Alhamisi, 31 Agosti 2017

Lugha inayozungumzwa na watu watatu pekee Afrika

     Katrina Esau anafanya kila awezalo ili lugha yake ya utotoni linasalia duniani hata baada ya kifo chake

Katrina Esau anafanya kila awezalo ili lugha yake ya utotoni linasalia duniani hata baada ya kifo chake
Katrina Esau anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa lugha yake asili, ambayo kwa sasa inazungumzwa na watu watatu pekee, haiangamii.
Bi Esauni, 84, ni mmoja wa watu watatu walio hai ambao wanazungumza kwa ufasaha lugha iitwayo N|uu, mojawapo ya lugha zinazozungumzwa nchini Afrika Kusini ya jamii ya San, ambao pia wanafahamika kama Bushmen.
Lugha ya N|uu inachukuliwa kama lugha asili ya taifa la Afrika Kusini.
Huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye anaweza kuzungumza kwa ufasaha lugha hiyo isipokuwa watu wa familia yake, lugha hiyo imetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama "lugha iliyo katika hatari kubwa ya kuangamia".
"Nilipokuwa mtoto, nilikuwa nikizungumza tu Ki- N|uu na nikawasikia watu wengi mno wakiongea lugha hii.

Ilikuwa ni habari njema, tuliipenda sana lugha yetu, lakini hilo kwa sasa limebadilika," anasema Bi Esau huko Upington, mji ulioko katika jimbo la Northern Cape.
Kwa karne nyingi, watu wa kabila la San, walikuwa wakitembea kwa uhuru mkubwa katika maeneo haya, wakikusanya matunda na mimea, huku wakiwinda wanyama ili kulisha familia zao.
Lakini leo, tabia hiyo ya kitamaduni ya wa- San, imekwisha kabisa, na watu wa ukoo huo wananiambia kuwa, lugha ni jambo miongoni mwa mambo machache yaliyosalia ambayo yanawaunganisha na buyu la historia yao.
Ndani ya nyumba moja ndogo ya mbao, anawafunza watoto wa mtaa huo sauti 112 na Sauti mwaliko 45 za N|uu.
"Nawafunza lugha hii kwa sababu, sitaki ipotee, mara baada ya kufa kwetu," Bi Esau alisema.
"Nataka kuwafunza kabisa hadi waelewe, kwa sababu nafahamu hatuna muda mrefu uliosalia."
Huu ni mwaka wa 10 kwa Bi Esau ambaye amekuwa akiendesha shule hiyo nyumbani kwake.
Watu wa jamii hii, akiwemo Bi Esau, wanazungumza Ki -Afrikaan, ambayo inafanana na liugha inayozungumzwa na walowezi wa Kiholanzi, waliofika Afrika Kusini karne ya 17 wakitokea Uholanzi.

"Tungepigwa vibaya sana iwapo ungepatikana na mzungu ukizungumza lugha hii," amesema.
"Kwa sababu ya historia yetu, watu leo hawataki kabisa kuzungumza lugha hiyo, kwani inazungukwa na machungu makubwa.
"Tuliitupilia mbali lugha ya N|uu na tukaanza kujifunza na kuzungumza lugha ya Afrikaan, hata ingawa sisi sio wazungu- hiyo imetatiza pakubwa utambulisho wetu," ameongeza.
Dadake Bi Esau, Hanna Koper na Griet Seekoei - wote wenye miaka 95- wanasikiza kwa makini sana, huku akizungumza kwa machungu waliyopitia wakiwa watoto wadogo.
Hawazungumzi sana lakini wanaitikia kwa kutikiza vichwa vyao, huku dada yao akiongea.
Leo hii, Ouma Geelmeid, anavyofahamika na wengi, ana matumaini ya kuondoa aibu inayoandama lugha hiyo ya N|uu.
Wakati wa mafunzo, huku akiwa na kijiti mkononi, Bi Esau anagusa majina ya Ki- N|uu katika mchoro ulio na viungo vya mwili wa binadamu, huku wanafunzi wakisoma kwa mpigo.
Sawa tu na lugha nyingi za bara Afrika, ambazo zimekuwa zakipasishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kuzungumza tu- lakini lugha hii sasa imo katika hatari ya kuangamia.
Hadi hivi majuzi, hakukuwa na rekodi yoyote ya maandishi ya lugha hii.
Watoto wa jamii ya Khoisa, wengi wao Afrikaans, Bi Katrina Esau ana matumaini makubwa ya kuwafunza hadi hali itakapobadilika na kuwa kama zamani
Watoto wa jamii ya Khoisan, wengi wao Afrikaans, Bi Katrina Esau ana matumaini makubwa ya kuwafunza hadi hali itakapobadilika na kuwa kama zamani
Bi Esau anafanya kazi na mtaalamu wa lugha, Sheena Shah kutoka Chuo cha Masomo kuhusu Afrika na Mashariki ya Kati (Soas) Jijini London na Matthias Brezinger wa taasisi ya The Centre for African Language Diversity Centre Jijini Cape Town, Afrika Kusini ili kubuni alfabeti ya lugha ya Ki- N|uu na misingi imara ya alfabeti na sheria ya msingi ya sarufi.
"Kutokana na kazi aliyoifanyia jamii ya Ouma Geelmeid, tulielewa kuwa jamii hizi zinaitazama lugha kama kitambulisho chao, na hivyo ni kigezo muhimu mno kwa muingiliano wa binadamu," anasema Bi Shah.
"Utambulisho wa mtu binafsi ni jambo nzuri mno, hasa sasa kote duniani."

