Jumatano, 27 Septemba 2017

Wabunge watwangana makonde mazito nchini Uganda

Uganda

Wabunge nchini Uganda wakipigana ndani ya ukumbi wa bunge
Wabunge nchini Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika siku ya pili ya kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo.
Katika ugomvi huo wabunge hao walirushiana viti, kuharibu vipaza sauti katika kikao hicho kilichoongozwa na Spika wa bunge, Bi.Rebecca Kadaga.

Mwanamke ajioa mwenyewe nchini Italia

Laura Mesi, who married herself, cuts her wedding cake

 Furaha yangu haitegemei uwepo wa mwanamume
Mwanamke mmoja nchini Italia amejioa yeye mwenyewe kwenye sherehe iliyokuwa na vazi kamili la harusi, keki na wageni 70.
"Ninaamini kuwa kila mmoja wetu ni lazima ajipende," alisema Luara Mesi mwenye miaka 40
Wanaounga mkono ndoa kama hizo wanasema kuwa suala kuu ni kujipenda.

Laura anasema kuwa suala la kujioa lilimjia miaka miwili iliyopita, baada ya miaka 12 ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Jumanne, 26 Septemba 2017

Wanandoa waliokamatwa Urusi wamekiri kuua watu 30

Generic shot of Krasnodar

 Mji wa Krasnodar umeshangazwa sana na tukio hili

Wanandoa waliokamatwa kwenye mji ulio kusini magharibi mwa Urusi wa Krasnodar, wamekiri kuwaua hadi watu 30.
Dmitry Baksheev, 35, na mke wake Natalia, walikamatwa baada ya mwili uliokuwa umekatwakatwa ulipopatikana kwenye kambi ya jeshi ambapo wawili walikuwa wanaishi.
Polisi walithibitisha kuwa bidhaa kadhaa za chakula na nyama vilivyopatikana nyumbani kwao vinachunguzwa ikiwa vina vinasaba (DNA) vya binadamu.
Simu ya mkononi iliyookotwa na wajenzi wa barabara mapema mwezi huu ikiwa na picha za miili iliyokuwa imekatwakatwa ndiyo ilikuwa chanzo cha kugundulika uhalifu huu.
Picha moja ilyochapishwa na vyombo vya habari nchini Urusi ilimuonyesha Bw Baksheev akiwa na  sehemu ya mwili wa binadamu kwenye mdomo wake jambo lililoashiria kuwa walikuwa wakila nyama ya binadamu.
Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 kisha uliripotiwa kupatikana katika chuo cha kijeshi ambapo wawili hao wanaishi.
Mwili huo ulikuwa umekatwakatwa na mkoba ulio na mali za muathiriwa nao ulipatikana.
Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi ilithibitisha kuwa mwanamume aliye kwenye picha hizo ametambuliwa na kukamatwa.
Picha zimetolewa kwa vyombo vya habari nchini Urusi zinazoripotiwa kuonesha polisi wakipekua nyumba ya wawili hao.
Vipande kadhaa vya miili ya binadamu vilioneshwa kwenye picha huku vingine vikiwa ndani ya ndoo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa picha zilizopatikana zimechapishwa kwenye ukuta na kwenye simu zilionesha kuwa mauaji hayo huenda yalianza karibu miongo miwili iliyopita.
Picha moja ni ya tarehe 28 Disemba mwaka 1999 na inaonyesha kichwa cha binadamu kikiwa kwenye sahani pamoja na tunda.

Jumatatu, 25 Septemba 2017

Chapisho la Twitter lamfanya kupokonywa taji la malkia wa Urembo Uturuki

Malkia wa urembo nchini Uturuki 2017 Itir Esen katikati

Malkia wa urembo nchini Uturuki 2017 Itir Esen katikati
Mshindi wa tuzo la malkia wa urembo wa Uturuki 2017 amepokonywa taji hilo baada ya mojawapo ya machapisho yake ya mtandao wa Twitter kufichuliwa.
Itir Esen mwenye umri wa miaka 18 alilitaja jaribio la mapinduzi ya mwaka uliopita nchini humo na kufananisha damu iliomwagika kutukokana na hedhi yake.
Waandalizi wa shindano hilo walisema kuwa chapisho hilo halikubaliki na kuthibitisha uamuzi wao wa kumpokonya taji hilo saa chache tu baada ya kupata ushindi.
Hata hivyo bi Esen amesema kupitia mtandao wake wa Instagram kwamba chapisho hilo silo la kisiasa.
Chapisho hilo lilichapishwa wakati wa maadhimisho ya mapinduzi hayo manmo tarehe 15 mwezi Julai wakati ambapo takriban watu 250 walifariki wakikabiliana na jaribio hilo la mapinduzi lililotekelezwa na upande mmoja wa jeshi.
Aliandika: Nimepata hedhi yangu asubuhi ya leo kusherehekea watu waliopoteza maisha yao mnamo mwezi Julai Ninasherehekea siku hiyo kwa kuvuja damu ya watu waliopoteza maisha yao.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akiwaita ''mashahidi'' watu waliofariki wakipinga mapinduzi hayo.

