Jumatano, 18 Aprili 2018

Nape Nnauye Ahoji Kuhusu Soko la Mbaazi Bungeni.......Serikali Yajibu Soko ni Baya, Watanzania Waitumie Kula Maana ni Chakula Kizuri


SeeBait
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.

Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa kilimo, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.

Neema yaja kwa watumishi wa umma


SeeBait
SERIKALI imetangaza neema kwa watumishi wa umma 4,812 baada ya jana kubainisha kuwa kuna fursa za mafunzo 659 zitakazotolewa na Serikali ya China.

Fursa hizo za mafunzo zimejikita kwenye maeneo ya kipaumbele cha taifa yaliyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21).

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari na Elimu ya Bunge mjini hapa jana, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema mafunzo yamejikita kwenye uhandisi wa viwanda, mawasiliano na usafirishaji.

Dk. Ndumbaro pia alisema mafunzo hayo yatajikita kwenye kilimo, elimu, afya, biashara na uchumi, Tehama na utawala bora.

Serikali Kuajiri Walimu 6,000 June


SeeBait
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu inatarajia kuajiri walimu 6,000 wa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upunguzu wa walimu wa Hisabati na Sayansi.

Pia, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona ndio chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. Alisema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari.

Kadhalika, alisema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo.

AJIRA ZA UTUMISHI WA UMMA 2017- 2018

Cheki www.mabumbe.com

Alhamisi, 11 Januari 2018

Bendera: Tanzania na Korea Kaskazini zazozana

 

Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.                
Taifa la Tanzania limefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga aliambia BBC kwamba meli hizo zilionekana hivi karibuni katika bahari hindi eneo ambalo halipo mbali na Tanzania.
Hatahivyo hakutoa idadi kamili ya meli hizo.
''Meli za Korea Kaskazini zilipigwa marufuku na Umoja wa Mataifa na hazikuruhusiwa kusafiri ama hata kutia nanga'',alisema Mahiga.
''Kwa hivyo meli hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta njia kukiuka vikwazo hivyo ili kuweza kuendelea na biashara zao,na mbinu moja ni kupeperusha bendera za mataifa tofauti''.
Waziri huyo amesema kuwa malalamishi yametumwa katika serikali ya Korea Kaskazini wakilaumu biashara hiyo ya ujanja.
''Shirika la kimataifa la maswala ya baharini pia limeelezewa ili kuwakamata wamiliki wa meli hizo'',aliongezea Mahiga.

Meli yenye bendera ya Tanzania yanaswa Ugiriki ikipeleka vilipuzi Libya

 

Tanzania imefutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria.                   Mwaka 2016, Tanzania ilifutilia mbali usajili wa meli kadhaa za Korea Kaskazini kwa kupeperusha bendera za taifa hilo kinyume na sheria                
Maafisa wa Ugiriki wanaoshika doria baharini wamesema wanaizuilia meli iliyokuwa inapeperusha bendera ya Tanzania ambayo ilikuwa imebeba vilipuzi.
Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya, kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.
Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi ikiwemo.
"Maafisa wa kushika doria baharini wamezima bomu lililokuwa linasafiri," afisa mkuu wa walinzi hao wa Ugiriki Yiannis Sotiriou aliwaambia wanahabari, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ANA.
Wizara ya Safari za Baharini ilisema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikendi baada ya maafisa kupashwa habari na mdokezi.

Ilisindikizwa hadi katika bandari moja kisiwa hicho cha Crete na kufanyiwa ukaguzi.
Crete
Sotiriou alisema meli hiyo ambayo ilinaswa Jumamosi ilikuwa pia na kasoro nyingi na haikufaa kuwa baharini.
"Ingesababisha madhara makubwa sana kwa watu na mazingira pia," amenukuliwa na AFP.
Nahodha wa meli hiyo kwa jina Andromeda alidai ilikuwa inasafiri kuelekea Djibouti lakini baadaye ikabainika kwamba ilikuwa inasafiri kuelekea mji wa bandarini wa Misrata nchini Libya.
Shirika la AFP linasema mabaharia hao wanane waliokuwa kwenye meli hiyo watafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka leo.
Watano kati ya mabaharia hao ni raia wa India, wawili wa Ukraine na mmoja wa Albania.