Lugha ni zaidi ya suala fulani tu la kuwasiliana na mtu mwingine, pia inafungamanishwa na tamaduni na namna maisha ilivyo katika jamii, wataalamu wananiambia.
"Unapotizama lugha za kiafrika, unaelewa kuwa wanawasilisha hali ya maisha kwa njia tofauti mno, mahusiano, maswala ya kiroho, ardhi, afya na ubinadamu," anasema Bw Brezinger.
"Kuna upana mkubwa mno wa mawazo ujuzi na maarifa juu ya maisha, ambayo imepeanwa kutoka kizazi hata kizazi katika makabila asilia ya Afrika, ambayo mataifa ya magharibi yanafahamu vitu vichache mno na kwa hakika hawajui ni lini lugha hizi zinaangamia: pia ya namna maarifa ya kipekee pia wanapotea," anaendelea kusema.
Ramani ya Afrika Kusini
                                  Ramani ya Afrika Kusini
Ndani ya darasa, kunao watoto kama 20 hivi, wengi wao wakiwa na umri chini ya miaka 10, na chipukizi wachace.
Mary-Ann Prins, mwenye umri wa miaka 16, ni mwanafunzi bora zaidi wa Bi Esau, ambaye ana matumaini kwamba siku moja atafunza darasa hili.
"Napenda kuelewa lugha hii. Inanifanya kujihisi kuwa ndani yake, kwamba nimeshikamanishwa na babu wa mababu zangu. Naambiwa walikuwa wakiizungumza na leo naweza kuwa sehemu ya wanaoizungumza pia," alisema huku akitabasamu.
Hakuna mahali pa kuwa
N|uu sio lugha pekee barani Afrika ambayo imo katika hatari ya kuangamia nchini Afrika Kusini.
Masaa matatu kutoka hapa, katika mji wa Springbok, wazungumzaji wa lugha inayojulikana kama Nama, wamekuwa wakiishinikiza serikali ya Afrika Kusini, wakitaka kabila lao litambuliwe rasmi nchini humo.
Jamii ya Nama, wanataka kabila lao litambuliwe rasmi na serikali ya Afrika Kusini
   Jamii ya Nama, wanataka kabila lao litambuliwe rasmi na serikali ya Afrika Kusini
"Ni jambo la huzuni mno kwamba watoto wetu hawawezi kuzungumza Nama. Inanivunja moyo mno, kwamba watoto wetu hawawezi kuwasiliana na wazee wao kwa lugha yao ya kiasili," anasema Maria Damara, 95, mmojawepo wa wazungumzaji wa lugha ya Nama hapa.
"Je1 Siku zijazo itakuwa vipi, ni nini kitakachofanyika na watoto wetu?"

Lugha kubwa sita zinazozungumzwa nchini Afrika Kusini:
Zulu: Asilimia 22.7, Xhosa: Asilimia 16, Afrikaans: Asilimia13.5, Kiingereza: Asilimia 9.6, Setswana: Asilimia 8 na Sesotho: Asilimia 7.6
Kwa ujumla, Afrika Kusini ina lugha rasmi 11.
Kiingereza ndio lugha inayozungumzwa kwa wingi kama lugha rasmi na lugha ya kibiashara.
Chanzo: SA.info/Census 2011

Chuo chatuma dola milioni moja kwa mwanafunzi kimakosa Afrika Kusini

Chuo Kikuu cha Walter SisuluChuo Kikuu cha Walter Sisulu                

Chuo Kikuu kimoja nchini Afrika Kusini kimesema kwamba kilituma kimakosa jumla ya randi milioni 14 ambazo ni sawa na dola milioni moja za Marekani katika akaunti ya benki ya mwanafunzi mmoja nchini humo.
Pesa hizo zilitoka kwenye mfuko wa shirika la kufadhili wanafunzi kimasomo nchini humo NSFAS.
Chuo Kikuu cha Walter Sisulu, kinasema kuwa pesa hizo ziliwekwa miezi mitano iliyopita, huku makosa hayo yakijulikana baada ya risiti ya akaunti ya mwanafunzi huyo kuonyesha kuwa na mamilioni ya pesa baada ya kuwekwa katika mtandao wa kijamii.
Chuo hicho kikuu sasa kinachunguza ni kwa nini mwanafunzi huyo hakupiga ripoti ya kuwepo kiasi kikubwa hivyo cha pesa kwenye akaunti yake.
Mwanafunzi huyo amekanusha madai hayo.
Ripoti ya shirika la habari la EWN inasema picha zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha mwanafunzi huyo wa kike huyo akijisifu na kujionyesha kwenye sherehe moja huku akijiburudisha na vitu vizuri vizuri, kama vile simu mpya ya rununu.
Inaaminika kwamba mwanafunzi huyo tayari ametumia randi 400,000.
Msemaji wa Chuo hicho Kikuu Yonela Tukwayo, amesema kuwa pesa hizo ziliwekwa kwenye akaunti hiyo kimakosa na kampuni ambayo inasimamia fedha za hazina ya kitaifa za msaada wa karo ya wanafunzi (NSFAS) ambayo inajulikana kama Intellicard na kwamba ni sharti mwanafunzi huyo arejeshe fedha hizo:
''Pia tunaangalia sheria za NSFAS, inayoonyesha mtoto huyo alitia saini makubaliano ya kukubali....Masharti ya matumizi ambayo fedha hizo zinafaa kutumika.
Kwa hivyo itabidi mwanafunzi huyo alipe kila senti ya fedha alizotumia, hata akilipa kwa miaka 20 na zaidi."

