Jumatatu, 28 Julai 2014

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AONGOZA WAKAZI WA MOROGORO KUMZIKA MKE WA MWENYEKITI WA CCM MKOA


Mkuu wa mkoa akimpeleka Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wa staafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro CCM


Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake, Bi, Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi



Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris
Mbunge huyo akiingizwa kwenye chumba kilichowekwa jeneza lenye mwili wa mpendwa mke wake.

Diwani wa Kata ya Mji Mpya Wensislaus Karogerezi ambaye ni kaka wa mbunge huyo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kuondokewa na shemeji yake mpendwa
Mstakihi Meya wa Mji wa Morogoro Amir Juma Nondo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Boma akimbembeleza Diwani mwenzake Wensislaus Kalogeris  ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini
Mtoto wa Marehemu akiangua kilio baada ya mwili wa mpendwa mama wake kuwasili nyumbani kwao




Mbunge wa viti maalumu'CCM' Mhe Magreth Mkanga

Mbunge mstaafu wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Lotto akimpa pole Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh lnnocent Kalogeris Kwenye mazishi ya Mkewa Mbunge huyo.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mhe lnnocent Kalogeris akifarijiana na mama yake mzazi

Na Dustan Shekidele,Morogoro

LIBYA YAOMBA MSAADA WA KUSAIDIA KUZIMA MOTO


Libya yaomba msaada wa kimataifa kuzima moto unaochoma mafuta Tripoli

Serikali ya Libya imeomba msaada wa kimataifa ili kuzima moto mkubwa unaoendelea kuchoma hifadhi ya mafuta mjini Tripoli baada ya makombora ya wapiganaji wa Kiislamu kulipua hifadhi ya takriban lita milioni 6 ya mafuta yaliyosafishwa.

Serikali hiyo changa inayoyumbishwa na mapigano baina ya makundi yanayopinga utawala uliomrithi Kiongozi wa miaka mingi Maummar Gaddaffi aliyeuawa katika mapinduzi ya 2011.

Pipa hilo ni moja ya maghala yanayomilikiwa na kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini Libya - Brega

Msemaji wa kampuni hiyo Mohamed Al- Hariri anasema kuwa ikiwa moto huo utasambaa hadi kwenye mapipa mengine yaliyoko karibu basi itakuwa ni janga.

Serikali ya mpito nchini Libya imetaka kusitishwa mapigano ili kuruhusu wazima moto kuendelea na shughuli zao.

Makundi 2 ya wapiganaji yanazozania udhibiti wa uwanja wa ndege mjini Tripoli

Takriban watu 97 wamekufa kufuatia mapigano baina ya makundi hayo hasimu ya waasi wanaotaka kumiliki uwanja wa kimataifa wa ndege wa Tripoli.

Katika mji wa Benghazi mapigano yamechachamaa na kusababisha vifo vya watu 38 siku ya jumapili.

Mataifa kadhaa yameelezea nia yao ya kutuma msaada wa kuzima moto huo lakini wanazongwa na tahadhari iliyotolewa na mataifa ya Magharibi yaliyopelekea kuondoshwa mara moja kwa Wafanyi kazi wao na raia wao nchini Libya wakiongozwa na Marekani iliyofunga Ubalozi wake.

Mwandishi wa BBC mjini Tripoli Rana Jawad amesema kuwa wakaazi wa Tripoli wametahadharishwa kuhama makwao kabla makao yao hayajaghubikwa na moto unaotarajiwa kusambaa iwapo hautadhibitiwa haraka.

Ufaransa ilifuata mkondo wa Marekani ilipoagiza raia wake wote waondoke nchini humo.

Wapiganaji wa LROR wanapigana na Zintan

Mwito sawia na huo ulitolewa na Ujerumani Uingereza na Uturuki na Umoja wa Mataifa UN.

Wakati huohuo Serikali ya Libya imeziomba makundi yanayopigana kusitisha mapigano ilikuruhusu wazima moto kuingia katika eneo hilo la uwanja wa ndege na kusaidia kuuzima moto huo unaozidi kuwa mkubwa.

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Libya Revolutionaries Operations Room (LROR) wanakabiliana na kundi la Zintan likitaka kuing'oa Zintan kutoka eneo hilo.

