Jumatatu, 16 Machi 2015

BREEEKING NEWWZZZZ: Moto wazuka Hosteli za Mabibo

Taarifa zlizotufikia hivi punde ni kuwa moto mkubwa umezuka katika Jengo D lililopo ndani ya Mabibo Hostel zinazomilikiwa na kuendeshwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Shuhuda aliyekuwa eneo la tukio ametujuza kuwa Askari wa Zimamoto wamechelewa kufika na athari zilishaanza kuwa kubwa, jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea.


Quote By Mapengo 17 View Post
Kutoka Mabibo Hostel DSM.

Kwa taarifa ambazo zimetufikia muda huu zinadai kuwa Bweni la Wanaume Mabibo Hosteli jijini Dar es Salaam linaungua moto muda huu, bado sababu na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, waandishi wetu wanaelekea sehemu ya tukio kuthibitisha hili na watatufahamisha zaidi nasi tutakufahamisha.

Chanzo:
ITV


Chanzo bado hakijafahamika!
Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name: mabibo.jpg 
Views: 0 
Size: 42.3 KB 
ID: 234958   Click image for larger version. 

Name: mabibo1.JPG 
Views: 0 
Size: 73.6 KB 
ID: 234963   Click image for larger version. 

Name: mabibo2.JPG 
Views: 0 
Size: 102.3 KB 
ID: 234964  

MAANDAMANO MAKUBWA MONDULI: WANANCHI WAMWOMBA LOWASSA AGOMBEE URAIS


makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
 
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la Monduli

Jumapili, 15 Machi 2015

IKO SIKU NITAKUWA MTU MKUBWA - ZITTO


Zitto: Iko siku nitashika nafasi kubwa Tanzania

 
Wananchi wa Kijiji cha Nyalubanda wakiwa wamembeba Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alipowasili katika kijiji hicho jana katika hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa alilotoa ahadi katika kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2010. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Na Antony Kayanda na Saumu Mwalimu, Mwananchi

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema kutimuliwa uanachama na Chadema ni dhoruba inayomkumba mwanasiasa yeyote anayefanikiwa na kwamba iko siku atashika “nafasi kubwa ya uongozi ya kuwatumikia Watanzania”.
Zitto aliwasili mjini hapa juzi, ikiwa ni siku chache baada ya Chadema kutangaza kumtimua uanachama kwa kosa la kupeleka mgogoro wa ndani ya chama kwenye mahakama.
Alifungua kesi Mahakama Kuu akitaka imuamuru katibu mkuu wa Chadema kumpa nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua madaraka yote na baadaye kukizuia chama hicho kumjadili. Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali shauri lake na Chadema ikatangaza mara moja kumtimua.
Akihutubia mamia ya watu kwenye Kijiji cha Nyarubanda ambako alikabidhi gari la wagonjwa, Zitto aliwatoa hofu wananchi hao walioonyesha shauku ya kujua hatma yake na kuwaeleza kuwa hajawatupa, ataendelea kuwahudumia.
“Hakuna kiongozi aliyefanikiwa kisiasa bila kupitia misukosuko ya kupingwa,” alisema Zitto ambaye anamalizia kipindi cha pili cha ubunge wake kwenye jimbo hilo.
“Waziri Mkuu za zamani ya India, Indira Gandhi alifukuzwa na chama chake na aliamua kuunda chama kipya na baadaye kuwashinda waliomfukuza katika uchaguzi. Kwa hiyo nawatoa hofu kwa maana ninajengwa zaidi kisiasa.
“Nipo kwenye dhoruba ambayo inanijenga kisiasa na ipo siku nitawatumikia Watanzania katika nyadhifa kubwa za uongozi.” Katika mkutano huo ambao wananchi walimpokea wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kama “Mheshimiwa Zitto tulikuchagua wewe na siyo chama,” huku mengine yakiandikwa “chama siyo bora, ubora ni utendaji kazi”.
Viongozi mbalimbali wa CCM na vyama vingine vya siasa walijumuika kwenye uwanja huo kumpokea Zitto na kushiriki naye kucheza ngoma za asili.
Baadhi ya viongozi hao ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Hamisi Betese, mkurugenzi wa halmashari hiyo, Michael Mwandezi na viongozi wengine wa serikali za mitaa.
Akiongea katika hadhara hiyo, Betese alisema kuwa kitendo cha Zitto kutoa gari ambayo aliwaahidi wananchi kipindi cha uchaguzi ni utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo ndiyo chama tawala.
Aliongeza kuwa yeye kama mwenyekiti wa halmashauri bado anamtambua Zitto kama mbunge wa Kigoma Kaskazini mpaka hapo taarifa rasmi zitakapotolewa.
Wanakijiji hao walishukuru Zitto kwa kutoa gari hilo wakisema litawasaidia kuokoa fedha nyingi walizokuwa wakitumia kutafuta magari binafsi wanapokuwa na wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.

VATICAN YASEMA KUNA HAJA YA KUTUMIA NGUVU DHIDI YA IS


Askofu mkuu wa Vatican Silvano Tomasi
Makao makuu ya kanisa katoliki duniani Vatican yanasema kuwa nguvu inaweza kutumiwa kusitisha mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa Islamic State dhidi ya wakristo na makundi mengine madogo .
Askofu mkuu Silvano Tomasi ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja wa mataifa mjini Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha mauaji ya halaiki.
Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.
Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati.

WENGER ASEMA ARSENAL ITAIFUNGA MONACO


kocha wa arsenal Arsene Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya kuibandua Monaco katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza ya mechi hizo.
Arsenal itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumapili huku ikiwa hakuna timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama hayo katika michuano hiyo.
Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo''.
''Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya kushinda''.
 