Ajali mbaya ya basi yazuiwa na mtalii baada ya dereva kuzimia Austria

Emergency response at the site of a bus crash on the Zillertaler Hoehenstrasse (High Road) near the town of Kaltenbach, Austria, 24 September 2017

Ajali mbaya ya basi yazuiwa na mtalii baada ya dereva kuzimia Austria
Mtalii mmoja kutoka nchini Ufaransa aliyechukua hatua za haraka amesifiwa baada ya kulizuia basi kupingirika chini ya mteremko katika milima ya Alps nchini Austria baada dereva wa abasi hilo kuzimia.
Gari hilo lilikuwa likipitia eneo la milima likiwa na abiria 21 wakati dereva mwenye umri wa miaka 76 alipozimia ghafla.
Wakati basi lilikuwa likielekea chini ya mlima raia huyo wa Ufaransa alifanikiwa kukanyaga breki.
Basi hilo liligonga kizuizi kando ya barabara kisha likasimama. Watu wanne walipelekwa hosptalini kwa matibabu baada ya kupata mshtuko.

CITY YAJIKITA KILELENI EPLL WAKATI CRYSTAL PALACE WAKINGANGANIA MKIA

  Team P W D L GD Pts
1 Man City 6 5 1 0 19 16
2 Man Utd 6 5 1 0 15 16
3 Chelsea 6 4 1 1 7 13
4 Tottenham 6 3 2 1 5 11
5 Liverpool 6 3 2 1 1 11
6 Watford 6 3 2 1 -1 11
7 Arsenal 6 3 1 2 1 10
8 Huddersfield 6 2 3 1 2 9
9 Burnley 6 2 3 1 1 9
10 Newcastle 6 3 0 3 1 9
11 Southampton 6 2 2 2 -1 8
12 West Brom 6 2 2 2 -2 8
13 Brighton 6 2 1 3 -2 7
14 Everton 6 2 1 3 -7 7
15 Swansea 6 1 2 3 -4 5
16 Stoke 6 1 2 3 -5 5
17 Leicester 6 1 1 4 -3 4
18 West Ham 6 1 1 4 -7 4
19 Bournemouth 6 1 0 5 -7 3
20 Crystal Palace 6 0 0 6 -13 0

Jumatano, 20 Septemba 2017

Tetemeko laua zaidi ya watu 200 Mexico

Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi

 Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi
Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.

Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.
Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
 
Tetemeko laua zaidi ya watu 100, Mexico
Tetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico
Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea.
''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sekunde thelathini tu, lakini ilionekana kama limedumu daima...'' anasema Daniel Lieberson
Kwa upande wake Natasha Pizzey mwandishi wa habari katika mji huo anasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.
  Juhudi za uokoaji zikiendelea
Juhudi za uokoaji zikiendelea
''..Tunafahamu kuna watu walionusurika katika majengo ya makazi yaliyoporomoka, hatukuwa na uwezo wa kuwaokoa. Kuna mamia ya wafanyakazi wa kujitolea waliokwenda katika eneo la tukio...'' ameongezea kusema
Aidha pia kumetokea madhara mabaya katika majimbo ya jirani ya Morelos na Puebla.
Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
 Tetemeko laua zaidi ya watu 100, Mexico
Tetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico

Kijana mwenye miaka 17 aliyejitengenezea simu

Mo Omar

 Mo Omer anatarajia kuuza zaidi simu alizotengeneza katika mataifa hasa ya Afrika
Kijana wa miaka 17 kutoka nchini Canada ambaye alijitengenezea mwenyewe simu baada ya mama yake Msomali kusema kuwa hana uwezo wa kumnunulia simu ya smartphone amezungumza na BBC.
Mo Omer - ambaye anajiita "tech nerd" - alitengeneza simu ya smartphone kuanzia mwanzo, na anasema ataiuza kwa dola $180.

"Ina kila kitu unachoweza kukipata katika simu ya kawaida, ni kwamba tu haina gharama kubwa ," ameiambia BBC.
Simu "sio vifaa vigumu kutengeneza", aliongeza- na akasema ana azma ya kuzipeleka katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
"Tumepokea maombi kutoka Nigeria na Algeria na maeneo mengine mengi. Ni soko linalokua kwa kasi ambalo tungependa kuingia "

Jumatatu, 18 Septemba 2017

HII KIBOKO!!!!!! Apple yazindua simu mpya ya iPhone X inayofunguka kwa kutumia uso

Apple yazindua simu mpya ya iPhone X

Apple yazindua simu mpya ya iPhone X
Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka.
Apple imesema kuwa simu hiyo inayojulikana kama Iphone 10 pia inaweza kutumia utambulisho huo wa uso nyakati za usiku kufunguka na kwamba ni vigumu kuidanganya ikilinganishwa na mfumo wa kutumia kidole.
Ndio simu ghali zaidi kuzinduliwa na Apple.

Mabasi 7 yakamatwa usiku wa manane kwa kuzidisha mwendo

Mabasi saba ya abiria yamekamatwa  na kutozwa faini kwa kosa la mwendokasi na kutofuata sheria za usalama barabarani huku wakihatarisha maisha ya abiria.

Kamatakamata hiyo  ambayo imesimamiwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani   Fotunatus  Muslim akiwa na timu ya viongozi na askari  mkoa wa Morogoro imefanyika usiku wa kuamkia leo.

Zoezi la ukamataji mabasi hayo limefanyika eneo la Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani hapa, zoezi lilichukua takribani masaa mawili ambapo mabasi hayo yamezuiwa kuondoka mpaka asubuhi huku yakitozwa faini.

Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu


Harnaam Kaur ni mwanamke anayefuga ndevu
Mwanamke anayefuga ndevu
"Nilianza kufuga ndevu nilipokuwa na umri wa miaka 16.
Nilikuwa na nywele zilizojaa usoni tangu nibalehe, ikafikia wakati ambapo nilifikiri iwapo nywele hizo zingeendelea kuota katika uso wangu nitazikubali na kuziruhusu kumea.
Nilichokozwa shuleni kutokana na nywele zilizokuwa zikimea usoni.
Wazazi wangu walikuwa na wasiwasi na hali yangu ya afya kwa jumla.
Uchunguzi wa hospitali ulibaini kwamba nina homoni nyingi za kiume ikilinganishwa na zile za kike swala linalosababisha kumea kwa ndevu hizo" anasema Harnaam.

Nilijaribu kila njia kuzinyoa nywele zilizokuwa zikimea usoni mwangu.
Nilijaribu kubadili rangi ya ngozi, kunyoa, kutumia mafuta ya kuondoa nywele bila mafanikio.
Nilinyoa kila siku. Lakini nywele hizo ziliendelea kuwa nyeusi na ndefu zaidi.
Nilikuwa na marafiki walionitunza walionijali sana huku ndugu yangu akinisaidia sana.
  Mwanamke anayefuga ndevu asema hajuti kufanya hivyo
Mwanamke anayefuga ndevu asema hajuti kufanya hivyo
Kuhusu nduguye alisema amekuwa mtu ambaye nimekuwa nikimtegemea sana.
Alikosana na marafikize waliomchokoza alipoanza kuachilia ndevu zake kumea.
Niliugua na kuchoka na uchokozi huo na nilitaka kupinga tamaduni za kijamii kuhusu urembo.
Kuna watu wengi ambao ni waathiriwa wa uchokozi na aibu za kimwili, kwa hivyo mimi huifanya kuwa kazi yangu kutoa hamasa na kuwasaidia watu kukabiliana na madhara ya tatizo hilo.
Nimegundua kwamba nina nguvu, mimi ni mrembo na mtu asiyeogopa.
Sikujua nina vipaji vyote hivi.
Wakati unapochokozwa kile unachosikia ni mambo mabaya kukuhusu.
Kwa hivyo wakati nilivyoanza kujipenda na msimamo wote huo dhidi yangu ndiposa nilianza kugundua kwamba mimi ni mrembo, nikijiambia kwamba nina thamani.
Niligundua kwamba mimi nina nguvu zaidi ya watu wanavyojua.
Wakati huohuo, sidhani nimefika kiwango ambapo najiamini sana.
  Haarnmkaur na nduguye
Haarnmkaur na nduguye
Kutokana na hali yangu mwili wangu huwa unabadilika mara kwa mara kwa hivyo ninalazimika kuweka juhudi za kujikubali.
Kwa sasa nina ugonjwa unaobadili rangi yangu tumboni- ulianza kwa ghafla kwa hivyo nalazimika kuukubali.
Safari ya kujipenda ni swala linalofanyika katika kipindi cha miezi ama hata miaka.

Bado naendelea kubadilika, naendelea kukuwa na kila siku inayopita, najaribu kutafuta kitu kipya cha kujipenda.
Kuna watu wengi ambao wamesahau umuhimu wa kujipenda .
Tunataka watu wengine kutupenda, lakini iwapo hatuwezi kujipenda, ni vipi tutaweza kueneza mapenzi hayo na watu wengine?
Nimegundua kwamba stori yangu inawasaidia watu kukutana nami.
Wanaweza kujieleza kwangu ili niwasaidie."

Ijumaa, 15 Septemba 2017

Breaking Newwwwzzzz: Mlipuko waripotiwa katika treni Uingereza

Maafisa wa zima moto wakiwasili katika eneo la mlipuko nchini Uingereza

 Maafisa wa zima moto wakiwasili katika eneo la mlipuko nchini Uingereza
Ripoti za hivi punde kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa mlipuko umetokea kwenye treni zinazokwenda chini kwa chini katika eneo la Kusini magharibi mwa mji mkuu wa London.
Abiria katika kituo cha wazi cha Parsons Green wamesema katika mitandao ya kijamii kwamba baadhi ya watu wamepata majeraha ya uso na kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa wakati watu walipokuwa wakijaribu kutoka katika treni hiyo.
Idara za kutoa huduma ya dharura zimewasili katika eneo hilo.

Picha zimeonyesha ndoo nyeupe ikiungua ndani ya mfuko unaotumika katika maduka ya jumla, lakini mlipuko huo hauonyeshi uharibifu mkubwa ndani ya treni hiyo.
Mashahidi wameelezea kuona abiria mmoja akiwa na majeraha ya uso.
  Mfuko uliokuwa ukichomeka ndani ya treni hiyo
Mfuko uliokuwa ukichomeka ndani ya treni hiyo
Wengine wamesema kuwa kulikuwa na wasiwasi huku abiria wakitoka ndani ya treni hiyo katika kituo cha treni cha Parsons Green.
Huduma ya ambalensi inasema kuwa imetuma kikosi cha kukabiliana na majanga katika eneo hilo.
Mtangazaji wa BBC Riz Lateef aliyekuwa katika kituo hicho cha treni akielekea kazini alisema: kulikuwa na wasiwasi mwingi huku watu wakitoka ndani ya treni hiyo wakihofia maisha yao huku wakisema kulikuwa na mlipuko.
Wengi walipata majeraha ya kukatwa wakijaribu kutoroka eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Sophie Raworth anasema kuwa alimuona mwanamke mmoja akiwa na majareha ya moto usoni na miguuni.