Maafisa wa NSFAS imekanusha madai hayo, ikisema kuwa chuo kikuu hicho cha Walter Sisulu ndicho kinachofaa kulaumiwa.
Gazeti moja nchini Afrika Kusini limewauliza wasomaji ni kwa njia gani wangetumia pesa nyingi kama hizo iwapo wangeamka na kuzipata kwenye akaunti.
Shirika la habari la News24 baadaye limemnukuu msemaji wa chuo kikuu hicho Yonela Tukwayo, akisema kuwa kuhamishwa kwa fedha hizo hadi kwenye akaunti isiyokusudiwa, yalikuwa ni makosa ambayo yangekunduliwa na NSFAS, ambayo inasimamia malipo hayo.
NSFAS imekanusha madai hayo kupitia msururu wa ujumbe kwenye Twitter, huku ikisema kuwa siyo yenye kulaumiwa kwa makosa hayo.
NSFAS imesema chuo kikuu ndicho kinachofaa kulaumiwa                   NSFAS imesema chuo kikuu ndicho kinachofaa kulaumiwa                
Bi Tukwayo anasema kuwa, mwanafunzi huyo tayari ametumia, dola 38,000 (£30,000), huku akitakiwa kulipa kila ''senti aliyotumia''.
Ripoti hiyo inasema kuwa mwanafunzi huyo anashikilia wadhifa wa uongozi katika chama cha wanafunzi wa Chuo Kikuu.
Mwenzake katika chama hicho cha wanafunzi wa Chuo Kikuu, ameiambia News24 kuwa, ujumbe katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook unadai kuwa amepokea fedha hizo kwa njia halali.

Ujumbe wa mwanafunzi huyo unasema kuwa pesa hizo tayari zimerejeshwa: "Jibu ni rahisi, NSFAS ilifanya makosa kwa kuweka pesa nyingi katika akaunti isiyokusudiwa na akaunti hiyo ikawa ni yangu. Kwa hivyo sikanushi chochote, pesa kwa hakika ziliwekwa tarehe 1 mwezi Juni na kurejeshwa Agosti 13.

Je wewe ungefanya nini ikiwa ni wewe

Madaktari wagombana wakati wa upasuaji wa mgonjwa India

     Madaktari wanaonekana wakitukanana kwa Kihindi

                            Madaktari walionekana wakitukanana kwa Kihindi
Picha ya madaktari wawili wakikorofishana wakati walipokuwa wakimfanyia mgonjwa upasuaji, imesambaa katika mitandao ya kijamii
Madaktari hao wawili wamesimamishwa kazi kwa muda nchini India, baada ya video kusambaa mitandaoni wakigombana vikali, huku wakiwa wamesimama kandokando ya mama mmoja mja mzito, wakati wa upasuaji.
Taarifa kutoka Hospitali hiyo imethibitisha kuwa wawili hao wamesimamishwa kazi kwa muda.
Video ya kisa hicho kilichotokea katika Hospitali ya Umaid iliyoko kaskazini mwa mji wa Rajasthan, imesambazwa pakubwa na kusababisha malalamishi makubwa.
Afisa mmoja mkuu wa Hospitali hiyo ameiambia BBC kuwa, mwanamke aliyekuwa akifanyiwa upasuaji na mwanawe wako salama.
Chanzo cha video hiyo bado haijabainika, lakini wakuu wamethibitisha kuwa kisa hicho kilifanyika hospitalini humo.
Matusi mtandaoni
Mara baada ya kuonekana kwa mkanda huo wa video mtandaoni, ripoti nyingi ilidai kuwa mwanamke anayeonekana akiwa katika meza ya upasuaji alimzaa mtoto ambaye alifariki baadaye.
Lakini Dkt Ranjana Desai, mkuu wa Hospitali hya Umaid mjini Jodhpur, amekanusha madai hayo na kusema mtoto na mamake wako salama u salmini.
''Wakati nilipoina video hiyo, na kufanya uchunguzi wa ndani kwa ndani, vyombo vya habari tayari vilikuwa vimetangaza kuwa, mtoto huyu alikuwa amefariki," ameiambia BBC.
Kuna mtoto amefariki lakini siye ambaye vyomo vya habari vilitangaza, amesema.
Mita chache kutoka hapo, kwenye meza nyingine ya upasuaji, kwenye chumba hicho hicho hospitalini, mama mwingine alizalishwa mtoto ambaye alikuwa amefariki tayari.
"Visa hivi viwili havina uhusiano hata kidogo," Dkt Desai ameiambia BBC.
Kwenye Video, ambayo imesambazwa pakubwa mitandaoni, madaktari wawili wanasikika wakirushiana matusi mazito mazito kwa lugha ya Kihindi, na kuanza baadaye kugombana ikiwa mgonjwa huyo alikuwa amekula kabla ya upasuaji.
Dkt Desai amewatambua madaktari hao wawili na kutaja majina yao kama Dkt Ashok Nanival na Dkt Mathura Lal Tak.
Amesema kuwa madaktari hao hawajafutwa kazi bali wamesimamishwa tu kazi kwenye Hospitali hiyo, huku mamlaka kuu ya Hospitali hiyo ikiendeleza uchunguzi dhidi ya kisa hicho.
Mahakama kuu ya jimbo la Rajasthan imeamuru Hospitali hiyo kutoa ripoti ya kina, huku mahakama hiyo ikitekeleza uchunguzi wao kuhusiana na kisa hicho.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

