Hakuna mtu yeyote aliyekiri kufanya mashambulizi hayo, ila kuna hisia kuwa ni kazi ya Al Shaabab. Kenya imekuwa ikishuhudia ongezeko la mashambulizi tangu kuanza kujihusisha na vita nchini Somalia mwaka 2011. Jeshi la Kenya linasaidiana na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kupambana na kundi la wanamgambo la Al Shabaab.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini humo kufuatia shambulizi hilo ambalo limekuja siku chache tu baada ya polisi kunasa washukiwa watatu wa ugaidi wakiwa na mabomu mawili makubwa tayari kufanya shambulizi kubwa. Pia walinasa vilipuzi vingine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi. Mji wa Mombasa wenye sifa ya utalii, umekuwa ukikumbwa na suitofahamu ya kiusalama kutokana na vijana wengi kujiunga na itikadi kali za dini hiyo
Jumatatu, 31 Machi 2014
JELA KWA MIAKA 65 KWA KUMPA UJAUZITO MTOTO WAKE WA KUMZAA.
MKAZI wa Mtaa wa Uhamila katika mji mdogo wa Rujewa,
mkoani Mbeya, amehukumiwa miaka 65 jela kutokana na makosa matatu tofauti,
yaliyotokana na kumpa ujauzito mwanawe wa kumzaa.
ABIRIA WANUSURIKA VIFO KATIKA AJALI ZA MABASI YA SUMRY NA NGANGA
Watu 29 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea katika barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam kwenye maeneo ya Mikese na Mkambarani, mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema zilihusisha mabasi ya abiria; moja likiwa basi la Nganga lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya na la Sumry lililokuwa likitoka Tunduma.
Ajali ya kwanza ambayo majeruhi ni 15 saa 2:30 usiku, ilitokea juzi eneo la Mkambarani, Morogoro Vijijini.
Ilihusisha basi la kampuni ya Sumry yenye namba za usajili T 888 BWK . Ilikuwa ikiendeshwa na Muhina Mohamedi (39) mkazi wa Mbeya ikitoka Tunduma kwenda Dar es Salaam.
Basi hilo liligongana uso kwa uso na basi dogo la abiria aina ya Coaster yenye namba za usajili T273 CCV ambayo dereva wake hakufahamika. Ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.
Chanzo cha ajali kilitokana na basi la Sumry kutaka kupita gari la mbele yake.
Kwa upande wa ajali ya basi la Nganga lenye namba za usajili T252 AZU, ilikuwa ikiendeshwa na Alex Eliya (49) mkazi wa Misufini kabla ya kupasuka tairi la mbele kulia na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.
Idadi ya majeruhi katika ajali hiyo ni 14 ambao walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Ajali hiyo ilitokea jana saa 3:30 asubuhi katika eneo la Miembeni Mikese, Wilaya ya Morogoro.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hizo, akiwemo Esau John na Jane Lawa waliokuwa kwenye basi hilo la Nganga, walisema kilichosaidia kutokuwepo vifo ni kwa kuwa basi halikuwa kwenye mwendo wa kasi.
Mganga wa zamu katika hospitali hiyo ya mkoa, Dk Alex Makala, alisema jana walibaki majeruhi 12 baada ya wengine kutibiwa na kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha madogo (TK).
SHAMBULIZI LA KIGAIDI LAWAUA 6 NAIROBI
Watu sita wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi.
Polisi wamesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika mkahawa mdogo ulio karibu na kituo cha mabasi mtaani humo.
Walioshuhudia shambulizi walisema kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha hilo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo. Chanzo BBC Swahili
LIVERPOOL YAIADHIBU SPURS KWA BAO 4-0 NA KUSHIKILIA USUKANI BAADA YA KUISHUSHA CHELSEA WA LIGI KUU ENGLAND
Suarez akifunga bao lake la 29 katika ligi kwa
msimu huu wakiizamisha Spurs kwa 4-0
VIJOGOO wa Anfield,
Liverpool imekwea hadi kileleni mwa Ligi Kuu ya England wakiiporomosha Chelsea
baada ya kuifumua bila huruma Tottenham Hotspur iliwatembelea kwenye uwanja
wao.
Liverpool
iliitambia vijogoo wenzao wa London kwa kuwakandika mabao 4-0, na kuwafanya
wafikishe jumla ya pointi 71, mbili zaidi ya Chelsea ambao jana walifumuliwa bao
1-0 na Crystal Palace.
Wageni
walianza kujitabiria janga baada ya Younes Kaboul kujifunga dakika ya pili ya
mchezo kabla ya Luis Suarez kuandika bao la pili dakika ya 25 na wenhyeji kwenda
mapumziko wakiwa mbele kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Liverpool kuandika
bao la tatu kupitia kwa Phillipe Countinho dakika ya 55 kabla ya Jordan
Henderson katika dakika ya 75 na kuifanya Liverpool kukalia kiti cha uongozi
kilaini (TK).
HAWA NDIYO NDUGU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI MJINI MOSHI.
Lori la
mizigo aina ya Fusso likiwa limegongana na gari ndogo aina ya Toyota Hilux Pick
Up katika eneo la Hedaru, wilayani Same, Kilimanjaro, juzi na kusababisha vifo
vya watu 12. Picha na Alex Shirima.
MOSHI.
MJI wa Hedaru uliopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro,
jana ulizizima kwa vilio na simanzi baada ya waombolezaji 12 wote ndugu,
kufariki dunia kwa ajali ya barabarani.
