Alhamisi, 29 Mei 2014

WATUHUMIWA WA MABOMU ARUSHA KIZIMBANI

Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.
Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.
WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu, kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

 
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13, katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena Juni 12 CHANZO MTAA KWA MTAA

PEP GADIOLA AFUNGA PINGU ZA MAISHA

2,w=650,c=0.bild
Hatimaye kocha wa klabu bingwa ya Ujerumani Bayern Munich, Pep Guardiola amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Cristina Serra leo hii, na bosi huyo wa Bayern na mchumba wake waaliamua kufanya ndoa hiyo kwa kawaida kabisa bila shamra shamra zozote.Ndoa hiyo imefungwa kiserikali huko Matadepera, Catalonia, Spain.Pep na mchumba wake Cristina, kwa pamoja na watoto wao watatu na wazazi wao, walifanya sherehe ndogo kuhalalisha mapenzi yao.Tazama picha hapo chini namna ndoa ya Guardiola ilivyokuwa

o_MDSIMA20140529_0125_1
Guardiola mwenye shati la kaki na mkewe Cristina mwenye suruali nyeusi pamoja jaketi jekundu na begi jekundu wakisindikizwa na ndugu zao kwenda kufunga ndoa.
i_MDSIMA20140529_0126_1

Jumatano, 28 Mei 2014

NDOA ILIYOVUNJA REKODI YA SIKU 13 YAVUNJWA NA WHATUS


Taarifa iliyoibuka nchini Kenya imeeleza kuwa ndoa ya Boniface Oduor na mrembo Sheila imedumu kwa muda mfupi baada ya kufungwa kwa baraka zote ikiwemo kukamilika taratibu za kuanzia kwa wazazi hadi kanisani.


Oduor alisema kuwa mkewe alimsaliti katika ndoa yao baada ya siku 13 ya harusi yao iliyofanyika wiki ya pasaka ambapo alimfumania mkewe akishiriki tendo la ndoa na mwanaume mwingine ikiwa ni siku 13 tu baada ya harusi yao kwa kumkuta moja ya hoteli jijini Nairobi Kenya.

Wawili hao walikua wakirejea nyumbani baada ya honeymoon ya siku tano pamoja katika jiji la kifahari la Malindi pwani ya Kenya ambapo harusi yao ya kufana ilifungwa kwenye kanisa la Pentecostal Assemblies of God Diani Mombasa.

Oduor amedai harusi yake ilikua ni ya kupoteza muda na pesa na ameapa kutoishi tena na mwanamke huyo na kujihusisha na uhusino wa kimapenzi tena kwani hana imani tena na Wanawake.

Kuachana kwao pia kulifanyika kwa kasi baada ya kugundua kwamba Sarah alikua amesambaza picha zake za uchi kupitia WhatsApp.

MSAADA MSAADA MSAADA! KUMUOKOA MWAMKE WA SUDAN ALIYEHUKUMIWA KIFO

140527142840 mama sudan 512x288 bbc nocredit 9905b
Mwanamama Meriam siku ya harusi yake
Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.
Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
Meriam aliyezaliwa na baba muislam na mama mkristo, alihukumiwa na mahakama ya ya kiislam.
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiislam ambayo inasema kuwa mwanamke muislam hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimhukumu adhabu ya mijeledi mia moja, adhabu ambayo itatekelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo, dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muislam hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014 aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muislamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waislam ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
JAMII YA KIMATAIFA INAOMBWA LUSAIDIA KUMUOKOA MAMA HUYU AMBAYE KIMSINGI ANASTAHILI KUISHI. INGEFAA KAMA MTU ANGEANZISHA PETITION AMBAYO WAPENDA AMANI WATAWEZA KUSAINI ILI KUSAIDIA KATIKA HILI. (TK)
CHANZO BBC

MWANAMKE ACHANWA NA WEMBE DAR

Stella Mbinga akiwa na majeraha ya viwembe.

INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa viwembe na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama na kuringishiana hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi, mwingine anafanya vile. Cha kushangaza huwa wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba nani anakula vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa juzi Stella alikuwa amekaa kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita akawakuta wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na vicheko vyao, akahisi wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa Stella, kumbe alikuwa na kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja wa majirani wa wanawake hao.

