kusikiliza kisiri mawasiliano ya simu kati ya waisilamu na hata kuzuru maeneo yanayotembelewa sana na waisilamu.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa kitengo hicho kiliwahi kushitakiwa mara mbili kwa mbinu zao za ujasusi na pia kulaaniwa na makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu.

Pia kiliwaghadhabisha waisilamu hasa kwa kuwachunguza.

"mageuzi haya ni hatua muhimu sana katika kuondoa hali ya wasiwasi na kutoaminiana kati ya polisi na jamii ili jamii iweze kusaidia polisi kuwashika wahalifu,'' ilisema taarifa kutoka katika ofisi ya meya wa New York Bill de Blasio.

Hatua ya kusitisha mpango huo, ilifikiwa na kamishna mpya wa polisi wa kituo hicho, na inaonekana kama njia moja ya kubadili mbinu za kukusanya ujasusi ambazo wengi wanasema zilichangia mashambulizi ya Septemba 11

Kitengo hicho, kilichoanzishwa mwaka 2003, na baadaye kuitwa, ' Zone Assessment Unit ' kilipeleleza waisilamu hasa maeneo walikofanya kazi, kuswali, kununua mahitaji madukani na hata migahawa walikokuwa wanakula.

Wakuu wa kitengo hicho wanasema kuwa kazi yao iliathiri sana uhusiano kati ya jamii na polisi