Ijumaa, 29 Agosti 2014

MIMBA NI YA MR MBASHA SIO GWAJIMA - FLORA MBASHA


Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambae pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima,Flora amesema hayo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live .Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila MchungajiGwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora.


wakati akijibu ya maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumeo kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti,Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.






"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo wa


baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili"


SIJAACHANA NA MBASHA KISA GWAJIMA





Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote hajaachana na Mbasha sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu zaidi.bali amekuwa na matatizo katika ndoa yake kati yake na mumewe na ni matatizo yao ya ndani ambayo asingependa kuyaweka wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia heshima mumewe,maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe asingependa kuwa wazi sababu wanamtoto mkubwa sasa.


"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"


Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambae ni Emmanuel Mbasha maana ameishi nae katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe na kwenda kwenye michepuko hivyo huo ujauzito ni wa Mume wake Emmanuel Mbasha na siyo Gwajima.

CHANZO: EATV



Links

RONALDO MCHEZAJI BORA ULAYA

RONALDO_0109c.jpg
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Uefa, na kuwapiku kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer na Arjen Robben.

Ronaldo, 29, kutoka Ureno alipachika mabao 17 na kuisaidia Real Madrid kunyakua Kombe la Klabu Bingwa Ulaya - Uefa Champions League- msimu uliopita.
"Nimefurahi sana, kwa hiyo lazima niwashukuru wachezaji wenzangu kwa sababu bila timu, tuzo binafsi ni vigumu kuzipata." Amesema Ronaldo.

Ronaldo aliwazidi Neuer na Robben katika kura zilizopigwa na jopo la waandishi wa habari 54.
Neuer, 28, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia, huku Robben, 30, akifunga magoli 21 ya Bayern na matatu kwa timu ya taifa ya Uholanzi iliyofika nusu fainali Brazil.
Ronaldo alifunga mabao matatu - hat-trick - wakati Ureno ilipoichapa Sweden katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, ingawa hakuweza kuwika Brazil, kwani Ureno ilitolewa katika ngazi ya makundi.
Hata hivyo, kiwango chake katika ngazi ya klabu kiliweza kushawishi jopo lililopiga kura, ambalo lilitakiwa kuchagua mshindi kati ya watatu hao baada ya mchujo kutoka wachezaji 10

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA AFRIKA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Peter Pinda amefungua mkutano wa Mawaziri wa Afrika wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika jijini Dar-es-salaam leo.(Martha Magessa)
Mkutano huo ambao ufunguzi wake uliongozwa na agenda kuu iliyozungumzia mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabianchi, na ambavyo nchi za Afrika zitakavyoweza kunufaika na rasilimali zinazotolewa na nchi zinazoendelea ili kukabiliana na janga hilo.
Aidha Waziri mkuu Pinda alielezea kuwa mkutano huo pia una umuhimu kwa nchi za bara la Afrika pia utahusisha namna ambavyo serikali za Afrika zinaweza kukabiliana athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabiachi. Pia alisema kuwa mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika mjini Newyork Marekani unaotegemewa kufunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Baink Moon.

"Wote tunafahamu kwamba mabadiliko ya Tabianchi yanaathari kubwa kwa dunia nzima ila madhara yake yanatofautiana kutokana na mabara, vizazi, umri, nafasi, matabaka pamoja na kipato" Aliongeza kuwa kutokana na uchumi tegemezi wa nchi nyingi za Afrika nchi hizo zimekuwa zikiathirika zaidi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kiwango kidogo cha kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi na kuwa na uchumi mbovu.
Aliendelea kusema kuwa Afrika na Jamii za kimataifa zinatakiwa kuwa na utashi wa kisiasa katika kuungana kwa pamoja ili kuweza kushirikiana katika kupunguza uzalishaji wa gesi joto pia katika kuhimili na kukabiliana na athari hizo.
Mkutano huo wa Mabadiliko ya tabianchi uliofanyika leo jijini Dar-es-salaam umehusisha baadhi ya Mawaziri wa Mazingira na Mawaziri wa Mambo ya nje ambao ni wajumbe wa kamati ya nchi za Afrika ya Mabadikliko ya Tabianchi.

