Alhamisi, 24 Julai 2014

MAAJABU YA MWAKA: KIJANA ANG'OLEWA MENO 232

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.

WAZIRI MKUU AHUDHURIA KIKAO CHA WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NAIROBI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini tamko la Mkutano Maalum wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu mikakati ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana kupitia Uendelezaji Miundombinu na uwekezaji, uliofanyika kwenye hoteli ya Kempinski jijini Nairobi Julai 24, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Batilda Burian na wapili kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

NDEGE NYINGINE YAANGUKA NA KUUA WATU 40

 
Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne.
ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio.
Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua.
Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku viwili vya kutunzia kumbukumbu ya ndege ya malaysia iliyoangua nchini Ukraine tarehe 17 mwezi huu vikiwa vimefika mikononi mwa wataalamu wa masuala ya anga ili kuchunguza ni ni kitu gani kiliisibu ndege hiyo.Chanzo BBC Swahili

Jumatano, 23 Julai 2014

MIILI YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA YAPELEKWA UHOLANZI


Mabaki ya ndege ya Malaysia yakiwa yamezagaa

Kwa mara ya kwanza miili iliyopatikana kutoka kwenye ndege ya Malaysia iliyotunguliwa juma lililopita nchini Ukraine itasafirishwa mpaka nchini Uholanzi kwa ajili ya kutambuliwa.

Uholanzi iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 298 waliokufa kwenye ajali hiyo, 193 kati yao raia wa Uholanzi.

Maafisa wa kiintelijensia wa nchini Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo, vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.

Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.

Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.

WATU WATATU WAFA BAADA YA KULA FUTARI

Tanga. Watu watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kwasunga wilayani Handeni wamekufa baada ya kula futari ya mihogo inayosadikiwa kuwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku eneo la Kwasunga Handeni na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni.
 
Kamanda Massawe aliwataja waliokufa kuwa ni Juma Jumbe (6), Abdi Jumbe (10) na Ramadhani Jumbe (15). Pia alisema kuwa wazazi wa watoto waliwahishwa hospitali ambako walipatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

POLISI WAKAMATA MABOMU 7 NA RISASI


Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni: 
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2. ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
4. JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
6. SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja. Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
………………...…………..

ISAYA MNGULU-CP

MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

JE SABUNI YAWEZA KUREJESHA UBIKIRA???



Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.

Sabuni hiyo inadaiwa kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa kushiriki tendo la ngono na mwanaume.

Baadhi ya wasichana waliohijiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha hali ya ubikira.

Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni hatari.

Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani (BBC)

Jumanne, 22 Julai 2014

ISIS INATESA WAKRISTO - OIC


Wapiganaji wa ISIS

Jumuiya ya kimataifa ya kiislamu amewalalamikia wapiganaji wa kundi ISIS kile kinachodaiwa kuwanyima haki za kibinadamu wakristo waliopo katika mji wa Masul nchini Iraq ambapo baadhi yao wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya kiislam OIC, Iyad Madani, kulazimika kukimbia makazi yao kwa wakristo kwa sababu ya wapiganaji hao ni kinyume na misingi ya dini ya kiislam inayosisitiza uvumilivu na ustahimilivu.

Maelfu ya Wakristo waliukimbia mji wa Mosul baada ya wapiganaji wa ISIS kuwalazimisha kubadili dini na kuwa waislam, kulipa kodi ama kuuawa kama wangekaidi.

Mwishoni mwa wiki ISIS walitangaza kuwa wanashikilia eneo jingine karibu na Mosul (TK).

BASI LA NAJIMUNISA LAPATA AJALI NA KUUA

Hivi punde tumepokea habari mbaya kutoka mkoani Shinyanga, Basi la super Najimnisa limepata ajali mbaya baada ya mipira ya matairi kupasuka,unaambiwa wapo baadhi ya waliokufa na majeruhi ni wengi sana na bado hatua za kuokoa bado zinaendelea muda huu, tutaendelea kuwajuza kupitia kwa mtaoa habari wetu ambaye ni msanii alikuwa anatoka mwanza kuelekea Dodoma ambapo waliwa wanashoot muvi huko:

















 

Jumatatu, 21 Julai 2014

HALI YA KUTISHA!!! MIILI YA WATU ZAIDI YA 100 YAKAMATWA BUNJU USIKU

Miili ya watu zaidi ya mia moja imekamatwa kwenye machimbo ya kokoto Bunju. Tunaomba radhi kwa picha za kutisha.
 
 
Mmoja ya Kiungo cha Mguu