Kilabu ya Monaco inayotarajiwa kupepetana na Arsenal siku ya jumanne
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali.
Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. .

MABOMU YALENGA MAKANISA PAKISTANI

Wasichana walia kufuatia mashambulizi mawili yaliolenga makanisa Pakistan
Mabomu mawili yamelipuka yakilenga makanisa mawili yaliyokuwa yamejaa watu kwenye mji wa Lahore chini Pakistan wakati watu walipokuwa wakihudhuria misa ya jumapili.
Polisi wanasema kuwa takriban watu 6 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yanaoyoaminika kuwa ya kujitoa mhanga yalifanyika eneo lenye waumini wengi wa kikristo la Youhanabad

UGIRIKI YAONYA KUHUSU KUONDOLEWA KATIKA KANDA SARAFU YA EURO

Ugiriki imesema kama taifa hilo litakuwa kwenye hatua ya kuondoka katika kanda ya mataifa yanayotumia sarafu ya Euro, basi mataifa ya Uhispania na Italia yanaweza kufuata mkondo huo.
Bendera ya Ugiriki Bendera ya Ugiriki
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ulinzi wa Ugiriki, Panos Kammenos, wakati akizungumza na gazeti la Ujerumani la Bild, katika mahojiano ambayo yatachapishwa leo Jumamosi (14.03.2015). Kammenos amesema kama Ugiriki ikiondoka kwenye kanda inayotumia sarafu ya Euro, basi Uhispania na Italia zitafuata, na hata ikiwezekana Ujerumani pia.

WAKURDI WAPATA USHUNDI MUHIMU DHIDI YA DOLA LA KIISLAMU

Wapiganaji wa Kikurdi na wanamgambo wa kikristo wanapata mafanikio katika mapigano dhidi ya magaidi wa "Dola la Kiislamu" Kaskazini Mashariki mwa Syria. Hata hivyo pana taarifa juu ya mapigano makali.
Wapiganaji wa Kikurdi Wapiganaji wa Kikurdi
Kwa mujibu wa taarifa ya afisa mmoja wa kikurdi na asasi ya wanaharakati, katika mapambano dhidi ya kundi linaloitwa Dola la Kiislamu, wapiganaji wa kikurdi wanaoshirikiana na wanamgambo wa Kikristo, wanapata mafanikio.
Afisa huyo Nasser Haj Mansour kutoka wizara ya ulinzi katika jimbo la wakurdi la nchini Syria, amesema wapiganaji wa kikurdi wamekiteka kijiji kimoja katika jimbo la Hassakeh ambacho hapo awali kilikuwa kinadhibitiwa na wapiganaji wa Dola la Kiislamu.
Afisa huyo pamoja na wawakilishi wa asasi inayofuatilia haki za binadamu nchini Syria kutokea London, wamesema wapiganaji wa Peshmerga walikiteka kijiji hicho usiku wa juzi.

Ijumaa, 6 Machi 2015

MAAFA KAHAMA: SERIKALI YAANZA KUCHUKUA HATUA

Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi, 2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na Mwaguguma. Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba 137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.

Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda kuwahifadhi wananchi hao kwenye Shule.
Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;
i. Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita 1,126 na Sukari tani 1.3
ii. Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha blanketi 650, ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ; Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82
Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha waathirika kurejea katika maisha yao ya kawaida; inapenda kuwatangazia wale wote wanaoguswa na maafa haya kuwa Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo inahitajika kwa waathirika.
Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi; mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya; misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.) inahitajika sana.
Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.

Alhamisi, 5 Machi 2015

FORD YAGEUkIA BAISKELI


baiskeli inayotumia umeme
Kampuni ya kutengeza magari ya Ford imezindua baiskeli ya kielektroniki kwenye mkutano mkubwa wa magari duniani katika mpango wake wa upanuzi.
Kampuni zaidi za kutengeza magari zinatafuta njia mbadala za kutengeza pesa huku nyingi zikitengeneza kile kinachoitwa kama uchukuzi wa haraka.
Baiskeli hizo zinazotumia umeme ziko aina mbili, moja inayotumiwa na wasafiri na nyingine inayotumiwa kufanya biashara.
Baiskeli zote mbili zina programu za smartphone zinazoweza kumuelekeza anayeziendesha.
Jaribio la baiskeli hizo ni miongoni mwa mipango ya kampuni ya Ford kubuni mbinu mpya ya usafiri huku ikifanya utafiti kuhusu jinsi baiskeli hizo zinzovyoweza kuingiliana na magari pamoja na usafiri wa uma.
''Kuna mbinu nyingi za kuzunguka mjini. Lakini kile kinachohitajika ni njia za kuunganisha mbinu hizi zote za usafiri pamoja amesema Ken Washington'', makamu wa rais wa kitengo cha utafiti cha Ford

WATU WANNE KUNYONGWA HADI KUFA MWANZA


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Geita.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Joaquine De-Mello katika ukumbi uliokuwa umefurika wasikilizaji wakiwemo ndugu wa upande wa washtakiwa na baada ya kutolewa hukumu baadhi ya ndugu wa washtakiwa walitokwa na machozi
Waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni Masalu Kahindi[54]Ndahanya Lumola[42]Singu Nsiyantemi[49]na Nassor Said[47] ambaye alikuwa mume wa marehemu Zawadi Mangindu wote wamepatikana na hatia ya kula njama na kushiriki kumuua zawadi kwa kukusudia ambaye alikuwa mlemavu wa ngozi.
Katika hukumu yake Jaji De-mello alisema alikuwa amezingatia kwa makini na tahadhari kubwa katika kufikia uamzi huo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mashahidi 12 waliitwa na kutoa ushahidi pamoja na ule wa Utetezi na kisha kujiridhisha kuwa pasipo kuacha shaka yoyote washtakiwa walitenda kosa hilo.