REAL MADRID YABANWA MBAVU NA VALENCIA NYUMBANI

Real Madrid’s Marco Asensio.
Klabu bingwa ya Ureno na Ulaya Real Madrid imebanwa mbavu nyumbani ilipotoka sare ya mabao 2-2 jana usiku.

Hili ni dhahiri linatokana na kuwakosa nyota wake Christiano Ronaldo aliye na marufuku ya mechi 5 kufuatia kadi nyekundu na kumsukuma Refa

Pia mchezaji mwingine Sergio Ramos naye alizawadiwa kadi nyekundu.katika mechi iliyopita hivyo kuikosa mechi hiyo.

MAYWEATHER AMDUNDA McGREGOR

 Image result for Pambano la Mayweather na McGregor
Bondia maarufu duniani Floyd Mayweather amemdunda kwa TKO Bondia Conor McGregor katika raundi ya 10 katika mpambano wa raundi 12 usiokuwa wa ubingwa. Pambano hilo lililoitwa pambano la fedha Mayweather atanyinyakulia kitita cha zaidi ya dola milioni 100 wakati McGregor atanyinyakulia kitita cha zaidi ya  dola milioni 30. Pambano lilifanyika katika usiku wa kuamkia tarehe 27/8/2017 huko Marekani.

Bondia McGregor alikuwa na tambo nyingi kuwa angeshinda kwa TKO raunsi za mwanzo kabisa lakini mambo hayakuwa hivyo.

Mayweather alisema kuwa amefurahishwa na kupata mpinzani ambaye alimpa changamoto kubwa.
Image result for Pambano la Mayweather na McGregor
McGregor alianza pambano hilo kwa kuongoza raundi tatu za mwanzo na Mayweather akashinda raundi ya 4 hadi ya 9 na raundi ya 10 refarii alisimamisha pambano baada ya McGregor kuzidiwa vibaya.

Mayweather amejiwekea rekodi ya mapambano 50 bila kuhindwa na ametangaza kustaafu rasmi masumbwi.
Image result for Pambano la Mayweather na McGregor
Wakati huo huo McGregor naye amesema anafikiria kuachana na ndondi ili kurejea kwenye mieleka.

Baada ya kichapo cha Mbwa Wenger awataka mashabiki kudumisha imani

Wenger


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha sana baada ya klabu hiyo kucharazwa na Liverpool 4-0 katika mechi ya Ligi ya Premia Jumapili.
Gunners hawakuwa na kombora hata moja lililolenga goli baada ya uchezaji mbaya ambao ulikosolewa pakubwa na mashabiki na wachanganuzi wa masuala ya soka.
"Iwapo baadhi ya watu wanahisi kwamba mimi ndiye tatizo, basi naomba radhi kwamba mimi ndiye tatizo," Wenger aliambia Sky Sports.
"Lakini tunataka mashabiki wetu waendelee kuwa nasi hata baada ya uchezaji mbaya hivyo na kushindwa."
Aliongeza: "Jambo pekee ambalo tunaweza kufanya ni kurejea na kucheza vyema."
Wenger alitia saini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu uliopita, licha ya baadhi ya mashabiki kumtaka aondoke.
Klabu hiyo ilimaliza nafasi ya tano ligini msimu uliopita na kumaliza nje ya nafasi za kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21 ambayo wamekuwa na Wenger.
Hata hivyo, walifanikiwa kushinda Kombe la FA.
Wenger alimwacha mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingine na klabu hiyo Alexandre Lacazette kwenye benchi wakati wa mechi hiyo Anfield, lakini alimchezesha Alexis Sanchez kwenye kikosi cha kuanza mechi mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu.
Hata hivyo, vijana wake walipanguliwa na mabao kutoka kwa Roberto Firmino, Sadio Mane, Mohamed Salah na Daniel Sturridge.
Alipoulizwa nini kilikuwa kibaya na uchezaji wa vijana wake, Wenger alisema "kila kitu".
  Arsene Wenger
Arsene Wenger ambaye ameongoza Arsenal tangu 1996 alitia saini mkataba wa miaka miwili Mei
"Hatukuwa katika kiwango kifaacho tangu dakika ya kwanza - kimwili, kiufundi na kiakili - na tuliadhibiwa," alisema Mfaransa huyo.
"Uchezaji wetu leo haukubaliki. Ni kweli kwamba leo tulikuwa wapinzani wepesi kwa Liverpool.

