Jumapili, 10 Agosti 2014

RPC NJOMBE APATA AJALI



Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ASP Fulgence Ngonyani.
Na James Festo, Njombe.
KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani pamoja na dereva wake Nuaka Seme wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.


Jumamosi, 9 Agosti 2014

TAHADHARI YA VIBAKA KWA WATU WANAOHUDHURIA KILELE CHA MAONESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI NANE NANE MOROGORO.

Polisi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu.
TAHADHARI KWA WATU WANAOHUDHURIA KILELE CHA MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARIKI KATIKA UWANJA WA MWL JULIUS NYERERE, NANE NANE MOROGORO.



KUNA KUNDI LA VIBAKA WAMEHAMIA KATIKA MAONYESHO HAYO KWA KUIBA FEDHA KWA MITINDO YOTE IKIWEMO MCHEZO WA KARATA TATU, KUKWAPUA MIKOBA, KUCHANA MABEGI NYEMBE NA KUCHUKUA FEDHA NDANI YA MIKOBA HASA ILE YA AKINA MAMA NA WATU WANAONEKANA KAMA NI WASHAMBA MACHONI MWAO.

CHUKUE TAFADHALI KWA WATU WATAOENDA AMA WALIOPO NDANI NA MAONYESHO HAYO AMA KUMJULISHA AU KUMPA TAARIFA NDUGU, RAFIKI N:K.
MAENEO HATARI KATIKA MAONYESHO HAYO NI YALE YENYE MKUSANYIKO WA WATU WENGI IKIWEMO ENEO LA MABEMBEA NA ENEO LILILOTENGWA KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO MAARUFU KAMA WAMACHINGA JIRANI NA BANDA LA JKT

ALIYEUZA MVINYO BANDIA AFUNGWA JELA NCHINI MAREKANI



Bwana Kurniawan alipatikana na hatia ya kuuza Mvinyo bandia wenye thamani ya dola milioni 20
Mwanamume aliyewalaghai watu kwa kuwauzia mvinyo bandia, Rudy Kurniawan, 37, amefungwa jela kwa miaka kumi na kuamrishwa kulipa faini ya dola milioni 20 kwa kosa hilo.
Rudy aliuza Mvinyo ghushi wenye thamani ya mamilioni ya dola bila ya kujulikana kwa miaka mingi.
 
Pia ameamrishwa kulipa dola milioni 28.4 kwa waathiriwa wanaojumuisha tajiri William Koch.
Bwana Kurniawan ni mtu wa kwanza kuwahi kwenda jela kwa kuuza mvinyo bandia nchini Marekani.
Alipatikana na hatia ya kuchanganya mvinyo wa zamani na mvinyo wa mpya nyumbani kwake. Baada ya kuinchanganya aliuza Mvinyo huo kwa bei ghali mno akidai kuwa ni Mvinyo wa kipekee.
Vibandiko bandia alivyotumia bwana Kurniawan kuwahadaa waekezaji kununua bidhaa zake vilipatikana nyumbani kwake.
Kashfa hii aliifanya tangu mwaka 2004 hadi 2012 kulingana na viongozi wa mashitaka.
Mwezi Disemba alipatikana na hatia ya kuwalaghai watu kwa nja ya posta.
Kama raia wa Indonesia, Bwana Kurniawan atarejeshwa nchini Indonesia ili akafunguliwe mashitaka huko. Tayari amekuwa jela kwa miaka 2 tangu kukamatwa mwaka 2012.
Mnamo mwaka 2006, inaaminika kwamba aliuza chupa 12,000 za mvinyo bandia katika mnada.
Lakini maafisa wakuu walisema kuwa walipata maelfu ya vibandiko vya mvinyo mzuri zaidi wa Burgundy na Bordeaux pamoja na chupa ambazo hazikuwa zimwekwa vifuniko nyumbani kwake

Al QAEDA WAUA 14 YEMEN




Wanajeshi wa Yemen


Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Qaeda kusini mashariki mwa Yemen wamewateka na kuwaua takriban wanajeshi 14 waliokuwa wakirudi nyumbani kutoka kazini mashariki mwa taifa hilo.