ANAOGOPA KUISHI NJE YA KITUO

Mtoto Hassan Khamis ni miongoni mwa walemavu wa ngozi wanaohifadhiwa kwenye kituo cha Buhangija nchini Tanzania na sasa akiwa ameshakuwa mkubwa na kulazimika kutoka hapo, anasema hana uhakika wa maisha yake.
Watu wenye ulemavu wa ngozi katika kijiji cha Ruyigi, Burundi. Watu wenye ulemavu wa ngozi katika kijiji cha Ruyigi, Burundi.
Katika mfululizo huu wa ripoti maalumu mwezi mzima kuangazia masaibu, changamoto na maisha wanayopitia watu wenye ulemavu wa ngozi, maarufu kama albino, ambao hivi karibuni wamekuwa wakilengwa na kushambuliwa nchini Tanzania kwa imani za kishirikina, hapa Idhaa ya Kiswahili ya DW inazungumza na kijana Hassani mwenye umri wa miaka 17 sasa na ambaye amehifadhiwa katika kituo cha Buhangija kinachowashughulikia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi mjini Shinyanga, Tanzania.
Kusikiliza mahojiano na kijana Hassani, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Amina Abubakar

WATANO WAUAWA KWA KUTUHUMIWA KUZUIA MVUA MKOANI MARA

Jeshi la polisi mkoa wa Mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa Serikali ya kijiji cha Park Nyigoti katika kata ya Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano. 
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi ACP Ernest Kimola, amesema katika tukio hilo limesababisha watu wengine watatu kujeruhiwa na viboko hivyo na kulazwa katika hospitali teule ya Nyerere DDH Mjini Mugumu wilayani Serengeti.

JK AKUTANA VIONGOZI WA CHAMA CHA ALBINO NCHHINI

Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania wakiwasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyewakaribisha ili kuwasikiliaza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​
Rais Kikwete akisalimiana na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​

BAKOZI WA MAREKANI ACHOMWA VISU KOREA

BALOZI WA MAREKANI KWA KUCHOMWA KISU

Balozi Mark Lippet akiwa na majeraha baada ya shambulizi.
Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya serikali yao.
Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake huyo wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.'Balozi wa Marekani ashambuliwa

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2015/03/150305_us_ambassadorsouthkorea

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na kisu chenye urefu wa inchi kumi.'
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa katika shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi. Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote.
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kama hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan mjini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu .Askari wakiwa wamemzunguka Balozi aliyejeruhiwa
Naye msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye muandaaji wa mkutano huo, ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti .
Balozi Lippert, ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na ambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na bara la Asia, na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October mwaka wa jana.
Lippert amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama wa taifa katika operesheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba nyeusi wakati alipoitembelea Iraq.
Korea Kusini na Kaskazini walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya Korea na bado kiufundi wako vitani kwa kuwa mapigano yalisitishwa kwa suluhu .
Marekani na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko Kaskazini .
Pyongyang wanadai kuwa wanafanya mazoezi kwa kujiweka tayari na uvamizi wowote utakaotokea. Wakati huo huo Korea Kusini na Marekani wanadai kuwa mazoezi yao ni kwa kujihami tu .

Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao 30,000 vya kudumu vilivyopiga katika kambi za Korea Kusini.
CHANZO BBC

Jumanne, 3 Machi 2015

JENERALI HAFTAR KAMADA MKUU WA JESHI LIBYA

Jeneral Khalifa Haftar katika mji wa Abyar, mashariki ya Benghazi, Mei 31 mwaka 2014.
Jeneral Khalifa Haftar katika mji wa Abyar, mashariki ya Benghazi, 

Viongozi wa Tobrouk, ambao wanatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, wamemteua Jumatatu wiki hii Jenerali Haftar kuwa kamanda mkuu wa jeshi lao. Uteuzi huu umeweka matatani hali inayojiri wakati huu nchini Libya.

Viongozi wa Tobrouk, ambao wanatambuliwa na jumuiya ya kimataifa, wamemteuwa Jumatatu wiki hii jenerali Haftar kuwa kamanda mkuu wa jeshi lao. Uteuzi huu umeweka matatani hali inayojiri wakati huu nchini Libya.
Khalifa Haftar amekua kiongozi wa majeshi ya serikali ya Tobrouk tangu mwaka mmoja uliyopita. Jenerali Khalifa Haftar ndiye alianzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa makundi ya kiislamu katika mji wa Benghazi.
Jenerali Khalifa Haftar alihudumu katika jeshi wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Libya Moammar Kadhafi
Jumuiya ya kimataifa haijawahi kumhukumu wala kumuunga mkono hadharani jenerali Haftar nchini Libya.
Mwezi Mei, wakati Jenerali huyu alipoanzisha operesheni aliyoiita “Operesheni ya kiutu”, akimaanisha “ kutokomeza ugaidi”, Marekani iliona kuwa ni shambulio dhidi ya makundi hasimu yenye lengo moja. Baada ya mamia ya watu kuuawa na eneo moja la Benghazi kutekwa, mapigano yameendelea kushuhudiwa hadi leo.
Kundi la Ansar Al Shariah, lenye mafungamano na Al Qaeda, ambalo liliwekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi ni moja ya makundi yanayopigana katika mji wa Benghazi na maeneo mengine nchini Libya.
Kundi hilo lilihusika pia katika shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani Septemba 11 mwaka 2012 na kuhusika pia katika kifo cha balozi Chris Stevens.

LESOTHO KUUNDA SERIKALI YA SHIRIKISHO?

Lesotho yajiandaa kuunda serikali ya muungano

Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane, akipokelewa na wafuasi wake, katika mji mkuu wa Lesotho, Maseru, Februari 26 mwaka 2015.
Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane, akipokelewa na wafuasi wake, katika mji mkuu wa

Lesotho inaelekea kuunda serikali ya muungano kutokana na kile kinachoonekana kuwa hakuna atakayepata ushindi wa moja kwa moja katika Uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita.

Hadi sasa chama cha Waziri Mkuu Thomas Thabane cha All Basotho Convention kinaongoza na tayari kimepata viti 40 vya ubunge ikilinganishwa na chama cha Waziri Mkuu wa zamani cha Democratic Congress ambacho kina viti 33.
Mshindi anahitajika kupata ushindi wa viti 61 kati ya 120 ili kuweza kuunda serikali bila ya kushirikiana na chama kingine.
Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema matokeo yanaonesha wazi kuwa uwezekano ni mkubwa wa kuundwa kwa serikali ya muungano.
Waangalizi wa Uchaguzi huo wanasema, zoezi hilo limekuwa huru na haki na wananchi wa Lesotho walipiga kura kwa amani.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye anaongoza waangalizi wa Umoja wa Afrika licha ya kuusifu uchaguzi huo kuwa huru na haki ameonya kuwa huenda kukatokea na mvutano kati ya jeshi na polisi katika nchi hiyo ikiwa mkataba wa kutoingilia siasa hautaheshimiwa.
Matokeo ya mwisho yatafahamika kesho Jumatano katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika ambalo lililazamika kuandaa uchaguzi huo kutokana na jaribio la kuipundua serikali mwaka jana.

BOKO HARAM YASHAMBULIA VISIWA ZIWA CHAD

Nchi nne zinachangia ziwa Chad : Chad, Cameroon, Niger na Nigeria.
Nchi nne zinachangia ziwa Chad : Chad, Cameroon, Niger na Nigeria.

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo bado ni ya muda, lakini kwa mujibu wa mashahidi katika vijiji hivyo, watu tisa kwa uchache waliuawa.
Wanamgambo wa Boko Haram waliingia katika vijiji hivyo wakitumia mitumbwi kwenye saa mbili usiku Jumapili Machi 1, na kuanza kushambulia kwa risasi na vilipuzi katika nyumba mbalimbali za vijiji hivyo.
Katika kisiwa cha Kui Keleha, watu wawili waliuawa, na wengine walichomwa moto ndani ya nyumba zao, na wengine tena walikufa maji wakati wakijaribu kuokoa nafsi zao, kama alivyothibitisha, El Adj Aboubacar, mbunge wa Bosso.
“ Walichoma moto watu tisa kwa wakati mmoja, na mtumbwi uliyokuwa ukiwasafirisha wanawake na watoto, ambao walikuwa wakijaribu kuokoa maisha yao ulizama ziwani. Watu wanane walifariki dunia", amesema El Adj Aboubacar.
Kwa uchache watu 19 walifariki baada ya shambulio lililoendeshwa katika vijiji vya Kui Kaleha na Toumbu Buka, visiwa ambavyo vinapatikana katika ziwa Chad kwenye mpaka na Nigeria. Eneo ambalo ni vigumu kutoa ulinzi.
Karibu na eneo hilo, kijiji cha Bosso kimekuwa kikishuhudiwa mara kwa mara mashambulizi ya hapa na pale tangu Boko Haram iliposhambulia kijiji hicho Februari 6 mwaka huu.

HUSSEIN RADJAB ATOROKA JELA


Prosper Niyoyankana (picha), mwanasheria wa Hussein Radjabu.
Na RFI
Kiongozi wa zamani wa chama tawala Cndede-Fdede nchini Burundi, Hussein Radjabu anasadikiwa kuwa ametoroka jela usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Machi 2 mwaka 2015. Hussein Radjabu alikua akizuiliwa jela kwa kipindi cha zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2007.
Hussein Radjabu alifungwa jela kwa tuhuma za kupanga njama za mapinduzi dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza. Alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela.
Wadadisi wanasema kutoroka kwa Hussein Radjabu ni pigo kubwa kwa utawala wa Pierre Nkurunziza.
Hata hivyo wafuasi wengi wa kinara huyo wa zamani wa chama tawala Cndede-Fdede, wanahisi kwamba huenda ameondolewa jela na kuuawa.

KUFUATIA KUONDOLEWA MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA AFRICA AZAM YATIMUA MAKOCHA

Kocha mkuu Omo g na msaidizi wake
 
Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14. Hii inatokana na timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na timu ya El Mireikh ya Suda na kutolewa nje ya mashindano hayo.

Omog ambaye ni raia wa Cameroon ndiye aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondolewa pamoja na msaidizi  wake Ibrahim Shikanda kutoka Kenya.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe. 

Habari hizi zinategemewa kuzua mjadala mkali kwa kuwa timu ya Azam ilitolewa kwa kufaniwa fujo, visa na vurugu na mashabiki wa timu ya El Mireikh. Fujo hizo ni pamoja na risasi za moto kupigwa na basi lao kupigwa mawe.