Jumanne, 27 Mei 2014

SIMU YA JUMA ILIVYOMLETEA MAJANGA NA KUMWINGIZA MATATIZONI.

http://www.cellphonebeat.com/wp-content/uploads/strwiki/1336990079.jpgBwana Juma ni Dereva Taxi maeneo ya Mwanyamala kwa Kopa siku moja alifuatwa na jamaa mmoja ampeleke sinza kwenye nyumba Fulani ya wageni .

Walipokaribia pale Yule jamaa akasema ameishiwa chaji kwenye simu yake akamuomba juma simu yake atumie kupiga ili awasiliane na mwenyeji wake pale nyumba ya wageni, simu ya juma haikuwa na hela .


Walipokaribia ile nyumba ya wageni Yule jamaa akaomba kushuka anunue vocha atie kwenye simu ya Juma ili awasiliane na mwenyeji wake, Juma akakubali, jamaa akanunua vocha akaitia kwenye simu ya Juma halafu akawasiliana na mwenyeji wake .

Walipofika sehemu husika jamaa akashuka akaingia ndani ya nyumba kumfuata mwenyeji wake ambaye alikuwa mwanamke huku Juma akiwa ameshaondoka zake kwa sababu alikuwa ameshakamilisha shughuli yake .

Siku iliyofuata iligundulika maiti ya mwanamke ndani ya kile chumba, simu ilikuwa mezani na vitu vingine vyote hakukuonesha kama kulikuwa na vurugu au mikikimikiki yoyote ile.

Uchunguzi wa awali ulifanyika pale chumbani kwenye kifaa cha kuwekea taka na simu ya yule mwanamke, hapo mwili wake ulikuwa chumba cha maiti ukifanyiwa uchunguzi pia.


Kwenye kifaa cha kuwekea taka iligundulika vocha moja iliyotumika, ilipofuatiliwa iligundulika iliwekwa kwenye simu ya Juma yule dereva taxi na ikatumiwa kumpigia huyu mwanamke aliyekutwa na mauti.

Dereva wa taxi akatafutwa akapatikana, kukaguliwa gari yake ikagundulika vocha ingine ya simu iliyotumika katika moja ya milango ya taxi hiyo .

Bwana Juma yuko ndani kwa mashtaka ya mauaji na uchunguzi unaendelea kufanyika mpaka hapo itakapokuja kudhihirika kuwa si yeye aliyefanya tukio hilo.

Inawezekana wewe ukawa ni bwana Juma ajaye, unayependa kugawa simu yako tu kwa watu wapige, watu waingize vocha zao, watu waandike ujumbe mfupi au wafanyie chochote kile bila kujua unachofanya kinaweza kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia.


Simu na namba yako ni mali yako imesajiliwa kwa jina lako, wakati unasajili uliingia mkataba wa kutumia kifaa hicho bila kuvunja sheria zozote za nchi muda wote .


Kina Juma wako wengi, tazama usiwe mmoja wao

MBUNGE WA NKASI ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI


Mbunge wa Nkasi mh. Ally Kessy asema Wazanzibar Wanachosha, ni Mzigo.
Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu kuwa wanabaguliwa, wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu.

Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki, na pia hata umeme hawalipi na maji pia .


Jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo, kuomba muongozo na Kumtaka naibu Spika amwambie Mhe Kessy kamwe asikanyage Zanzibar, hii ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu, na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu.

Mbunge huyu alilalamika kuwa "Naibu Spika Mhe. Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka, sijui nini maana yake"

BOTI YAZAMA ZIWA VICTORIA NA KUUA WATANO

Watu watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria.Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Kagera, George Mayungaalisema ajali hiyo ilitokea Mei 23 mwaka huu saa 8 usiku. Boti
ya Mv Kitoko II waliyokuwa wakisafiria kutoka Bugombe kupitia Kasenye kwenda Mganza wilayani Chato, ilizimika ghafla ikiwa katikati ya ziwa. Alisema boti hiyo inayomilikiwa na Mama Chacha aishiye Muganza ,
ilikuwa na abiria hao watano ambao wote walikufa maji. Maiti
aliyepatikana ni mfanyabiashara raia wa Rwanda, Jane Mlekatete (36)
ambaye mwili wake ulikutwa ukielea. Wengine waliozama ambao
hawajapatikana ni Chikola Filbert (22) mkazi wa Muganza, Mapinduzi
Daud ( 38 ) mkazi wa Mwanza, Asha na Suzy waliotambuliwa kwa jina moja
moja, wote wakazi wa Kasenyi na Mavombe (23) ambaye ni mkazi wa
Muganza. Alisema chanzo cha ajali hiyo ni boti kubeba mzigo mkubwa. Kwa
mujibu wa Kamanda, ilikuwa imebeba magunia 210. Chanzo kingine cha
ajali hiyo ni kwamba licha ya kubeba mzigo mkubwa, ilisafiri usiku
wakati kukiwa na upepo mkali na mawimbi yaliyosababisha injini ya
boti hiyo kuzimika kabla ya kuzama.