Mapigano haya ndiyo mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu kuondoka kwa Kanali Gaddafi.

Huko Benghazi, kundi la wapiganaji wanomuunga mkono generali aliyeaasi Khalifa Haftar linaendelea kukabiliana na majeshi ya Serikali (TK).

GARI LATUMBUKIA KWENYE MTARO JIJINI MBEYA


Wasamaria wema wakijaribu kulinasua gari aina ya Toyota Corolla (namba zake za usajili hazikuweza fahamamika mara moja kutokana na kutokuwepo) 
 
Gari aina ya Corolla limetumbukia kwenye mtaro baada ya dereva wake kuzidiwa maarifa ya kiudereva na kujikuta akiingia mtaroni katika eneo la Mafiat mkabala na kituo cha mafuta cha Oilcom jijini Mbeya asubuhi hii. Dereva wa Gari hilo pamoja na mtu mwingine mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa hospital kwa matibabu. Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa ni mwendo kasi aliokuwa nao Dereva wa gari hilo.
Wasamaria wema hao wakiangalia namna ya kuweza kulichomoa gari hilo.
Hayaaaa..... Moja.... mbili.... tatuuu twendeeeeeeee......

Mara wakafanikiwa kulitoma kwenye mtaro huo.
Picha na Fadhil Atick,Mbeya

MARUFUKU YA KUTUMIA MAGARI NCHINI NIGERIA


Jeshi la Nigeria likiwa katika doria  katika jimbo la Borno nchini Nigeria

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari kwa siku tatu katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa taifa hilo ili kuzuia tishio la wanamgambo wa Boko Haram.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa hatua hiyo itazuia utumiaji wa magari kutekeleza mashambulizi ya kujitolea mhanga wakati wa siku kuu ya Eid ul Fitr.

Wakati huohuo kumekuwa na ripoti ambapo mlipuaji wa kujitolea muhanga amewaua watu kadhaa katika mji wa kazkazini wa KANO.

Kundi la Boko Haram limetishia kulipua bomu la gari

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa Wanajeshi hao waliwashauri waislamu kuhudhuria swala za Eid karibu na viwanja vilivyopo karibu na makaazi yao kwa kuwa kundi hilo lilikuwa linapanga kutekeleza mashambulizi katika viwanja,masoko pamoja na maeneo mengine ya uma wakitumia magari.

Gavana wa Borno Kassim Shetima amesema kuwa anawaonea huruma maelfu ya watu waliolazimika kutumia mda wao mwingi kutembea hadi katika viwanja vya kufanyia salah,lakini akaongezea kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda .

Jeshi la Nigeria limepiga marufuku utumizi wa magari katika jimbo la Borno

Kundi la Boko haram linadaiwa kuiteka miji kadhaa kusini mwa Borno na kuweka bendera zake.

Jeshi la Nigeria hivi majuzi lilikiri kwamba baadhi ya wanajeshi wake walikuwa wanatoroka kutokana na uvamizi wa wanamgambo hao (TK).

BOMU LALIPUA HIFADHI YA MAFUTA LIBYA


Vikosi vya zima moto vya Libya vikipambana kujaribu kuuzima moto.
 

Kombora la roketi limelipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta.


Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.

Serikali ya muda ya Libya imetaka usitishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.

DEREVA WA BODABODA AKWAPUA SIMU ANUSURIKA KIFO

Dereva wa bodaboda anayetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) mara baada ya kunaswa kwa wizi wa simu.

Ule mchezo wa kukwapua vitu na kukimbia umemtokea puani dereva wa pikipiki almaarufu bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu ya bei mbaya ya mrembo aitwaye Zaituni Hamisi. Tukio hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda huyo alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.