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITATUMIA BN 55 KWA UMEME MBEYA

index
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatumia shilingi bilioni 55 kuvipatia umeme vijiji 244 vya mkoa wa Mbeya kupitia Miradi ya Umeme Vijijini (REA).
Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 2, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.
“Nimeambiwa kuwa katika mwaka 2014/15, jumla ya vijiji 244 vitapatiwa umeme kupitia REA. Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo: Chunya viko 13, Mbeya ni 32, Mbarali (56), Mbozi (14), Momba (15), Kyela (30), Ileje (18) na Rungwe (66) na jumla ya shilingi bilioni 55/- zitatumika kwa madhumuni hayo,” alisema.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kusimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini na kukamilisha awamu ya kwanza ya miradi ya umeme vijijini katika vijiji 17 vya mkoa huo.
“Nimeelezwa kuwa miradi hiyo iliyogharamu ya shilingi billioni 7.6 katika vijiji 17 imekamilika kwa asilimia 100. Katika  Halmashauri ya Mbeya kuna vijiji vitano, Mbozi vijiji vinne, Chunya vijiji sita na Rungwe vijiji viwili; na imeweza kuunganisha wateja 650,” alisema.
Alisema taarifa zinaonesha kuwa vijiji vilivyopangwa kupata umeme wa REA mwaka 2015/2016 ni 51 na kwamba hivi sasa ujenzi wa njia kubwa ya umeme wa 11Kv na 33Kv unaendelea. “Pia ujenzi wa njia ndogo ya umeme 400v unaendelea kujengwa na utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 42.3,” aliongeza.
Aliwahimiza viongozi wa mkoa huo kuongeza jitihada za kusambaza umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme ni makubwa kwa wananchi wengi

RAIS AMLILIA KEPTEN KOMBA


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika hali ya majonzi wakati wasanii walipokuwa wakiimba wimbo maalumu wa kumuaga Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Marehemu John Komba katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Spika wa Bunge, Anne Makinda. Picha ndogo ni jeneza lililobeba mwili wa Komba. Picha na Anthony Siame.

Kilio kina ushawishi mkubwa katika majanga mbalimbali hasa pindi unapomtizama mtu anayelia ni rahisi mtu mwingine kulia kutokana na yeye kuvuta hisia katika tukio husika.


Dar es Salaam
. Wimbo wa John Komba aliouimba katika msiba wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999, jana uliibua majonzi na kusababisha viongozi mbalimbali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutoa machozi ulipoimbwa kumuaga mbunge huyo.


Wimbo huo uliobadilishwa maneno yanayohusu Mwalimu Nyerere na kuingizwa yanayomtaja mbunge huyo wa Mbinga Magharibi, mbali na Rais Kikwete ulimliza pia Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba na waombolezaji wengine.

Sehemu ya mashairi ya wimbo huo uliokwenda kwa jina la “Nani Yule” ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wa bendi nchini, na kuwatoa watu machozi iliimbwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

“Kapteni Komba familia yako umeiacha na nani, chama chako umekiacha na nani, nenda baba msalimie Mwalimu, mweleze hali ya Watanzania ilivyo hivi sasa, mweleze hali ya nchi yetu ilivyo hivi sasa hasa wakati huu, msalimie Mzee Kawawa Simba wa Vita”.

Baadhi ya wanamuziki walioshiriki kuimba wimbo huo ni King Kiki, Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata, Jose Mara ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu na Luiza Mbutu wa African Stars.

Wakati wanamuziki hao wakiendelea kuimba wimbo huo, idadi ya watu wanaolia ilizidi kuongezeka, hasa wanafamilia ndugu na jamaa wa marehemu.

Waombolezaji walisikika wakilia huku wakisema, “Jamani alikuwa akitunga nyimbo kuwaimbia wenzake waliofariki dunia, sasa leo anaimbiwa yeye.”

Alipofariki Mwalimu Nyerere Oktoba 14, mwaka 1999, aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Komba akiwa na bendi ya TOT alitunga nyimbo za maombolezo ukiwamo wa “Nani Yule’, ‘Kwaheri Mwalimu’, ambazo jana zilitumiwa na wanamuziki kumuimbia yeye, wakibadilisha baadhi ya maneno.

Mwili wa mbunge huyo (61) aliyefariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu, uliagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo salamu mbalimbali za rambirambi zilitolewa kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda Songea mkoani Ruvuma.

Hata wakati wa kuagwa mwili huo, idadi kubwa ya wabunge wenzake waliohudhuria walishindwa kujizuia kulia huku wakikumbushana ucheshi aliokuwa nao Komba enzi za uhai wake.

Pengine msiba huo utakuwa umewagusa wengi wanaomfahamu kwa mambo mengi, na kwa kuwa kipindi hiki nchi inajiandaa kupata rais mpya, kwa kuwa kazi yake kubwa ilikuwa ni kuipigia debe CCM kupitia uimbaji wake.

Kulingana na maelezo ya waombolezaji, Mwanajeshi huyo aliyestaafu akiwa na cheo cha kapteni alikuwa ni mtu ambaye hakusita kueleza kile alichokiamini, jasiri asiyekubali kushindwa, mcheshi wakati fulani na mtu wa kutoa misaada.

Kijana mmoja ambaye alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kulia kwa uchungu, alilazimika kuondolewa katika viwanja hivyo baada ya kutaka kwenda kuaga tena mwili wa mbunge huyo, huku akisisitiza kuwa ndiyo aliyekuwa akimsomesha.

“Kapteni jamani umeondoka, hivi nani atanisomesha mimi. Niacheni nikamuage kwa mara nyingine huyu ni kama baba yangu mzazi, nitakuwa mgeni wa nani,” alisema kijana huyo na kuzidisha vilio, hasa kwa watoto wa marehemu.

Watu kutoka maeneo mbalimbali walifika katika viwanja vya Karimjee kumuaga mbunge huyo kuanzia saa tatu asubuhi, akiwamo mama mmoja aliyedai kuwa ametoka mkoani Mwanza kuja kuuaga mwili wa mbunge huyo.

Huku akilia mama huyo alisema, “Komba baba nimetoka Mwanza kwa ajili yako jamani, nenda ndugu yangu, nenda tu ipo siku tutaonana.”

Shughuli hiyo ilianza saa 3 asubuhi kwa wanamuziki mbalimbali wa bendi, muziki wa kizazi kipya na waigizaji wa filamu kuimba nyimbo za kumkumbuka mbunge huyo.

Wakazi wa Dar es Salaam walimiminika katika viwanja hivyo na tofauti na shughuli nyingine kama hizo, hakukuwa na ulinzi mkali wala watu kukaguliwa na vifaa maalumu.

Mara baada ya viongozi wa Serikali kumaliza kuaga mwili wa mbunge huyo, wananchi wengine nao walipewa fursa ya kuaga na kusababisha askari wa Bunge kutumia nguvu ya ziada kuwazuia kutokana na kutofuata utaratibu uliowekwa.

Watu hao walionekana kuwa na shauku ya kuaga mwili wa mbunge huyo, baadhi wakilalamikia kitendo cha kuzuiwa na askari hao wakisema kuwa Komba alikuwa mtu wa watu na wao wana haki ya kumuaga.

Hata hivyo, baadaye askari hao waliwahimiza watu hao kufuata utaratibu uliokuwa umepangwa na wote wakapata fursa ya kuaga mwili huo hadi shughuli zilipomalizika saa 7:30 mchana.

Salamu za CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema, “Sauti ya Komba imezimika lakini imefuatiwa na sauti ya vilio vya watu waliompenda wakiomboleza. Alikuwa mwalimu, mwanajeshi, kiongozi, mbunge, mwanasiasa na mwanamuziki mwenye kipaji cha kutunga nyimbo zinazoendana na wakati.”

Kinana alisema nyimbo zilizotungwa na Komba zilitumika kuwapa hamasa wanajeshi wa Tanzania waliopigana vita vya Tanzania na Uganda mwaka 1978 hadi 1979 vilivyouondoa utawala wa Iddi Amin nchini humo.

“Katika msiba wa Mwalimu Nyerere nyimbo alizozitunga ziliwaliza Watanzania, atabaki kuwa mfano wa kuigwa. Kifo chake ni pigo wa CCM, bendi yake, wasanii na wana familia yake,” alisema Kinana na kufafanua kuwa chama hicho kimetoa rambirambi ya Sh5 milioni.

Kambi ya Upinzani
Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alisema kifo cha Komba kimewagusa wabunge wote bila kujali itikadi zao za vyama.

“Kifo hiki kinatukumbusha kuwa hapa duniani binadamu tunapita tu. Tunatakiwa kutenda mema kwa ndugu, rafiki na Taifa letu,” alisema.

Kamati ya Bunge
Mbunge wa Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ambayo Komba alikuwa makamu wake, Said Matanda alisema kuwa alizungumza na marehemu saa tano kabla ya kufikwa na mauti.

“Tulikuwa tukizungumzia safari ya kamati yetu kwenda Ethiopia ambayo ilikuwa tuifanye kesho yake (Jumapili iliyopita), lakini saa tano baadaye nikapata ujumbe kuwa amefariki dunia, sikuamini,” alisema.

Alisema marehemu alikuwa zaidi ya kiongozi kwa kutunga nyimbo zenye ujumbe mzuri kwa jamii na alikuwa na uzoefu wa miaka tisa katika kamati hiyo na ndiyo maana wajumbe wa kamati hiyo hawakusita kumchagua kuwa makamu mwenyekiti wao.

Salamu za Serikali
Akitoa salamu za Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge), Jenista Mhagama alimwelezea Komba kama kiongozi aliyejitolea katika kila jambo.

“Juhudi na mipango aliyoifanya Komba katika jimbo lake Serikali kupitia ilani ya CCM itatekeleza. Serikali itatoa rambirambi zake kwa familia ya Komba wakati mwafaka,” alisema.

Ujumbe wa Makinda
Spika Makinda aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusamehe hata kama wametendewa mambo yanayowakwaza.

“Hapa duniani tunapita tu, hatutakiwi kuwatendea watu mambo ambayo sisi hatupendi kutendewa. Tusidhani kuwa kila tunachokitaka na kukiamini kitadumu, si hivyo. Komba ameondoka kama moto wa kibatali unavyozimika,” alisema.

Makinda alisema kama Komba angepewa dakika 15 za mwisho kabla ya kufariki ili aseme jambo lolote, ni wazi kuwa angesema kama kuna aliowakosea wamsamehe.

Alisema binadamu wote ni ndugu na hata wakifa inaelezwa na viongozi wa dini kuwa wanakwenda kukutana na raha au shida ambazo zinategemea na matendo yao waliyokuwa wakiyafanya duniani.

“Wanachama wa CCM tunamwombea marehemu na tunaamini kuwa Mungu atatupa Komba mwingine,” alisema.

Salamu za familia
Msemaji wa familia ya Komba, Dominick Mwakangale alisema mwili wa mbunge huyo ambao baadaye jana jioni uliagwa na wakazi wa Songea, utazikwa leo kijijini kwake Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Wengine ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) Jaji Damian Lubuva, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga, Katibu wa Shughuli za Bunge John Joel, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. MWANANCHI

NETANYAHU KUHUTUBIA BUNGE LA MAREKANI LEO

Obama na Netanyahu watofautiana kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wana mitazamao tofauti kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran huku Obama akionya kuwa Netanyahu amekuwa na mtazamo potovu kuhusu mpango huo
Hii leo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu atalihutubia bunge la Marekani ambapo anatarajiwa kuendelea na msimamo wake kuwa mpango wa kinyuklia wa Iran ni kitisho kikubwa kwa Israel na una shahidi wa kutosha kuthibitisha hilo.
Lakini Rais Obama na maafisa wake wa masuala ya sera za kigeni hawajamuachia uwanja Netanyahu kuuponda mpango wa kinyuklia wa Iran na mazungumzo yanayoendelea kati ya Iran na nchi tano zenye nguvu zaidi duniani pamoja Ujerumani, kwa kusema mazungumzo hayo ya kulenga makubaliano ndiyo njia bora zaidi ya kuusuluhisha mzozo huo.

WATATU WANUSURIKA KIFO WAKIENDA KWENYE MAZIKO YA KEPTENI KOMBA


Watu zaidi ya watatu wamenusurika kifo baada ya gari yao kupata ajali eneo la Lutukila mkoani Ruvuma katika barabara kuu ya Njombe -Songea wakielekea kumzika mbunge wa Mbinga Magharibi Kepten John Komba.


Ajali hiyo ilitokea Majira ya saa 7 usiku lakini katika tukio hilo hakuna aliyepoteza Maisha zaidi ya gari kuharibika vibaya likiwa na abria watatu, wawili kati yao ni wanawake na mwanaume ni mmoja.

Wakili wa Katiba auawa Msumbiji

Wakili mmoja mashuhuri katika maswala ya katiba amepigwa risasi na kuuawa mjini Maputo msumbiji
Mmoja wa wanaharakati wakuu wa kupigania haki za kikatiba nchini Msumbiji ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Maputo.
Gilles Cistac, ambaye anaasili ya Ufaransa amehusika pakubwa katika mchakato wa kugawanya madaraka katika serikali ya majimbo na ugavi wa mamlaka nchini Msumbiji.
Cistac alikuwa anapigania sera hiyo iingizwe katika katiba ya taifa jambo ambalo lilimfanya kutizamwa kama mtu anayependelea chama cha upinzani Renamo.
Afisa mkuu wa Afya katika hospitali kuu ya Maputo Joao Fumane amesema Cistac alipoteza maisha yake muda mchache baada ya kufanyiwa upasuaji.
'Mtu maarufu'
Awali msemaji wa rais Filipe Nyusi alikashifu mauaji hayo akisema kuwa hiyo ilikuwa tukio la kukera zaidi.
Mwanaharakati huyo ambaye pia ni mkufunzi katika chuo kikuu kitivo cha sheria alichangia kwa kina mchakato wa kubadilisha vipengele vya mamlaka ya urais.
Cistac alikuwa amepata uraia wa taifa hilo baada ya kuishi huko kwa tangu mwaka wa 1993.
Aidha mbali na kufundisha katika chuo kikuu cha Eduardo Mondlane, alikuwa amehudumu kwa kipindi kirefu kama mshauri wa maswala ya sheria katika wizara mbalimbali.
Katika miaka ya hivi punde kulikuwa na shauku ya kuzuka upya vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kundi la Renamo, kulalamika kuwa uchaguzi uliofanywa nchini humo haukuwa wa haki.
Renamo ilisitisha mapigano mwaka wa 1992 baada ya kukabiliana na serikali kwa kipindi cha miaka 16.
Kiongozi wake Afonso Dhlakama alikubalia mwito wa kujaribu kutafuta uwiano kupitia kwa bunge la taifa.
Inaaminika kuwa rais Filipe Nyusi, ndiye aliyewashawishi wabunge wa Renamo kujiunga na serikali .
Chama hicho kilichojizolea asilimia 36% ya kura za urais zilizopigwa mwezi Oktoba.

Mpinzani wa Urusi aliyeuwawa azikwa

Waombolezaji nchini Urusi wamejitokeza nje ya kituo cha haki za binadamu mjini Moscwo kwa ajili ya kuhudhuria maziko ya kiongozi wa upinzani aliyeuwawa Boris Nemtsov.
Warusi wauaga mwili wa kiongozi wa Upinzani aliyeuwawa na serikali,Nemtsov Boris Warusi wauaga mwili wa kiongozi wa Upinzani aliyeuwawa na serikali,Nemtsov Boris
Kiongozi huyo wa upinzani aliuwawa kwa kupigwa risasi ijumaa jioni wakati akitembea kwenye daraja la karibu na ikulu ya Kremlin akiwa pamoja na mpenzi wake. Hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Mwili wa marehemu Nemtov umelazwa kwenye sanduku ukiwa umevishwa sanda nyeupe katika kituo cha haki za binadamu cha Sakharov mjini Moscow, kituo ambacho kimepewa jina la aliyekuwa mpinzani enzi za utawala wa kisovieti na aliyewahisi kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel Andrei Sakharov. Mauaji ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Boris Nemtsov yameitikisa kwa kiasi kikubwa jamii ya vuguvugu dogo öla upinzani na ambalo limetengwa nchini Urusi.
Misururu ya waombolezaji waliojitokeza katika mazikoni,Moscow 
  Misururu ya waombolezaji waliojitokeza katika mazikoni, Moscow
Wengi wa wafuasi wa upinzani nchini humo wanashuku mauaji hayo yamefanywa kwa amri ya serikali ya Urusi kama hatua ya kulipiza kisasi kauli za mpinzani huyo za kumkosoa rais Vladmir Putin. Maafisa wa Urusi wameashiria kwamba kuna uwezekano mkubwa wa sababu zamauaji hayo kuwa zimetoakana pia na uchokozi ulioonekana kulenga kumchafua rais Putin. Nemtsov anazikwa leo mjini Moscow wakati ambapo baadhi ya wabunge maarufu kutoka Ulaya wamearifu kwamba wamezuiwa na nchi hiyo ya Urusi kuhudhuria maziko hayo.
Mabalozi wengi wa nchi za magharibi walitarajiwa kuhudhuria shughuli ya maziko iliyoanza asubuhi ya leo kwenye kituo cha Sakharov kabla ya maiti kuzikwa mchana wa leo kwenye makaburi yaliyoko nje ya eneo hilo. Hadi sasa kuna wawili mashuhuri kutoka Ulaya waliosema wamezuiwa na Urusi kuhudhuria maziko hayo.
Wafuasi wa upinzani wamejitokeza kwa wingi kumzika Nemstov akiwemo Mama yake mzazi Wafuasi wa upinzani wamejitokeza kwa wingi kumzika Nemstov akiwemo Mama yake mzazi
Aliyekuwa waziri wa nje wa Latvia Sandra Kalniete ambaye ni mbunge katika bunge la ulaya amesema lizuiwa na walinzi kuingia kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow jana usiku.Mbunge huyo ametoa taarifa baada ya kuzuiwa uwanja wa ndege akisema licha ya uamuzi huo wa serikali ya Putin anataka kuifahamisha familia ya Nemtsov pamoja na marafiki zake na wananchi wote wa Urusi wanaounga mkono Demokrasia watambue kwamba Ulaya ipo pamoja nao wakati huu wa majonzi.
Mwingine aliyezuiliwa na Urusi kuhudhuria maziko hayo ni rais wa baraza la seneti la Poland Bogdan Borusewicz aliyesema kwamba amenyimwa visa ya kuingia nchini humo.Shahidi mkuu wa tukio la mauaji ya Nemtsov ni mpenzi wake aliyekuwa naye wakati huo wa tukio Anna Duritsskaya ambaye anaendelea kushirikiana na kamati ya uchnguzi.Hata hivyo bibi huyo amerudi nyumbani kwao Ukraine.
Mwandishi:Saumu Mwasimba