MFALME MSWATI KUFILISIKA?


Mfalme Mswati III wa Swaziland, nchi yake yakumbwa na tisho la kufilisika.
Taarifa kutoka nchi ya kifalme ya Swaziland zinasema kima cha fedha katika benki kuu ya nchi hiyo kimebaki dollar laki 8 pekee.
Kamati inayohusika na sera za fedha imesema hela hiyo iliyobaki inaweza kununua bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi kwa mahitaji ya mda wa miezi minne pekee.
Uchumi wa Swaziland umeathirika pakubwa kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi wanaoitegemea sana jirani zao Afrika kusini ambayo ndio soko kubwa la bidhaa za Swaziland.
Zimebaki dola laki 8 pekee katika benki kuu ya Swaziland.
Hata hivyo Patrick Ndzinisa wa benki ya akiba nchini humo ameiambia BBC kuwa hawana wasiwasi kwani kanuni za kimataifa zanatambua uwezo wa nchi kuagizia bidhaa zake kwa muda wa hadi miezi mitatu.
Mwaka 2011 Swaziland iliiomba Afrika Kusini msaada wa dharura baada ya kuishiwa na hela.
Swaziland ilipiga marufuku vyama vya kisiasa nchini humo tangu 1973 na imeshtumiwa kwa rekodi yake mbaya ya uvunjaji wa haki za binadamu. Wakereketwa wa kupigia kampeni mageuzi ya
ki-demokrasia mara nyingi hukamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi kisha kuzuiliwa magerezani.
Mfalme Mswati na familia yake wameshutumiwa kwa ubadhirifu na ufujaji wa fedha huku wengi wa raia wa Swaziland wakibaki kuwa miongoni mwa maskini zaidi duniani (TK).

MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU NCHINI MALAWI VURUGU TUPU

Chaotic Malawi election sparks legal battle
Mgombea Urais kwa tiketi ya Democratic Progressive Party (DPP) presidential elections Peter Mutharika (R) akitoka nyumbani kwake akiwa na mgombea mwenza Saulos Chilima, Blantyre, Jumapili. PHOTO/AFP
BLANTYRE - Wiki moja baada ya Uchaguzi Wamalawi bado hawajapata matokeo ya kura zao hadi sasa wagombea wanaburutana mahakamani wakiashiria vurugu.
Asilimia 90 ya kura hizo ilikuwa imehesabiwa hadi Jumapili, haikuwa wazi kama wasimamizi wa kimataifa watatangaza matokeo hayo na kama yatakubalika.

Huku kukiwa na taarifa za uchakachuaji tume ya uchaguzi, rais Banda na Mpinzani wake wamefungua kesi za kupinga matokeo hayo mahakamani.

President Joyce Banda amesema kuwa kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi na hivyo kusema kuwa inabidi kura irudiwa ndani ya siku 90 na kuwa yeye hatashiriki.

Aidha, hakuna uhakika kama ana mamlaka ya kufanya hivyo kikatiba. Mahakama imemuru kura ziendelee kuhesabiwa.

Siku ya Ijumaa iliyopita wakati uhesabuji wa kura ukiendelea Mpinzani mkuu wa rais Joyce Banda bwana Peter Mutharika alikuwa akiongoza kwa asilimia 42 wakati Rais Banda alikuwa na kura asilimia 23 tu.

wananchi wakipiga kura. PHOTO/AFP
 

Jumatatu, 26 Mei 2014

KWA NINI UNAKATA TAMAA HEBU MFUATILIE NICK VUJICIC - NEVER GIVE UP

MAISHA BILA MIGUU WALA MIKONO
Watu wengi wana viungo vyote lakini wanakata tamaa na kumlaumu Mungu kuwa hakuwapa hiki au kile. Hebu fuatilia video za Nick Vujici muaustralia ambaye amezaliwa bila mikono wala miguu lakini anasema hakuna kukata tamaa.