Jumatano, 10 Januari 2018

Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda

Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda

              Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
Mfugaji mmoja wa nguruwe kaskazini mwa Rwanda amepata siri ya aina yake kuwafanya nguruwe anaofuga kuongeza uzalishaji.
Siri hiyo ni muziki unaotumbwiza saa 24 katika mazizi yao.
Mfugaji huyo maarufu Sina Gerald anasema muziki huwasaidia nguruwe kunona, kujifungua vizuri na kutumia chakula kidogo ikilinganishwa na nguruwe wasiosikia muziki.
Mzee Theophile Hakizimana ambaye ni mpokezi ya wageni shambani anasema kuna aina mbili za nguruwe, Landras ambao ni nguruwe warefu na Large White ambao ni wafupi lakini wanono.
Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
                             Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
Ana nguruwe wapatao 700 pamoja na chakula cha kawaida , nguruwe hawa hupata muziki saa 24.
"Muziki huu unasaidia nguruwe kuwa watulivu,kuwa na afya nzuri,na pengine niseme kuwa nguruwe wanatoa uzalishaji mwingi wakati wanapata muziki kama huu" anasema Hakizimana.
Anasema kwa muda mrefu wamekuwa wakiendesha utafiti kuhusu nguruwe na uzalishaji wao kwa ujumla
Kuna pia faida kubwa kwa mfugaji kwa sababu Nguruwe wakipata muziki kama hivi wanakula chakula kidogo sana ukilinganisha na nguruwe ambao wanakula bila kusikia muziki.
Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
                                   Jinsi muziki unavyotumiwa kuongeza mazao ya nguruwe Rwanda
"Hapa nalinganisha na chakula tunachowapa nguruwe wengine tulionao ambao wao hawapati muziki. Hii ni kwa mjibu wa utafiti tuliofanyia nguruwe katika kituo chetu''
Ufugaji wa nguruwe umeshika kasi nchini Rwanda kutokana na faida yake ya haraka kibiashara.
Nyama ya nguruwe ndiyo ghali kuliko nyama nyingine sokoni. Kilo moja ikiwa ni franga si chini ya elfu 4 za Rwanda kama dolla 5.
Kitoweo cha nguruwe ni miongoni mwa vitoweo vyenye mvuto wa hali ya juu kwenye vilabu vya pombe katika majiiji ya Kigali na Kampala kikifahamika kwa jina maarufu ''Akabenz''

Mwanamume achoma moto nyumba akiua buibui California, Marekani

    

A wolf spider at Sydney Wildlife World on July 18, 2008.                  Buibui huyo anaaminika kuwa buibui mkubwa aina ya 'wolf spider'                
Mwanamume mmoja katika mji wa Redding kaskazini mwa California, Marekani anadaiwa kuchoma moto nyumba akijaribu kumuua buibui.
Kisa hicho kilitokea Jumapili kwa mujibu wa vyombo vya habari Marekani.
Mmoja wa walioshuhudia, ambaye alikuwa anaishi katika nyumba hiyo kubwa ya makazi, ameambia gazeti moja California kwamba buibui huyo huenda alichangia kueneza moto huo chumbani, akikimbia akiwa anaungua.
Haijabanika iwapo buibui huyo alinusurika.
Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, lakini wakazi wa jumba hilo walioondolewa salama.

Afisa wa idara ya zimamoto eneo hilo Gerry Gray ameambia BBC ni kwenye kwamba moto ulizuka katika jumba hilo lakini akasema chanzo cha moto huo bado kinachunguzwa.
"Taarifa kuhusu 'buibui' zilitolewa na raia walioshuhudia, waliokuwa eneo la tukio, na bila shaka zinatumiwa katika uchunguzi.
Buibui huyo alikuwa aina ya 'wolf spider' ambao ni buibui wakubwa.
Idara ya zima moto imeambia gazeti la Redding Record Searchlight kwamba dalili zinaonesha moto huo uliwashwa na mwenye nyumba.
California map
Redding, eneo ambalo kisa hicho kilitokea, ni mji ulio maili 162 (261km) kaskazini Sacramento.
Walioshuhudia wanasema buibui huyo alieneza moto alipokimbia na kujificha kwenye mto.
Mto huo ulishika moto na moto huo, na ingawa wakazi waliweza kuuzima hapo, ulikuwa tayari umeenea maeneo mengine ya jumba hilo.