Waombolezaji hao wanawake, walipewa lifti ya gari na
Diwani wa Kata ya Hedaru, Gerard Mgwena (CCM), kwa ajili ya kuwapeleka msibani
eneo la Majengo ambako mtu mmoja alifariki kwa kusombwa na maji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Robert Boaz
alithibitisha ajali hiyo akisema ilitokea juzi saa 2:00 usiku na kwamba ilikuwa
mbaya zaidi tangu kuanza kwa mwaka 2014.
“Ni ajali iliyohusisha
magari matatu kwa wakati mmoja…; watu 11 walifariki pale pale na mwingine
alifariki dunia leo (jana), asubuhi Hospitali ya Rufaa ya KCMC,”alisema Boaz.
Hata hivyo, alisema hakuwa na nafasi nzuri ya kufafanua kwa undani
ajali hiyo kwa vile alikuwa nje ya Mkoa wa Kilimanjaro na kuelekeza atafutwe
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO), Joseph Mwakabonga.
Akizungumza kwa niaba ya RPC, Mwakabonga alisema, lori aina ya
Mitsubish Fusso lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar liligonga kwa nyuma gari
aina ya Toyota Hilux Pick-Up.
Alisema kuwa baada ya kuligonga gari
hilo lililowabeba waombolezaji hao, nalo lilisukumwa na kwenda kuligonga lori
aina ya Scania lililokuwa na tela lake.
Lori hilo aina ya Scania
lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi likiendeshwa na dereva wake,
Gabriel David. Madareva wawili wa Toyota Pick-Up na Toyota Fusso wote
hawajulikani waliko.
Taarifa zilizopatikana baadaye, zilisema dereva
wa Fusso alikuwa amelazwa katika Hospitali ya KCMC, wakati Kigogo wa CCM
aliyekuwa amewabeba waombolezaji akilazwa hospitali moja jijini Arusha.
Mwakabonga aliwataja waliofariki kuwa ni Stella John(45), Salma
Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George (29) na Sophia
Mbike (51).
Wengine ni Ritha Kalani (55), Mama Kalani Stephano (55),
Kolina Mmatha(55), Bahati Daud(25) na Farida Kiondo mwenye umri wa miaka 25.
Majeruhi mmoja, Maria John (33) ambaye ni miongoni mwa watu 10
waliojeruhiwa, alifariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC
alikolazwa kwa ajili ya kuokoa maisha yake (TK)
WARIOBA AMSHUKIA Prof SHIVJI, ASEMA CHANZO NDIYE YEYE CHA UCHOCHEZI ZANZIBAR.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa gazeti hili,
nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana. Picha na Edwin
Mjwahuzi.
DAR ES SALAAM.
DAR ES SALAAM.
MJADALA wa Mabadiliko ya Katiba jana ulihamia nje ya
Bunge wakati Jaji Joseph Warioba alipomchambua mhadhiri maarufu nchini, Profesa
Issa Shivji akimueleza kuwa si mkweli bali mpotoshaji wa Rasimu ya
Katiba.
Jaji Warioba, ambaye ni mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, pia amemtuhumu Profesa Shivji kuwa ndiye mwanzilishi wa chokochoko za Zanzibar za kudai serikali tatu, jambo ambalo sasa analigeuka kutokana na kuona hali imekuwa mbaya.
Kauli ya Warioba imekuja baada ya Profesa Shivji kuichambua Rasimu ya Katiba jana asubuhi kwenye Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo lililokuwa na dhima ya Vijana Katika Kuimarisha na Kuendeleza Muungano Baada ya Miaka 50. Tamasha hilo lilifanyika kwenye hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo, Profesa Shivji alisema katika kujadili Muungano, wananchi hawana budi kuzingatia mambo mawili ambayo ni nchi zinazozungumziwa kwenye Rasimu kuwa ni Zanzibar, Tanganyika au Tanzania, ambayo alisema haina mamlaka katika pande hizo mbili za Muungano.
Pia alisema suala la maadili kwa viongozi halina budi kuangalia kuwa linazungumzia maadili ya viongozi wa Zanzibar, Tanganyika au Tanzania na kwamba rasimu inazungumzia viongozi wa Tanzania ambao hawana mamlaka kwa Tanganyika na Zanzibar.
Katika majumuisho yake, Profesa Shivji, ambaye aliikosoa Rasimu kuwa haiwakilishi matakwa ya Watanzania kwa kuangalia sampuli zilizotumika, alisema kwamba wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba walikuwa hawana nia njema.
Lakini Shivji akaenda mbali zaidi kwa kusema “the road to hell is paved in good intention,” akimaanisha kuwa njia ya kuzimu imetengenezwa kwa nia njema.
Akijibu hoja hizo, Jaji Warioba alisema
Profesa Shivji amegeuka maandishi yake yaliyokuwa yanachochea utaifa wa Zanzibar
na sasa anaona Tanganyika ndiyo hatari kwa Muungano.
“Shivji ni msomi na mimi najua anaelewa
matumizi ya takwimu,” alisema Jaji Warioba, ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wakati alipozungumza na gazeti hili nyumbani kwake
jana jioni.
“Nasema hapa, Shivji akiwa msomi, amekuwa
intellectually dishonest (si mkweli kiusomi). Anapotosha kwa
makusudi.”
Jaji warioba alisema Shivji ndiye amekuwa chanzo cha uchochezi wa kitaifa Zanzibar kupitia maandishi yake. Alisema waliokuwa wanadai serikali tatu kwa muda mrefu walikuwa wananchi wa Zanzibar.
“Shivji alikuwa anasema Tanganyika imejificha kwenye Muungano ili inufaike. Kwa hiyo anasema Tanganyika iwe wazi isijifiche,” alisema Jaji Warioba.MWANANCHI
MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU WAMZIKA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA
Kilosa, Morogoro
Makamu wa Rais Mhe Mohamed Gharib Billali pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB)Jumamosi tarehe 29/3/2013 walishiriki mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe John Gabriel Tuppa ambaye alifariki ghafla wiki iliyopita.