"Uchezaji wetu ulikuwa mbaya mno. Sitaki kutekwa na hisia, lakini tuna safari ndefu, na kuna sababu zinazosababisha hilo, na wachezaji sasa wanaelekea kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini lazima tujifunze kutokana na uchezaji wetu leo."
  Alexis Sanchez aliondolewa na nafasi yake akaingia Alexandre Lacazette dakika ya 62
Alexis Sanchez aliondolewa na nafasi yake akaingia Alexandre Lacazette dakika ya 62
Mohamed Salah amefungia Liverpool mabao mengi msimu huu (matatu) kuliko aliyoyafunga mwaka mzima aliokaa Chelsea
  Mohamed Salah

Picha za Uharibifu wa Kimbunga Harvey Marekani

Brad Matheney akimsaidia mtu mwenye kiti cha magurudumu Galveston

 Kimbunga hicho kimesababisha mafuriko katika maeneo mengi
Kimbunga Harvey kilifika maeneo ya Marekani bara Ijumaa jioni na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Upepo wa kasi ya hadi 130mph (215 km/h) ulipiga maeneo ya pwani ya Texas.
Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kuwahi kupiga maeneo ya Marekani bara katika kipindi cha miaka 13 na kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo hayo.
Mji wa Rockport ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Magari na majumba yaliharibiwa katika uwanja wa ndege wa mji huo...
  Destroyed vehicles and buildings at Rockport Airport
magari...
 A light plane sits upside down at Rockport Airport
...sawa na ndege kadhaa ndogo.
  A Rockport firefighter goes door to door on a search and rescue mission as he looks for people that may need help
Mji wa Rockport ulipigwa na kimbunga hicho usiku kucha.
  A woman walks away from a destroyed apartment building
 Jessica Campbell hugs Jonathan Fitzgerald (L-R) after riding out Hurricane Harvey in an apartment on August 26, 2017 in Rockport, Texas
A man tries to kick open a door of an apartment to find his friends
Wakazi wa mji wa pwani Corpus Christi pia waliathirika pakubwa. Nguvu za umeme zilikatika na eneo lote likajaa giza.
Stewart Adams, of San Marcos, Texas, battles the winds in Corpus Christi U.S. on 25 August, 2017
Local residents sit at the bar in the dark after a citywide power failure as Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas, on August 25, 2017
A man walks near the bay waters as they churn from approaching Hurricane Harvey on August 25, 2017 in Corpus Christi, Texas
People walk through high winds in Corpus Christi
Jumamosi, wengi waliamka kupata barabara hazina watu na majumba yameharibiwa. katika baadhi ya maeneo, moto ulizuka.
Lakini uharibifu katika mji huo haukufikia uharibifu ulioshuhudiwa Rockport.
A burnt out house and cars that caught fire are seen after Hurricane Harvey hit Corpus Christi, Texas on August 26, 2017
A white SUV car is seen submerged
Ijumaa, kabla ya kimbunga kufika bara, watalii wanaopenda kufuatilia vimbunga walikuwa wamefika kwenye fukwe kujionea mawimbi na kupiga picha. Wengi baadaye walikimbilia maeneo salama.
  A resident photographs the beach in Corpus Christi
Watu wengi walihama miji na biashara kufungwa kuzuia uharibifu.
Sign on a business reading
Maafisa wameonya kwamba maeneo mengi yatashuhudia mafuriko mabaya katika kipindi cha siku chache zijazo.
Tayari kumetoka mafuriko Galveston.
  People walk dogs through flooded streets as the effects of Hurricane Henry are seen August 26, 2017 in Galveston, Texas
Na mjini Port Lavaca.
Floodwaters outside a house in Port Lavaca
Mjini San Antonio, wanyama pia walihamishwa...
Woman looks over bare refrigerator shelves in a Walmart in Houston
Wakazi wa Houston - mji wa nne kwa wingi wa watu Marekani - wamekuwa wakijiwekea chakula cha akina. Rafu nyingi katika maduka ya jumla hazina bidhaa.
An oil tank damaged by Hurricane Harvey is seen near Seadrift, Texas, August 26, 2017
Kimbunga Harvey kimeathiri sana uchimbaji wa mafuta Ghuba ya mexico pamoja na uchukuzi wa ndege.
Asilimia 45 ya usafishaji wa mafuta Marekani hufanyika katika ghuba hiyo.
Tangi la mafuta liliharibiwa akribu na mji wa Seadrift, katika wilaya ya Calhoun.
This NASA image from August 25, 2017, taken by NASA astronaut Jack Fischer shows Hurricane Harvey (top) from the cupola module aboard the International Space Station.
Picha za Nasa zimeonesha kimbunga hicho kilivyoonekana kutoka anga za juu.
Haki miliki ya picha AFP/NASA

Jumamosi, 26 Agosti 2017

Trump aagiza watu waliobadili jinsia kutoajiriwa jeshini

Wanaharakati wa watu waliobadili jinsia wakianda,mana wakipinga agizo la rais Trump

Wanaharakati wa watu waliobadili jinsia wakiandamana wakipinga agizo la rais Trump
Rais Donald Trump ameagiza idara ya ulinzi Marekani kusitisha uajiri katika jeshi wa watu waliobadilisha jinsia zao.
Trump aliashiria hatua hiyo ghafla katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mwezi jana.
Katika ilani kwa waziri wa ulinzi Jim Mattis, Trump amesema Pentagon ni lazima irudishe marufuku hiyo.
Idara hiyo ya ulinzi itaamua hatma ya watu ambao wamebadiisha jinsia na ambao tayari wanalitumikia jeshi .
Agizo hilo pia linasitisha nafasi ya wanajeshi wa kiume na wa kike kufanyiwa upasuaji wa kubadili jinsia zao.