Maafisa wanasema moto huo ulisababisha uharibifu wa takriban $11,000 (£8,000) na baadhi ya vyumba vya jumba hilo vitahitaji kukarabatiwa kabla ya watu kuishi huko tena.
Hiyo ni hasara ya kuogopa vitu hata kama havina madhara ambayo kwa kiingereza huitwa "phobia" ambapo watu huogopa hata chura, kinyonga, jongoo nk

Jumatatu, 8 Januari 2018

Meli inayoteketea baharini hatarini kulipuka na kuzama

     

Oil tanker on fireMeli inayoteketea baharini iko katika hatari ya kulipuka na kuzama                
Kuna hofu kubwa ya kutokea janga la kimazingira Kusini mwa bahari ya China wakati meli ya kubeba mafuta inazidi kufuja siki mbili baada ya kugongana na meli nyingine ya mizigo.
Maafisa nchini China wameviambia vyombo vuya habari kuwa meli hiyo iko kwenye hatari ya kulipuka na kuzama.
Wakoaji wanaojaribu kufika eneo hilo wanazuiwa na moshi mkubwa.
Wahuhudumu 30 raia wa Irana na 2 wa Bangladesh bado hawajulikani waliko licha ya jitihada za kimataifa kuwaokoa.

Kiwango cha uchafuzi wa mazingira bado hakijulikani. Chombo hicho bado kilikuwa kinateketea leo Jumatatu.
Licha ya kuwa na usajili wa Panama meli hiyo inamilikiwa na kampuni ya Iran.
Sanchi ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta ya Iran wakati iligongana na meli ya mizigo ya China Jumamosi usiku.
Wahudumu 21 wa meli ya mizigo ya China waliokolewa.
Map
        Wahudumu 30 raia wa Irana na 2 wa Bangladesh bado hawajulikani waliko licha ya jitihada za kimataifa kuwaokoa.            
Watu wanaoshughulikia mazingara mnasemaje?    

Njia za kukabiliana na upara

Mwanamume mwenye upara

Tatizo la kunyonyoka kwa nywele na kuwa na kipara limekuwa likiwatatiza wanaume wengi kwa muda.
Shida hii mara nyingi huanza wanaume wakiwa wana miaka 30 hivi, na kufikia umri wa miaka 50 ambapo nusu ya wanaume huwa wanakabiliwa na tatizo hili.
Tatizo hili hutokana na vinyweleo vya nywele, ambavyo huwa kina cha ukuaji wa nywele, kunywea. Shughuli hii huendelea pole pole kwa muda mrefu.
Kuna wengi wanaodai kuwa na tiba ya tatizo hili, baadhi wakitumia dawa za kisasa na wengine za kiasili lakini ufanisi wake huwa tofauti.
Ni njia gani hufanikiwa?
Kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Afya Uingereza (NHS) kupandikizwa kwa nywele ni moja ya njia zinazofanikiwa sana.
Lakini gharama yake huwa ya juu mno.
Kupandikizwa nywele kunaweza kugharimu kuanzia £1000 hadi £30,000 [sawa na shilingi za kitanzania milioni 3 hadi 90].
Wakati mwingine, daktari wako anaweza kupendekeza utumie dawa yenye kiungo fulani ambacho hujulikana kama Finasteride. Kiungo hiki hubadilisha viwango vya homoni fulani zinazodhibiti mfumo wa uzazi katika binadamu.
Utafiti unadokeza kwamba tiba hii inaweza kusisimua ukuaji wa nywele tena katika theluthi mbili ya wanaume wenye upara.

Dawa nyingine kwa jina Minoxidil iligunduliwa kibahati miaka ya 1950 watafiti waliokuwa wanatafuta tiba ya shinikizo la damu. Inaaminika kwamba hufanya kazi kwa kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye ngozi ya kichwa maeneo yenye nywele na kufungua vinyweleo vya nywele.
Ikitumiwa vyema, inaweza kufanikiwa kwa asilimia 80 ya wanaoitumia, lakini huhitaji kutumiwa kwa muda mrefu.
Kutumia dawa hizi mbili kunaweza kukugharimu maelfu ya pesa kila mwaka.