UGUNDUZI WA GESI ASILIA YENYE UJAZO WA TRILLIONI 50.5 NCHINI TZ


Na Anitha Jonas – Maelezo
Tanzania imegundua gesi asilia katika maeneo 19 ya mwambao na kina kirefu cha maji baharini ambayo ina ujazo wa trilioni 50.5.
Kati ya maeneo hayo 19 yaligundulika gesi hiyo ,matano yanapatikana katika mwambao na 14 yapo katika kina kirefu cha maji baharini .(Martha Magessa)
Hata hivyo gesi iliyogundulika katika maeneo ya mwambao kama Songo songo na Mnazi Bay kwa sasa inatumika kufua umeme na pia kwa ajili ya matumizi ya viwandani,majumbani na kwenye magari.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakati akifungua kongamano la wadau wa mafuta na gesi linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wadau hao watumie muda wao kutoa maoni yatakayosaidia kuwa Sera ya Mafuta na Gesi asilia itakayowanufaisha watanzania pindi itakapoanza kutumika.
Kandoro ameongeza kuwa ni vema Sera hiyo ikasaidia Serikali kupata mapato yake yatakayotokana na Mafuta na Gesi asilia kwa ajili ya kuleata maendeleo mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wake.
"Uandaaji wa sera hii ulipitia marejeo ya nyaraka mbalimbali ikiwemo sera ya petroli za nchi zilizogundua nishati ya mafuta na gesi asilia zikiwemo Uganda,Ghana,Sierra Leone na Pakistani".
Mpaka Oktoba mwaka jana (2013) Serikali ilikuwa imekamilisha sera ya gesi asilia ,hii ni kwa ajili ya kutoa muongozo wa kusimamia na kuendesha biashara ya gesi asilia katika uchakataji,usafirishaji na usambazaji", alisema Kandoro.
Amesema kuwa Sera hiyo itazingatia na kuangalia kwa ukaribu suala la udhibiti wa mazingira ukomo wa uzalishaji wa rasilimali hiyo pale utakapoanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Jiolojia kutoka Wizara ya Nishati na Madini Adam Zuberi amesema lengo la sera hiyo ni kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha watanzania wote kwa mapato yatakayopatikana katika maeneo husika kwani asilimia 3 itabaki Halmashauri kwa matumizi ya wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba ameishauri Serikali kuwa makini katika makubaliano na makampuni yatakayochimba gesi katika mgawanyo wa mapato kama inavyoonyesha katika sera kuwa asilimia 60 ya mapato itapelekwa Serikalini. Pia umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika kwenye makubaliano hayo.
Mkutano huo wa wa siku moja uliandaliwa na wizara ya Nishati na Madini na kujumuisha wataalam mbalimbali waliobobea katika masuala ya mafuta ,wawakilishi wa ofisi za ubalozi zilizopo nchini ,Vyama vya siasa , viongozi wa dini, Wakuu wa Mikoa na asasi za kiraia .

AJALI YAUA 10 MBEYA

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita
 
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso iliyokuwa ikiingia barabarani.
Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga
Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo

NI ADHABU NDOGO LAKINI... MHE FILIKUNJOMBE

deo_1ff9d.png

Na Mathias Canal, Kwanza jamii-Iringa
Taarifa kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dsm, imemuhukumu kwenda jela miaka mitatu (03) aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS Charles Ekerege, ni taarifa njema kwa Watanzania wote tunaojali maisha na afya zetu.
Pamoja na kwamba hukumu iliyotolewa ni hukumu ndogo mno ukilinganisha na kosa lenyewe.
Hukumu hii ni ushindi mkubwa kwa iliyokuwa Kamati Bunge ya Hesabu za Mashirikia ya Umma (POAC).
Hukumu hii ni ushindi kwa Bunge. Ni ushindi kwa watanzania wote.
Kwasababu pamoja na kwamba Ekelege ameshitakiwa kwa kuipotezea mapato serikali - ukweli ni kwamba sisi (POAC) tulipo kwenda kuikagua TBS tulikuta hakuna ukaguzi wowote uliokuwa ilifanyika kwa bidhaa zilikuzokuwa zinakuja Tanzania.
Ilikuwa ni 'audit query' iliyoletwa kwetu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Tukaunda Kamati ndogo ya uchunguzi.
Tukiwa kazini, Bwn. Ekelege alifanikiwa kuidanganya Kamati ya Bunge kwamba TBS wana ofisi Hong Kong.
Akatupeleka wabunge wa Kamati ya Bunge kwenye ofisi "feki" ya TBS. Tukambaini hadaa zake.
Lakini pia, tukiwa Hong Kong tulikuta sticker za ukaguzi na ubora za TBS zinauzwa mitaani 'Chun King Mansion' kwa yoyote anayezitaka - hali iliyotuthibitishia zaidi kuwa hakuna chochote cha maana kilichokuwa kinafanywa na TBS, kule Hong Kong.
Pamoja na kudai kwamba TBS wana ofisi nyingine ya ukaguzi, kule Singapore, tulipoambatana naye kwenda Singapore kwa uchunguzi, Bwn. Ekelege alishindwa kutuonyesha hata hizo ofisi zake za TBS zilipo.
Pamoja na kwamba Mhe. Kangi Lugola ni Mlokole, bado Mhe. Kangi alipandwa na hasira; akitaka kumpiga ngumi Bwn. Ekelege, kwa udanganyifu mkubwa wa Bwn. Ekelege.
Kangi alikuwa ni mmoja ya wabunge niliopewa na Spika kwenda kumchunguza Ekelege.
Tukiwa kule, tulibaini kwamba Ekelege (TBS) alikuwa anaruhusu bidhaa za nje kuingia Tanzania bila ya kukaguliwa, bila kujali ubora wake.
Tulikuta matairi feki yanaruhusiwa kuingia nchini. Tulikuta mafuta feki yanaruhusiwa kuingia nchini. Tulibaini kuwa blue band zinaingia Tz bila kukaguliwa ubora wake. Etc.
Ni kweli huyu bwana alikuwa anatumia madaraka yake vibaya; Tulimkuta na mlolongo wa tuhuma ambazo POAC tuliziwasilisha bungeni pamoja na mapendekezo stahiki.
Ni kwa mara ya kwanza, mwaka ule wa 2011/2012 swala la Ekelege na TBS likatuunganisha wabunge wote; Tuliweka itikadi zetu pembeni...
Deo Filikunjombe,
Makamu Mkiti - PAC.

BOKO HARAM WANATISHA KAMA NJAA


Wanajeshi hao walikuwa wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram

Wanajeshi 480 wa Nigeria wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa wamewekwa katika shule .


Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.


Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.

Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.

Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''


Kiongozi wa Boko Haram Shekao ametangaza himaya ya Kiislamu Kaskazini mashariki mwa Nigeria

Maelfu ya watu wameuawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.

Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.

Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.BBC

JK ASIMIKWA KUWA CHIFU CHIDUKILA


CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo

CHIFU wa Waluguru Kingalu
Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha “muibukaji”, kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.

CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

BASI LA HOOD LAGONGWA NA LORI


Raia wakishuhudia ajali ya basi la Hood ilivyotokea.

Basi la Hood lililokuwa likitoka Arusha kwenda Iringa llimepata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha. Basi hilo lilitaka kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, ndipo katika kukwepana ikatokea ajali hiyo. Abiria wa basi wamenusurika , ila lori lilidumbukia darajani na hakukuwa na mtu aliyepoteza maisha.
Basi la Hood lililopata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha.

POLISI AGONGA MTOTO HUKO MORO NA KUKIMBIA AKIACHA GARI


Mtoto Zahara Almeda aliyegongwa na polisi huyo.

MOROGORO. Polisi mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara ya Mji Mpya.

Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi alilishuhudia, mara tu baada ya kumgonga mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua magimbi na mihogo, askari huyo aliteremka na kukimbia akiliacha nyuma gari lake lililokuwa bado halijazimwa, ambalo ndani yake kulikuwa na kofia yake.
Polisi wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio.
Wananchi waliojawa na hasira baada ya tukio hilo walilizingira gari hilo na kutaka kulichoma moto, lakini busara za baadhi yao ziliwezesha kitendo hicho kutofanyika na baadaye trafiki alifika kudili na tatizo hilo.
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo iliyolihusu gari aina ya Toyota Baloon lenye namba za usajili T 553 AUE, alisema mtoto aliyegongwa alikuwa akitokea sokoni Mji Mpya, akiwa amebeba kikapu kichwani.

Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi Kiwamba, alisema binti huyo alikuwa ameshavuka barabara, lakini wakati akijiandaa kuvuka msingi wa pembeni gari hilo lilimfuata katika jitihada za kumkwepa mwendesha pikipiki.
Watu wakishuhudia tukio hilo.
Hata hivyo, siku moja baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea vizuri na mtu aliyemgonga alikwenda hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa amefariki.

Alhamisi, 28 Agosti 2014

ARSENAL YAFUZU UEFA 2014


Mchezaji wa Arsenal(kushoto) akipambana na mchezaji wa Basiktas(kulia). Arsenal ilishinda 1-0
Asernal imefuzu kucheza fainali za kombe la UEFA kwa msimu wa 17 mfululizo baada ya kuichabanga Besiktas ya Uturuki kwa jumla ya goli 1-0.
Katika mchezo wa awali wiki moja iliyopita, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana.
 
Hata hivyo, mchezaji mpya aliyejiunga na Arsenal msimu huu, Alexis Sanchez ndiye aliyeiwezesha Asernal kusonga mbele baada ya kufunga goli la kwanza tangu ajiunge na Arsenal akitokea Barcelona mwezi mmoja uliopita.
Sanchez aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni milioni 35 kutoka Barcelona kwa kipindi chote cha mchezo alihaha kutafuta goli, ambapo katika dakika moja ya nyongeza katika kipindi cha kwanza cha mchezo aliweza kutumbukiza kimiani goli pekee kwa Arsenal na kufuzu kutoka hatua ya makundi kucheza fainali za UEFA kwa mwaka huu.
Arsenal ilipata nafasi za kumaliza mchezo mapema, lakini wachezaji wake Santi Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain walipoteza nafasi nyingi za wazi walizopata.
Zikiwa zimebaki dakika 15 kumaliza mchezo kipindi cha pili, Arsenal ilipata pigo baada ya mlinzi wake wa kulia Mathieu Debuchy alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano. Lakini Arsenal waliendelea kupambana hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Timu nyingine zilizofuzu kucheza fainali za UEFA kwa mwaka huu katika michezo ya Jumatano usiku ni Athletic Bilbao iliyopata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Napoli. (Jumla 4-2), Bayer 04 Leverkusen 4, FC Copenhagen 0, jumla(7-2).
Ludogorets Razgrad 1 - 0 Steaua Bucharest
Malmö FF 3 - 0 FC Red Bull Salzburg

MTOTO WA MIAKA ( AMUUA MWALIMU WAKE

Hii ni sehemu ya picha ya mafunzo hayo kabla ya tukio.
 
Pale ambapo kwanza unaweza kushtushwa na umri mdogo wa mtoto mwenyewe aliyekuwa anafundishwa kufyetua risasi kwenye bunduki, hii imetokea Arizona nchini Marekani ambapo mtoto wa miaka 9 ndio kichwa cha habari kwenye mafunzo ya kutumia submachine gun (SMG) iliyotengenezwa Israel.
 
Mtoto huyu wa kike anayetokea New York alikuwa kwenye mapumziko na matembezi kama mtalii kwenye mji wa Arizona ambako pia ndio alichukuwa time yake ya ziada kujifunza kutumia bunduki lakini kwa bahati mbaya risasi ikafyetuka na kumjeruhi mwalimu wake aitwae Charles Vacca mwenye umri wa miaka 39 ambaye alifariki baadaye hospitalini.
Wakati tukio linatokea mtoto huyu alikuwa na wazazi wake ambapo tovuti ya bullets and burgers imesema watoto kati ya miaka 8 na 17 wanaweza kufyetua risasi kama iwapo tu watakuwa chini ya uangalizi wa Mzazi au Mwalimu.

Hii sio mara ya kwanza kwa tukio kama hili, ilishawahi kutokea mwaka 2008 ambapo mtoto wa miaka 8 alijiua kwa bahati mbaya kwa risasi kwenye onyesho la bunduki hukohuko Marekani.