Spika Ndugai:Wabunge Msikae Baa Muda Mrefu

Spika Ndugai leo amewausia wabunge wanzake kuwa makini na usalama wao kwa kuchukua hatua zaidi za kujilinda, ikiwemo kutokaa baa mpaka usiku wa manane ili kujiepusha na matatizo mbali mbali yatakayoathiri usalama wao. .

Akizungumza muda mfupi leo Ijumaa kabla ya kuahirishwa kwa Bunge, Ndugai aliwataka wabunge kutokaa sana katika mabaa.

“Yaani tuchukue hatua katika maisha yetu kama mnavyosikia matukio ni mengi katika nchi yetu. Ni vizuri usalama unaanza na wewe mwenyewe kwanza,” amesema.

Amesema vyombo vya usalama vinavyowalinda vinakuwa vinaongezea kidogo na kuwataka kutazama nyendo zao za namna ambavyo wanaishi.

“Kwa wale tuliozoea saa 7 ndio tunarudi nyumbani  basi tuanze kurudi mapema kidogo. Lakini pia tuangalie usalama wa familia zetu na tuwaambie wapigakura naona siku hizi watoto wanapotea, watoto wanauawa,” amesema.

Amewataka wabunge kuwapelekea familia  ujumbe huo kuwa wawe makini na watoto wao wakati wa kwenda shule na maeneo mengine kwa kuhakikisha wanajua mtu anayewapeleka shule na kuwachukua.

“Hayo mambo yanayofanana na hayo. Ushauri ni wa ujumla tu,”amesema.

Aliwataka wabunge kuendelea kumuombea Tundu Lissu na wale watakaopata nafasi ya kwenda kumuona jijini Nairobi wampelekee ujumbe.

Amesema pia wabunge wawaombee wenzao ambao wamekwenda kumuuguza mbunge huyo lakini wanatukana kwa sababu hawajui watendalo.

Ushauri huo umekuja siku chache baada ya Lissu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Jumanne, 12 Septemba 2017

Mpigapicha ashinda kesi kuhusu 'selfie ya tumbili'

Monkey selfie

Peta walidai huo alikuwa tumbili jike kwa jina Naruto lakini Bw Slater alidai alikuwa tumbili tofauti
Mpigapicha mmoja ameshinda kesi iliyodumu kwa miaka miwili dhidi ya kundi la kutetea haki za wanyama kuhusu haki za kumiliki picha ambayo ilipigwa na tumbili.
Tumbili kwa jina Naruto alidaiwa kujipiga picha hiyo katika msimu mmoja Indonesia mwaka 2011 alipoichukua kamera iliyokuwa inamilikiwa na David Slater kutoka Monmouthshire.
Majaji nchini Marekani wamesema tumbili huyo hangekabidhiwa haki miliki ya picha hiyo.
Watetezi wa haki za wanyama kutoka kwa kundi la People for the Ethical Treatment of Animals (Peta), ambao walikuwa wamewasilisha kesi hiyo kwa niaba ya tumbili huyo, walisema mnyama huyo anafaa kufaidi kwa njia fulani.

Kesi hiyo ya Peta "kwa niaba ya tumbili" imetupiliwa mbali lakini Bw Slater amekubali kutoa asilimia 25 ya mapato yatakayotokana na picha hiyo siku zijazo.
Kwenye taarifa ya pamoja, Peta na Bw Slater, wamesema mpiga picha huyo atatoa robo ya pesa atakazopata kupitia uuzaji wa selfie za tumbili huyo kwa mashirika ya hisani yaliyosajiliwa "ambayo yamejitolea kulinda maslahi au makazi ya Naruto".
"Kesi hiyo ya Peta ilikuwa imezua mjadala mkubwa kimataifa kuhusu haki za kimsingi za wanyama kwa jumla, na si zaidi kwa jinsi wanavyotumiwa na binadamu kujifaidi," wakili wa Peta, Jeff Kerr amesema.
Bw Slater, kutoka Chepstow, alikuwa amejitetea kwamba anafaa kuimiliki picha hiyo akisema alifanya juhudi sana kabla ya kuipata picha hiyo.
Alisema juhudi zake hazingeweza kulipwa hata kwa kudai hakimiliki pekee.
  David Slater na tumbili Indonesia
David Slater amesema ilimchukua siku tatu za 'kazi ngumu' kupata picha hiyo
Bw Slater akijitetea alisema ilimchukua siku tatu za 'kazi ngumu' kupata picha hiyo. Alisema pesa zinazotokana na kutumiwa kwa picha hiyo, aliyoipiga katika kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia mwaka 2011, ni zake.
"Ilinichukua siku tatu za kutoa jasho kupata selfie hii kuhakikisha ninakubalika na kundi la kima kabla yao kunikubali kiwakaribie vya kutosha na kuwaonyesha kamera yangu," Bw Slater aliambia BBC mwaka 2015.
"Tatizo ni kwamba, watu wengine wanajaribu kuiba haki zangu za umiliki na nitapinga hilo."
  David Slater
Slater alikuwa amesema angekuwa taabani kifedha akishindwa kwenye kesi hiyo au aamrishwe kulipa gharama ya kesi
Selfi hiyo ilisambazwa sana kote duniani na mtandaoni. Waliompinga Slater wanasema hawezi kuwa na hakimiliki ya picha hiyo kwa sababu ilipigwa na mnyama.
    Bw Slater amesema yeye ni mhifadhi wa wanyama na mazingira na kwamba kuvuma kwa picha hiyo kumewasaidia sana wanyama Indonesia.
    Kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kama "Naruto v David Slater" lakini kulikuwa pia na mzozo kuhusu utambulisho wa tumbili aliyehusika.
    Peta walidai alikuwa tumbili jike kwa jina Naruto lakini naye Bw Slater akadai alikuwa tumbili tofauti wa kiume.
    Lakini majaji wa mahakama ya rufaa mjini San Francisco wamekubali hoja za Bw Slater baada ya vuta nikuvute ya miaka miwili mahakamani.
    Taarifa ya pamoja ya Peta na Bw Slater imesema kesi hiyo "iliibua masuala muhimu kuhusu kupanuliwa kwa haki za kisheria kwa wanyama, ambao si binadamu".

