Mwanamume ambaye
alipata pauni 260,000 baada ya kuegemea mlango wa kampuni ya Charles de
Gaulle kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa na mlango ukafunguka na kukuta kitita cha fedha anaaminiwa kuwa mtu asiye
na makazi.
Polisi wanasema kuwa walimtambua mwanamume huyo kupitia
kwa kamera za CCTv kama mmoja wa watu wanaolala karibu na uwanja wa
ndege.Mlango wa kampuni inayoshughulikia masuala ya fedha ya Loomis terminal 2F, ulikuwa umeachwa bila kufungwa na mwanamume ambaye umri wake unakisiwa kuwa miaka 50 hivi alitoka nje akiwa na mifuko miwili ya pesa.
Kwa sasa anasakwa na polisi.
Mwendo wa saa (16:30 GMT) Ijumaa iliyopita king'ora kililia katika kampuni hiyo inayohusika na masuala ya fedha.
Maafisa waliochunguza video ya cctv waligundua kuwa mwananamume huyo alikuwa akichakurachakura kwenye ndoo za taka nje ya ofisi hizo ili kupata chochote kitu, na kuonekana kushangazwa wakati mlango aliokuwa ameegema ulipofunguka ghafla.
Aliingia ndani na muda mfupi baadaye akaondoka akiwa amebeba mifuko miwili.
Mwanamume huyo aliacha mfuko wake nyuma lakini haukuwa na stakabadhi yoyote ambayo ingesababisha atambuliwe.
Pesa alizochukua zinatajwa kuwa jumla ya pauni 260,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 750. AMELALA MASKINI AKAAMKA TAJIRI usikate tamaa hadi uingie kaburni!!!!.