SIKUSHANGAZWA NA KIPIGO CHA MBWA: ASEMA VAN GAAL KOCHA WA MAN U


Sikushangaa kulazwa4-0 na MK Dons
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amewaudhi wapenzi wa klabu hiyo baada ya kusema kuwa hakushangazwa na kichapo cha mabao 4-0 mikononi mwa klabu ya daraja la kwanza MK Dons katika mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la Capital One .
Man U ilibwagwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa katika mechi tatu za kwanza akiwa mkufunzi.
''mimi sishangazwi na matokeo hayo kwa sababu najua kilichofanyika .
''Timu haijengwi kwa mwezi mmoja''
" Milton Keynes walicheza vizuri sana na pia walikuwa na bahati nzuri walipofika mbele ya lango"
Katika mechi hiyo Jonny Evans alifanya makosa na kumruhusu Will Grigg kufungua mvua hiyo ya mabao .
Grigg alifanya mabao kuwa mawili kwa nunge kunako dakika ya 60 ya kipindi cha pili kabla ya mchezaji wa Arsenal aliyeko huko kwa mkopo Benik Afobe kufumania nyavu mara mbili na kuzamisha matumaini yeyote ya Man U kukomboa mechi hiyo.
Van Gaal alisema kuwa alikuwa anataka kujua uwezo wa kikosi chake cha pili haswa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita.
Nilikuwa nawajaribu wachezaji wetu wa timu ya pili
''Najua tulifanya makosa mengi mno lakini tena unajua ilikuwa ni jaribio''
"nilibadilisha mfumo na nikawataka wachezaji mmoja mmoja ili niweze kusaili uwezo wao lakini unaona kilichotokea .''
''Tulicheza vyema na kupata nafasi nyingi tu lakini haikuwa siku yetu''
Van Gaal alitua Old Trafford baada ya United kumaliza katika nafasi ya 7 katika ligi kuu ya Uingereza na amewanunua wachezaji wengi tu kwa gharama ya pauni milioni 131.7 akiwemo
mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Uingereza Angel Di Maria aliyegharimu pauni milioni 59.7 alipotokea Real Madrid .
Kichapo hicho kwa kikosi kilichogharimu chini ya nusu milioni kukiweka pamoja ni ishara ya jinsi hali imezidi kudorora tangu aondoke kocha Alex Fergusson

NJIA 5 ZA KUEPUKA EBOLA


Njia za kuepuka kuambukizwa Ebola
Ebola:Njia tano za kujiepusha virusi hatari vya homa ya Ebola

Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
1. Sabuni na maji
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.

Osha mikono kwa sabuni na Maji
Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida.
Kusalimiana kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan International aliarifu BBC, kwani Ebola husambazwa haraka watu wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua.
Dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika.
Tumia njia zingine za kujuliana hali

UGUNDUZI: RANGI ZA KUCHA KUTUMIKA KUZUIA UBAKAJI



Wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha North Carolina nchini Marekani, wanatengeza rangi mpya ya kucha ambayo inaweza hubadili rangi katika sehemu yoyote iliyo na madawa ya kulevya yanayotumiwa na wanaume kama mtego kwa wasichana na wanawake kwa ujumla.
Vijana hao wanasema kuwa wanawake hujipata hatarini wanapopelekwa nje au kwenye 'Date' na wanaume wenye nia mbaya nao.
 
Wanasema rangi hii mpya ya kucha itaweza kuonyesha ikiwa kinywaji kimewekwa dawa za kulewesha kama vile GHB na Rohypnol.
Lengo la kampuni hio inayomilikiwa na wanafunzi hao ni kubuni teknolojia ambazo zinawapa wanawake uwezo wa kujikinga dhidi ya ubakaji au dhuluma za kingono.
Ukarasa wao wa Facebook unasema rangi hio ya makucha inaweza kumlinda msichana au mwanamke yeyote kwani anaweza kuingiza kidole chake katika kinywaji alichonunuliwa na mwanamume na kuona ikiwa amewekewa chochote humo kwani rangi hiyo ya kucha inabadili rangi ikiwa kinywaji kile kina dawa za kulevya.
Rangi hiyo inatengezwa na kampuni ya wanafunzi hao inayoitwa....'Undercover Colours' na tayari imependwa sana na maelfu ya watu ishara ikiwa ukurasa wa Facebook na Twitter wa vijana hao. Lakini hisia mchanganyiko ndizo zimeshuhudiwa zaidi.
Mmoja wa wasichana walioonekana kufurahishwa na ugunduzi huo Adam Clark Estes anayeandikia Gizmodo, alisema kwenye ukurasa wa Facebook wa Undercover colours kwamba, ''kuna vitu vingi vya kuchunguza ikiwa kinywaji cha mtu kimewekwa dawa yoyote ya kulewesha. ''Ila ni vigumu kubeba vifaa hivyo hasa nyakati za usiku unapokuwa umetoka nje ya mwanamume.
Jessica Valenti anayeandikia jarida la Guardian, alisema ''Nafurahi kuwa vijana hawa wanataka kuzuia ubakaji, lakini kwa kuwa ujumbe huu unaelekezwa kwa wanawake kuwa wajizuie na ubakaji, sio sawa.''
Picha hizi za wanamitindo nchini India zilizua hisia kali kwani zilileta tasiwira ya kusifu ubakaji
Jesica anasema kusisitiza kuwa waathiriwa wa ubakaji ndio wanaopaswa kujikinga kutokana na ubakaji , ni kama kuwalaumu waathiriwa ambao wengi ni wanawake.
''Tayari wanawake wanafanya kila juhudi kujikinga kutokana na ubakaj,'' asema Tara Culp-Ressler.
Sasa eti kukumbuka kujipaka rangi ya makucha ili kujizuia na ubakaji kwa kuingiza kidole ndani ya kinywaji, ni jambo linalopaswa kukemewa.''
Pia la kushangaza ni kundi moja linalopinga ubakaji kukemea wenye kutengeza rangi hio ya makucha wakihoji je wanaume watajipaka vipi rangi hiyo, ni vyema kukomesha ubakaji sio tu kuuzuia, bali kuukomesha kabisa.
Kama unavyoona hapa haya ni maoni mseto kuhusu rangi hii ya makucha

BALOZI AMJERUHI MTOTO WAKE


Polisi wa jiji la Washington

Polisi nchini Marekani wameshindwa kumkamata balozi wa Equatorial Guine mjini Washngton, kwa tuhuma za kumpiga binti yake kwa mguu wa kiti cha mbao, balozi huyo hajakamatwa mpaka sasa kutokana na kinga yake ya kibalozi aliyonayo .

Msemaji wa polisi Dustin Sternbeck amesema kwamba walipewa taarifa mapema wiki hii kuwa kuna tukio nyumbani kwa balozi huyo, na walipofika wakamkuta binti huyo mdogo akiwa na jeraha kubwa kichwani mwake ambaye alihitaji tiba na hivyo kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Pamoja na hayo yote Dustin alisema kuwa polisi hawana mamlaka kwa kesi za namna hiyo zinazowahusisha wanadiplomasia lakini wamekwisha iarifu serikali juu ya suala hilo

HASHEEM TABEET AUZWA

NYOTA wa mpira wa kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet ameuzwa na klabu yake ya Oklahoma City Thunder kwenda Philadelphia 76ers.
Uhamisho huo umefanyika juzi Jumanne japo kuna madai kuwa nyota huyo huenda asikae sana katika timu hiyo na kwamba atauzwa hivi karibuni.

Jumatano, 27 Agosti 2014

MJI MMOJA NCHINI BRAZIL UNAOENDESHWA NA KINAMAMA UNATAFUTA WANAUME

Mji wa Noiva do Cordeiro, Brazil unaendeshwa na kinamama watupu na hakuna mwanamume anayeishi humo moja kwa moja.

Huu ni mji wa milimani nje ya mji wa Belo Horizante ambao unaongzwa na kinamama pekee.Mji huu una wakazi wapatao  600 wengi wao wakiwa hawajaolewa na wenye miaka 20 na 25. Watoto wa kiume wakifikia miaka 18 wanaondolewa na wanaume waliooa humo wamepigwa marufuku kukaa humo mpaka wikiendi tu.

Kwa sasa wanawake hao wameomba serikali iwaletee wanaume  lakini wafuate sheria za mji huo.
Mji huo ulianzishwa mwaka 1891 na Maria Senhorinha de Lima, ambaye alitengwa na Kanisa mwa uzinzi baada ya kumuacha mumewe ambaye alikuwa amemuoa kwa nguvu. Baada ya muda wanawake wengine walijiunga naye Mwaka 1940, mchungaji wa kievanjelist, Anisio Pereira, alimchukua msichana mmoja wa wasichana wa mji huo kama mke na akaanzish kanisa na kuweka sheria ngumu. Alipokufa mwaka 1995, waliapa kutorudia tena kosa la kuongozwa na kuvunja kanisa la Pereira's.

Mkazi mmoja wa mji huo Nelma Fernandes, 23, alisema, "wanaume pekee tunaokutana nao sisi ni waume wa watu au ndugu zetu. Wote tunatamani kuwa na waume zetu . Lakini tunaishi hapa na hatuhitaji  kuondoka mji huu ili kutafuta wanaume. Mwanamume anayetaka kuja huku aje lakini akubali kufuata sheri zetu.

Jumatatu, 25 Agosti 2014

MATEKA WAPIGISHWA KWATA NCHINI UKRAINE


Wafungwa wakipitishwa barabara za Donetsk siku ya kuadhimisha uhuru wa Ukrainee

Wapiganaji wa mashariki mwa Ukraine wanaoipendelea Urusi wamewaendesha kwata katika barabara za mji wa Donetsk, wanajeshi kadha wa Ukraine waliowateka.

Donetsk ni ngome ya wapiganaji hao.

Watu waliosimama kando ya barabara waliwazomea "mafashisti" wafungwa hao walioonekana wachafu.

Mambo hayo yamejiri siku ya kuadhimisha uhuru wa Ukraine.

Katika kuadhimisha siku hiyo Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, aliahidi kutumia dola bilioni 3 kulipatia jeshi zana mpya katika miaka mitatu ijayo.

Akitoa hotuba kwenye gwaride katika mji mkuu, Kiev, Rais Poroshenko alisema Ukraine imekuwa ikipigana vita hasa dhidi ya uvamizi wa kigeni, na Ukraine itakabili tishio la kijeshi kila mara katika siku za usoni:

"Kufuatana na mpango wa mwaka 2015-17 dola bilioni 3 zitatumiwa kununua silaha na zana mpya za kijeshi.

Hiyo itawezesha kukarabati, kununua na kulipatia jeshi ndege, helikopta, manuwari na mashua.

Huu ndio mwanzo tu." alisema rais Poroshenko

SERIKALI NA RENAMO WAKUBALIANA HUKO MSUMBIJI



Wapiganaji wa Renamo nchini Msumbiji

Habari kutoka Msumbiji zinasema serikali ya nchi hiyo imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo ili kumaliza uhasama kuelekea uchaguzi wa mwezi Oktoba.

Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya chini kwa chini kati ya wafuasi wa Renamo wenye silaha na majeshi ya serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo walijitoa katika mkataba wa amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, mkataba ambao ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Wiki iliyopita ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza kuwaachilia wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi karibuni.

Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani

EBOLA YATINGA DRC

ebola
Waziri wa Afya wa Democratic Republic of Congo amethibitisha habari ya kwanza kuwepo kwa watu 8 waliopimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola. Mr Felix Kabange Numbi alisema,”The results are positive. The Ebola virus is confirmed in DRC”.

DRC imekuwa ni nchi ya kwanza nje ya Africa Magharibi kuthibitisha uwepo wa wagonjwa wa Ebola. Ugonjwa huu umeshasababisha vifo vya watu 1427 hadi sasa

AGONGWA NA COASTER MOROGORO NA KUFA

Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali.
Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa ndani ya gari.
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mgogo, ambaye ni dereva wa bodaboda amegongwa gari na kufariki papo hapo, jioni hii mkoani Morogoro.Gari iliyomgonga dereva huyo ni aina ya Coaster inayofanya safari ya Kihonda Mjini mkoani humo