DROO YA YUROPA HII HAPA

Wayne Rooney akiichezea Everton

Wayne Rooney akiichezea Everton

Hii hapa:
Group A: Villarreal, Maccabi Tel Aviv, Astana, Slavia Prague.
Group B: Dynamo Kiev, Young Boys, Partizan Belgrade, Skenderbeu.
Group C: Sporting Braga, Ludogorets, Hoffenheim, Istanbul Basaksehir.
Group D: AC Milan, Austria Vienna , Rijeka, AEK Athens.
Group E: Lyon, Everton, Atalanta, Apollon Limassol.
Group F: FC Copenhagen, Lokomotiv Moscow, Sheriff Tiraspol, FC Zlin.
Group G: Vitoria Plzen, Steaua Bucarest, Hapoel Beer-Sheva, FC Lugano.
Group H: Arsenal, BATE Borisov, Cologne, Red Star Belgrade.
Group I: Salzburg, Marseille, Vitoria Guimaraes, Konyaspor.
Group J: Athletic Bilbao, Hertha Berlin, Zorya Luhansk, Ostersund.
Group K: Lazio, Nice, Zulte Waregem, Vitesse Arnhem.
Group L: Zenit St Petersburg, Real Sociedad, Rosenborg, Vardar.

Ijumaa, 25 Agosti 2017

KUMBE WAHADZABE WANAKULA ASALI,MATUNDA NA NYAMA PORI HASA NUNGUNUNGU?

Hadza man carrying meat on a stick
Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, inadhaniwa kuwa jamii hii imeishi kaskazini mwa Tanzania, ikila matunda na mizizi, na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka 40,000.
Mwandishi wa BBC, Dan Saladino alikwenda kuwashuhudia wakikusanya na kuwinda, na kuchunguza iwapo lishe yao ni suluhu kwa matatizo mengi yanayowasibu binadamu kwa sasa.
Angalizo: Baadhi ya picha ni za wanyama waliouawa ni huenda zikawa za kuogofya.
Wakati nikiwa nimelala kifudifudi, niliweka kichwa changu ndani ya shimo lenye giza nikahisi harufu ya mnyama
Lakini sikuamini kuwa mtu ataingia mle ndani na kumtoa mnyama huyo. Mtu huyo ni Zigwadzee, na mnyama alikuwa nungunungu, amini usiamini.
Baada ya kukabidhi uta, mshale na shoka lake kwa mwindaji mwenzake wa Kihadzabe, Zigwadzee alishika fimbo fupi iliyochongoka na akaingia shimoni.

Jumanne, 15 Agosti 2017

Uchaguzi Kenya: Odinga achelewa kutangaza hatua atakayochukua



Bw Odinga na Bw Mudavadi

Bw Odinga na Bw Mudavadi
Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) umeahirisha kikao cha kutoa tangazo kuhusu mweleko wa chama hicho kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alikuwa ameahidi kwamba angetangaza ni hatua gani atachukua leo baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Ijumaa, ambapo mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi.
Ajenti mkuu wa Nasa Musali Mudavadi amesema sasa muungano huo unapanga kutoa tangazo keshi Jumatano.
"Tunasikitika kwamba mashauriano yanachukua muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa na Nasa kwa hivyo hawataweza kuwahutubia Wakenya kama walivyotarajia leo."
Bw Mudavadi hata hivyo amesema mashauriano "yanaendelea na yanaendelea vyema".
Rais Kenyatta alitangazwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.
Hapo jana, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake kususia kazi kabla ya kutoa tangazo kubwa leo.
Watu wengi hata hivyo walionekana kupuuza wito wa kususia kazi.
Baada ya kutokea kwa maandamano katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi na mji wa Kisumu, hali ya utulivu ilianza kurejea Jumatatu.
Viongozi wa muungano huo wa upinzani wanadai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na watu wenye uhusiano na serikali ya Jubilee na kwamba watu hao waliingilia na kuchakachua matokeo kumfaa Rais Uhuru Kenyatta aliyekuwa akishindana na Bw Raila Odinga kwa mara ya pili.
Tume ya uchaguzi ilisema mwanzoni ilikuwa haina taarifa kuhusu udukuzi kama huo lakini kwamba ingelifanya uchunguzi. Saa chache baadaye, tume hiyo ilisema hakuna jaribio lolote la udukuzi lililokuwa limefanyia katika sava ya matokeo ya uchaguzi.
Muungano wa upinzani pia umeikosoa IEBC kwa kutoa matokeo ya urais bila kuwasilisha fomu za kutangazwa kwa matokeo katika vituo vya kupigia kura na pia katika maeneo bunge, Fomu 34A na Fomu 34B.
Muungano huo umesema hautaenda kortini kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Alhamisi, 10 Agosti 2017

Mwanamume apatikana akisafirisha mikono ya binadamu China

Mkono ulivyoonekana kwenye mtambo wa usalama
Maafisa wa usalama kusini magharibi mwa China walipigwa na butwaa hivi majuzi walipogundua mwanamume mmoja alikuwa akisafirisha mikono miwili ya binadamu.
Kwa mujibu wa Pear Video, mzee wa miaka 50 kwa jina Zheng alisimamishwa na maafisa wa polisi katika kituo cha mabasi cha Duyun, katika mkoa wa Guizhou baada ya mikono miwili ya binadamu kugunduliwa na mtambo wa kiusalama tarehe 31 Julai.
"Nilimuuliza alikuwa amebeba nini kwenye mkoba wake, na akanijibu kwamba ulikuwa ni mkono," afisa wa usalama aliambia Pear Video.
Kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post, alizuiliwa mara moja, wakimshuku kuwa huenda alikuwa amehusika katika mauaji.