Katika Mazishi hayo yaliyofanyika Kilosa mjini Mkoani Morogoro yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mheshimiwa Steven Wassira, Waziri wa Ardhi Prof Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Hawa Ghasia. Aidha Manaibu Waziri kadhaa walikuwepo akiwepo Mhe Aggrey Mwanri (MB), Naibu Waziri wa OWM TAMISEMI, Mhe Kebwe Stephen Kebwe (MB) Naibu Waziri wa Afya. Wakuu wa Mikoa nao walishiriki mazishi ya mwenzao.
Aidha Wakuu wa Wilaya kadhaa nao walishiriki wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Mara na Morogoro na Wakurugenzi wao.
Makamu wa Rais akitoa heshima za mwisho
Makamu wa Rais akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Tuppa
Makamu wa Rais akiweka shada la Maua
Makamu wa Rais akimfariji mke wa Marehemu Tuppa
Makamu wa Raisi akimfariji baba mzazi wa Marehemu Mzee Gabriel Tuppa
Makamu wa Raisi akimfariji baba mzazi wa Marehemu Mzee Gabriel Tuppa
Pichani Waziri Mkuu akiweka udongo katoka kaburi la marehemu Tuppa
Mhe Pinda akimfariji Mzee Gabriel Tuppa ambaye ni baba mzazi wa Marehemu John Tuppa
KISWAGA AKIWEZESHA KIKUNDI CHA VIKOBA CHA TWIYENDAGE KALENGA
Mtendaji wa kijiji cha Kalenga akimkaribisha Kiswaga kuzindua kikundi hicho |
MKURUGENZi wa kampuni ya simu ya Tigo kanda ya nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga amechangia kiasi cha Tsh 700,000 kwa ajili ya kukiwezesha kiuchumi kikundi cha Vicoba cha Twiyendage kata ya Kalenga wilaya ya Iringa .
Kiswaga alikabidhi msaada huo leo wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho chenye wanachama 30 kama njia ya kuunga mkono jitihada za wanawake hao katika kujiletea maendeleo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Kiswaga aliwataka wanachama wa kikundi hicho kuzidi kuwahamasisha wenzao kujiunga na vikundi kama hivyo kama njia ya kujikwamua kiuchumia na kuwataka wanachama kujenga utamaduni wa kurejesha mikopo pindi wanapokopeshana .
Kwani alisema iwapo wanachama wengi zaidi watahamasishwa kujiunga na vikundi hivyo vya kiuchumia upo uwezekano mkubwa wa serikali na taasisi mbali mbali za kifedha kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo.
"Awali ya yote ninapenda kuwashukuru wanachama kwa kunialika kuwa mgeni rasmi hapa leo ila bado napenda kuwatia nguvu kwa kuwachangia kiasi cha Tsh 700,000 ili kuongeza mtaji wenu zaidi ... ili kuweza kujikomboa kimaisha ni lazima kuanzisha vikundi kama hivi vya kiuchumia"
Awali mwenyekiti wa kikundi hicho Mwahija Witala alisema kuwa kikundi hicho kina wanachama 30 kutoka makundi mbali mbali ya kijamii wakiwemo walimu, wakulima wafanyabiashara na wa wale wasio kuwa na ajira .
Witala alisema hadi sasa kikundi hicho kina mtaji wa Tsh milioni 3 na lengo ni kuendelea kusaidiana zaidi ikiwa ni pamoja na kusaidia makundi mbali mbali ya jamii yaayowanzunguka wakiwemo watoto yatima.
KASEBA ASHINDWA KWA POINTI
Thomas Mashali (kulia) akipambana na Japhert Kaseba.
Baada ya kushushiwa kipigo, bondia Japhet Kaseba amesema jambo lililompa faraja ni kutopigwa kwa Knock Out (KO) na Thomas Mashali katika pambano lao la kuwania ubingwa wa UBO Afrika lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam juzi.
Majaji wote watatu, Pembe Ndava, Robert Amos na Omary Yazidu walimpa ushindi Mashali wa pointi 97-94.
Kaseba alisema anaheshimu matokeo ya majaji kwani wao ndiyo waamuzi wa mwisho na kueleza kuwa angejutia zaidi kama angepigwa kwa KO, lakini kwa pointi bondia yoyote anaweza kupewa ushindi.
Alisema licha ya kupigwa, hakuna cha ajabu alichokifanya mpinzani wake kwenye pambano hilo ila raundi nne za mwanzo ndizo zilimpa ushindi Mashali.
"Nilichelewa kufungua na kushambulia raundi nne za mwanzo nikidhani namvutia muda mpinzani wangu ili achoke nami nimalize mchezo, lakini ikawa ndivyo sivyo, mahesabu tu ndiyo yalikataa hakuna kingine, najuta kwa nini nilimuachia acheze raundi za mwanzo," alisema Kaseba.
Katika pambano hilo la uzani wa light heavy, Kaseba alianza vizuri raundi ya kwanza na dakika ya pili aliachia konde la mkono wa kulia lililompata sawia Mashali na kumpeleka chini ingawa alikuwa mwepesi kunyanyuka na kuendelea na mchezo kabla ya mwamuzi wa pambano, Anthony Lutha kumhesabia.
Mashali alizinduka raundi ya pili hadi ya tano na alicheza kwa kushambulia hali iliyosababisha mpinzani wake kujihami kwa kukumbatia, kitendo kilichomfanya azomewe na mashabiki wa Mashali waliojitokeza kwa wingi.
Raundi ya saba, nane na ya tisa, Kaseba alibadilisha mchezo na kushambulia hivyo kumpa wakati mgumu mpinzani wake ambaye katika raundi hizo alitumia muda mwingi kujihami.
"Kaseba alikuwa anaongea sana. Aliahidiwa gari kama angenipiga hivyo zawadi hiyo imeota mbawa. Tangu mwanzo nilisema Kaseba hana uwezo wa kunipiga akabisha sasa naamini amekubali kiwango chake bado," alitamba Mashali dakika chache baada ya kuvikwa mkanda wa UBO Afrika.
Mashali alisema baada ya kipigo hicho hivi sasa anajipanga 'kumnyamazisha' Karama Nyilawila ambaye atapigana naye Mei Mosi jijini Dar es Salaam kuwania ubingwa wa dunia wa UBO.
Kaseba ana rekodi ya kushinda mapambano 5 (3 kwa KO) amepigwa mara 4 (3 kwa KO) hajawahi kutoka sare tangu 2000 alipoingia kwenye ngumi za kulipwa.
Wakati Mashali ameshinda mapambano 10 ( 5 kwa KO), amepigwa mara 2 zote kwa KO na kutoka sare mara moja tangu 2009 alipoingia kwenye ngumi za kulipwa.
Chanzo, mwananchi (TK)
AJALI MBAYA SANA WATU 22 WAFA KIBITI, RUFIJI
Watu 22 wamefariki dunia katika ajali mbaya imetokea Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 5 na wengine 11 kujeruhiwa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.
Awali ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX), iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea Dar ambalo lilikwenda kukwaruzana na Lori(T 132 AFJ) kwa nyumba, ambalo lilikuwa limeharibika na kusimama barabarani.
Alisema baada ya kulikwaruza lori hilo, mlango wa Hiace uling'oka na kubaki kwenye roli ambapo gari hiyo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Canter(T 774 CJW) na kupinduka.
"Katika ajali hii, watu 14 walifariki dunia papo hapo, na wakati polisi na baadhi ya wananchi wakiendelea kuwaokoa majeruhi ili wakimbizwe hospitali, likatokea basi la kampuni ya Mining (majeruhi na kuwaua wengine na idadi ya waliokufa imefikia 22.
Jumatano, 26 Machi 2014
BREAKING NEWS: MVUTANO MKALI BUNGENI BUNGE LAAHIRISHWA
Bunge Maalum la Katika limekutana leo jioni hii kuendelea na shuguli zake Lakini mvutano mkubwa umejitokeza hali iliyosababisha vurugu kubwa Iliyoambatana na zomea zomea. Mvutanho huo uliibuka pale mjumbe wa Bunge hilo Mhe. Tundu Lissu aliposimama kuomba muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni kmbayo Tundu Lissu anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Hilo kupitia Kamati ya Uongozi kuleta Marekebisho Kinyume cha kanuni zilizopitishwa na bunge hilo la Katiba.
Jumanne, 25 Machi 2014
BRITISH TOURIST KILLED BY ELEPHANTS IN INDIA IN ONE A MILLION SAFARI ACCIDENTS
The inquest heard the 67-year-old had travelled on the latest of several trips to visit local friends for a safari in southern India
A retired teacher was killed by a stampeding elephant as he tried to achieve his lifelong dream of seeing a tiger in the wild, an inquest heard.
Colin Manvell, 67, was on holiday in India photographing wildlife when he was trampled by the beast.
The hearing was told he suffered multiple fractured ribs and died of a lung injury en route to hospital.
Recording a verdict of accidental death, Coroner David Horsley said: “We do not know any more than an elephant must have come out of the undergrowth making trumpeting sounds and he was in its way.
“He has been out on holiday photographing wildlife...and unfortunately he has been in the way of a stampeding elephant.
“It is the first time I have encountered anything like this as a coroner, he was clearly out in India doing what he loved.
“It was maybe the way he would have wanted to go.”
The coroner said that he had received very little information from the Indian authorities about the incident.
The inquest heard the only report sent to him had been photocopied badly and was incomplete.
Colin died at the Masinagudi National Park in the state of Tamil Nadu on September 19 last year.
The retired geography teacher had been to the country twice a year for the past five or six years.
He was chasing his dream of seeing a tiger in the wild when he died.
After the inquest Colin’s nephew, Roger Manvell, 48, said: “It was a big shock to us and the family.
He was always a very keen traveller and died doing something he loved and we still have his photographs from his travels which we will hold very dear to us.
“It was quite unbelievable when it happened at the time, it’s a one-in-a-million.”
Roger added that Colin had also visited Sri Lanka, Thailand and the Amazon.
He said: “He had always travelled a lot ever since I can remember. I think he had been there a week or so before he had died.
“He’s very keen on his photography, particularly birds, flowers.
“He was always interested in looking for a tiger on his travels and every time he got back he had been a bit closer to seeing it.
“He never actually got to see a tiger but he was just interested in everything.
“He was not a thrill-seeker or anything, just enjoyed seeing the culture out there and spending time with friends he met there.”
Speaking of the incident, he added: “I would assume that he was taking some photos of some wild birds by a water hole, it sounds like he was on his own because if there had been someone else there this might not have happened.”
Reports at the time suggested Colin may have been surprised by the elephant because he was hard of hearing.
But there was no mention of this at the inquest in Portsmouth, Hants.
The inquest was told that Colin suffered from glaucoma and was awaiting surgery to cataracts in his eyes.
But his nephew Roger said: "Both his hearing and eyesight were reasonable."
Colin Manvell, 67, was on holiday in India photographing wildlife when he was trampled by the beast.