  • Nick Vujicic ni Mchungaji (Pastor) ana historia ndefu na hii hapa ni kwa ufupi tu.

    1. Nicholas James "Nick" Vujicic ni Muaustralia Mkristo muinjili na anaendesha mihadhara ya kuwapa watu motisha wa maisha. Yeye alizaliwa na ugonjwa wa "tetra-amelia syndrome", ambao ni hutokea mara chache sana (rare) ambapo mtu huzaliwa bila miguu wala mikono tazama Wikipedia

    2. Kuzaliwa: December 4, 1982 (age 32), Melbourne, Australia
    3. Mke: Kanae Miyahara (m. 2012)
    Wewe je ni kwa nini unakata tamaa wakati Mungu amekupa viungo vyote au karibu viungo vyote?

    BREAKING NEWZZ: MSANII RECHO HATUNAYE TENA


    Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.

    Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
    PICHA: Makatab za GPL

    MACHINGA WAUA ASKARI WA JIJI

    KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana wanaodaiwa ni Wamachinga wamemuua askari mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga na stuli kichwani wakati akitimiza majukumu yake.Marehemu Stephano Benjamin Komba (36) ambaye aliyekuwa na cheo cha sajenti.

    Akizungumza na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa kuuaga mwili huo, Mkuu wa Oparesheni Manispaa ya Ilala, Charles Wambura alimtaja marehemu kwa jina la Stephano Benjamin Komba (36) aliyekuwa na cheo cha sajenti.
    Mke wa marehemu Stephano Benjamin Komba (mwenye kilemba cheupe).
    Alisema tukio hilo lilijiri Mei 16, mwaka huu, saa 7.30 mchana kwenye Mtaa wa Raha Kariakoo.
    “Marehemu alikuwa na askari wengine walikamata baadhi ya bidhaa za Wamachinga kwa lengo la kuwaondoa lakini ghafla walivamiwa na kundi la wafanyabiashara hao ambapo Sajenti Komba akapigwa kichwani kwa stuli hali iliyomfanya apoteze fahamu kwa kuvuja damu nyingi.
    “Askari walipambana na hao Wamachinga na kufanikiwa kumuokoa Sajenti Komba lakini akiwa na hali mbaya.
    Mke wa Marehemu Stephano Benjamin (katikati) akisaidiwa na jamaa wa karibu msibani kumuaga marehemu mume wake.
    “Walimkimbiza Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo walimpeleka Muhimbili ambapo alifariki dunia saa 2:00 usiku,” alisema Wambura.
    Mwili wa marehemu uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mbagala na kusafirishwa kwao Songea, mkoani Ruvuma kwa mazishi.
    Mapadri wakiongoza ibada ya kumuaga marehemu Stephano Benjamin kwa safari yake ya mwisho.
    Wambura aliongeza kuwa, hakufurahishwa na kitendo hicho cha Wamachinga kuchukua sheria mkononi.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutii sheria bila shuruti (TK).

    APIGWA HADI KUFA NA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA KARANGA NA BAISKELI WILAYANI KAHAMA

    MKAZI wa Shinyanga Julius John [30] ameuawa na wananchi wilayani Kahama, kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba baiskeli na karanga zenye ujazo wa gunia moja.
    Tukio hilo limetokea baada ya Julius kwenda nyumbani kwa shangazi yake Justina John [48] katika kijiji cha Kasomela Kata ya Kinamapura wilayani Kahama na kisha kufanya uhalifu huo.
    Mlinzi wa amani kwenye Kata hiyo Clement Bilike ameeleza kuwa baada ya Julius kuwa ugenini, shangazi yake alisafari huku akimuacha nyumbani kwake na watoto.

    Hata hivyo Julius alichukua baiskeli pamoja na gunia moja la Karanga na kuanza kutoroka mnamo mida ya saa moja jioni hadi kijiji cha jirani cha Ilemve ambapo baiskeli ilipata pancha.

    Akiwa katika harakati za kutafuta namna za kuziba tairi ya baiskeli hiyo alikamatwa na wananchi na kuanza kupigwa hadi kupoteza maisha na baadaye kuchomwa moto na wananchi hao waliokusanyika baada ya kupigwa yowe.

    Polisi wilayani Kahama walifika kwenye tukio na kuruhusu mabaki ya mwili wa marehemu Julius kuzikwa na kwamba uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.
     
    Hata hivyo wananchi wanashauriwa kuacha kuchukua sheria mikononi mwao badala yake wawapeleke watuhumiwa wa uhalifu kwenye vyombo vya dola (TK).

    Ijumaa, 23 Mei 2014

    RAIS UHURU APUNGUZA GHARAMA ZA KUTALII ILI KUVUTIA WATALII ZAIDI TZ MPOO

    NAIROBI, KENYA: President Uhuru Kenyatta on Friday announced a raft of specific measures aimed at revamping the tourism sector.
    He said Kenyans working in corporate and business entities will now enjoy paid up vacations in the tourism sector as one way to energise the industry.
    Making the announcement after holding a meeting with tourism sector stakeholders at State House Nairobi, President Kenyatta said the Government is taking specific measures to stimulate the tourism sector including giving  at least 25,000 Kenyans a chance to go for a week’s holiday every month at the expense of their employers.
    Other measures taken to revamp the sector include exemption of VAT Act, 2013; on air ticketing services supplied by travel agents as well as payment of all income tax related refunds owed to tourism industry players by the Kenya Revenue Authority not later than Thursday next week.
    The President also said the Government will reduce park fees to Sh6,960 ($80) for regional and international tourists and to Shs 1000 for domestic tourists from US Dollar 90 and Shs 1,200 respectively.
    To increase flights to Moi international Airport and Malindi Airport, the President announced the reduction of landing charges for both local and international flights by 40 percent and 10 percent respectively.

    UCHAKACHUAJI WA KURA MALAWI


    Shughuli ya kuhesabu Kura Malawi
    Uchaguzi wa Malawi ulikumbwa na visa vingi vya wizi wa kura pamoja na udukuzi wa mitambo iliyokuwa inatumiwa kujumlisha kura. Haya ni madai ya Rais Joyce Banda.
    Rais Joyce Banda ametaka kura hizo kuhesabiwa upya bila ya kutumia mitambo ya elektroniki ya kuhesabu kura.
     
    Bi Banda alikumbwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne kutoka kwa wagombea watatu akiwemo, waziri wa zamani wa mambo ya nje Peter Mutharika.
    'Waziri ajiua'
    Mapema Alhamisi naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi alijipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
    Godfrey Kamanya alikuwa anagombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini.
    Alijiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
    Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
    Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
    Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
    Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatuma matokeo kwa njia ya barua pepe (TK)

    WATU WAWILI WAJERUHIWA KWA BOMU MJINI MOMBASA, KENYA



    Usalama unaimarishwa Kenya kutokana na ongezeko la mashambulio
    Watu wawili wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea mjini Mombasa pwani ya Kenya.
    Miongoni mwa wawili hao ni afisa wa polisi aliyekimbizwa katika hospitali ya mkoa kupokea matibabu.
    Shambulio hilo lilitokea wakati maafisa wa polisi walipomkamata mshukiwa wa ugaidi, na hapo pakatokea mtu wa pili aliyewarushia guruneti katika jitihada ya kumuokoa mshukiwa aliyekamatwa na alifanikiwa kuondoka naye huku akimwacha polisi na mjeraha ya bomu na kumpiga risasi moja makalioni.
    Mbunge wa Mvita kutoka eneo hilo, Abdulswamad Sharrif ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika katika eneo hilo punde baada ya mlipuko huo, amelaumu udhaifu katika idara ya ujasusi Kenya kwa kutoweza kutambua mipango ya mashambulio kama hayo kabla ya yafanyike, ili kuweza kuyatibua.
    Akizungumza na BBC Abdulswamad amesema, 'Ni lazima tuweze kukubali kasoro iko wapi, ili tuweze kujua suluhisho litakuja vipi'.
    Shabulio hilo limetokea wakati usalama umeimarishwa nchini Kenya kutokana na tisho la kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya maeneo ya umma.
    Katika siku za hivi karibuni Kenya imekuwa ikikabiliwa na mashambulio kadhaa katika maeneo mbali mbali nchini ukiwemo mji huo wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.
    Ni hivi juzi tu watu 10 waliuawa huku zaidi ya hamsini walijeruhiwa katika milipuko miwili iliotokea katika Soko kubwa la nguo la Gikomba katika mji mkuu Nairobi.(TK)

    FACEBOOK YAOKOA MAISHA YA MPANDA MLIMA

    John All aliyeokolewa na facebook
    Mpanda milima mirefu ameokolewa kutoka futi karibu 20,000 bondeni alipoandika ''Nahitaji msaada'' katika mtandao wa Facebook
    Profesa huyo wa jiografia aliwaambia marafiki zake wa Facebook kuwa alikuwa ameanguka ndani ya bonde la Himalaya umbali wa futi 19,600 kwenda chini.
    Profesa John All aliandika taarifa hii kwenye ukurasa wa facebook wa ‘'American Climber Science Program’' baada ya kuanguka kwenye bonde hilo. All mwenye umri wa miaka 44 aliteguka bega, kuvunja mbavu tano, goti, na kiwiko.
    All aliandika, ‘’ tafadhali muwafahamishe waokoaji wa Global, kuwa John amevunjika mkono, mbavu na huenda anavuja damu ndani ya mwili. Tafadhali harakisheni’’
    Marafiki wake wa Facebook waliona video ya All akiwa na majeraha na kuwajulisha waokoaji kilichokuwa kikitendeka na kisha kuwasiliana na All na kumwambia kuwa atapata msaada.
    Baada ya saa kadhaa, All aliandika kwenye ukurasa huo wa Facebook kuwa waokoaji hawangeweza kumpata kwa kutumia helikopta kwa hivyo angejitahidi ingawa kulikuweko na baridi na alikuwa na maumivu mengi.
    Baada ya saa 19, profesa All aliokolewa na kupelekwa hospitalini mjini Kathmandu ambako anapata matibabu(TK)

    JESHI LAPINDUA SERIKALI NCHINI THAILAND


    Jeshi la Thailand
    Mkuu wa majeshi nchini Thailand ametangaza mapinduzi  akisema jeshi sasa linachukua udhibiti wa serikali.
    Katika taarifa iliyotolewa kupitia kwa televisheni, mkuu huyo wa majeshi alisema jeshi litarejesha utawala wa kisheria na kufanya mageuzi ya kisiasa.
    Majeshi yalizingira eneo la tukio mjini Bangkok ambapo makundi ya kisiasa yamekuwa yakifanya mazungumzo kwa siku ya pili na kuwachukua viongozi wao.
    Mapinduzi haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa na kuwekwa kwa sheria ya kijeshi.
    Jeshi litatuma vikosi na magari kuwasindikiza waandamanaji kutoka maeneo ya maandamano, afisa wa kijeshi alilieleza shirika la habari la Reuters.
    Ghasia za hivi karibuni zialianza katika mji mkuu wa Thailand mwishoni mwa mwaka jana, wakati waziri mkuu Yingluck Shinawatra alipovunja bunge la nchi hiyo .
    Waandamanaji waliweka vizuizi kwenye maeneo ya mji wa Bangkok katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Mapema mwezi huu , mahakama ilimuamuru kuondolewa madarakani kwa Bi Yingluck kwa madai ya kutumia vibaya mamlaka.
    Thailand imekabiliwa na mzozo wa kupigania mamlaka tangu kaka yake Bi Yingluck , Thaksin Shinawatra, kung'olewa mamlakani na jeshi kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006 (TK)

    FAMILIA YAMWACHIA MUNGU KIFO CHA MENEJA WA EWURA KUFUATIA UTATA ULIOGUBIKA


    Mwili wa Gashaza ulitarajiwa kuwasili kijiji cha Mulukulazo wilayani Ngara Mkoani Kagera jana jioni na leo saa 4:00 asubuhi utapelekwa katika Kanisa la Anglikana katika kijiji hicho kwa ajili ya sala na saa 6:00 mchana utaagwa kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.

    Aliyekuwa Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza anazikwa leo katika Kijiji cha Mulukulazo, Ngara mkoani Kagera huku familia yake ikisema haina cha kusema kuhusu kifo hicho, bali inamwachia Mungu.

    Akizungumza jana kijijini hapo, mdogo wa marehemu, Alex Gashaza alisema familia imepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kushangazwa na taarifa kwamba ulitokana na kujinyonga kama inavyodaiwa.


    Alisema baada ya kupokea simu kutoka Dar es Salaam kuhusu mazingira ya kifo hicho, wameshindwa kujua sababu za kifo kwa kuwa hakuna mtu aliyezungumza naye.


    Alisema kaka yake hakuwa na tatizo lolote na wanafamilia, ndugu wala jamaa zake wa karibu, hivyo familia haiwezi kuelezea jambo ambalo halina ushahidi, badala yake inaacha tukio hilo mikononi mwa Mungu.


    “Tumekuwa tukishirikiana naye kuendeleza familia yetu, kama unavyoona nyumba ilipokuwa imefikia hatua ya kuezekwa, kuna mchango wake mkubwa kifamilia,” alisema Alex.


    Mwili wa Gashaza ulitarajiwa kuwasili Mulukulazo jana jioni na leo saa 4:00 asubuhi utapelekwa katika Kanisa la Anglikana katika kijiji hicho kwa ajili ya sala na saa 6:00 mchana utaagwa kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwake.


    Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza mkoani Mwanza, Mchungaji Lazaro Manjelenga ambaye pia ni baba mkwe wa mdogo wa marehemu, alisema wana matumaini na Muumba kwa kile kilichotokea.


    “Siri ya Mungu na mwanadamu wake hakuna wa kuijua, hivyo tusihukumu,” alisema na kuongeza kuwa mazishi yatafanyika kwa mujibu wa taratibu za Kanisa hilo.MWANANCHI

    NAIBU WAZIRI MALAWI AJIUA KWA RISASI


    Bwanna Godfrey Kamanya enzi za uhai wake
    Naibu Waziri wa Serikali za Mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
    Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.

    Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.

    Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.

    Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.

    Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.BBC

    AJIFUNGUA WATOTO WANNE NA ANAHITAJI MSAADA WAKO

    Mkazi wa kunduchi Beachi katika manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam Riziki Daudi amejifungua watoto wanne alipojifungua kwa njia ya upasuaji wiki iliyopita katika hospitali ya Taifa Muhimbili hivi karibuni. Kutokana na maisha kuwa magumu anaomba wasamaria wema kumsaidia kwa hali na mali kutoka hali yake hususani nguo za watoto pamoja na misaada mingine. Watoto hao wanatunzwa katika chumba maalum katika jengo la wazazi.

     Anaomba kwa wale watakaoguswa na tatizo hilo kuwasiliana naye kupitia namba za simu 0783717648 ya Hadija Abeid na 0717 365040 ya Thuwaiba Mohamed au 088711458 Daudi Haji 

    Wadau naombashime tumsaidie mama huyu na wanae (TK)
    RIZIKI DAUD AKIWA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI WADI YA WAZAZI

    MTOTO ALIYEISHI KWENYE BOX MIAKA MINNE MIFUPA YAKE IMEATHIRIKIA


    POLISI mkoani Morogoro, inaendelea kuchungua kilichotokea mpaka mtoto mkoani hapa (jina limehifadhiwa), akateswa na mzazi mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, amesema, baba mzazi wa mtoto huyo, jina tunalo ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro alitakiwa kwenda kutoa maelezo kituoni leolakini  hakutokea.

    Kamanda Paul alisema jana kuwa, walimtafuta mzazi huyo kwa simu ili kumkumbusha umuhimu wa kufika Polisi kutoa maelezo, lakini simu zake zilikuwa zimezimwa.

    Gazeti hili lilifika kwa mwajiri wake katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambako hakuwepo kwa kuwa aliaga kwamba amekwenda katika Kituo cha Ustawi wa Jamii, alikodai kuwa aliitwa.

    Hata hivyo, gazeti hili lilipofika katika ofisi hiyo, lilihakikishiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii, Oswin Ngungamtitu, kuwa mtuhumiwa hakuwa amefika katika eneo hilo, wala hakukuwa na mwito wa yeye kufika katika ofisi hiyo.

    Katika tukio lingine la kutia shaka, gazeti hili lilipohojiana na Mtuhumiwa katika nyakati tofauti juzi, alitoa taarifa mbili tofauti, kuhusu sababu za kumuacha mwanaye kwa mama mkubwa wake, Mariam Said, aliyemuweka katika boksi kwa zaidi ya miaka mitatu.