Hata hivyo, Bw Zheng aliwafafanulia kwamba alikuwa akisafirisha viungo hivyo kwa kakae, ambaye alikuwa amekatwa mikono baada ya kuhusika katika ajali ya mtambo wa umeme.
Bw Zheng alisema kakake aliomba asaidiwe kusafirisha mikono hiyo hadi alikokuwa akiishi, ili atakapofariki, mwili wake na viungo hivyo, vizikwe eneo moja.
  China
Huwa kawaida kwa wasafiri kukaguliwa wakiwa vituo vya mabasi China
Bw Zheng aliachiliwa huru na maafisa wa serikali baada ya hospitali iliyokuwa ikimtibu kakake kuthibitisha kisa hicho.
Nchini China, watu huamini kwamba mwili unafaa kuchomwa ukiwa mzima au kuzikwa pia ukiwa mzima ndipo marehemu awe na amani.
Hata hivyo, wengi wa waliosoma taarifa hiyo mtandaoni wameshangazwa sana na kisa hicho, ikizingatiwa kwamba maafisa wa matibabu huhitaji kibali maalum kuruhusiwa kusafirisha viungo vya binadamu.

Mkojo wamchongea mwizi Marekani

Andrew Jensen alikamatwa mnamo mwezi Julai 28 mwaka mmoja baada ya uvamizi mwengine wa nyumba moja mnamo mwezi Oktoba 2016.

Andrew Jensen mwizialiyekamatwa
Mwizi mmoja amekamatwa baada ya maafisa wa polisi kusema kuwa aliwacha ushahidi muhimu katika eneo la wizi baada ya kushindwa kusafisha choo alichotumia kwenda haja.
Wachunguzi wanasema kuwa sampuli za mikojo za Andrew Jensen katika nyumba hiyo ya Los Angeles ya Thousand Oak inafanana na vinasaba vya data ya FBI.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 42 alikamatwa mnamo mwezi Julai 28 mwaka huu takriban mwaka mmoja baada ya uvamizi wa nyumba moja mnamo mwezi Oktoba 2016.
Polisi wanasema kuwa wanakusanya ushahidi ulioachwa katika eneo la uhalifu.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Ventura Tim Lohman alisema kuwaAndrew alijisaidia haja ndogo na hakusaficha choo.
''Watu wengine hawajui kwamba DNA zinaweza kupatikana kupitia maeneo mengine mbali na mate na nywele''.
''Tunachunguza ushahidi wowote ambao umeachwa. iwe sigara iliovutwa, ama mkebe ambao umeachwa tutautathmini''.
Bwana Jensen ambaye aliwachiliwa huru kwa dola 70,000 anazuiliwa.

Jumatano, 9 Agosti 2017

Polisi amnunulia mwizi nguo alizoshikwa akiiba dukani

Constable Niran Jeyanesan pictured in an interview

 Alisema kuwa alifika kwenye eneo hilo na kugundua kuwa mtu huyo akiiba nguo ili avae aende kufanyiwa usaili wa kutafuta ajira (interview)

Mwizi wa duka huko Toronto ambaye alishikwa akiiba nguo ili aweze kuivaa kwa usaili alipata fusra asiyoitarajia kutoka kwa polisi ambaye aliitwa kuja kumkamata.
Niran Jeyanesan alikiambia kituo cha habari cha CP24 kuwa mfanyakazi mmoja wa duka la Walmart, aliripoti kuwa mtu huyo wa umri wa miaka 18 alijaribu kuiba shati, tai na soksi.
Alisema kuwa wakati alipofika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa usaili wa kutafuta ajira.

Hapo ndipo aliamua kumuachilia na kumnunulia nguo hizo.
"Kijana huyu amekuwa akikumbwa na wakati mgumu maishani na anajaribu kutatua hilo kwa kuitafutia familia yake riziki kwa kujaribu kupata kazi," bwana Jeyanesan alisema.
Akiongea na BBC mkuu wa Jeyanean, Paul Bois alipongeza kitendo hicho. Chanzo BBC

BREEEAKING NYUZZZZZ: Hassan Mwakinyo Bingwa wa Afrika ndondi

 Image result for Hassan Mwakinyo
Mwakinyo akivikwa ubingwa 

Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo amemvua taji la WBA Super Welter weight Anthony Jarmann jana usiko kwa TKO ya raundi ya 11.

Pambano hilo lililofanyika jana usiku katika Hotel ya Grand Palm mjini Gaborone Botswana.
Hii ni faraja kubwa kwa watanzania ambao wamekuwa wakisindikiza wengine kwenye hii michezo.
Aidha hii inaleta faraja zaidi ka sababu mwezi Oktoba mwaka jana Bondia mtanzani Francis Cheka alipigwa na bondia kutoka Namibia hivyo Mwakinyo ametulipa kisasi.

Image result for Hassan Mwakinyo









Bondia Mwakinyo akimwandama Janmann katika pambano lao la raundi 12 jana

Jumanne, 8 Agosti 2017

Real Madrid waigaragaza Manchester United 2-1 Kombe la Super Cup Uefa

 Isco asherehekea dhidi ya Manchester United
 Isco amefunga mabao 10 katika mashindano yote mwaka 2017
Manchester United walizidiwa nguvu na mabingwa wa Uhispania na Ulaya Real Madrid kwenye mechi ya Kombe la Super Cup la Uefa iliyochezewa Skopje, Macedonia chini ya joto kali.
Madrid walidhibiti mchezo huo kuanzia kipenga cha kwanza kilichopulizwa.
Walikuwa kifua mbele pale Casemiro alipowafungia, bao muda mfupi baada ya kugonga mwamba wa goli.
Waliongeza la pili kupitia Isco aliyefunga akiwa hatua nane kutoka kwenye goli baada ya kubadilishana pasi na Gareth Bale, ambaye alichezeshwa safu ya mashambulizi badala ya Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji wa United aliyenunuliwa £75m Romelu Lukaku alikomboa bao moja lakini Marcus Rashford akapoteza fursa nzuri ya kufunga kwa kuutuma mpira nje.
Madrid wamekuwa timu ya kwanza kufanikiwa kutetea Kombe la Super Cup la Uefa tangu 1990.
Mechi hiyo ilichezewa katika uwanja chini ya joto kali la nyuzi joto 30C katika mji mkuu huo wa Macedonia.
Wachezaji walipewa muda mara mbili kupoesha joto, chini ya utaratibu wa Uefa.
Red Devils wametumia £146m majira ya joto kununua mshambuliaji wa Everton Lukaku (£75m), kiungo wa kati wa Chelsea Nemanja Matic (£40m) na beki wa Benfica Victor Lindelof (£31m) wakijaribu kujiimarisha baada ya kumaliza nambari sita ligini msimu uliopita.
Wachezaji hao watatu walichezeshwa na meneja Jose Mourinho dhidi ya Madrid.
 
Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo aliingia nafasi ya Karim Benzema baada ya dakika 83
Upande wa Madrid, ni Ronaldo pekee ambaye alikuwa hayupo kwenye kikosi kilichoanza mechi ukilinganisha na kikosi kilichocheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
United walihangaika dhidi ya Madrid, hasa kipindi cha kwanza ambapo Madrid walitawala kwa kasi na pasi.
Real Madrid walilaza Manchester United katika kombe la Super Cup 
Mourinho alitumia vipindi vya mapumziko ya kutuliza joto kuwashauri wachezaji wake

Jumatatu, 7 Agosti 2017

Bilionea Mrema wa Arusha kuzikwa shambani kwake Ngurdoto


MWILI wa bilionea wa Arusha, Faustine Mrema (65), atazikwa katika shamba lake lililopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha nyuma ya hoteli yake ya kifahari ya Ngurdoto iliyoko katika wilaya hiyo Mrema aliyekuwa anamiliki hoteli za kifahari ikiwemo yenye hadhi ya Nyota Tano ya Ngurdoto jijini hapa, unatarajiwa kuwasili jijini Arusha leo mchana ukitokea Johannesburg, Afrika Kusini alikofikwa na mauti.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia ya Mrema aliyekuwa pia mmilikiwa hoteli za Impala ya Moshi na Arusha, Naura Springs ya Arusha na kampuni kadhaa za utalii, nyumba na magari ya kukodisha, mwili wa bilionea huyo utazikwa Jumatano ijayo nyuma ya hoteli yake ya Ngurdoto iliyopo Usa River, wilayani Arumeru. Taarifa hiyo ilisema kuwa mwili wa Mrema unatarajiwa kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) majira ya saa 7 mchana.
Baada ya kuwasili, mwili huo utapelekwa moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Arusha. Taarifa hiyo imesema Jumanne mwili huo utapelekwa nyumbani kwake eneo la Uzunguni kwa ajili ya ibada .

ARSENAL MABINGWA WA NGAO YA HISANI UINGEREZA

Washika bunduki wa London timu ya Arsenal jana walifanikiwa kutetea ngao ya Jamii kwa kuifunga timu ya Chelsea magoli 4 - 1.






Petr Cech of Arsenal and Arsene Wenger, Manager of Arsenal celebrate with The FA Community Shield during the The FA Community Shield final between Chelsea and Arsenal at Wembley Stadium on August 6, 2017 in London, England
Kocha Arsene Wenger akiwa na ngao ya jamii waliyoshinda

Chelsea walikuwa wa kwanza kuata bao kupitia kwa Moses  katka dakika ya  47.
Arsenal walisawazisha katika dakika ya 82 kwa bao lililofungwa na Kolasinac.
Mpaka mwisho wa dakika 90 Arsenal 1 Chelsea 1.

 
Katika matuta Cahil aliifungia Chelsea na Walcot akaisawazishia Arsenal. Golkipa wa Chelsea Courtous akakosa na pia Morata akakosa. Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Nacho Monreal, Oxlade-Chamberlain na Girroud,