The hearing was told he suffered multiple fractured ribs and died of a lung injury en route to hospital.
Recording a verdict of accidental death, Coroner David Horsley said: “We do not know any more than an elephant must have come out of the undergrowth making trumpeting sounds and he was in its way.
“He has been out on holiday photographing wildlife...and unfortunately he has been in the way of a stampeding elephant.
“It is the first time I have encountered anything like this as a coroner, he was clearly out in India doing what he loved.
“It was maybe the way he would have wanted to go.”
The coroner said that he had received very little information from the Indian authorities about the incident.
The inquest heard the only report sent to him had been photocopied badly and was incomplete.
Colin died at the Masinagudi National Park in the state of Tamil Nadu on September 19 last year.
The retired geography teacher had been to the country twice a year for the past five or six years.
He was chasing his dream of seeing a tiger in the wild when he died.
After the inquest Colin’s nephew, Roger Manvell, 48, said: “It was a big shock to us and the family.
He was always a very keen traveller and died doing something he loved and we still have his photographs from his travels which we will hold very dear to us.
“It was quite unbelievable when it happened at the time, it’s a one-in-a-million.”
Roger added that Colin had also visited Sri Lanka, Thailand and the Amazon.
He said: “He had always travelled a lot ever since I can remember. I think he had been there a week or so before he had died.
“He’s very keen on his photography, particularly birds, flowers.
“He was always interested in looking for a tiger on his travels and every time he got back he had been a bit closer to seeing it.
“He never actually got to see a tiger but he was just interested in everything.
“He was not a thrill-seeker or anything, just enjoyed seeing the culture out there and spending time with friends he met there.”
Speaking of the incident, he added: “I would assume that he was taking some photos of some wild birds by a water hole, it sounds like he was on his own because if there had been someone else there this might not have happened.”
Reports at the time suggested Colin may have been surprised by the elephant because he was hard of hearing.
But there was no mention of this at the inquest in Portsmouth, Hants.
The inquest was told that Colin suffered from glaucoma and was awaiting surgery to cataracts in his eyes.
But his nephew Roger said: "Both his hearing and eyesight were reasonable."
NDEGE YA MALAYSIA MH370: NDUGU WA WALIOKUWEPO WAANDIKIWA SMS KWAMBA HAKUNA ABIRIA ALIYEPONA NA KWAMBA NDEGE IPO FUTI 23,000 CHINI YA BAHARI
Ndugu wa abiria waliosafiri na ndege ya Malaysia iliyopotea tarehe 8/3/2014 wametumiwa meseji (SMS) kuwa hakuna uwezekano wa kuwapata wakiwa hai abiria wote pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo.
Picha mpya za Satelilite zinaonesha kuwa ndege hiyo ilianguka katika sehemu moja ya bahari ya Hindi ikiwa na abiria 239.
Ujumbe wa simu ulisema: “Tunatakiwa kukubali kuwa ndege MH370 imepotea na hakuna abiria aliyepo hai.”
Jumatatu, 24 Machi 2014
WENYEVITI WA KAMATI MPYA ZA BUNGE LA KATIBA WALIOCHAGULIWA HAWA HAPA
Wenyeviti wa kamati za bunge waliochaguliwa hawa hapa:
Kamati Namba Moja:
Mwenyekiti ni Ummy Mwalimu, Makamu Mwenyekiti ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.
Kamati Namba Mbili:
Mwenyekiti ni Shamshi Vuai Nahodha, Makamu Mwenyekiti ni Shamsha Mwangunga.
Kamati namba tatu:
Mwenyekiti ni Francis Michael, Makamu ni Fatma Musa Juma.
Kamati namba nne:
Kamati namba tano:
Mwenyekiti ni Hamad Rashid Mohamed na Makamu ni Assumpter Mshama
Kamati namba sita:
Mwenyekiti ni Stephen Wassira na Makamu ni Dk. Maua Daftari.
Kamati namba saba:
Mwenyekiti ni Brigedia Jenerali (mstaafu) Hassan Ngwilizi na Makamu ni Waride Bakar Jabu.
Kamati namba nane:
Mwenyekiti ni Job Ndugai, Makamu ni Biubwa Yahya Othman.
Kamati namba tisa:
Mwenyekiti ni Kidawa Hamid Salehe na Makamu ni William Ngelleja.
Kamati namba 10:
Mwenyekiti ni Anna Abdallah, Makamu ni Salim Hawadhi Salim.
Kamati namba 11:
Mwenyekiti ni Anna Killango Malecela, Makamu ni Yusuf Hamad Masauni.
Kamati namba 12:
Mwenyekiti ni Paul Kimiti na Makamu ni Thuwayba Edington Kisasi
WIMBO WA BUFFALO SOLDIER WA BOB MARLEY
"Buffalo Soldier"
Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta:
There was a Buffalo Soldier in the heart of America,
Stolen from Africa, brought to America,
Fighting on arrival, fighting for survival.
I mean it, when I analyze the stench -
To me it makes a lot of sense:
How the Dreadlock Rasta was the Buffalo Soldier,
And he was taken from Africa, brought to America,
Fighting on arrival, fighting for survival.
Said he was a Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta -
Buffalo Soldier in the heart of America.
If you know your history,
Then you would know where you coming from,
Then you wouldn't have to ask me,
Who the 'eck do I think I am.
I'm just a Buffalo Soldier in the heart of America,
Stolen from Africa, brought to America,
Said he was fighting on arrival, fighting for survival;
Said he was a Buffalo Soldier win the war for America.
Dreadie, woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Buffalo Soldier troddin' through the land, wo-ho-ooh!