Dereva huyo wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye kuingia mtaroni.Raia walioshuhudia mkasa huo wakiitoa bodaboda kutoka mtaroni.
Ndani ya dakika sifuri, yule mkwapuaji alitoka nduki huku akimwacha bodaboda huyo aliyekiona cha moto.Kulia ni mrembo (Zaituni Hamisi) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha bodaboda hao.
Alisema ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo cha kufa mtu na wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba ya watu. Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua mafuta ya petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye alikuwa akijitahidi kutuliza ghasia hizo.
Dereva huyo wa bodaboda akichukuliwa na Polisi mara baada kunusullika kifo kutoka wa raia wenye hasira kali.
Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za kisheria.
Imeandaliwa na Chande Abdallah,

Alhamisi, 24 Julai 2014

BOKO HARAM WAUA 40 NIGERIA

Watu wapata 40, wameuawa katika milipuko mikubwa miwili iliyotokea katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Katika mlipuko wa kwanza wa kujitoa mhanga watu 25 waliuawa, huku wengine 15 wakiuawa katika eneo lililokuwa na msongamano wa watu katika mji wa Kawo.
Shambulio hilo pia lilimlenga kiongozi wa upinzani na kiongozi wa zamani wa kijeshi Jenerali Muhammadu Buhari.
Shambulio la kwanza lilimlenga kiongozi mashuhuri wa kiislam aliyeambatana na wafuasi wake alipokuwa akitoka katika eneo la katikati ya Kaduna alikomaliza kufanya muhadhara kwa ajili ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Maelfu ya watu walihudhuria tukio hilo la mwaka.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, watu 25 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulizi la pili lilimlenga kiongozi wa juu wa upinzani ambaye pia ni rais wa zamani Jenerali Muhammadu Buhari ambako nako wamekufa watu 19. Wote wawili, kiongozi wa kiislam na kiongozi wa upinzani wamenusurika bila kujeruhiwa.
Mwanahabari wa BBC amesema aliona viungo vya binadamu vikiwa vimetapakaa katika eneo kubwa la mlipuko. Kamishina wa polisi wa jimbo la Kaduna Alhaji Umar Usman Shehu amesema mlipuko ulisababishwa na anayehisiwa kujitoa muhanga.
Hakuna kundi lolote lililojitokeza kuhusika na mlipuko huo. Kundi la Boko Haram ambalo bado linawashikilia wanafunzi wasichana 200 kwa takribani siku 100 sasa, limeshafanya matukio ya kulipua mabomu kwa kujitoa muhanga katika miji mingi kaskazini mwa naijeria ukiwamo mji mkuu Abuja.
CHANZO BBC,

MWANAMKE WA SUDAN ALIYEBADILI DINI AKUTANA NA PAPA FRANCIS

Photo: Mwanamke Msudan aliyeepuka kunyongwa kwa kubadili dini amekutana na Papa Francis 

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/07/140724_meriam_sudan.shtmlMwanamke raia wa Sudan aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake waliondoka na ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo Pistelli Baba wa Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia ni muislamu na hawezi kubadili dini.

Aliyebadili dini Sudan akutana na Papa Francis
Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu. Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo, ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha hasira na malalamiko  dunia nzima.
Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo lakini alikamatwa tena na alipoacchiwa tena akakimbilia ubalozi wa Marekani mjini Khartoum (TK).

MAJANGILI WATATU MBARONI SERENGETI

Majangili waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi!
Wimbi la kuongezeka kwa majangili limeendelea licha ya kuwepo kwa ulinzi katika mbuga zetu za wanyama. Hii ni kutokana tukio lingine lililotekea kwenye hifadhi ya Serengeti ya kuwakamata majangili, ikiwa ni siku mbili tangu kuondoka kwa mmiliki wa Singita Grumeti ambaye alikuwepo kwa wiki mbili kama ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka.Askari wake wameendelea kukamata majangili ambapo usiku wa kuamkia leo wamewakamata majangili watatu wakiwa na swala.

MAJANGILI WATATU MBARONI SERENGETI

Majangili waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi!
Wimbi la kuongezeka kwa majangili limeendelea licha ya kuwepo kwa ulinzi katika mbuga zetu za wanyama. Hii ni kutokana tukio lingine lililotekea kwenye hifadhi ya Serengeti ya kuwakamata majangili, ikiwa ni siku mbili tangu kuondoka kwa mmiliki wa Singita Grumeti ambaye alikuwepo kwa wiki mbili kama ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka.Askari wake wameendelea kukamata majangili ambapo usiku wa kuamkia leo wamewakamata majangili watatu wakiwa na swala.
 
Swala aliyeuawa na majangili hao
swala aliyekuwa kauawa akiwa kapakiwa kwenye gari kwa ushahidi

MAAJABU YA MWAKA: KIJANA ANG'OLEWA MENO 232

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.