    Vimbunga vinavyopewa majina duniani

      Kimbunga Hermine

    Umewahi kusikia vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, kilichoitwa Matthew ambacho kilikumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani mwezi Oktoba mwaka 2016.
    Mwezi uliotangulia kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida.
    Lakini kinachokumbukwa sana ni kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama nchini Marekani.
    Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina?
    Uharibifu wa kimbunga Hermine

    Vimbunga vinavyopewa majina

    Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.
    Zamani, ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume yalianza kutumiwa.
    Huwa kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko.
    Hii ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena hadi 2022.

    Majina kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.
    Orodha hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu iliyotolewa.
      North Atlantic, Caribbean and Gulf of Mexico storm names
    World Meteorological Organisation

    Majina yanavyoacha kutumiwa

    Baadhi ya majina huacha kutumiwa, sana kunapotokea uharibifu mkubwa au hasara kubwa hivi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.
    Mfano ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu mkubwa Marekani.
    Kimbunga hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana uliathirika sana.
    Katika WMO kuna kundi la wataalamu liitwalo Kamati ya Vimbunga vya Tropiki ambalo hukutana kila mwaka.
    Kundi hilo ndilo huamua ni majina yapi yatatumika tena na ni yapi yataacha kutumiwa.

    Majina yaliyoacha kutumiwa

    Kando na Katrina, kuna majina mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mitch, kutokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
    Tegucigalpa nchini Honduras
    Kimbunga Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa. Majina hayo hayatumiwi tena.
    Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo yaMartinique, Barbados na St Eustatius.
    Wakati huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.

    Majina yaliyoacha kutumiwa tangu 1954.

    Retired hurricane names

    Majina maeneo mengine duniani

    Katika maeneo mengine duniani, huwa kuna utaratibu tofauti wa kuvipa majina vimbunga.
    Lakini majina yote hupitia kwa WMO.
    Kwa mfano, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini, kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.
    Baada ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata.
    Kwa mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na kitakachofuata kinafaa kuitwa Kaikui (jina la kwanza China).
    Kimbunga cha sasa maeneo hayo ni Chaba (jina la nafasi ya nne Thailand).

    Kilichotokea majuzi kiliitwa Megi na ambacho kiliathiri maeneo ya China na Taiwan. Jina hilo ni la nafasi ya nne chini ya majina ya Korea Kusini.
      List of Western North Pacific and South China Sea storm names
    World Meteorological Organisation
    Majina ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio.
    Kuna jina kwa kila alfabeti, isipokuwa Q, U, X, Y na Z, ambao ndio utaratibu unaotumiwa kuvipa majina vimbunga Atlantiki Kaskazini.

    Kisiwa cha bilionea Richard Branson chapigwa na Irma

    Richard Branson

    Bilionea Sir Richard akitathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Irma
    Sir Richard Branson amesema mengi ya majengo na mimea na miti katika kisiwa chake cha Necker katika eneo la Caribbean vimeharibiwa kabisa na Kimbunga Irma.
    Necker ni moja ya visiwa 50 ambavyo hujumuisha Visiwa vya British Virgin vya Uingereza (BVI).
    Sir Richard amesema alitembelea kisiwa kinachokaribia zaidi kisiwa chake cha Necker na kujionea "moja kwa moja ukali na ukatili wa kimbunga hicho".
    Kimbunga hicho kiliua watu watano katika eneo hilo la Uingereza.
    Waziri mkuu wa BVI ameomba usaidizi wa muda mrefu kutoka kwa Uingereza.
    Sir Richard na wenzake wako salama.
      Necker
    Majumba katika kisiwa cha Necker yaliyumbishwa na mengine kuporomoka
    Kimbunga Irma kilipitia Visiwa vya Virgin vya Uingereza katikati mwa wiki iliyopita.
    Sir Richard amesema: "Tulihisi nguvu kali zaidi za kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kupiga kutoka Bahari ya Atlantiki. Lakini tulikuwa na bahati sana kwamba tulikuwa na handaki imara ambalo tulikuwa tumelijenga katika Jumba Kuu la Necker na tulikuwa na kwamba watu wote waliokuwa kisiwani wakati wa kimbunga wako salama."
      Necker Island
    Sir Richard anasema mimea, miti na nyasi katika kisiwa hicho vimeharibiwa
    Amesema kinachofaa kuangaziwa zaidi ni "matukio ya maelfu ya watu ambao wamepoteza nyumba zao na bishara zao".
    Mawasiliano bado yamekatizwa katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Sir Richard kwa sasa yuko katika kisiwa cha Puerto Rico, kilomita kadha magharibi mwa visiwa hivyo vyake.
      Necker Island damage
    Alisema alikuwa ameenda huko "kuratibu zaidi juhudi za kutumwa kwa misaada zaidi na kusimamia mipango ya ukarabati wa mijengo katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na maeneo ya Caribbean kwa jumla."
    Sir Richard amesema atazungumza na serikali mbalimbali na mashirika ya misaada, pamoja na vyombo vya habari.
    Amesema baadaye atarejea kupigania zaidi kufanywa kikao cha kuchangsha misaada  kwa Visiwa vya Virgin vya Uingereza ili kusaidia juhudi za ukarabati.