Said he wanna ran, then you wanna hand,
Troddin' through the land, yea-hea, yea-ea.
Said he was a Buffalo Soldier win the war for America;
Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta,
Fighting on arrival, fighting for survival;
Driven from the mainland to the heart of the Caribbean.
Singing, woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Troddin' through San Juan in the arms of America;
Troddin' through Jamaica, a Buffalo Soldier# -
Fighting on arrival, fighting for survival:
Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta.
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy! [fadeout]
There was a Buffalo Soldier in the heart of America,
Stolen from Africa, brought to America,
Fighting on arrival, fighting for survival.
I mean it, when I analyze the stench -
To me it makes a lot of sense:
How the Dreadlock Rasta was the Buffalo Soldier,
And he was taken from Africa, brought to America,
Fighting on arrival, fighting for survival.
Said he was a Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta -
Buffalo Soldier in the heart of America.
If you know your history,
Then you would know where you coming from,
Then you wouldn't have to ask me,
Who the 'eck do I think I am.
I'm just a Buffalo Soldier in the heart of America,
Stolen from Africa, brought to America,
Said he was fighting on arrival, fighting for survival;
Said he was a Buffalo Soldier win the war for America.
Dreadie, woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Buffalo Soldier troddin' through the land, wo-ho-ooh!
Said he wanna ran, then you wanna hand,
Troddin' through the land, yea-hea, yea-ea.
Said he was a Buffalo Soldier win the war for America;
Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta,
Fighting on arrival, fighting for survival;
Driven from the mainland to the heart of the Caribbean.
Singing, woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Troddin' through San Juan in the arms of America;
Troddin' through Jamaica, a Buffalo Soldier# -
Fighting on arrival, fighting for survival:
Buffalo Soldier, Dreadlock Rasta.
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy!
Woy yoy yoy, woy yoy-yoy yoy,
Woy yoy yoy yoy, yoy yoy-yoy yoy! [fadeout]
WATU 100 WAKAMATWA MJINI MOMBASA KUFUATIA SHAMBLIZI LA KIGAIDI KANISANI
Watu 100 wamekamatwa mjini Mombasa Pwani ya Kenya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa ndani ya kanisa moja mjini humo siku ya Jumapili. Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na kufunika nyuso zao waliwapiga risasi waumini wa kanisa moja mtaani Likoni na kuwaua watu wanne Watu wawili walifariki papo hapo na wengine wawili walifariki hospitalini wakati wakipatiwa matibabu. Wengine 17 walijeruhiwa vibaya.
Polisi wanasema kuwa watu watatu waliokuwa wamejihami walivamia kanisa la Joy Jesus na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholelea. Kadhalika polisi walisema kuwa washukiwa wakuu wa shambulizi hilo wametoweka
Polisi wanasema kuwa watu watatu waliokuwa wamejihami walivamia kanisa la Joy Jesus na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholelea. Kadhalika polisi walisema kuwa washukiwa wakuu wa shambulizi hilo wametoweka
‘TUMEMALIZA KAZI YETU’ ALICHOZUNGUMZA RAIS KIKWETE NI MAONI YAKE - WARIOBA:.
DODOMA.
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Bunge na kuponda ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema jukumu walilopewa kwa mujibu wa sheria wamelikamilisha na wanawaachia wananchi waamue.
Akizungumza na Mwananchi jana asubuhi, Jaji Warioba alisema alichokizungumza Rais Kikwete ni maoni yake na kwamba hawezi kuyajadili.
“Rais Kikwete alichozungumza ni maoni yake, kwa sasa sipendi kuyazungumzia hayo, ” Jaji Warioba alieleza.
Alisema wamemaliza jukumu walilopewa na kwamba sasa jukumu lote lipo mikononi mwa Bunge.
Jaji Warioba alisema Tume yake ilikusanya maoni kutoka kwa wananchi, mabaraza ya wilaya ya Katiba na Taasisi mbalimbali, wakatengeneza rasimu ambayo sasa wameikabidhi kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Jaji Warioba pia alikataa kuzungumzia zogo lililoibuka bungeni na kusababisha rasimu kuwasilishwa Jumatano, baada ya kikao cha Jumanne kuvunjika.
Hali hiyo ilitokana na UKAWA kudai muda wa saa 1:30 uliokuwa umepangwa Jaji Warioba ahutubie bungeni uongezwe na kanuni inayoelekeza Rais Jakaya Kikwete ahutubie kabla Jaji Warioba hajawasilisha rasimu izingatiwe, baada ya kutangazwa kuwa Rais angehutubia baada ya rasimu kuwasilishwa.
Profesa Baregu
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu alisema alitarajia Rais Kikwete angezindua Bunge Maalumu na siyo kutoa maagizo na vitisho kwa wajumbe.
Alisema hajui lengo la Rais kufanya alichofanya lakini ana hakika kwa kutoa ufafanuzi wa hoja zilizotokana na maoni ya wananchi ndani ya rasimu, ameingilia kazi za Tume na hivyo amevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83 toleo la mwaka 2012), inayosema:
“21.-(b) atakayejifanya kuwa mjumbe wa Tume au Sekretarieti; au (c) atakayeendesha programu ya elimu juu ya mabadiliko ya katiba kinyume na masharti ya sheria hii, atakuwa ametenda kosa.
(3) atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa kinyume na Sheria hii, atawajibika kulipa faini isiyopungua Sh2,000,000 (milioni mbili) na isiyozidi Sh5,000,000 (milioni tano) au kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka mitatu au adhabu zote mbili faini na kifungo. (TK)
RAIS KIKWETE AZIFUNGUA BARABARA ZA MKATA – HANDENI NA KOROGWE – HANDENI MKOANI TANGA
RISASI ZA MOTO NA MABOMU ZATUMIKA NZEGA, DKT KIGWANGALA ALIPOKAMATWA NA WACHIMBAJI WADOGO WA NZEGA WALIVYOTAWANYWA NA POLISI
Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora jana limemkamata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya Mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania Limited.
Kabla ya hapo mbunge huyo alifanya mkutano mkubwa wa hadhara na wachimbaji hao katika kijiji cha Nzega Ndogo wilayani humo ambapo alielezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini Bw. Paulo Masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo kwenye eneo hilo.
Katika mkutano huo wachimbaji hao walidai ni vema serikali iangalie haki zao zilizotumika kwenye uendeshaji na uchimbaji wa mashimo hayo kuliko kuwafungia bila kujali ingawa eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa Resolute lakini wao ndiyo wamiliki wa ardhi hiyo.
Hata hivyo katika hoja hiyo mbunge huyo aliwataka wachimbaji hao kudai haki yao kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja.
Baada ya kauli hiyo mbunge huyo aliwaambia wachimbaji hao wadogo kuwa haki yao iko mikononi mwao hivyo ni uamuzi wao wa kudai haki yao na yeye kama mwakilishi wao yuko nyuma yao mpaka pale haki yao itakapopatikana.
Wachimbaji hao walimwomba mbunge huyo kuambatana nao kwenye maandamano ya amani kutoka kijiji cha Nzega Ndogo kwenda Mwashina yalipo machimbo yaliyofukiwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu kujionea hali halisi ya kufukiwa kwa eneo hilo na ikiwezekana kufanya mkutano mwingine wa hadhara kijijini hapo.
Kufuata hali hiyo wachimbaji hao walianza maandamano ambayo yaliungwa mkono na mbunge huyo hadi kijiji cha Mkwajuni kabla ya kufika Mwashina ambapo polisi waliibuka na kuyasambaratisha maandamano hayo kwa mabomu ya machozi na risasi za moto.
Katika na purukushani hizo polisi walifanikiwa kumkamata mbunge huyo na kumjeruhi mtu mmoja kwa risasi ya moto kwenye paji la uso ambapo waliondoka nae kwenye gari pamoja na mbunge huyo.
Awali askari wa jeshi hilo waliziba njia na kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa vitisho mbalimbali ingawa hali hiyo ilitulia baada ya maandamano ya wachimbaji kujitokeza.
Pichani ni mmoja kati ya waandamanaji hao aliyekuwa karibu na Dkt Kigwangalla akiwa chini baada ya kujeruhiwa na polisi |
Mlipuko wa mabomu kwa mbali |
Awali mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kigwangalla akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini hao katika kijiji cha Nzega Ndogo kabla ya maandamano |
Maandamano baada ya mkutano wa Dkt Kigwangalla kuelekea eneo la machimbo ya Mwashina wilayani Nzega. |
Kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda alipopigiwa simu na waandishi wa habari alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na maandamano hayo, kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Nzega na kutumika kwa risasi za moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo.
Tayari Dkt Kigwangala ametoka polisi usiku wa kumkia leo
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora
Na Kadama Malunde-Nzega,Tabora
NA JIACHIE BLOG
MATUMAINI YA KUPATA NDEGE YA MALAYSIA MH370 ILIYOPOTEA YAZIDI KUONGEZEKA
Matumaini ya kupata mabaki ya ndege ya Malaysia iliyopotea toka tarehe 8/3 yamezidi kuwa makubwa baada ya ndege za Ufaransa kugundua mabaki yanayoelea kwenye bahari ya Hindi.
Msako mkali unaendelea katika bahari ya Hindi.
MAMA APIGWA NA MWANAMKE MWENZIE KWA KUPITISHA NG'OMBE KWENYE SHAMBA
ANGALIA PICHA
MASIKINI wa Mungu mama huyu wa kijiji cha Buhundwe wilayani Rorya mkoani Mara akitambulika kwa jina la Catherine Benedicto, amepokea kichapo kikali toka kwa mwanamke mwenzie aliyetajwa kwa jina la Bi. Tatu Wambura kwa kosa la eti kupitisha ng'ombe kwenye eneo la shamba linalomilikiwa na Bi. Tatu.
Inatajwa kuwa jumatano katikati ya wiki tunayoimalizia majira ya saa sita mchana, Catherine akiwa anaswaga ng'ombe wake wapatao 30 hivi na ushee kutoka nyumbani kwake kuelekea malishoni alipitisha mifugo hiyo katika shamba la Bi Tatu Wambura, ambalo hata hivyo lilikuwa halijalimwa wala halikuwa na mazao yoyote na ndipo alipoonwa na Bi Tatu alivamiwa na kupewa kipigo kikali kilichoambatana na makofi na mangumi hata kumpelekea mwanamama huyo kupata maumivu makali sambamba na uvimbe katika baadhi ya sehemu zake za mwili hasa jichoni.
TRAFIK AGONGWA NA GARI MOROGORO.
Picha ya akari wa Usalama barabarani akisaidiwa na raia mwema baada ya kupata ajali
Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro ambaye anajulikana kama Crispin 'Mandela' amegongwa na gari eneo la Mtawala Barabara inayotoka Msamvu kuingia katikati ya Mji wa Morogoro. Hii ni Mara ya tatu kwa Askari Huyo Kugongwa na Gari Mkoani Hapa.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Askari huyo alipokuwa Eneo la Kituo cha kushusha Abiria Kwenye Shule ya Msingi ya Mtawala Mkoani hapa.
Kwa sasa Afande huyo amelazwa wodi namba moja hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na hali yake inaendelea vizuri (TK).
