Jumamosi, 28 Februari 2015

CC YAWASIMAMISHA TIBAIJUKA, CHENGE NA NGELEJA



KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo;Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.
Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.
CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.
Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.
> Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow ambao ni Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja na Mheshimiwa Andrew Chenge.

Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa kuhusika kwao katika kashfa hiyo.

> Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa Kamati Kuu.

AZAM NJE LIGI YA MABINGWA YACHEZEA KICHAPO CHA 3-0

AZAM YANG’OLEWA CAF, YACHAPWA 3-0

Azam FC imeng’oka katika michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh.
Azam FC ilishinda kwa mabao 2-0 jijini Dar, hivyo kufanya ing’oke kwa jumla ya mabao 3-2.
Katika mechi iliyochezwa leo jijini Khartoum, Sudan, Azam FC ilianza kukubali bao katika dakika ya 11 mfungaji akiwa Coffie.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza na ilikuwa ni kuhakikisha Azam wanakomaa hadi mwisho, lakini ikashindikana.
Merreikh ilipata mkwaju wa penalti kutokana na faulo ya Serge Wawa, lakini ikakosa.

MCHINJAJI WA IS NI MWINGEREZA

Mwanamgambo anayejulikana kwa jina la utani 'Jihadi John' wa kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la dola la kiislamu IS, ambaye amekuwa akionekana katika video akiwachinja mateka ametambuliwa kama Mohammed Emwazi
Mohammed Emwazi ni raia wa Uingereza, mtaalamu wa masuala ya programu za kompyuta anayetokea familia inayojiweza iliyoko mjini London na alikuwa akifahamika na maafisa wa usalama nchini Uingereza hata kabla ya kuelekea Syria.
Mwanamgambo huyo ambaye huonekana katika video za kundi la IS akiwa amevalia nguo nyeusi na kuufunika uso wake, kushikilia kisu na kuzungumza kizunguchenye lafudhi ya Kiingereza anaaminika kuwa mchinjaji wa mateka wa kundi hilo wakiwemo raia wa Marekani, Uingereza na Syria.

MAN U YAUNGURUMA

Wayne Rooney akipiga penati iliyozaa goli 
Mkwaju wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidia Manchester United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu.
Rooney alifunga baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya pingamizi kutoka kwa mashabiki.
Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.
Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
Matokeo mengine:
West Ham 1 - 3 Crystal Palace
Burnley 0 - 1 swansea
Newcastle 1 - 0 Aston Villa
Stoke 1 - 0 Hull
West Brom 1 - 0 Southampton

MWANASIASA MAARUFU AUAWA NCHINI URUSI

Boris Nemtsov kiongozi wa upinzani mwenye heba na mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin wa Urusi ameuawa kwa kupigwa risasi karibu na Ikulu Moscow Ijumaa usiku. (27.02.2015).
Boris Nemtsov mwanasiasa mashuhuri wa upinzani aliyeuwawa Urusi. Boris Nemtsov mwanasiasa mashuhuri wa upinzani aliyeuawa Urusi.
Kifo chake kinakuja siku moja kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika dhidi ya serikali hapo Jumapili ambapo alikuwa akitazamiwa kuhudhuria.
Kifo cha Nemtsov, mwenye umri wa miaka 55 naibu waziri mkuu wa zamani, kimezusha hasira miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wameishutumu serikali ya Urusi kwa kujenga hali ya kutovumilia upinzani wowote na kuyaita mauaji hayo ni ya kukusudia.
Rais Putin haraka alituma salamu zake za rambi rambi na kuyaita mauaji hayo kuwa ni ya uchokozi.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Boris Nemtsov baada ya kupigwa risasi na kuuwawa mjini Moscow. (28.02.2015)
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Boris Nemtsov baada ya kupigwa risasi na kuuawa mjini Moscow. (28.02.2015)

MHE WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA ZA WATUMISHI MBEYA

Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo. mi2 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo, Mbeya. mi4 
mi8Mojawapo ya nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Busokelo zinazojengwa na NHC kama zinavyoonekana leo. mi9 
Bango la Kumkaribishs Waziri Mkuu mi10 
Msoma Hotuba wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. Sanga akisoma hotuba hiyo mbele ya Waziri Mkuu leo. mi11 
M mi13 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo.
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wialaya ya Busokelo. mi15 
Baadhi ya Watendaji wa NHC na viongozi wa Wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya wakiwa wamejipanga kumkaribisha Waziri Mkuu mi16 
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akikaribishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya wakati akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mbeya. mi18 
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na Mbunge wa Rungwe Mashariki , Profesa Mark Mwandosya katika eneo la nyumba za gharama nafuu za watumishi za Busokelo, Mbeya zinazojengwa na Shirika hilo kabla ya kuwekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda.mi19 
Baadhi ya Wafanyakazi wa NHC wakifuatilia uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi huo wa nyumba za watumishi wilayani Busokelo. mi20Wafanyakazi wa NHC Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya shughuli ya uwekaji jiwe la msing

MHE WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA MBEYA

Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo. 