KESI YA MAUAJI YA KANUMBA HALI NI TETE

Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea.
Staa wa sinema za Kibongo, Lulu Elizabeth Michael, 'Lulu".
WATU WANATAKA KUJUA KINACHOENDELEA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba watu wengi wana kiu ya kujua kinachoendelea katika kesi hiyo ambapo ilidaiwa kwamba imehamishwa eneo la wazi (open) na kusikilizwa kimyakimya katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, huku usikilizwaji wa kesi hiyo ukiwa tofauti kama ilivyozoeleka.
Kwa mujibu wa shushushu wetu anayependa kufuatilia maisha ya mastaa wa tasnia tofautitofauti Bongo ndani ya mahakama hiyo, chombo hicho cha kusimamia sheria kimeamua kubadili aina ya usikilizaji wa kesi hiyo.
Wakili maarufu Bongo anayemtetea 'Lulu', Peter Kibatala.
YAHAMISHIWA BARAZA LA KESI ZA MAUAJI
Habari zilieleza kwamba, kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa kwenye kikao cha baraza la kusikiliza kesi za mauaji kwenye mahakama hiyo, kwa lugha ya kigeni kinaitwa High Court Murder Session.
“Kama ukienda pale mahakamani ili kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo, huwezi kufanikiwa kupata chochote kwa sababu ipo kwenye baraza la kusikiliza kesi za mauaji yaani High Court Murder Session ambalo huwa linasikiliza kesi kimyakimya tofauti na kesi nyingine zinazosikilizwa kwenye kizimba,” kilisema chanzo chetu hicho.
ETI LULU HAJUI KINACHOENDELEA
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba wakati hayo yakiendelea kortini hapo, aliyekuwa mwandani wa Kanumba aliyekuwa naye chumbani siku ya kifo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hajui chochote kinachoendelea na wala hajaitwa mahakamani.

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
“Tangu imeanza kusikilizwa hakuna siku Lulu ameitwa na sidhani kama anajua kinachoendelea.
“Labda anayejua kinachoendelea ni mama Kanumba (Flora Mtegoa) ambaye hupenda kuulizia kuhusu hatima ya mwanaye,” kilisema chanzo hicho.
WAKILI KIBATALA ANASEMAJE?
Baada ya kujikusanyia data hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta wakili maarufu Bongo anayemtetea Lulu, Peter Kibatala ili kupata ufafanuzi wa aina hiyo ya usikilizwaji wa kesi ya mteja wake ambapo alifichua siri hiyo juu ya kesi ya kifo cha Kanumba.
Wakili Kibatala alikiri kwamba kesi ya kifo cha Kanumba ambayo Lulu ni mshitakiwa wa kwanza akituhumiwa kuua bila kukusudia, imebadilishwa aina ya uitwaji huku akigoma kuingia kiundani kwani bado kesi hiyo ni mbichi na hairuhusiwi kwa wakili kuzungumza nje ya mahakama.

Aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.
“Ni kweli inaitwa hivyo, huyo aliyekueleza hajakosea na tunategemea mwezi huu wa nane kikao cha baraza hilo la usikilizaji kitaendelea lakini nisingependa kuongea sana kwani mimi siyo msemaji wa Lulu bali ni wakili na si maadili ya kazi yangu kuzungumza nje ya mahakama. Hata Lulu haruhusiwi kuzungumza chochote nje ya mahakama,” alisema Kibatala aliyewahi kuwa wakili wa mwigizaji Kajala Masanja na mwanahip-hop, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
TUMGEUKIE LULU
Mwanahabari wetu alipomtafuta Lulu ili kujua kama anajua chochote juu ya kesi hiyo, mkali huyo wa sinema za Kibongo aligoma kuzungumza chochote kama aliyoelekezwa na wakili wake, Kibatala.
TUJIKUMBUSHE
Kanumba aliyewatoa mastaa wengi wa filamu unaowaona kwa sasa, alifariki dunia April 7, 2012 nyumbani kwake, Vatican-Sinza jijini Dar. Kifo cha Kanumba kilidaiwa kwamba kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

Jumapili, 24 Agosti 2014

JK ATUNUKU NISHANI MONDULI

Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Oficer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuocha jeshi Monduli jana.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi Bora katika kozi ya muda mrefu ya jeshi Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe(watatu kushoto) pamoja na wazazi wake muda mfupi baada ya Rais Kuwatunuku kamisheni maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha Monduli Mkoani Arusha jana.
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha jana. (picha na Freddy Maro)

JK ATAKA VIONGOZI KUACHA WOGA MOROGORO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi
mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wataalamu walioshughulikia ufungwaji wa mtambo huowakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Morogoro mjini Mhe Aziz Aboud wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wadau wa mji wa Morogoro wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Jengo la mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014