Kuna ushahidi pia kwamba aina fulani ya vyakula vina uwezo wa kuzuia upara. Kuna utafiti ulioonyesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Omega 3 kwa wingi ulipunguza kunyonyoka kwa nywele pole pile.
Upara huhusishwa pia na upungufu wa madini ya chuma mwilini, hivyo kula mboga zenye rangi ya kijani (mfano spinachi) kunaweza pia kumfaa mtu.
Kando na kula vyakula vifaavyo, utafiti unadokeza pia kwamba kufanya mazoezi zaidi na kupunguza mfadhaiko ni mambo yanayoweza kupunguza kunyonyoka kwa nywele pia.

Alhamisi, 4 Januari 2018

Mlevi asafiri nchi tatu kwa kutumia teksi Ulaya mkesha wa Mwaka Mpya

A canal in Copenhagen lined with attractive multi-coloured buildings

 Mwanamume huyo alikuwa akinywa pombe hapa Copenhagen, mji mkuu wa Denmark
Mkazi mmoja wa mji wa Oslo anajutia aliyoyafanya akiwa amelewa mkesha wa Mwaka Mpya baada ya kugundua kwamba alikuwa anadaiwa $2,220 (£1,640)  sawa  na shilingi za Kitanzania milioni 5 kwa kutumia teksi.
Mwanamume huyo wa miaka 40 hivi alikuwa amesafiri kupitia mataifa matatu, kuanzia Copenhagen nchini Denmark, akapitia Sweden, na kisha akafika Oslo nchini Norway.
Alipofika nyumbani, aliingia ndani na hakumlipa nauli dereva wa teksi.
Dereva huyo alijipata amekwama baada ya betri ya gari lake yake kuisha chaji akiwa nje ya nyumba ya mwanamume huyo akisubiri atoke nje na pesa amlipe.
Aliamua kuwapigia simu polisi.
Kupitia Twitter, polisi wa Olso wanasema walimkuta mwanamume huyo akiwa amelala fo fo fo kitandani na kumwamsha.
Alikubali kulipa pesa alizokuwa anadaiwa.
Mwanamume huyo hana historia ya kutekeleza uhalifu, kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Norway ya NRK.
Safari hiyo ya kutoka Copenhagen hadi mtaa wa Abildso mjini Oslo ilikuwa ya umbali wa 600 km (maili 372).
Huenda akafikiria kutumia ndege siku zijazo...
Na dereva wa teksi? Gari jingine lilifika kumsaidia..

A BBC map showing the relative locations of Copenhagen and Oslo 

Hili ni fundisho kwa walevi kufanya maamuzi ya busara wakiwa wamelewa.

Benki tano zafutiwa leseni kuanzia leo Alhamisi


SeeBait

Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni 
  • Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, 
  • Efatha Bank Limited, 
  • Njombe Community Bank Limited, 
  • Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na
  •  Meru Community Bank Limited.
BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.”

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake. Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa BoT inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha.


Trump amshambulia msaidizi wake wa zamani Steve Bannon

Steve Bannon aliyekuwa afisa wa ikulu ya Marekani

Steve Bannon aliyekuwa afisa wa ikulu ya Marekani
Rais Donald Trump amemshambulia msaidizi wake wa zamani wa Ikulu ya White house Steve Bannon,kwamba alipoteza akili zake mara tu alipopoteza ajira yake.Trump amefikia hatua hiyo kufuatia Bannon kunukuliwa na kitabu kipya kilichopishwa akiwa anaelezea jinsi mtoto wa rais Trump alivyokutana kwa siri na kundi la watu kutoka Urusi ili kupanga njama za uchaguzi.
Ndani ya kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael Wolff,afisa huyo wa zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo Donald Trump mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi zilizolenga kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze kushinda.
Hata hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu hicho zilizopewa uzito na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white house,rais Donald Trump amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye binafsi na urais wake pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa huyo hakupoteza kazi yake tu lakini alipoteza akili zake pia.

''Steve alikuwa ofisa aliyekuwa akifanya kazi kwaajili yangu,mara baada ya mimi kuteuliwa kuwania urais baada ya kuwabwaga wagombea wengine 17,'' amesema Trump.
Amesema pia kuwa Steve anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.
Steve Bannon, ni afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha kazi mwezi August mwaka jana.