LEO NI SIKU YA WANYAMAPORI NA MAZAOPORI:BAN KI MOON AIONYA DUNIA

Mnyama aliye hatarini kutoweka ulimwenguni
Leo ni siku ya wanyama na mazao ya porini duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka umakini zaidi katika kushughulikia vitendo vya uhalifu dhidi ya maliasili hiyo.
Katika ujumbe wake, Ban amesema biashara haramu ya wanyamapori na bidhaa zitokanazo na viumbe hivyo ikiwemo ndovu, magogo na faru, imekuwa ikiibuka na mbinu mpya kila uchao na hata kuzidi ile ya usafirishaji haramu wa binadamu na dawa za kulevya.

Amesema kushamiri huko kunapigiwa chepuo na rushwa na uongozi dhaifu akiongeza kuwa kuna ushahidi thabiti wa kuhusika kwa mitandao ya kihalifu iliyopangwa na vikundi vilivyojihami.
Ban amesema biashara hiyo haramu siyo tu inakwamisha utawala wa sheria bali pia unatishia usalama wa taifa na ni kikwazo kikubwa kwa juhudi za wanavijiji na jamii za watu wa asili za matumizi endelevu za maliasili.

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametaka umakini wa kushughulikia uhalifu huo akitaka ushiriki wa jamii zote zinazohusika na matumizi ya maliasili hizo kwa ajili ya dawa, chakula, ujenzi, samani, urembo na nguo.

Amesema endapo usimamizi wa sheria utakwenda sambamba na ushirikishi wa jamii nzima kutawezesha kumaliza tatizo la matumizi haramu ya bidhaa za porini

ANGALIA MELI KUBWA LAO

Siku chache zilizopita, meli kubwa kuliko zote duniani iliwasili nchini Uingereza na kuwa kivutio kikubwa.Meli hiyo ya mizigo ina uwezo wa kubeba makontena 19,100 na ukubwa wake ni sawa na viwanja vinne vya kuchezea mpira.
Meli hiyo imesajiliwa Hong Kong na ilitentengenezwa nchini China, ina uwezo wa kubeba tani 57,000 ambao ni uzito mkubwa zaidi unaoweza kuchukuliwa na chombo cha usafiri duniani.
Ilisafiri kwa mwezi mzima kutoka Shanghai China hadi nchini Uingereza.

HOTUBA YA MHE JK YA MWEZI WA PILI HII HAPA

17
Utangulizi
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuzungumza kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa hotuba za kila mwisho wa mwezi. Kwa mwisho wa mwezi wa Februari nina mambo matano ninayopenda kuyazungumzia. 
Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura

Jumatatu, 2 Machi 2015

JK AONGOZA MAMIA KUMWAGA HAYATI KEPTEN JOHN KOMBA


Rais Kikwete (katikati) akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Anna Makinda katika viwanja vya Karimjee ili kumuaga marehemu Kapteni John Komba.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee.


Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Mkapa.

Jumapili, 1 Machi 2015

NDEGE YA JESHI YAANGUKA MWANZA

Muonekano wa ndege ya ndege ya jeshi baada ya kuanguka leo uwanja wa ndege wa Mwanza.(Picha na Mtandao)
NDEGE ya kijeshi imeanguka tarehe 27/2/2015 uwanja wa ndege wa Mwanza na kusambaratika wakati inatoka kaskazini mwa uwanja huo kuelekea kusini ambapo rubani wake, Peter Augustino Lyamunda, amevunjika mguu.
Chanzo cha ajali hiyo ni ndege aliyeingia kwenye moja ya injini za ndege hiyo ilipotaka kuruka, ikashindwa na kuanguka.
Ndege wanaozurura kwenye uwanja huo wamekuwa ni tatizo na wameripotiwa kulalamikiwa na marubani. Hata hivyo kuwaua ndege hao kunaweza kuaua malalamiko kwa watetezi wa haki za wanyama.