Wanajeshi hao walidaiwa kuwa katika likizo wakati basi lao liliposhambuliwa na wanamgambo hao kabla ya kutekwa nyara.

Maafisa katika eneo hilo wanasema kuwa walipata miili yao saa chache baadaye karibu na mji wa Sieyoun katika mkoa wa Hadramout.

Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wanajeshi wa serikali ya Yemen yanayotekelezwa na wanamgambo wa kundi la Al Qaeda(Tukuo)

NYANI MPIGA PICHA AZUA UTUTA WA KISHERIA


Mmiliki wa kamera iliyotumiwa na Nyani kujipiga picha anasema picha hiyo ni yake
Mtandao wa Wikipedia umekataa kufuta picha ambayo Nyani ilijipiga ikisema kuwa kwa sababu picha hiyo ilipigwa na Nyani ambaye ni mnyama wala sio binadamu, basi inakuwa mali ya umma.
Hii ni baada ya mpiga picha, mmiliki wa kamera iliyotumika na Nyani huyo kujipiga picha, kusihi Wikipedia kufuta picha hiyo na kudai kuwa Wikipedia ilikuwa inaingilia haki zake za umiliki wa picha hiyo.
Mpiga picha, David Slater, alikuwa akijaribu kunasa picha za Nyani kwa masaa kadhaa, wakati ambapo Nyani mmoja alichukua mojawapo ya kamera za David na kujipiga mamia ya picha.
Picha hiyo aliyojipiga Nyani bila shaka ni ya kusisimua na imempelekea David kuwa maarufu ulimwengu mzima.
La kusikitisha ni kuwa hatimaye Slater sasa amejikuta katika mvutano wa kisheria na Wikimedia kuhusiana na ni nani hasa mmiliki wa picha hiyo.
David, ambaye hutegemea upiga picha kama jinsi moja ya kujikimu kimaisha, yuko makini kuhakikisha picha hiyo imeondolewa kwa tovuti ya Wikipedia mara moja, huku Wikipedia ikidai kuwa iwapo kuna mmliki wa picha hiyo basi ni Nyani aliyejipiga picha hiyo.
Mvutano wa kisheria ilirejelewa kuangaziwa kufuatia uamuzi wa Wikipedia kuchapisha maombi yote iliyopata kuhusu kufuta au kuhariri habari au picha au video zozote ilizoweka kwenye tovuti zao.
Mojawapo ya maombi hayo ni David Slater kutaka picha aliyojipiga Nyani kuondolewa kwenye tovuti ya Wikipedia mara moja kwani ikiwa kwenye tovuti hiyo iko wazi kwa umma

WATU SITA WAUAWA KWENYE GHASIA SOMALIA


Wapiganaji wa Al-shabaab

Takriban watu sita wameuawa katika ghasia katikati mwa Somali.

Ijumaa usiku, wanamgambo kutoka kundi la Alshabaab walishambulia kambi moja ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji wa Buloburde, yapata kilomita 200 kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Vikosi vya Amisom viliuteka mji wa Buloburde kutoka kwa Alshabaab mapema mwaka huu, lakini wanamgambo hao bado wanadhibiti eneo kubwa la viunga mwa mji huo.

Wameendelea kutekeleza mashambulizi mjini Mogadishu ili kujaribu kuiondoa serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa.(TK)

EBOLA NI JANGA LA KIMATAIFA -WHO


Idadi ya watu waliofariki kutokana na Ebola Afrika Magharibi inasemekana kufika 900

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura.

WHO imesema kuwa mataifa yalio na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa kimataifa.

Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Geneva kuhusu uwezekano wa kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari zaidi.

Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika .

Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia visa vimeripotiwa nchini Nigeria

SHUGHULIKA


Nipende kuwashukuRu vijana wenzangu na hasa kwa wale wanaopenda kusoma makala zangu.Tuzidi kuombeana uhai. leo napenda kuongelea kuhusu swala la kujishugulisha ambalo wengi limekuwa likiwasumbua sana hasa kwa sisi vijana. Nimekutana na vijana wengi ambao wamemaliza Masomo yao wakiwa na matumaini ya kupata kazi kubwa na kukaa maofisini lakini kwa bahati mbaya wakawa bado hawajapata kazi na kuhisi labda wana tatizo. Ukweli ni kawaida kwa mambo kama hayo kutokea kwa sababu kwa sasa hivi kila mtu anatafuta kazi na wengi hupenda kazi zenye mishahara
Mikubwa. Tunaishi katika kipindi ambacho mashindano na ubinafsi umekua wa kasi sana kwa sababu wengi huwapa kazi ndugu jamaa na marafiki hata kama hawana vigezo vya kutosha.
 