Jumatano, 3 Januari 2018

Wazimbabwe waishi uwanja wa ndege Bangkok kwa miezi 3

Uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi airport, mjini Bangkok

 Suvarnabhumi ni uwanja wa ndege kubwa zaidi nchini Thailand
Familia moja kutoka Zimbabwe wamefanya uwanja wa ndege mjini Bangkok kuwa makazi yao kwa karibu miezi mitatu.
Kwa mujibu ya ofisi ya uhamiaji wa Thailand, watoto wanne wenye umri chini ya miaka 11 na watu wazima wanne walifika jijini Bangkok mwezi wa Mei, lakini walikataa kurudi Zimbabwe kwa misingi ya usalama wao.
Taarifa yao iliibuka baada ya mfanyakazi wa uwanja wa ndege huo alipoweka picha katika mtandao wa kijamii wa Facebook, akimpatia mtoto wa kike Mwafrika, zawadi ya Krismasi.
Picha hio,ambayo imefutwa sasa, iliambatana na ujumbe wa Kanaruj Artt Pornsopit akisema kuwa familia hiyo ilikuwa ikiishi katika jengo hili kwa miezi mitatu kwa sababu ya "hali ya sintofahamu" nchini mwao.
 
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamekuwa wakitoa msaada wa chakula kwa familia hio.
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamekuwa wakitoa msaada wa chakula kwa familia hio.
Msemaji wa ofisi ya uhamiaji Pol Col Cherngron Rimphadee aliiambia BBC kuwa awali familia hiyo iliwasili nchini Thailand kama watalii. Walijaribu kupanda ndege kutoka mjini Bangkok mwezi Oktoba hadi mji wa Barcelona nchini Uhispania kwa kupitia Kieve nchini Ukraine.
Lakini walikatiliwa kuingia katika ndege kwa sababu ya kukosa vibali vya kuingia Uhispania.
Pamoja na hayo walishindwa kurudi tena na kuingia nchini Thailand sababu kibali chao cha mwanzo cha kitalii kilichowakubalia miezi mitano kilipitwa na wakati na ilibidi walipie faini kubwa.
Familia hiyo imekataa kurudi Zimbabwe ikisema wanahofia usalama wao baada ya vurugu iliyotokea Novemba iliyomwondoa madarakani rais Mugabe aliyedumu kwa miaka 37.
Hata hivyo, kwa sasa hamna taharuki yeyote inayoendelea nchini Zimbabwe, kwa baadhi nchini humo wameyashuku madai yao kuhofia usalama wao.
Kwa mujibu wa Col Rimphahdee familia hiyo imewasilisha maombi ya kuomba makazi kwa Umoja wa Mataifa, wakati wakihudumiwa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi.
Aliimabia idhaa ya BBC Thai kuwa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR , limeomba familia hiyo ibaki nchini Thailand wakati jitahada za kuwapeleka nchi nyingine zikifanyika.
Nchi Picha ya ndani ya jengo la uwanja wa ndege wa Suvarnabhumiya Thailand haina sheria ya kuwapatia makazi wakimbizi au watafuta hifadhi.
 
Picha ya ndani ya jengo la uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi

Jumanne, 2 Januari 2018

Tapeli ahukumiwa kifungo cha miaka 13,275 jela nchini Thailand

Takriban watu 40,000 wamedaiwa kudanganywa na tapeli huyo

 Takriban watu 40,000 wamedaiwa kudanganywa na tapeli huyo
Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela.
Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu.
Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake.
Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu.
Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita.
Huenda asihudumu zaidi ya miaka 20 kwa kuwa sheria ya Thai inatoa miaka 10 kwa makosa mawili aliyopatikana nayo.
Waendesha mashtaka waliambia mahakama kwamba Pudit aliandaa semina ambapo waliohudhuria walishawishiwa kuwekeza katika kile alichosema ni biashara zinazohusiana na ujenzi ,urembo, uuzaji wa magari yaliotumika uuzaji wa bidhaa nje ya nchi miongoni mwa vitu nyengine.
Kulingana na gazeti la Bangkok Post, wawekezaji waliahidiwa mapato makubwa na marupurupu iwapo wataleta wanachama wapya.
Na kama mradi mwengine wowote wa Piramidi, wawekezaji waliowekeza fedha zao wa kwanza wanalipwa kuwalipa wanachama wao wa kwanza.
Pudit alikuwa anazuiliwa katika jela ya Bangkok tangu alipokamatwa mwezi Agosti wakati aliponyimwa dhamana.
Mahakama ilizipiga faini kampuni zake mbili ilio sawa na dola milioni 20 kila moja.
Pudit na kampuni zake aliagizwa kulipa takriban dola milioni 17 kwa waathiriwa 2,653 pamoja na riba ya kila mwaka ya 7.5%

Namna nzuri ya kutimiza malengo ya Mwaka Mpya

feet in trainers running
Kwa kawaida, Mwaka Mpya unapowadia, watu hujiwekea maazimio na malengo mengi ya kutimiza katika mwaka husika.
Mara nyingi huwa ni kupunguza uzani, kufanya mazoezi zaidi, kuacha kuvuta sigara, kujifunza lugha mpya na kadhalika.
Lakini mara nyingi malengo haya huwa hayatimizwi.
Hatuwezi kukuambia ni maazimio gani yanafaa kuwekwa, lakini kuna utafiti uliofanywa ambao unaweza kukuelekeza jinsi ya kujiwekea malengo ambayo utaweza kuyatimiza na pia njia bora zaidi ya kuhakikisha unatimiza malengo hayo.
Kuna ushahidi kwamba mara nyingi binadamu huongozwa na hamu ya "kupunguza hasara" - yaani, huwa mara nyingi tunaongozwa na kufuta hasara ambayo tumepata badala ya kupiga hatua mbele.
Kuweka maazimio kwa njia ambayo lengo lako zaidi litakuwa kupunguza au kufuta hasara, kwa maana ya kupata kitu ulichokipoteza, huenda yakawa rahisi kutimiza kuliko maazimio ya kukipata kitu kipya.
Mfano, inaweza kuwa rahisi kwako kuurejelea uraibu uliokuwa nao awali au kujiweka sawa kimwili kufikia kiwango cha awali kuliko kuboresha muonekano wako au uwezo wako kufikia viwango ambavyo haujawahi kuvifikia awali.
Hili pia linatuelekeza kwenye ushauri mwingine muhimu unapojiwekea malengo yako ya mwaka - lazima yawe na uhalisia na yanayoweza kutimizika.
woman running in mountains

Washirikishe wengine

Mwanafalsafa katika Chuo Kikuu cha Warwick Dkt John Michael hutafiti kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii yanayowasaidia watu kutimiza malengo na ahadi zao.
Anasema kuwa kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kutimiza ahadi na maazimio iwapo tutayatazama kuwa na umuhimu kwa watu wengine - kwamba maslahi ya wengine yatakuwa hatarini iwapo tutashindwa.
Hii huenda ikawa ni kwenda darasani na rafiki yao.
Ufanisi unaweza kuwa hata zaidi iwapo utalipa karo mapema - ukihisi kwamba mtu amewekeza pesa na muda wake, na kwamba vyote vitapotea, basi kuna uwezekano kwamba utajizatiti kutimiza malengo hayo.
Utafiti wa Dkt Michael pia unaonesha kwamba watu huenda wakahamasishwa kuendelea na kazi wasiyoipenda iwapo mtu mwingine wa maana kwao amewekeza kitu hapo.
Sifa na hadhi ya mtu huwa muhimu sana, na vinaweza kutumika kama kichocheo.
Kuyafanya maazimio yako wazi kunaweza kukuhamasisha kuyatimiza kwani utahofia kwamba hadhi yako itashuka iwapo hutayatimiza.
"Huwa hakuna anayetaka kupata sifa za kuwa mtu asiyeaminika, kwa hivyo kutangaza mipango yetu hadharani kunaweza kukupatia motisha. Kuweka dau kunaweza pia kuwa kichocheo zaidi," anasema Prof Neil Levy wa Chuo Kikuu cha Oxford.