MWANDISHI UINGEREZA AIBUA MAMBO MAPYA MENO YA TEMBO
Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ahadi ya kuteketeza maelfu ya meno ya tembo yaliyo kwenye ghala la Serikali, imeelezwa kuwa uwezekano huo ni mdogo.
Mwandishi wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Martin Fletcher ameeleza kushtushwa na hali ya ulinzi kwenye ghala hilo lililosheheni meno 34,000 ya tembo ambayo kwa biashara ya magendo nchini China yanagharimu Pauni 150 milioni za Kiingereza (Sh403.5 bilioni)
Fletcher, ambaye aliandika habari ya kuhusika kwa wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa Tanzania katika biashara haramu ya meno hayo kiasi cha kuifanya nchi kuwa muuzaji mkuu wa nyara hizo, aliandika hayo kwenye taarifa kuhusu ziara yake nchini iliyochapishwa na gazeti hilo jana.
Habari ya awali ilitikisa ulimwengu ambao unapambana kulinda viumbe walio hatarini kutoweka ikiwatuhumu wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa nchini kuhusika, huku Serikali ikishindwa kuwadhibiti.
Habari hiyo iliifanya Serikali ya Tanzania kufungua milango kwa vyombo vya habari vya nje kuja nchini kupata habari sahihi kuhusu tatizo hilo, akiwamo Fletcher wa Daily Mail.
Katika ziara yake, Fletcher alipata nafasi ya kutembelea ghala la nyara hizo, kuzungumza na maofisa wanyama pori pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
POLISI NZEGA WAMKAMATA MBUNGE KINGWANGWALA
Jeshi la polisi wilayani Nzega mkoani Tabora limemkamata mbunge wa jimbo la Nzega Dkt. Hamis Kigwangalla aliyekuwa kwenye maandamano ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ya kupinga kufungwa kwa machimbo yao ya mwashina yaliyo jirani na mgodi wa Resolute Tanzania limited.
Kabla ya kukamatwa kwa mbunge huyo askari wa jeshi hilo wametumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuwatawanya wachimbaji hao wadogo waliokuwa wamemzunguka mbunge huyo ili asikamatwe.
Awali mbunge huyo amefanya mkutano mkubwa wa hadhara na wachimbaji hao katika kijiji cha Nzega ndogo wilayani humo ambapo ameelezwa matatizo ya kufungwa kwa machimbo hayo na kamishna wa madini nchini bw. Paulo masanja bila kujali gharama walizoingia wachimbaji hao wadogo kwenye eneo hilo
Kufuatia hali hiyo Dkt. Kigwangalla amewataka wachimbaji hao kudai haki yao kwa kufuata taratibu zinazostahili bila kujali tofauti zao kisiasa, kikabila na kidini na badala yake wawe kitu kimoja na kuwa japo eneo hilo liko ndani ya leseni ya mgodi wa Resolute lakini mgodi huo hauna uwezo wa kuchimba dhahabu kwa kuwa ardhi hiyo ni ya wananchi ambao hawajalipwa fidia
Kamanda wa polisi mkoani Tabora Bi. Suzan Kaganda alipopigiwa simu na ITV amesema hana taarifa yoyote kuhusiana na maandamano hayo, kukamatwa kwa mbunge huyo wa jimbo la Nzega na kutumika kwa risasi za moto na mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo (TK).
Ijumaa, 21 Machi 2014
MARUFUKU KUMPA MTOTO MAJINA HAYA SAUDIA
.
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.
Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
NJIA MPYA YA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA ILIYOGUNDULIWA BAADA YA KUWANASA WANAIGERIA NA MTANZANIA
RAIA watatu wa Nigeria na mwanamke wa Kitanzania wamekamatwa na polisi jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa kujaribu kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini Liberia. Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa mbioni kutuma mihadarahi hiyo, ikiwa kwenye vitabu, kwa kutumia Wakala wa Usafirishaji Mizigo ya DHL.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salam, Suleiman Kova alitaja majina ya Wanaijeria hao kuwa ni Sunday Chaidikaobi (42), Chukwuma Favour (31), na Franklin Indubuisi (41). Mtanzania aliyebambwa pamoja na Wanaijeria hao ametajwa kuwa ni bi Hadija Ngoma (43), mkazi wa Kimara Temboni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, polisi walipata taarifa juzi, Machi 18, kuwa kuna watu wanne wanajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya waliokuwa katika ofisi za DHL zilizopo Barabara ya Sam Nujoma.
Kufuatia taarifa hizo, Kamanda Kova amesema “makachero walifuatilia suala hilo na hatimaye siku hiyo saa 8:30 mchana watu hao walikamatwa wakiwa na kifurushi wakijiandaa kukisafirisha kwenda nchini Liberia.”
Alisema polisi walipopekua kifurushi hicho, walikuta vitabu vitatu vya Kiingereza. Walipopekua vitabu hivyo, walikuta madawa aina ya heroin katika kurasa za mwanzo.
“Katika vile vitabu kurasa ya kwanza inayofunika lile jalada gumu kwa ndani, walikuwa wamefunua na kuweka unga huo na katika ukurasa wa nyuma vivyo hivyo kwa vitabu vyote,”aliongeza.
Unga huo unaokadiriwa kuwa na uzito wa nusu kilo, umepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi kubaini thamani na uthibitisho wa madawa hayo. H/T HabariLeo
Inaonekana Wanigeria wanakuja kwa kasi kwenye biashara hii ndani ya Afrika Mashariki. Miezi kadhaa iliyopita, Wanigeria wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya, wakijaribu kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya takriban shilingi milioni 120; (TK)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)