    Visiwa vya Virgin vya Uingereza ni eneo linalojitawala la Uingereza ambalo humtambua Malkia Elizabeth wa Uingereza kama kiongozi wa taifa.
    Waziri mkuu wa visiwa hivyo Orlando Smith amesema watahitaji misaada kwa kipindi kirefu kutoka Uingereza.
      Necker island before the storm
    Kisiwa cha Necker kabla ya kimbunga

    Jumatatu, 11 Septemba 2017

    Watu 7 wauawa kwa kupigwa risasi Dallas Marekani

    A video screengrab shows police vehicles arriving at the scene of the shooting in Plano, Dallas, Texas

    Watu 7 wameuawa kwa kupigwa risasi Dalllas Marekani

    Mtu mwenye bunduki amewaua watu saba kwenye nyumba moja mjini Dallas, Texas nchini Marekani, kabla ya kuuawa kwa kipigwa risasi na polisi.
    Watu wawili ambao nao walipigwa risasi wako hospitalini.
    Msemaji wa polisi David Tilley alisema kuwa mshambuliaji aliuawa na polisi kwa kwanza ambaye aliyefika wakati wa ufyatulianaji wa risasi. Polisi huyo hakujeruhiwa.
    Kile kilichochangia shambulizi hilo bado hakijulikani au ikiwa mshambuliaji aliwafahamu waathiriwa bado ni kitendawili.

    "Tunajaribu kuangalia suala hili kwa kina," Bwa Tilley alisema.
    Gazeti moja huko Dallas liliripoti kuwa wale waliouawa walikuwa wakitazama timu ya Dallas Cowboys, ambayo ni timu ya kandanda ya Marekani wakati waliposhambuliwa.
    Polisi hawajatoa jina la mshambuliaji au muathiriwa yeyote lakini wote wametajwa kuwa watu wazima.

    Miili iliyohifadhiwa kwenye kaburi karne ya 16 yagunduliwa Misri

    An Egyptian antiquities worker works on a coffin in the recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom, at the Draa Abu-el Naga necropolis near the Nile city of Luxor

    Miili iliyohifadhiwa kaburini karne ya 16 yagunduliwa Misri
    Wana akiolojia wamegundua kaburi lenye miili ya mwanmke na watoto wake waliokuwa wamehifadhiwa karne kadhaa zilizopita.
    Kaburi hilo linaloaminika kuwa la karne ya 16 hadi 11 BC lilipatikana karibu na mji wa Luxor kilomita 70 kutoka Cairo.

    Kati ya vifaa vilivyo patikana ndani ya kaburi hilo ni sanamu ya mfua viuma Amenemhat akiketi kando na mke wake.
    Egyptian archaeologists work on mummies at a recently discovered tomb in the Draa Abul Nagaa necropolis, Luxor's West Bank, 700km south of Cairo, Egypt, 9 September 2017
    Kaburi lilipatikana eneo la Draa Abul Naga
    Kulingana na wana akiolojia mama alifariki akiwa na miaka 50, na uchunguzi ulionyesha kuwa alifariki kutoka na ugonjwa wa mifupa.
    Watoto wawili wa kiume walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30 na walikuwa wamehifadhiwa katika hali nzuri,
    Skulls and hands are seen next to coffin in the recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom, at the Draa Abu-el Naga necropolis 
    Miili hiyo ilitajwa kuwa katika hali nzuri
      A carved sandstone statue depicting the tomb's owner Amenemhat sitting on a high back chair beside his wife at a recently discovered tomb in the Draa Abul Nagaa necropolis, Luxor's West Bank, 700km south of Cairo,
    Kati ya vifaa vilivyo patikana ndani ya kaburi hilo ni sanamu ya mfua viuma Amenemhat akiketi kando na mke wake.
      Egyptian antiquities worker brushes a coffin in a recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom at the Draa Abu-el Naga
    Miili iliyohifadhiwa kaburini karne ya 16 yagunduliwa Misri
    Chanzo: BBC

    Jumatatu, 4 Septemba 2017

    Askari ya FFU akamatwa sakata la utekaji watoto

    Wakati Mtuhumiwa wa matukio ya utekaji watoto, Samsom Petro (18), ambaye jana alifikishwa Arusha kwa ajili ya kuonyesha sehemu alipowaficha watoto, amebainika kuwa anaishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa.

    Inadaiwa kuwa askari huyo pia anashikiliwa na polisi kwa mahojiano tangu Agosti 27 wakati kikosi maalum cha polisi kilipozingira nyumba aliyopanga.

    Petro, ambaye alikamatwa juzi akiwa Katoro mkoani Geita, anatuhumiwa kuwateka watoto wawili, Moureen David(6) na Ikram Salim(3) na hadi jana jioni alikuwa ameandamana na polisi katika eneo la Njiro ambako alidai aliwatelekeza watoto hao.

    Lina Kajuna ambaye ni mmiliki wa nyumba ya aliyekuwa amepanga askari huyo wa FFU, alisema ana miaka miwili tangu ampangishe.

    Kajuna alisema mtuhumiwa wa utekaji, Samson Petro alifika Arusha mwezi Juni na amekuwa akiishi na kaka huyo na tangu amefika amekuwa akimuona kuwa na tabia ambazo sio nzuri, kama wizi wa kuku.

    “Alipofika muda mfupi tulianza kuona matukio ya wizi nikaibiwa kuku na pesa mimi nikamlalamikia kaka yake lakini akasema tuendelee kumchunga,”alisema

    Alisema baada ya hali ya wizi kuendelea, alikwenda kulalamika kwa balozi wa eneo wanaloishi ambalo ni Mtaa wa Olkeria, Daniel Kichau kutaka wamchunguze.
     
    Hata hivyo, alisema wakati akichunguza, ndio matukio ya utekaji yakaanza na tangu Agosti 25 alitoweka nyumbani hadi jana walipopata taarifa kuwa amekamatwa.
     
    Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari alisema jana kuwa kikosi chao cha wananchi walifika kwenye nyumba hiyo na kubaini alikuwa anaishi na askari huyo wa FFU .
     
    “Tumemhoji mama mwenye nyumba ametupa ushirikiano mkubwa na ni kweli Samson alikuwa anaishi kwenye nyumba yake na kaka yake ambaye alikamatwa tangu Agosti 27,” alisema.
     
    Katika msako wa jana, polisi walikwenda peke yao na mtuhumiwa na kuwaacha wazazi wa watoto hao wakiwasubiri kituo kikuu cha polisi. Askari walisema wanaendelea na msako wa watoto hao wawili.

    Rubani wa jeshi adondoka kutoka kwenye helikopta Ubelgiji

       

    Agusta helicopter, July 2012 file pic 
    Helikopta aina ya Agusta hutumiwa na majeshi mengi na idara za polisi duniani                
    Wanajeshi wa Ubelgiji wanamtafuta rubani wa helikopta ya jeshi ambaye alianguka kutoka kwa ndege hiyo wakati wa maonesho ya ndege za kivita.
    Wanajeshi watatu waliruka kutoka kwa helikopta hiyo aina ya Agusta A-109 wakiwa na parachuti, lakini rubani huyo na msaidizi wake hawakuwa na parachuti, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti.
    Taarifa zinasema rubani msaidizi aliwasaidia wanajeshi hao watatu kuruka nje, lakini aliporudi kutazama kiti cha rubani akashangaa kupata rubani hayupo.

    Alichukua usukani na kuanza kuiongoza ndege.
    Maonesho hayo yalikuwa yakifanyika katika eneo la Amay, karibu na mji wa Liège.
    Rubani huyo alianguka mita mia kadha kutoka angani.
    Sababu ya rubani huyo kuanguka bado haijulikani.
    Belgian search in Amay, 3 Sep 17Wanajeshi wanamtafuta rubani huyo maeneo ya mashambani Amay, 28km (maili 17) kutoka Liège                


    Jumapili, 3 Septemba 2017

    Njiwa aliyetumiwa kusafirisha mihadarati hadi gerezani Argentina

      Pigeon found carrying drugs in KuwaitMaafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na tembe za madawa ya kulevya                

    Polisi nchini Argentina walimpiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja, kwa mujibu wa mamlaka za gereza.
    Njiwa huyo alionekana akiruka hadi uwanja wa gereza lililo mji wa Santa Rosa.
    Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake uliokuwa na tembe za madawa ya kulevya.
    Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.

    Gazeti la Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe uliokuwa na tembe 44 za madawa ya kulevya.
    Magereza nchini Argentina yalionya mwaka 2013 kuwa walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.
    Watu watatu walikamatwa na njiwa 15 kupatwa baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.
    Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.

    Jumamosi, 2 Septemba 2017

    KENYATTA HOI RAILA KICHEKO baada ya Mahakama kufutilia mbali ushindi wa Kenyatta

      Rais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakoraRais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakora                


    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelitaja jopo la majaji wa mahakama ya juu liliobatilisha uchaguzi wake wa urais kuwa 'Wakora' .
    Awali alikua ametaka kuwepo na utulivu na kusema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama lakini baadaye akaonyesha msimamo tofauti katika mkutano wa hadhara.
    Mahakama hiyo ilisema kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulikumbwa na udanganyifu na kuagiza kufanyika kwa uchaguzi mwengine katika kipindi cha siku 60.
    Uchaguzi huo uliokuwa umezua wasiwasi wa kutokea kwa ghasia za baada ya uchaguzi kama zile zilizotokea 2007.

    Ijapokuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliopita hazikufikia kiwango cha 2007, ghasia za siku kadhaa zilisababisha vifo vya watu 28.
    Tume ya uchaguzi nchini Kenya ilikuwa imemtangaza rais Kenyatta kuwa mshindi kwa kiasi cha kura milioni 14 lakni matokeo hayo yakapigwa mahakamani na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.
    Katika uamuzi wake Jaji mkuu David Maraga alisema kuwa uchaguzi huo wa tarehe 8 mwezi wa nane haukufanyika kulingana na katiba na hivyo basi kubatilisha matokeo yake.
    Katika hotuba aliyotoa katika runinga, rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa ni muhimu kuheshimu sheria hata iwapo unatofautiana na uamuzi wa mahakama ya juu.
    Alitaka kuwepo kwa utulivu akisema: Jirani yako ataendelea kuwa jirani yako licha ya lololote litakalotokea.
    Ujumbe wangu muhimu leo ni Amani. Lakini alikuwa na msimamo mwingine wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika soko moja jijini Nairobi.
    Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta                                   Raila Odinga akifurahia uamuzi wa mahakama uliofutilia mbali uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta                
    Aliwataja jaji Maraga na majaji wenzake kuwa ni wakora, akisema aliamua kubatilisha uchaguzi wake.
    Alimuonya jaji Maraga kwamba baada ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali bado yeye ndio rais na sio tena rais mteule kama ilivyokuwa.
    Mnanielewa? Maraga anafaa kujua kwamba hivi sasa anakabiliana na rais aliye madarakani, alisema bwana Kenyatta mwenye umri wa miaka 55.
    Tunawaangalia kwa karibu. Lakini wacha tumalize uchaguzi mwanzo, Hatuogopi.
    Kufuatia uchaguzi huo waangalizi wa kimataifa kutoka muungano wa Ulaya, ule wa Afrika pamoja na wale wa Marekani walikuwa walisema kuwa hakuna udanganyifu uliofanyika na kumtaka Odinga kukubali kushindwa.

    Watia mimba wanafunzi watafuta kinga kwa waganga wa kienyeji


    IMANI potofu zinadaiwa kutumiwa na watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapewe kinga wasikamatwe.
    Diwani wa kata ya Manchali, Mary Mazengo alisema hayo juzi wakati wa mkutano uliowahusisha viongozi wa wilaya, madiwani, watendaji wa vijiji na kata ulioandaliwa na Shirika lisilokuwa na Kiserikali linalojihusisha na utetezi wa wanawake na watoto la Woman Wake Up (Wowap). Alisema baadhi ya watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi wamekuwa wakikimbilia kwa waganga wa kienyeji ili wapate kinga wasikamatwe ambapo huko hutaja majina ya watu waliokuwa wakiwafuatilia.
    “Imani potofu imekuwa ikiingia katika ufuatiliaji wa watia mimba kwa wanafunzi kwa baadhi ya maeneo watu wanakwenda kwa waganga wa kienyeji na kuwataja wanaowafuatilia,” alisema. Alisema hilo ni tatizo kubwa katika maeneo ya vijijini na elimu zaidi inahitajika ili imani hiyo isitumike katika kuharibu maisha ya wasichana wadogo ambao wana ndoto za kujiendeleza kielimu.
    Alisema viongozi wana wajibu wa kuhakikisha wanawafuatilia watuhumiwa ili wafikishwe kwenye mikono ya sheria na si kutishika na wanaotumia imani hizo kuwa kama kinga kwao ili wasikamatwe. Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai alisema elimu imekuwa ikitolewa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kwenye majukwaa kama vile mikutano ya vijiji, magulio, sherehe za kimila, mikutano ya vijana, matukio ya michezo juu ya haki za binadamu, jinsia na ukatili wa kijinsia.

    Majambazi wateka basi, wapora abiria na madiwani


    MAJAMBAZI sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana.
    Miongoni mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana.
    Akizungumzia tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge.
    Shumbi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na wengine mapanga na fimbo.
    Alisema watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwachukua abiria takribani dakika 10 wakigoma kushuka kabla ya baadhi walioonekana kutishika zaidi kuanza kushuka kwa kuruka kupitia madirishani.
    Alisema baadaye iliwalazimu abiria wote kushuka na ndipo jambazi wakaanza kuwasachi na kunyang’anya fedha taslimu na simu za mikononi huku walioonekana kubisha, wakipigwa viboko.
    “Baada ya kushuka tulilazwa chini na kuanza kukaguliwa ambapo walichukua fedha na simu na mimi mwenyewe ni muathrika wa simu na fedha kidogo nilizokuwa nazo. Ushauri wangu ni kuwa mabasi kama haya yaanze safari saa moja asubuhi badala ya saa kumi na moja ama kumi na mbili,” alieleza diwani huyo.

    MTOTO APAMBANA NA SIMBA AJERUHIWA PAJA


    MTOTO wa kiume, Nyutuliangila Madirisha (13) amejeruhiwa vibaya paja lake la kulia baada ya kuzinduka usingizini na kwa ujasiri wa kipekee, akamshambulia simba aliyekuwa akimpapasa mwilini kwa kumpiga ngumi usoni.
    Kutokana na tukio hilo, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Isinde Kata ya Mtapenda katika Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele mkoani Katavi, amelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa matibabu baada ya simba huyo kumjeruhi vibaya paja lake la mguu wa kulia.
    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda, Dk Theopister Elisa amethibitisha kuwa mtoto huyo amepokelewa na kulazwa hospitalini hapo kwa matibabu, akiwa amejeruhiwa paja lake la mguu wa kulia.
    Akisimulia mkasa huo, mtoto huyo alisema kuwa usiku huo wa tukio alikuwa amelala fofofo pembeni mwa zizi la ng’ombe lililopo nyumbani kwao, lakini alishtuka ghafla usingizini baada ya kuhisi kuwa alikuwa akipapaswa mwilini na mnyama.
    Baba mzazi wa mtoto huyo, Madirisha Lubinza ambaye pia anafuga mbwa wengi kwa ajili ya ulinzi, alieleza kuwa usiku wa tukio hilo alisikia kelele za mtoto wake akiomba msaada huku simba akiunguruma kwa nguvu, ambapo alitoka nje ya nyumba yake. Alidai aliwaita na kuwaamuru mbwa wake, wamshambulie simba huyo ndipo walipoanza kumbwekea na kumtisha na baadaye simba huyo aliingiwa hofu na kukimbilia porini.