MAREKANI YATUMIA NDEGE KUPAMBANA NA WANAMGAMBO WA IS NCHINI IRAQ

Ndege za Marekani zilizotekeleza mashambulizi dhidi ya IS
Wizara ya ulinzi nchini Marekani inasema kuwa ndege za jeshi la Marekani zimefanya mashambulizi ya angani dhidi wanamgambo wa kundi la Islamic state kaskazini mwa Iraq. Pentagon ilisema kuwa ndege zilishambulia vituo vilivyokuwa vikitumiwa kushambulia vikosi vya kikurdi vinavyopigana kulinda ngome ya mji wa mji wa Irbil. Siku ya Alhamisi rais wa marekani Barack Obama aliamrisha kufanyika kwa mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa kisuni ambao wameteka kiasi kikubwa cha ardhi ndani ya Iraq na pia ndani ya Syria.
Jamii ya Yazidi inayolengwa na IS

Rais Obama alisema kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State watalengwa iwapo wataelekea kwenye mji wa kikurdi wa Irbil au kwa lengo la kuzuia kile alichokitaja kama vitendo vya mauaji ya halaiki dhidi ya wakristo na jamii za Yazidi.

Hatua ya Marekani inajiri kukiwa na wasiwasi mkubwa wa uwezo wa wanamgambo hao kuteka sehemu kubwa zaidi ya Kaskazini mwa Iraq mbali na sehemu kubwa ya Syria.

Rais Obama amewashutmu wanamgambo wa Islamic State kwa kujaribu kuiangamiza jamii nzima na ya Yazidi akisema kuwa serikali yake itachukua hatua za kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki.
Wapiganaji wa Kikurdi wanaokabiliana na IS

Ndege za jeshi la marekani zimekuwa zikiangusha misaada huku nayo Uingereza ikisema kuwa itajiunga kwenye jitihada za kutoa misada.

Kiongozi wa dhebu la shia nchini Iraq Ayatollah Ali al Sistani amewataka wanasiasa nchini Iraq kungana na kumaliza ghasia huku naye kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis akisema kuwa atatuma mmoja wa viongozi wa kanisa hilo kama njia ya kuonyesha umoja .

Mnamo mwezi juni IS, awali ikijulikana kama Isis, iliteka mji wa Mosul kisha kundi hilo likauteka mji wa wenye wakristu wengi Qaraqosh.
Wakimbizi wa ndani kwa ndani Iraq

Kulingana na Idara ya usalama ya Marekani Pentagon ndege mbili za F/A-18 zilidondosha mabomu yenye paundi 500 ilikukaharibu ngome ya mashambulizi ya IS inayotumika kuishambulia mji wa Irbil.

Mji huo wa Irbil ni mwenyeji wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani.

Hii ndiyo mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kujihusisha katika mapigano ndani ya Iraq tangu mwaka wa 2011.

Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry ameonya jamii ya kimataifa kugutuka na kutahadhari dhidi ya ufanisi wa kundi hilo la wanamgambo wa IS.
CREDIT:BBC

BREKI ZAFELI NA KUONGEZEWA SHITAKA

NOUMER SANA
Kijana huyu akiwa anapelekwa mahakamani
 
Kijana mmoja aliyekuwa na kesi ya jinai mahakamani, amejikuta akiongezewa mashtaka baada ya kuulizwa maswali magumu sana na hakimu ana hatimaye akajikuta breki zimefeli na kuachia ushuzi mkubwa uliofanya mpka watu walioenda kusikiliza kesi ile kutoka nje na kuondoka kabisa mahakamani. Habari za kimahakama zinasema kuwa aliongezewa shtaka