Vitu vya kukukumbusha

Kuweka maelezo zaidi na ufafanuzi kwenye maazimio yako pia husaidia, anasema.
Mfano kwenda kwenye chumba cha mazoezi Jumanne alasiri na Jumamosi asubuhi, kwa mfano, ni bora kuliko kusema tu kwamba utaenda kufanya mazoezi mara nyingi zaidi, anasema Prof Levy.
Anapendekeza uhusishe maazimio yako na viashiria au vitu fulani vya kukukumbusha.
Iwapo unataka kujifunza lugha nyingine, unaweza kwanza kuweka ahadi ya kusikiliza makala ya lugha hiyo kila asubuhi ukisafiri kwenda kazini asubuhi.
Kisha, ndipo ujiwekee nafasi ya kufanikiwa zaidi, unaweza kuweka ujumbe wa kukukumbusha kufanya hivyo kwenye simu yako au kidhibiti mweleko wa gari kila jioni kabla ya kulala.
Hapo, unaeleza nia na pia kuchukua hatua kuhakikisha unaitekeleza nia hiyo.

Kuweka masharti

Prof Levy anaonya pia dhidi ya kujiwekea masharti ambayo yanaweza kuwa kielelezo baadaye.
"Kubali wazi kwamba kuna baadhi ya mambo yanayoweza kukuzuia kufanya jambo (Sitakwenda kwa mazoezi iwapo nyumba itawaka moto). Lakini usipanue masharti haya au kuyafanya kuwa mtindo kwani yanaweza kukuzuia kutekeleza maazimio yako.
"Siku yangu ya kuzaliwa, inaweza kuwa siku ya kipekee na inakubalika. Lakini nikianza kutambua mambo yanayofanyika mara kwa mara - pengine iwapo ni wiki ya mwisho ya mwezi, kuwepo kwa baridi kali - basi itakuwa mazoea," anasema.
  airport departures board
Yafanye maazimio yako kuwa sehemu ya mipango yako ya muda mrefu

Kufanya maazimio kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu

Naye Dkt Anne Swinbourne, mwanasaikolojia katika chuo kikuu cha James Cook, Australia, anasema kuwa maazimio bora zaidi ni yale ambayo yanaoana na malengo ya muda mrefu ambayo umejiwekea wewe binafsi, kuliko yale ambayo hayana msingi au ni matamanio tu.
Iwapo hujawahi kuonesha nia ya kushiriki katika michezo, kujiwekea malengo ya kuwa mwanariadha stadi ni lengo ambalo bila shaka utatatizika kutimiza.
Kwa sababu umekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kusafiri sana kujionea ulimwengu kabla ya kutimiza miaka 50, lengo la kusafiri zaidi linaweza kutimizika.
Na pia, kutimiza malengo yote hutegemea mipango yako.
Tambua ni mambo gani yanakuchochea kufanya mambo usiyoyapenda au usiyoyapenda. Iwapo hutaki kunywa pombe sana, panga kukutana na marafiki au wageni wako kwenye mgahawa badala ya baa, vilevile, ukipanda kuacha kuvuta sigara, vyema zaidi ni kuacha kujihusisha na wavutaji sigara sana.
Malengo yako ya mwaka ni vyema ukayaandika vizuri na kuyabandika mahali ambapo utayasoma mara kwa mara mfano kwenye kitanda chako !!!!!

Alhamisi, 14 Desemba 2017

ALALA MASKINI AKAAMKA TAJIRI Ufaransa

People watching departure boards at Paris Charles de Gaulle airport

Mwanamume asiye na makazi amepata pesa nyingi uwanja wa ndege Ufaransa
Mwanamume ambaye alipata pauni 260,000 baada ya kuegemea mlango wa kampuni ya Charles de Gaulle kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa na mlango ukafunguka na kukuta kitita cha fedha  anaaminiwa kuwa mtu asiye na makazi.
Polisi wanasema kuwa walimtambua mwanamume huyo kupitia kwa kamera za CCTv kama mmoja wa watu wanaolala karibu na uwanja wa ndege.
Mlango wa kampuni inayoshughulikia masuala ya fedha ya Loomis terminal 2F, ulikuwa umeachwa bila kufungwa na mwanamume ambaye umri wake unakisiwa kuwa miaka 50 hivi alitoka nje akiwa na mifuko miwili ya pesa.
Kwa sasa anasakwa na polisi.
Mwendo wa saa (16:30 GMT) Ijumaa iliyopita king'ora kililia katika kampuni hiyo inayohusika na masuala ya fedha.