BREAKIN NEWZZZZ: MHE JOHN KOMBA AMETUTOKA

 


Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.

Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi itatangazwa baadaye

YANGA YASONGA MBELE LICHA YA KUFUNGWA NA BDF

DSC_0863-794466
Dk 29, Ngassa analiifungia Yanga bao safi kwa kichwa cha kuchupa baada ya basi nzuri ya Amissi Tambwe aliyeuwahi mpira alioutema kipa wa BDF. 
 
Kipindi cha pili BDF XI walirudi na moto na kufanikiwa kuwabana Yanga na kurudisha bao na kuongeza la pili lakini na matokeo kusomeka mwisho wa mchezo 2-1. 
 
Kwa kuwa Yanga wanafaida na bao la ugenini na pia ushindi wa 2 bila majibu walioupata Tanzania katika mchezo wao wa Tanzania uliwahakikishia kuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano. 
 
Kwa hiyo kwa matokeo hayo Yanga wanasonga mbele kwa kuwa na magoli 3  kwa mawili ya BDF XI.
 
Habari zilizotufikia hivi punde timu hiyo itarejea kesho kupitia Nairobi

Agriculture

  • Soil has vital nutrients for plants. As a result, it is used in agriculture to nourish plants. The roots of a plant receive nutrients from the soil to help it grow. The North Carolina Department of Agriculture and Consumer Services notes that 13 essential plant nutrients come from the soil.

Building

  • Soil is an important part of the building process. Soil compaction, which increases the density of the soil, is done as part of the building process. The purpose of the compaction is to improve the load support. If not done, structural failure can result. Soil can also be used as building materials such as adobe and red bricks.

Pottery

  • Clay soil is used in making ceramics, or pottery. When water is added to clay soil, it can be used to create the ceramics. Once formed, you can leave it to dry and it will retain its shape. Any type of ceramic can be created with the clay soil, such as a vase, bowl, cup or sculpture.

Medicine

  • Soil is commonly used in antibiotics. Microbes created in the soil are harmful to bacteria, which is why soil is used in medicine. Medicines created by soil include skin ointments, tuberculosis drugs and anti-tumor drugs.

Beauty Products

  • Some beauty products are made with soil. Commonly used beauty products where used soil is used in the production include blush and foundation. Soil rich in clay can also be used in facial masks and toothpastes.


Read more : http://www.ehow.com/info_10057531_5-uses-soil.html

Ijumaa, 27 Februari 2015

MBUNGE KWEIGYIR AMFARIJI MAMA WA YOHANA

Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amemtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino, Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.
Katika ziara hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crecencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport Financial Services mkoani Mwanza. Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Esther ambaye ni mama mzazi wa hayati Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.
Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau, hususan wale wenye ulemavu wa ngozi wakiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.
Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki ambao ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir kulia akiwa na Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari wakimpa pole mama mzazi wa Yohana ambaye alikuwa ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

BINTI AANZA CHUO KIKUU NA MIAKA 10

estaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa 
Kipaji cha mtoto huanza kuonekana taratibu wakati anaendelea kukua, mara nyingi wazazi huwa wanakua wa kwanza zazi ndio wakati wa kutambua mwanaye anataka nini kwa
maisha yake ya baadaye lakini kipaji cha mtoto Esther Okade kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja.
Unaweza usiamini lakini huu ni ukweli, Esther ambaye ana umri wa miaka 10 amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha Uingereza miezi mitatu iliyopita akisomea shahada ya hesabu.
Eshte
Mtoto huyo ambaye anatokea katika mji wa Walsaw uliopo Midlands, Uingereza sio mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake, mdogo wake wa kiume mwenye miaka sita anasoma masomo ya kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
MOM
Esther akiwa na mama yake mzazi, Ife
Pamoja na Esther kudahiliwa miezi mitatu iliyopita ameonekana kufanya vizuri kuzidi wenzake darasani.
Mama yake Esther aitwaye Ife anasema kitendo cha mwanae kujiunga chuo kikuu kilikuwa la kushangaza kutokana na umri wake kuwa mdogo lakini mwenyewe alijiamini na kuona anaweza.
YOUNG
Esther akiwa na mdogo wake Isaya
Tangu akiwa na miaka saba alikuwa na shauku ya kujiunga na chuo kikuu ili atimize ndoto zake, alikua na kipaji cha aina yake darasani na baada ya miaka mitatu aliuliza tena ikabidi tumpeleke ili kuona kama kweli atamudu“– amenukuliwa Ife, mama wa Esther.
Historia inaonyesha kuwa Esther ni wa kwanza kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri mdogo ingawa mtoto aitwaye Ruth Lawrance alijiunga na chuo kikuu cha Oxford mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 12 na kuhitimu mwaka 1985 (baada ya miaka miwili tu). Baadaye alisoma shahada nyingine ya kwanza ya fizikia kabla ya kusomea PhD ambayo aliimaliza akiwa na umri wa miaka 17. Kwa sasa Ruth ni Profesa wa mahesabu katika chuo Kikuu cha Hebrew Univeristy of Jerusaleem.

Jumatano, 25 Februari 2015

POLISI YASHIKILIA VIJANA 5 WAHITIMU WA JKT

http://www.jukwaahuru.com/wp-content/uploads/2013/06/askari-1200x545_c.jpg Picha: Jeshi la Kujenga Taifa likionesha ukakamavu wao hivi karibuni -  Maktaba.  
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia vijana watano wa kundi la wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za kufanya uchochezi na kufanya mikusanyiko isiyo halali jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema vijana hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti kwa makosa ya kuunda kikundi kisicho halali kwa mujibu wa sheria za nchi na kuwahamasisha wenzao, kuandamana hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira za kudumu.

SUAREZ APIGA 2 BARCA IKIIGARAGAZA CITY KWAO

 
Luis Suarez akifunga bao
Barcelona imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora. Barcelona imeshinda kwa mabao hayo ugenini dhidi ya wenyeji wake Manchester City huku Luis Suarez akiwa shujaa kwa kufunga mabao yote mawili. Lionel Messi alipata nafasi ya kufunga mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa na Zabaleta katika dakika ya 90 lakini Joe Hart akaokoa, mpira ukamrudia Messi, akakosa.
Sergio Aguero ndiye alifunga bao pekee la Man City, akionyesha juhudi binafsi na kufanikiwa kufunga bao tamu kabisa.

TEVES ANG'ARA ATUPIA GOLI MOJA JUVE 2 DORTMUND 1

Carlos Tevez ameendelea kuwa mtamu zaidi ya Mcharo baada ya kuingoza Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 Bora.
Tevez ndiye alifunga bao la kwanza huku Alvaro Morata akitupia la pili.
Marco Reus alifunga bao pekee la Dortmund waliokuwa ugenini hivyo kufanya mabao yote ya mechi hiyo kuwa yamefungwa katika kipindi cha kwanza.
Tevez alikuwa mwiba kwa mabeki wa Dortmund, hata hivyo walijitahidi kuhakikisha hawafungwi mabao mengi zaidi.

WANANCHI WAFUNGA BARABARA ILULA IRINGA

Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo.
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.

WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.

RAIA 100 WA ETHIOPIA JELA NCHINI KENYA

Raia mia moja wa Ethiopia wakifuatilia kesi yao mahakamani leo hii
Raia mia moja wa Ethiopia hii leo wamehukumiwa kifungo cha miezi kumi na mbili gerezani nchini Kenya au walipe faini ya takriban dola 600 baada ya kupatikana na hatia ya kuwemo Kenya kinyume na sheria.
Polisi waliwakamata wahamiaji wao haramu siku ya Jumatatu katika mtaa mmoja mjini Nairobi. Maryam Dodo Abdalla anaarifu zaidi.

WAKRISTO WANA HALI MBAYA SYRIA

Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kaskazini mwa Syria.
Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake, watoto na wazee.
Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka.
Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha.
Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristo hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza.
 
Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi
Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristo kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.
Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini wametekwa.
Huku hayo yakiarifiwa waumini wengine wa kikristo wameanza kukimbia vijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na washirika wao wa kikristo katika mji wa Hassaka.

CHENGE AKATAA KUHOJIWA NA BARAZA LA MAADILI KTK SAKATA LA ESCROW

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi katika Bunge Maalum la Katiba (BMK) Andrew Chenge akitoka katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
...Akihojiwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio.

UTAMADUNI MWINGINE HAUFAI: NDUGU KUKATWA VIDOLE KILA AKIFIWA

Utamaduni wa watu duniani unatofautiana, moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya huu utamaduni wa jamii ya watu wa Dani iliyoko Magharibi mwa Papua, New Guinea ambapo utamaduni wao unahusisha inapotoke msiba wa ndugu yoyote basi ndugu wa marehemu wanaomboleza kwa kujikata vidole.Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale waliobahatika kuitembelea basi ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka jamii hiyo wamekatwa vidole na ndugu yoyote wa marehemu anakatwa vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa sana hivyo hata watoto pia wanaguswa na hii moja kwa moja.

Utaratibu huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa marehemu.