    Katika mahojiano ya awali, alidai baada ya mzazi mwenzake, Mwasiti Ramadhan kufariki dunia, alishindwa kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke.

    Alidai kwa kuwa alikuwa ameoa, alikubaliana na upande wa pili wa familia ya marehemu, kuwa mwanaye huyo alelewe na mama yake mkubwa, Mariamu.

    Katika mahojiano na mwandishi mwingine wa gazeti hili juzi hiyo hiyo,  alidai mwanae huyo alichukuliwa na Mama yake mkubwa ili kumlea akiwa na umri ndogo na mara zote alikuwa akipeleka fedha za matumizi.

    Alidai kwa mara ya mwisho alimwona mwanae huyo miezi miwili iliyopita akiwa na afya ya kuridhisha, wakati taarifa zilizotolewa na Mariam, zilidai kuwa mtoto huyo hajaogeshwa tangu Julai mwaka jana.

    “ Kila nikienda kumwona nyumbani kwao sikubahatika kumwona , nilikuwa nikiambiwa amelala ama ametoka na watoto wenzake...isipokuwa miezi miwili iliyopita,” alidai Rashid kauli inayoonesha kuwa mtoto huyo alikuwa akitoka na wenzake wakati majirani walitoa ushahidi kuwa hawakuwahi kufahamu uwepo wa mtoto katika nyumba hiyo.

    Taarifa kutoka katika Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, zimeeleza kuwa baada ya uchunguzi wa awali wa afya ya mtoto huyo, alibainika kuwa na niumonia, ulegevu wa viungo ikiwa ni pamoja na baadhi ya mifupa katika mwili wake kuvunjika.

    Daktari Bingwa wa watoto, Dr Hores Msaky alipozungumza na gazeti hili jana, alisema walimpokea mtoto huyo juzi alikuwa katika hali ya uchafu usio wa kawaida.

    Msaky alisema waliamua kumfanyia vipimo vya awali pamoja na picha za X ray, wakagundua kuwa mifupa yake si ya kawaida, inaonekana imevunjika ingawa hawajajua nini kimemvunja.

    BIBI ANASWA NA "UNGA" DAR


    Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
    Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.
    Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.
    Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
    Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata.
    "Huyu mwanamke achana naye, akisimama mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa karatasi inayofanana na ganda la sigara," alisema Selemani.
    Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo maalumu inayogundua dawa za kulevya.
    Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya ukaguzi.
    Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo.
    "Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya.
    "Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri wake," alisema Nzowa.
    Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria ya Nigeria, anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

    MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATZ WAISHIO JAPAN


    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na watanzania waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otani, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo, jana Mei 21, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Tanzanite Society) David Semiono, akisoma risala ya Jumuiya yao wakati wa hafla ya chakula cha jioni na Makamu wa Rais Dkt. Bilal, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, jana usiku Mei 21, 2014.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na watanzania waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otani, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo, jana Mei 21, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
    Baadhi ya Watanzania waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa wakiwahutubia katika hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, jana Mei 21, 2014.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwanamuziki Mtanzania wa bendi ya The Tanzanite, Abuu Omar, wakati alipokuwa akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Japan, waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha jioni. Kulia ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal.

    Alhamisi, 22 Mei 2014

    FISI AJIFICHA KWENYE TUMBO LA TEMBO KUJIOKOA NA SIMBA

    Na Stratton Hatfield
    Katika kujiokoa kwenye hatari yeyote ile si tu watu ambao wanaweza kupata wazo la ajabu la kutenda ilimradi tu kuepukana na mauti, fisi mmoja aliyekuwa katika lishe yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimika kujificha kwenye tumbo la mzogo wa tembo ili kumkwepa simba aliyemvamia ghafla.
    Fisi huyo aliyaona mauti yaleeeeee, lakini aliona ni heri kukaa ndani ya tumbo la tembo kulikoni kuliwa na simba. picha zifuatazo zinaonyesha namna fisi huyo alivyojificha na baadae kufanikiwa kukimbia baada ya kupata upenyo.
    Tukio hilo halijatokea mbali bali ni kule Masai Mara nchini Kenya, pata uhondo huo..