Maafisa waliochunguza video ya cctv waligundua kuwa mwananamume huyo alikuwa akichakurachakura kwenye ndoo za taka nje ya ofisi hizo ili kupata chochote kitu, na kuonekana kushangazwa wakati mlango aliokuwa ameegema ulipofunguka ghafla.
Aliingia ndani na muda mfupi baadaye akaondoka akiwa amebeba mifuko miwili.
Mwanamume huyo aliacha mfuko wake nyuma lakini haukuwa na stakabadhi yoyote ambayo ingesababisha atambuliwe.
Pesa alizochukua zinatajwa kuwa jumla ya pauni 260,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 750. AMELALA MASKINI AKAAMKA TAJIRI usikate tamaa hadi uingie kaburni!!!!.

Mpanda majengo marefu ahofiwa kufariki baada ya kuanguka China

Wu Yongning uses a selfie stick to photograph himself reclining on top of a structure far above the surrounding buildings

Mpanda majengo marefu afariki baada ya kuanguka China
Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amehofiwa kufariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.

Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.



 
A composite image shows Wu Yongning, left, facing outward on the exterior of a wall high above the city skyline, holding on with just one hand from a ledge above ; and right, sitting on a steel girder which is projecting over the edge of a very tall building into the street
Mpanda majengo marefu akionesha manjonjo huko China

PENZI LIKIKOLEA HATARI: Mwanamke aliyemuua mume wake ili aishi na mpenzi wake India

Swati and Sudhakar Reddy

 Swati Reddy (kulia) na mpenzi wake wanadaiwa kumuua mume wake Sudhakar (kushoto) mwezi uliopita
Wapenzi wiwili nchini India wamekamatwa kwa kumuua mume wa mwanamke na kisha kujaribu kumfanyia upasuaji wa kubadilisha sura mwanamume mpenzi ili aweze kuchukua mahala pake,
Tindi kali ilimwagwa kwenye uso wa mwanamume, mpenzi wa mwanamkea, katika shambulizi lililopangwa, huku wapenzi hao wakipanga kusema kuwa sura yake ilikuwa imebadilika baada ya upasuaji.
Lakini ndugu wa bwana wa mwanamke aligundua mpango huo alipofika hospitalini.
Alitoa malalamiko yake kwa polisi ambao walifanya uchunguzi wa vidole na kugundua njama huyo.
Mke, Swati Reddy amekamatwa. Polisi waliiambia BBC kuwa watamkamata pia mpenzi wake, Rajesh Ajjakolu mara atakapotibiwa majeraha yake na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
 
Rajesh Ajjakolu
Rajesh Ajjakolu alilazwa hospitalini akiwa na majeraha ya uso
Bwana Sudhakar Reddy anadaiwa kuuliwa usiku wa tarehe 26 Novemba na mwili wake kutupwa siku iliyofuatia. Hadi sasa mwiwi huo bado haujapatikana.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo amekiri kuwa walimuua mume wake.
Rajeshi Ajjakolu alilazwa hospitalini tarehe 28 Novemba huku Bi Reddy akiwajulisha familia ya mume wake kuhusu shambulizi la tindi kali.
Polisi wanasema kuwa wazazi wa Bw. Reddy waliamini kuwa mwanamume ambaye alikuwa akipata matibabu alikuwa ni mtoto wao na kulipa hadi dola 7,758 kama bili ya hospitali.
Njama hiyo haikugunduliwa hadi tarehe 9 mwezi Disemba, wakati ndugu yake Reddy, alifika hospitalini humo na kuwajulisha polisi aliposhuku kuwa mwanamume huyo hakuwa ndugu yake.

Jumatatu, 11 Desemba 2017

RAILA AUFYATA: aahirisha Shughuli za kumuapisha kama Rais wa Kenya

Raila Odinga

Raila Odinga Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya.
Shughuli hiyo ilikuwa imepangwa kufanyikasiku ya Jumanne tarehe 12 mwezi huu.
Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye.
Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu  nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.
Wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 mwezi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuunganisha taifa katika muhula wake wa pili uongozini katika sherehe ambayo ilisusiwa na viongozi wa upinzani.
Akihutubu baada ya kula kiapo uwanjani Kasarani, Nairobi, kiongozi huyo alisema ameyasikia baadhi ya mapendekezo ya upinzani na atazingatia baadhi.
Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa upinzani kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo.