Wanasayansi
wanasema kuwa wamegundua kile wanaamini kuwa ni mti mrefu zaidi barani
Afrika. Mti huo uko bonde moja lililo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania.
Wanasayansi
kutoka chuo cha Bayreuth nchini Ujerumani, wanasema wanaamini kuwa mti
huo unaopatiknan karibu na mlima Kilimanjaro ndio mrefu zaidi barani.
Mmoja
wa wanasayansi hao alisema kuwa aliona mtu huo miaka 20 iliyopita,
lakini ni hadi hivi majuzi wakitumia vifaa maalum walifaulu kupima urefu
wake.
Mti huo kutoka familia ya Entandrophragma excelsum una urefu wa mita 81.
Wanasayansi nchini Tanzania bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusu ugunduzi huo.
Wanasayansi waliogundua mti huo sasa wanataka ujumuishwe kwenye kumbukumbu ya miti isiyo ya kawaida duniani
Rais wa Brazil Michel Temer atangaza siku tatu za
maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya wachezaji vilivyosababishwa na
ajali ya ndege.
Rais wa Brazil Michel Temer ametangaza siku tatu za maombolezo ya
kitaifa kufuatia vifo vya wachezaji wa timu ya soka ya Chapecoense,
ambao walikuwa miongoni mwa abiria 81 waliokuwemo kwenye ndege
iliyoanguka kwenye milima ya Colombia jumatatu hii, na kusababisha vifo
vya abiria 76, na wengine watano kunusurika.
Ndege hiyo ndogo ya
shirika la ndege la LAMIA awali ilitoa taarifa ya hali ya hatari
iliyosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa umeme, na hatimaye kuanguka
muda mfupi baadaye karibu na mji wa Medelin.
Ndege hiyo ilikuwa
imebeba wachezaji wa timu ya Chapecoense Real ya Brazil, iliyokuwa
ikielekea kucheza mechi ya fainali ya michuano ya kuwania ubingwa wa
kombe la Amerika ya Kusini (Copa Sudamericana) ambayo ni ya pili kwa
ukubwa katika Bara la Amerika ya Kusini, iliyotarajiwa kuchezwa kesho
jumatano dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.
Rais wa Brazil, Michel Temer ametoa siku tatu za maombolezo ya wahanga wa ajali hiyo
Pamoja
na Rais Temer kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kumeendelea
pia kutolewa rambirambi kutoka kona mbalimbali Barani Ulaya, ambapo
Rais wa shirikisho la soka duniani, FIFA, Gianni Infatino amesema, "
Hili ni tukio la kusikitisha sana kwenye anga la soka, na limetokea
katika kipindi kigumu. Mawazo yetu yapo kwa wahanga wa ajali hiyo,
familia na jamaa zao" amesema Infatino. FIFA inatoa pole kwa mashabiki
wa Chapecoense, jumuiya ya soka na vyombo vya habari vya nchini Brazil.
Mmoja
wa wajumbe wa bodi ya timu hiyo, Plinio De Nes, amesema wachezaji hao
waliiaga bodi wakisema wanaenda kutimiza ndoto yao waliyoiota kwa muda
mrefu.
Mshambuliaji wa timu ya Colombia Radamel Falcao, yeye
ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter akisema, "maombi yangu ni kuwa
na mshikamano na manusura, familia na jamaa ya wachezaji hao katika
kipindi hiki kigumu."
Timu ya Atletico Madrid, nayo imetuma
salamu za pole kupitia Twitter, ikiandika, "Tumeshtushwa sana na ajali
hiyo inayohusisha klabu ya mchezaji mwenzetu wa zamani, Cleber Santana
ambaye kwa sasa alikuwa ni kapteni wa timu hiyo ya Chapecoense, "salamu
zetu za pole ziwafikie familia zao. Pumzikeni kwa amani.
Rais wa FIFA, Gianni Infatino amesema ajali hiyo imetokea katika kipindi kigumu
Mawazo
ya kila mmoja wa Manchester United yapo kwa wahanga wa ajali ya ndege
wa timu ya soka ya Chapecoense na wale wote walioathirika na janga hilo
la Colombia, imeandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa timu ya Manchester
United ya Uingereza, ambayo nayo iliwahi kupoteza wachezaji wanane mnamo
mwezi Februari mwaka 1958, wakati ndege yao ilipoanguka ikiwa inaondoka
kutoka uwanja wa ndege wa Munich.
Timu ya Real Madrid, kupitia
tovuti yake, nayo imeeleza kusiktitishwa kwake na tukio hilo, na kutoa
salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa wahanga hao, huku pia ikiwatakia
kuimarika kwa haraka afya za majeruhi wa ajali hiyo. mawazo yetu yapo
pamoja na Chapecoense na kila mmoja aliyeguswa na ajali hii na familia
zao, hatuna neno la kuongeza, ameandika kapteni wa Real madrid, Sergio
Ramos, kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Timu za FC Barcelona, AS Roma na FC Porto nazo zimetuma salamu za pole kupitia kurasa za Twitter, kutokana na ajali hiyo.
Wachezaji
tisa wa timu hiyo hawakusafiri. Ndege hiyo hiyo iliwabeba wachezaji wa
timu ya Argentina wiki mbili zilizopita ikiwa na mchezaji Lionel Messi
walipokuwa wakielekea san Juan Argentina kwa ajili ya mechi ya kufuzu
kucheza kombe la dunia. Mwandishi: Lilian Mtono/ http: AFPE/ APE/ //www.dw.com/en/plane-crash-kills-76-in-colombia-6-survive/a-36565336. Mhariri: Saumu Yusu
Huku maeneo mengi
ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa kupita kiasi,
Uholanzi ina tatizo tofauti. Uhaba wa wafungwa.
Katika kipindi
cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake na mengine
zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili liliwezekana - na kwa
nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya
kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya mahabusu na katika
jengo zima. Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao cha jioni. Mwanamume
mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliyofungwa juu.
"Hawawezi
kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel,
naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko
kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "
"Lakini wanaweza kuazima visu vidogo vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini."
Baadhi
ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba
watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni
moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya
kawaida mara baada ya kufunguliwa
"Katikka magereza ya Uholanzi tuanaangalia kila mmoja," anasema Van der Spoel.
"Kama
mtu fulani ana matatizo ya mihadarati tunatibu hali yake, kama ni wenye
hasira tunawapatia ushauri wa kudhibiti hasira zao , kama wana matatizo
ya pesa tunawapatia ushauri nasaha. Kwa hiyo tunajaribu kuondoa kile
kinachosababisha mtu afanye uhalifu . Mfungwa mwenyewe lazima awe na
utashi wa kubadilika lakini njia yetu imewafaa sana. Kwa zaidi ya miaka
10 , kazi yetu imeboreka zaidi na zaidi.''
Wafungwa wanaofuata
maelekezo hatimaye hupewa kifungo cha miaka miwili na msururu wa mafunzo
katika mpango wa kuwarejesha katika hali ya kawaidi . Chini ya 10%
hurejea gerezani baada ya kuachiliwa huru.
Hewa safi ni muhimu kwa
hiyo wafungwa huruhusiwa kutembea wakisindikizwa hadi maktaba , kwenye
kliniki ama mgahawa na hilo huwasaidia kuendelea na maisha ya kawaida
punde wanapomaliza kifungo cha gerezani.
Muongo mmoja uliopita Uholanzi ilikuwa ni mojawapo
ya nchi zenye kifungo cha muda mrefu zaidi barani Ulaya, lakini sasa
inadai kuwa nchi yenye wafungwa wachache zaidi, yaani wafungwa - kati
ya watu 100,000 , ikilinganishwa na wafungwa 148 Uingereza na Wales.
Lakini
mpango wa kutoa ushauri nasaha si sababu pekee iliyosababisha kupungua
kwa watu katika magereza ya Uholanzi - kutoka wafungwa 14,468 mwaka
2005 hadi wafungwa 8,245 mwaka jana - kiwango hicho kikiwa sawa na
asilimia 43.
Kupungua zaidi kwa idadi hiyo mwaka 2005
kulisababishwa kwa sehemu kubwa na kuboreshwa kwa upekuzi katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Amsterdam-Schiphol, ambako kulisababisha
kubainika kwa idadi ya wauzaji wa mihadarati kukamatwa wakiwa wamebeba
cocaine.
Angeline van Dijk, Mkurugenzi wa huduma za magereza
nchini Uholanzi, anasema magereza sasa yanatumiwa kuwahifadhi wale ambao
ni hatari sana kuachiliwa, ama wahalifu waliomo hatarini wanaohitaji
usaidizi wakiwa ndani ya gereza.
"Wakati mwingine ni vyema kwa
watu kukaa katika kazi zao, wakae na familia na kufanya adhabu kwa namna
nyingine," anasema kulingana na uzoefu wake wa kazi hiyo.
"Tuna
hukumu za muda mfupi za gerezani na kupunguza viwango vya uhalifu hapa
Uholanzi, kwa hiyo hili linaacha magereza yetu kuwa matupu ."
Mojawapo
ya gereza lililokosa watu liligeuzwa kuwa Hoteli ya kifahari kusini
mwa mji wa Amsterdam, ni hoteli ya nne kwa kuwa ghali, ikipewa majina
... The Lawyer, The Judge, The Governor na The Jailer.
Lakini mengine yaligeuzwa kuwa vituo vya kuwapokea wahamiaji, na kutoa ajira kwa baadhi ya walinzi wa zamani wa magereza.
Azma ya kulinda ajira za magereza imetoa suluhu ya kushangaza - kuletwa kwa wafungwa wa kigeni kutoka nchi za Norway na Ubelgiji
Waziri mkuu wa
jimbo la Telangana nchini India amezua hisia baada ya kuhamia katika
nyumba mpya inayogharimu walipa kodi dola milioni 7.3.
Jumba hilo lina ukubwa wa mita 9,000 mraba katika mji wa Hyderabad. Jumba hilo lina vyoo vilivyo na uwezo wa kukinga
risasi kuingia, ukumbi ulio na viti 250 na eneo la mikutano linaloweza
kuingiza watu 500. Jumba hilo lilibarikiwa na mshauri wa maswala
ya kidini wa waziri huyo huku choo hicho kinachoweza kuzuia risasi
kuingia kikifanyiwa masikhara.
Alana Annette Savell aliwafyatulia risasi wageni wake
Mwanamke mmoja
katika jimbo la Florida nchini Marekani, aliwafyatulia risasi wageni
waliokuwa wamemtembelea kwa sababu walikuwa wamekaa sana na walikuwa
wanapiga kelele, polisi wanasema.
Alana Annette Savell, 32,
alikuwa mwenyeji wa wageni hao wawili, wapenzi, katika jiji la Panama
pale walipoanza kupiga kelele sana. Polisi wanasema aliwaamrisha kuondoka kutoka nyumbani kwake, kabla ya kuwapiga risasi miguuni. Walijipeleka hospitalini wakiwa na majeraha, ambayo hayakuwa mabaya sana. Bi Savell ameshtakiwa kwa kuwashambulia watu akitumia bunduki. Ofisi
ya Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Bay iliiambia BBC kwamba mwanamke
huyo kwa jina Kristy Jo Mohr alikuwa amefika na mpenzi wake, ambaye
walikuwa wamekutana kwenye baa, nyumbani kwa mshtakiwa mwendo wa saa
saba usiku Jumatatu.
Wanafunzi kadha wa shule moja
eneo la Sichuan, China wamepata ngazi mpya kuwasaidia kupanda na kushuka
urefu wa mita 800 kufika na kuondoka shuleni.
Kijiji cha Atuler kimepewa
jina la utani "kijiji cha mwamba". Kijiji hiki hupatikana mita 800 juu
kwenye nyika eneo la Sichuan, China. Wanaoishi hapa ni watu wa jamii ya
Yi, ambao pia hupatikana Vietnam na Thailand.
Hadi kufikia sasa, kulikuwa
na ngazi 17 za mbao ambayo ilikuwa njia pekee ya wakazi wa kijiji hiki
kutoka nje ya kijiji chao. Kupanda ngazi hizi lilikuwa jambo hatari na
watu zaidi ya saba walifariki wakizikwea, wakazi wanasema.
Watoto karibu 20 kutoka
kijiji cha Atuler husomea shule ya bweni, na ndipo waweze kufika
hutakiwa kushuka kwa kutumia ngazi hiyo. Wakati wa likizo, shule
zinapofungwa, hutakiwa kupanda ngazi tena kurejea kijijini.
Sasa, ngazi ya chuma
imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa
muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua.
Watu wa jamii ya Yi wanaoishi
Atuler wamekuwa wakikwea mwamba huo kwa miaka na mikaka na wana hata
kanuni za kupanda. Wakati wa kupanda, wanaume wanawajibika kuwabeba na
kuwatunza watoto. Watoto wa chini ya miaka 16 hawaruhusiwi kupanda au
kushuka kwenye ngazi hiyo wakiwa peke yao.
Ngazi hiyo ya chuma ilijengwa
baada ya habari za kijiji hicho kugonga vichwa vya habari kimataifa
mwezi Mei. Ingawa wengi wanasifu ujenzi wa ngazi hiyo, wapo watu
wanaoshangaa ni kwa nini wanakijiji hao hawawezi kuhamia eneo
linalofikiwa kwa urahisi. Lakini wakazi waliambia wanahabari China
kwamba hawataki kuacha nyumba zao, hasa kuhamia mijini ambapo maisha
wanaamini ni magumu sana.
Bennie Hart anasema alitumia nambari hiyo ya usajiri wa gari akiwa Ohio bila shida zozote
Mmarekani
asiyemtambua Mungu amewashtaki maafisa katika jimbo la Marekani la
Kentucky baada ya kukataliwa kuweka neno "IM GOD" ama '' MIMI NI
MUNGU'' badala ya namba za ya gari lake za usajili.
Bennie Hart
anasema nia ya kuweka maneno hayo kwenye pango la nambari ya gari lake
ni kuonesha kuwa inawezekana kumkosoa yeyote anayedai kuwa ni Mungu. Lakini
wakuu wa uchukuzi katika jimbo hilo lenye kukaliwa na watu wenye imani
kali za kidini wameamuru kuwa maneno hayo yanaweza kupoteza umakini wa
madereva wengine na kwamba hayapendezi. Wanaharakati wa uhuru wa kujieleza wamelivalia njuga suala hilo na sasa wanaunga mkono kesi ya Bwana Hart. Anasema alikuwa na namnbari hiyo hiyo ya gari alipokuwa akiishi katika jimbo la Ohio kwa miaka 12 bila matatizo. "Ninataka tu fursa sawa ya kuchaguza ujumbe wa mtu kwa ajili ya nambari
ya usajili kama tu dereva mwingine yeyote yule ,"alisema Bwana Hart,
anayeishi katika kaunti ya Kenton, Kaskazini mwa Kentucky. "
Hakuna matusi yoyote ama lugha isiyokubalika kuhusu maoni yangu kwamba
imani za kidini zinategemea namna mtu binafsi anavyoelewa. Muungano
wa Marekani unaopigania uhuru wa kujieleza huko Kentucky (ACLU-KY) na
wakfu wa uhuru wa kuabudu wamewasilisha kesi kwa niaba ya Bwana Hart
dhidi ya katibu wa mamlaka ya uchukuzi ya jimbo Greg Thomas kuhusu
uhuru wa kujieleza
Mwanamume nchini Japan amefariki siku tatu baada yake kusongwa na wali wakati wa shindano la kula kwa kasi.
Mwanamume mmoja, ambaye jina lake halijatolewa, alizimia wakati wa shindano hilo
eneo la Hikone, Shiga mnamo 13 Novemba akijaribu kula matonge matano ya
wali katika kipindi cha dakika tatu. Tonge la wali nchini Japan, kama
lililo pichani, hufahamika kama Onigiri. Alifariki siku tatu
baadaye baada ya kukaa siku hizo zote akiwa hajapata tena
fahamu, waandalizi wa shindani hilo wameambia vyombo vya habari Japan. Mashindano ya kula chakula kwa kasi ni maarufu na huandaliwa mara kwa mara maeneo mengi Japan. Wataalamu wanaonya kwamba kando na kusongwa na chakula, walaji huwa wamo hatarini ya kuharibu tumbo au koo.
Mtu mwenye HIV aliyefanya mapenzi na wanawake 104 Malawi afungwa miaka 2 jela
Mahakama moja
nchini Malawi imempatia hukumu ya miaka miwili jela mtu mwenye virusi
vya HIV ambaye alikiri kufanya tendo la ngono na zaidi ya wanawake 100
na wasichana bila kutangaza hali yake.
Katika uamuzi mkubwa
uliotarajiwa na wengi, Eric Aniva alipatikana na hatia ya ''kutekeleza
mila zenye madhara'' chini ya sheria za kijinsia za taifa hilo baada ya
uchunguzi wa BBC kubaini vile alivyolipwa ili kuwafanyia sherehe za
kutakasa wasichana wadogo pamoja na wanawake wajane. Eric Aniva
ni mwanamume wa kwanza kufungwa jela kwa kuwa 'fisi' neno linalotumika kwa
mwanamume anayelipwa ili kushiriki ngono na wanawake pamoja na wasichana
ikiwa ni miongoni mwa tamaduni za kutakasa. Katika mahojiano na
BBC, Eric alikiri kufanya mapenzi na wanawake 104 na wasichana bila kuwalezea
kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya HIV. Ijapokuwa hakuna
msichana aliyejitokeza, kulalamika, alipatikana na hatia ya kutekeleza
mila zenye madhara baada ya wanawake wawili kutoa ushahidi wao. Wote
wawili ni wajane ambao wanasema walilazimishwa kufanya mapenzi na mtu
huyo ili kutakasa roho za waume zao baada ya vifo vyao. Kesi hiyo
imezua maoni tofauti nchini Malawi huku baadhi yao wakidai kwamba sheria
kali za kijinsia zinaingilia utamaduni na kwamba bw Aniva anasulubiwa . Wakati
huohuo mashirika ya haki za kibinaadamu yanaamini kwamba kesi hiyo ni
ushindi katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kingono.
Watu 140 wameuawa na wengine zaidi 150
wamejeruhiwa wakati treni ilipoacha reli katika jimbo la Uttar Pradesh
kaskazinii mwa India Jumapili (20.11.2016).
Maafisa wa polisi wamesema takriban watu 20 bado hawajulikani walipo
wakati mamlaka zikijaribu kutafuta chanzo kilichosababisha kuanguka kwa
ghafla kwa mabehewa 14 kutoka kwenye reli huko Pukhran kiasi cha kilomita 65
kusini mwa mji wa Kanpur wakati treni hiyo ilipokuwa ikisafiri kati ya
mji wa kaskazini mashariki wa Patna na mji wa kati wa Indore.
Huku
kukiwa na hali ya taharuki na kuchanganyikiwa manusura wamekuwa
wakihangaika kuwatafuta ndugu zao na wengine wamekuwa wakijaribu kuingia
kwenye mabehewa yalioharibiwa kuwaokoa jamaa zao na kukusanya vitu
vyao.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani Jumapili
(21.11.2016) amethibitisha kwamba atagombea tena ukansela katika
uchaguzi wa mwaka 2017.
Wajerumani wamekuwa wakisubiri kwa hamu kwa miezi kadhaa sasa kutaka
kujua iwapo Kansela Merkel ambaye amekuwepo madarakani tokea mwaka 2005
atawania muhula wa nne au la wakati wa uchaguzi iliopangwa kufanyika
mwezi wa Septemba mwaka 2017.
Baada ya miezi kadhaa ya tetesi
inaripotiwa kuwa Kansela huyo amewaambia wanachama wenzake wa chama cha
CDU mjini Berlin kwamba yuko tayari kukiwakilisha chama hicho katika
uchaguzi huo wa mwakani.
Rais Robert Mugabe be amekuwa mamlakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980
Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe, mwenye umri wa mika 92, anazungumzia kuhusu kustaafu ,
lakini swali ambalo bado watu wanahoji ni ikiwa kweli anamaanisha hilo.
Mwishoni mwa juma Bwana Mugabe aliuambia mkutano wa watu wapatao 400-
walio piagania uhuru kwamba ikiwa atastaafu anapaswa kupewa fursa
"inayofaa" kufanya hivyo.
Pia aliwakosoa baadhi ya viongozi wa chama chake cha Zanu-PF kwa kumuombea afe na kujaribu kumroga ili wachukue nafasi yake.
Malumbano
ya ndani kwa ndani miongoni mwa wafuasi wa chama tawala ya kutaka
kumrithi Bwana Mugabe yameongezeka huku kiongozi huyo akionekana
kuendelea kudhoofika zaidi.
Lakini si mara ya kwanza Kwa Bwana Mugabe kuongelea kuhusu kuachia madaraka.
Mtu mweusi nchini
Afrika Kusini ambaye alidaiwa kulazimishwa kuingia katika jeneza na
wakulima wawili weupe kwa kupita katika shamba lao amesema kuwa anahofia
maisha yake.
Victor Mlotshwa alikuwa akizungumza nje ya mahakama
ya mji wa kaskazini mashariki wa Middelburg ambapo waliotaka
kumshambulia walifikishwa mahakamani.
Ghasia ziliibuka baada ya nyani anayemilikiwa na mtu
wa kabila moja kushambulia kundi la wanafunzi wa kike wa kabila
jingine.
Maafisa na wanaharakati nchini Libya wanasema kwamba makabiliano mabaya baina ya makabila yameanzishwa na nyani mdogo. Taarifa
haziko wazi zote, lakini duru kutoka katika mji wa kusini wa Sabha
zinasema kuwa ghasia ziliibuka baada ya nyani anayemilikiwa na mtu wa
kabila moja kushambulia kundi la wanafunzi wa kike wa kabila jingine.
Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.
Katika
taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, mchungaji
aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua
wadudu inayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.
Kampuni
inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu,
huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha
malalamiko.
Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.
Chini ya sheria za Singapore, mtu anayepatikana
akiwa na zaidi ya gramu 500 za bangi anaweza kuhukumiwa kifo.
Mwanamme mmoja raia
wa Nigeria amenyongwa kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya
baada ya kupatikana na kilo 2.6 za bangi.
Mwanamme huyo Chijioke Stephen Obioha wa umri wa miaka 38, alinyongwa leo katika gereza la Changi.
Obioha
ambaye ana shahada ya kemia ya viwanda kutoka chuo cha Benin, alihamia
nchini Singapore mwaka 2005, akiwa na matumaini ya kuwa mawanasoka.
Sadhvi Deva Thakur mara nyingi huonekana ameshika bunduki
Polisi nchini India
wanamtafuta Sadhvi Deva Thakur, mwanamke aliyeko mafichoni baada ya
kufyatua risasi kwenye sherehe ya harusi
Shaghaziye bwana harusi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.
Kwenye
video ya tukio hilo lililotokea siku ya Jumanne katia jimbo la
Kaskazini la Haryana, Sadhvi Deva Thakur anaonekana akifyatua risasi
akitumia bunduki aina ya revolver.
Na WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karimjee.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mtoto wa marehemu, William
Mungai alisema ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja hivyo
saa 5.00 asubuhi.
Hata hivyo mtoto huyo wa marehemu hakutaka kuingia kwa undani kuhusu
chanzo cha kifo cha baba yake, badala yake alisema familia iachwe
iendelee kushauriana na daktari.
Alisema pamoja na hayo, kifo hicho kimewashtua kwa vile kimetokea
ghafla na kwamba baada ya kuisha kwa ibada ya kuaga mwili huo,
utasafirishwa hadi Mafinga, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa kwa
mazishi.
“Hadi sasa familia tunajua kwamba marehemu aliugua tumbo la kawaida
na tulimpeleka hospitalini ambako alifariki dunia, tunaomba familia
iachwe, kwa sababu bado tunashauriana na daktari wake.
“Tumekubaliana mwili wake uagwe kesho (leo) saa tano Viwanja vya
Karimjee ambako pia historia yake yote na familia itasomwa,” alisema
William.
MWANASIASA mkongwe na waziri wa zamani wa Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne, Joseph Mungai.
Na MWANDISHI WETU, DAR ES SAALAM
MWANASIASA mkongwe na waziri wa zamani wa Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne, Joseph Mungai, amefariki dunia.
Mungai aliyezaliwa Oktoba 24,1943 alifariki dunia Dar es Saalam jana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa za kifo cha kiongozi huyo mstaafu, zilianza kusambaa kupitia mitandao mbalimbali ya jamii jana saa 12 join.
Akizungumza na MTANZANIA jana, mtoto wa marehemu, William Mungai,
alisema baba yake alifariki dunia wakati akipelekwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Alisema kabla ya kifo hicho baba yake alianza kulalamika kuumwa na
tumbo na kutapika ambako alipelekwa katika hospitali moja ambayo
hakutaka kuitaja.
Alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo, hali yake ilizidi
kubadilika na kuwa mbaya zaidi na hivyo wakaamua kumkimbiza Muhimbili
kwa matibabu zaidi.
“Ni kweli baba amefariki dunia saa 10 jioni leo (jana) wakati
tukimpeleka Muhimbili baada ya kulalamika kuumwa na tumbo. Hivi
tunavyoongea, ndiyo tunatoka Muhimbili ila taarifa zaidi tutawapatia
baada ya kikao cha ndugu,” alisema William kwa kifupi.
Ikiwa watapiga kura ya ndio karibu robo ya
wamarekani watakuwa na kibali cha sheria cha kuvuta mmea huo kwa
kujifurahisha ama sababu za matibabu
Kando na kumpa rais mpya, wamarekani wanakaribia kuamua ikiwa watapanua eneo kubwa zaidi ambako bangi inakubalika kisheria.
Katika majimbo tisa , katika siku ambayo uchaguzi unafanyika, wapiga
kura watapata fursa pia kuwa na kauli yao kuhusu kuidhinishwa
kisheria kwa matumizi ya bangi.
Ikiwa watapiga kura ya ndio
karibu robo ya wamarekani watakuwa na kibali cha sheria cha kuvuta mmea
huo kwa kujifurahisha ama sababu za matibabu watakapotimiza umri
unaokubalika kisheria.
Katika kipindi cha miaka 20 suala hili lilikuwa ni mwiko nchini Marekani.
Wamarekani wamemchagua Donald Trump kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo.
Amejipatia sauti 276 dhidi ya 218 za wawakilishi wa majimbo. Rais
mteule Trump amewahutubia wafuasi wa chama chake na wamarekani kwa
jumla. Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton amekubali kushindwa na ameshazungumza kwa simu na Donald Trump kumpongeza.
Polisi nchini Kenya
katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana
na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa
pesa, ATM.
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi
hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la
uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Akizungumza
na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi
waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka
kukata chuma.
Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata maarifa
utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi
wa benki unazidi kubadilika sana.
Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000
Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa Samwel Sitta
amefariki dunia katika Hospitali ya Technical University of Munich
nchini Ujerumani saa 7:30 kwa muda wa Ujerumani alikokuwa akitibiwa
ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume.
Historia yake:
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo
Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950
– 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na
kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle
School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya
Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.
Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka
1964 na kuhitimu mwaka 1971.