WAZIRI MKUU AHUDHURIA KIKAO CHA WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NAIROBI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini tamko la Mkutano Maalum wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu mikakati ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana kupitia Uendelezaji Miundombinu na uwekezaji, uliofanyika kwenye hoteli ya Kempinski jijini Nairobi Julai 24, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Batilda Burian na wapili kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

NDEGE NYINGINE YAANGUKA NA KUUA WATU 40

 
Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne.
ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio.
Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua.
Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku viwili vya kutunzia kumbukumbu ya ndege ya malaysia iliyoangua nchini Ukraine tarehe 17 mwezi huu vikiwa vimefika mikononi mwa wataalamu wa masuala ya anga ili kuchunguza ni ni kitu gani kiliisibu ndege hiyo.Chanzo BBC Swahili

Jumatano, 23 Julai 2014

MIILI YA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA YAPELEKWA UHOLANZI


Mabaki ya ndege ya Malaysia yakiwa yamezagaa

Kwa mara ya kwanza miili iliyopatikana kutoka kwenye ndege ya Malaysia iliyotunguliwa juma lililopita nchini Ukraine itasafirishwa mpaka nchini Uholanzi kwa ajili ya kutambuliwa.

Uholanzi iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 298 waliokufa kwenye ajali hiyo, 193 kati yao raia wa Uholanzi.

Maafisa wa kiintelijensia wa nchini Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo, vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.

Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.

Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.

WATU WATATU WAFA BAADA YA KULA FUTARI

Tanga. Watu watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kwasunga wilayani Handeni wamekufa baada ya kula futari ya mihogo inayosadikiwa kuwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku eneo la Kwasunga Handeni na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni.
 
Kamanda Massawe aliwataja waliokufa kuwa ni Juma Jumbe (6), Abdi Jumbe (10) na Ramadhani Jumbe (15). Pia alisema kuwa wazazi wa watoto waliwahishwa hospitali ambako walipatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

POLISI WAKAMATA MABOMU 7 NA RISASI


Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) Isaya Mngulu akishauriana na maafisa wake leo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni: 
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
2. ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
4. JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
6. SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja. Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
………………...…………..

ISAYA MNGULU-CP

MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

JE SABUNI YAWEZA KUREJESHA UBIKIRA???



Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.

Sabuni hiyo inadaiwa kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha wakati wa kushiriki tendo la ngono na mwanaume.

Baadhi ya wasichana waliohijiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia sababu hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha hali ya ubikira.

Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Tanzania anasema kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni hatari.

Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani (BBC)

Jumanne, 22 Julai 2014

ISIS INATESA WAKRISTO - OIC


Wapiganaji wa ISIS

Jumuiya ya kimataifa ya kiislamu amewalalamikia wapiganaji wa kundi ISIS kile kinachodaiwa kuwanyima haki za kibinadamu wakristo waliopo katika mji wa Masul nchini Iraq ambapo baadhi yao wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya kiislam OIC, Iyad Madani, kulazimika kukimbia makazi yao kwa wakristo kwa sababu ya wapiganaji hao ni kinyume na misingi ya dini ya kiislam inayosisitiza uvumilivu na ustahimilivu.

Maelfu ya Wakristo waliukimbia mji wa Mosul baada ya wapiganaji wa ISIS kuwalazimisha kubadili dini na kuwa waislam, kulipa kodi ama kuuawa kama wangekaidi.

Mwishoni mwa wiki ISIS walitangaza kuwa wanashikilia eneo jingine karibu na Mosul (TK).

BASI LA NAJIMUNISA LAPATA AJALI NA KUUA

Hivi punde tumepokea habari mbaya kutoka mkoani Shinyanga, Basi la super Najimnisa limepata ajali mbaya baada ya mipira ya matairi kupasuka,unaambiwa wapo baadhi ya waliokufa na majeruhi ni wengi sana na bado hatua za kuokoa bado zinaendelea muda huu, tutaendelea kuwajuza kupitia kwa mtaoa habari wetu ambaye ni msanii alikuwa anatoka mwanza kuelekea Dodoma ambapo waliwa wanashoot muvi huko: