Watakaokiuka sheria ya uvutaji sigara mjini Beijing kupigwa faini kali
Serikali
ya China,imepiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya wazi
katika mji wa Beijing. Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika
maeneo yote ya wazi na watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa
faini.
Hata hivyo China ina wavuta sigara milioni mia tatu wakati
sheria ya kusitisha wavutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa
Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa
kutekelezeka.
Ripoti inasema kuwa watu wengi wanadhani sheria hiyo ya
kukataza kabisa uvutaji sigara haitafanya kazi.
Waziri Mkuu Mizengo wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Ametoa
wito huo wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho
ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)
yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia uandishi wa wosia mbele ya
wakili, Waziri Mkuu alisema uandishi wa wosia ni suluhisho la migogoro
mingi inayosababishwa na wanandugu ambao wakati mwingine wala
hawakushiriki kuchuma mali wanayogombea.
“Kuandika wosia siyo uchuro kama ambavyo watu wengi wanadhani…
ninatoa wito kwa watanzania kuandika wosia mapema kwani inasaidia
kuondoa matatizo ya mirathi baada ya mmoja wao kuondoka duniani,”
alisema.
Benki ya Afrika ya Maendeleo, ADB imepata rais mpya, waziri wa kilimo wa
Nigeria Akinwumi Adesina, ambaye amewashinda wapinzani 7 katika duru 6
za uchaguzi. Anachukua nafasi ya Donald Kaberuka anayemaliza muda wake.
Akinwumi Adesina, rais mteule wa Benki ya Afrika ya Maendeleo, ADB.
Akinwumi Adesina aliibuka mshindi baada ya duru sita za uchaguzi,
zilizomalizika jana jioni katika makao makuu ya Benki ya Afrika ya
Maendeleo mjini Abidjan, Cote d'Ivoire. Adesina, msomi mwenye shahada ya
uzamili katika masuala ya uchumi na maendeleo, anachukua hatamu za
benki hiyo ambayo inajikuta katika mazingira mapya kifedha barani
Afrika.
Baada ya kupata ushindi wa karibu asilimia 60 ya wajumbe wa bodi ya
magavana wa benki hiyo, Akinwumi Adesina alisema atakuwa rais mwenye
kujituma.
''Nataka kuwahakikishia, kwamba kama rais wa benki hii, nitakuwa rais
mwenye kuwajibika, mwenye bidii, na mwenye mwelekeo. Nitakuwa rais
atakayefanya kazi pamoja nanyi, katika hali ya ushirikiano, kujengea
kwenye msingi mzuri kabisa unaoachwa na rais Kaberuka''. Amesema
Adesina.
Forum cc yaendelea yaendesha semina ya siku mbili katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi FDC Njombe.
Akizungumza
wakati wa matembezi ya mafunzo baada ya mafunzo ya ndani ya kilimo
biashara na utunzaji wa mazingira ambacho kimetolewa na taasisi ya Forum
CC kwa kushirikiana na taasisi ya Seco Njombe, afisa mtendaji wa kata
ya Luponde, Stanley Mkondola alisema kuwa wananchi kwa sasa wamekuwa
waoga kuchukua mikopo kutoka halmashauri.
Rais mpya wa Nigeria aliyeapishwa rasmi hii leo Muhammadu Buhari
amesema, Ufisadi, ugaidi, ukosefu wa ajira na matatizo ya umeme ni mambo
ambayo yanapewa kipaumbele katika masuala ya kisiasa ya Nigeria.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Buhari, mwenye umri wa miaka 72 aliapishwa rasmi mjini Abuja Nigeria,
mbele ya takriban wageni 20,000 walioalikwa wakiwemo marais zaidi ya 50
na wawakilishi wa serikali kuu ulimwenguni. Buhari alijipatia ushindi wa
asilimia 54 ya kura katika uchaguzi uliofanyika tarehe 28 mwezi Machi,
dhidi ya rais wa zamani Goodluck Jonathan aliyeiongoza Nigeria kwa miaka
mitano.
Mwana
wa mfalme wa Uingereza, Prince William ametoa wito kwa shirikisho la
soka duniani FIFA kuweka maslahi ya soka mbele ya matamanio ya
kibinafsi.
Kwenye hotuba yake kabla ya fainali ya kombe la FA
nchini Uingereza, William ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka la FA
nchini Uingereza, ameilinganisha sakata ya FIFA na ile ya jiji la
Salt Lake ilivyofanyika wakati Marekani ilikuwa inasaka tiketi ya
kuandaa mashindano ya olimpiki ya barafu mnamo mwaka wa 2002 na
kuilazimu kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuimarika.
Aliyekuwa mlinzi wa timu ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand amestaafu kucheza kandanda ya kulipwa.
Ferdinand
amesema kupitia kwa taarifa kwa meza ya michezo ya BT kuwa anahisi
wakati umewadia kwake kufunganya virago na kushabikia mchezo anaoupenda.
Hatua hiyo ya mlinzi hiyo inafuatia kuruhusiwa kwake kuondoka na klabu ya Queens Park Rangers.
Klabu
hiyo ya QPR ilimruhusu kuondoka baada ya kushushwa daraja baada ya
kumaliza katika nafasi ya 20 katika ligi ya msimu huu iliyokamilika juma
lililopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amesema ''nafikiri huu ndio wakati wa kustaafu kutoka kwenye mchezo ninaopenda''
''Lakini najivunia kuiwakilisha taifa langu katika mechi 81 za kimataifa'
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chris Ramsey, Harry Redknapp, David
O’Leary na David Moyes ambao waliniwezesha katika nyakati tofauti katika
maisha yangu ya soka bila ya kusahau wafanyakazi wengine katika timu
ambao walionyesha kunijali kwa miaka yote. Pia wachezaji wote ambao
nimewahi kucheza nao. Ningependa kutoa shukrani kwa timu iliyonisaidia
wakati nikiwa nje ya mchezo huu, Jamie Moralee na kila mtu katika
kipindi hiki kipya ninachokianza rasmi.”
“Kushinda
makombe kwa kipindi cha miaka 13 nikiwa na klabu ya Manchester United
ilinifanya nifanikiwe kila kitu nilichokuwa nikikitamani katika tasnia
ya soka. Tangu utotoni mpaka wakati huu, hicho ndicho nilichokuwa
nikikiwaza mara zote. Vyote hivyo sidhani kama vingewezekana bila ya
kiungo muhimu kabisa ambaye ni, Sir Alex Ferguson. Upeo wake mkubwa
katika macho yangu utaendelea kudumu daima. Kwa mtazamo wangu yeye ndiye
atabaki kuwa kocha bora kabisa katika historia ya mpira wa Uingereza.”
“Pia
ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu Rebecca na
familia yangu, akiwemo mama na baba yangu kwa kujitolea maisha yote juu
yangu pia faraja na ushauri wao waliokuwa wakinipa kwa kipindi chote
nilichokuwa nikisakata soka”
“Na
mwisho kabisa, ningependa kuwashukuru mashabiki wote katika klabu zote
kwani bila yao mpira huu uliojaa utaalamu wa hali juu usingekuwepo.
Nitamkumbuka kila mmoja wenu kwenye jioni hii ya siku ya Jumamosi.”
Watu
10 wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa na mawe na mapanga wamemnyang’anya
bunduki aina ya SMG na risasi 30, askari polisi wa Kituo cha Tazara
kilichopo eneo la Yombo Station na kutokomea kusikojulikana.
MLONGE
kwa jina la kitaalam unajulikana kwa jina moringa oleifera. Mti huo wa
kipekee ambao asili yake ni India, siku hizi unapandwa sehemu nyingi za
kanda za kitropiki na nusutropiki. Hapa
nchini kuna miti ya aina mbalimbali ikiwemo ile inayotambulika na jamii
kutokana na umaarufu na pia ipo ambayo haifahamiki kabisa.
Mfano
wa miti inayofahamika kiasi kwamba hata ukiitaja katika kundi la watu
wengi wao wanakuwa wanaifahamu ni pamoja na mti wa muarobaini na mbuyu,
ambayo imekuwa ikifahamika kuwa ni miti dawa na imekuwa ni msaada mkubwa
kwa wale wanaofahamu matumizi yake.
Maelfu
ya watu wamefanya maandamano ya amani nchini Venezuela wakipitia
barabara za mji mkuu Caracas wakitaka kuachiliwa kwa viongozi wa
upinzani ambao wamekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Wanasiasa
hao ni pamoja na mameya wawili wa zamani Leopoldo Lopez na Daniel
Ceballos ambao wanazuiliwa kwa mashtaka ya kuchochea maandamano ya
kuipinga serikali.
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro amewalaumu
kwa vifo 43 vilivyotokea wakati huo.
Wiki hii viongozi hao wa zamani wa upinzani walitangaza
kuanza mgomo wa kutokula wakiwa gerezani
Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono
maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa
Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jana, wakati wa kutangaza nia
yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mwanamke ambaye kakake alikufa katika ajali mbaya ya barabarani amekutana na mtu aliyepewa uso wa marehemu.
Amini
usiamini mtu huyo aliyefanyiwa upasuaji huo wa kihistoria alipandikizwa
uso mpya baada yake kuishi kwa miaka 15 akiwa bila pua.
Bwana huyo Richard Norris alimshukuru mwanamke huyo kwa niaba ya kakake marehemu aliyemwezesha kupata mwanzo mpya maishani.
Mwanamke huyo bi Rebekah Aversano alionekana akiugusa uso wa kakake akiwa haamini macho yake.
Bwana Richard Norris, anayetokea Virginia, Marekani alijeruhiwa katika ajali ya ufyatulianaji wa risasi miaka 15 iliyopita.
Yamkini Norris hakuwa amewahi kutoka nyumbani kwake katika kipindi hicho chote.
Watu
29 wameuawa katika mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua
ndani ya msikiti.
Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulizi
hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri
lililoendeshwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Wanamgamabo hao walifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13.
Picha ya maktaba mwanaume akiwa ameshika panga. Wakati wananchi wakilalamikia
uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo mpya wa
kielektroniki wa Biometric Voters Registration (BVR), maofisa 10 wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) wameshambuliwa na kujeruhiwa na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakienda kuandikisha wapigakura
wilayani Momba, mkoani Mbeya.
CCM ipo kwenye wakati mgumu wa kutafuta
mrithi wa Jakaya Kikwete katika nafasi ya urais na mwenyekiti wa chama
hicho kikongwe nchini baada ya Rais huyo wa sasa kuongoza nchi kwa
vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja na hivyo kulazimika kuondoka
Ikulu kutokana na utashi wa kikatiba.
Dar es Salaam. Ni siku tatu za
hekaheka na kujenga hoja za kujinadi kuanzia kesho wakati makada wa CCM
watakapotangaza kwenye mikutano ya hadhara sababu zilizowasukumu kuomba
kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
CCM ipo kwenye wakati mgumu wa kutafuta mrithi wa
Jakaya Kikwete katika nafasi ya urais na mwenyekiti wa chama hicho
kikongwe nchini baada ya Rais huyo wa sasa kuongoza nchi kwa vipindi
viwili vya miaka mitano kila kimoja na hivyo kulazimika kuondoka Ikulu
kutokana na utashi wa kikatiba.
Kutokana na hilo, zaidi ya makada 20 wanatajwa
kuwa na nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais ili kuongoza Serikali
ya Awamu ya Tano na watatakiwa kutangaza, kuchukua fomu na kuzirudisha
ndani ya takribani siku 32 kabla ya Julai 2 ambayo ni siku ya mwisho
iliyowekwa na chama hicho.
Tembo
wakiwa wamemzunguka mwenzao kumpatia msaada. SUALA la umoja si kwa
wanadamu pekee bali hata wanyama kama tembo nao wanao umoja miongoni
mwao.
Katika
tukio lililonaswa kwenye video huko nchini Afrika Kusini na kuwekwa
kwenye mtandao wa Youtube linawaonyesha tembo walioamua kufunga barabara
na kusababisha foleni ya magari ili wamuokoe mwenzao aliyedondoka
katikati ya barabara hiyo.
Tembo
huyo akiwa chini baada ya kudondoka.Tembo huyo mdogo alidondoka wakati
akitembea barabarani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kruger iliyopo Afrika
Kusini.
Polisi 12 wamekamatwa nchini Malaysia kufuatia tuhuma za kushirikiana na walanguzi wa binadamu.
Waziri
wa maswala ya usalama wa ndani Wan Junaidi Tuanku Jaafar amesema wawili
kati ya maafisa hao 12 wamehusishwa na usafirishaji wa wahamiaji.
Waziri huyo pia amekariri kuwa makaburi 139 yaliyogunduliwa karibu na mpaka wa Thailand majuzi, hayakuwa ya halaiki.
Raia
15 wa China wamefunguliwa mashitaka nchini Marekani kwa tuhuma za
udanganyifu wa matokeo na nyaraka za kitaaluma walizozitumia kujiunga na
elimu ya juu nchini Marekani.
Kwa mjibu wa waendesha mashtaka
nchini humo,wamebaini kuwa vijana hao wa China wamekuwa fanya
udanganyifu wa kutumia simu wakati wa majaribio ya kujiunga na vyuo
hivyo. Idara ya sheria nchini Marekani imesema kuwa kwa kipindi cha
minne iliyopita wamekuwa wakikwepa mfumo halali wa uchaguzi wa majina ya
chuo na badala yake kutumia majina bandia na pasi bandia za kusafiria.
Iwapo
watakutwa na hatia kutokana na tuhuma hizo, raia hao wa China watafungwa
hadi miaka 20 jela.
Muhudumu mmoja wa baa amepatikana na hatia ya mauaji baada ya kumpa mteja wake jumla ya vipimo 56 vya pombe na kisha akafa.
Raia
huyo wa Ufaransa alimpa Renaud Prudhomme, mwenye umri wa miaka 56,
''shoti'' 56 za mvinyo katika baa yake kwa nia ya kuvunja rekodi ya
mywaji pombe nambari moja.
Marehemu Prudhomme, aliyekuwa ameandamana na binti yake kujiburudisha, alipelekwa nyumbani akiwa mlevi chakari.
Inaarifiwa kuwa alikimbizwa hospitalini ambapo alipatikana ameaga dunia siku iliyofuatia.
Hata
hivyo mahakama ilimpata na hatia mhudumu huyo Gilles Crepin, mwenye
umri wa miaka 47, kwa kumchochea marehemu Prudhomme aendelee kubugia
mvinyo ilihali alikuwa mlevi kupindukia.
Mahakama ilisema kuwa
Crepin aliendelea kuandika nani anayeshikilia rekodi hiyo kwenye ubao
uliotundikwa hadharani kwa wateja wake.
Sasa Crepin amehukumiwa
kifungo cha nyumbani cha miezi minne na kupigwa marufuku ya kufanya
kazi katika baa yeyote kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Wakili wake Renaud Portejoie tayari amesema kuwa atakata rufaa dhidi ya kauli hiyo ya mahakama.
"kauli hii haina hata chembe
ya haki bali ni hisia tu zilizotumika hapa ,ninavyoona mimi hizi ni
jitihada za amahakama kutoa hukumu ili iwe funzo''
Awali alikuwa
ameiambia mahakama kuwa kifo cha Prudhomme hakikutokea kimsingi na
kufuatia matukio ya mteja wake kwani marehemu alikuwa na maradhi ya
kupumua mbali na kuwa mraibu wa tembo.
''kwa hakika hatuwezi kuwalazimisha wateja wote wa pombe kutoa ithibati kuwa wako katika hali nzuri ya afya''
Wakili wa mwanawe marehemu Antoine Portal, alisema kuwa familia yao imetulizwa na marufuku hiyo ya Crepin ya mwaka mmoja.
''Nilikuwa nataka tu kuwakumbusha wahudumu wa baa kuwa ni kinyume cha sheria kuendelea kumpa pombe mlevi''
Kanisa Katoliki nchini Burundi limejiondoa katika mchakato mzima wa uchunguzi na uongozi wa aina yoyote katika uchaguzi huo.
Uamuzi huo umekuja wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo
Kanisa
katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini
Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya
tisini.
Rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA Sepp Blatter,amekataa kata kata kujiuzulu.
Rais wa shirikisho la soka barani ulaya Michel Platini amewambia waandishi wa habari kuwa Blatter amekataa wito wa kujiuzulu.
Platini
amesema kuwa kufuatia uamuzi huo UEFA sasa itashiriki uchaguzi hapo
kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura mpinzani wa Blatter
mwanamfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Shirikisho la soka la Afrika Kusini SAFA, limekanusha madai yote ya kuhusishwa na hongo.
Afisa
wa mawasiliano wa Safa Dominic Chimhavi amewataka wote wenye ushahidi
dhidi ya shirikisho hilo kuuweka wazi ili kuondoa shaka iliyoibuka
kufuatia kukamatwa kwa maafisa wakuu wa FIFA.
Tuhuma hizo
ziliibuka baada ya polisi wa Uswisi kuwakamata maafisa wakuu 7 wanaotuhumiwa kwa kushiriki ufisadi na kula kiinua mgongo cha takriban
dola million 150 ndani ya kipindi cha miaka 20.
Waziri
mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair amejiuzulu nafasi ya ujumbe wa
umoja wa kimataifa katika kamati unaoshughulikia usuluhishi wa mgogoro
wa Mashariki ya kati Quartet, unaohusisha nchi ya Israel na Palestina
nafasi ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka minane.
Vyanzo vya
habari vilivyokaribu na Blair vinasema ataendelea kuwepo akijihusisha na
baadhi ya shughuli na eneo hilo. Watoa habari hao wanasema kuwa waziri
mkuu huyo anaamini kuwa mtazamo mpya unahitajika. Lakini wakosoaji
wanasema Blair alipambana katika jukumu ambalo lilikuwa na mipaka katika
maendeleo ya kiuchumi na ameshindwa kuleta matokeo chanya.
Afisa mmoja
wa Palestina amemlaumu Blair kwa kufanya kazi ili kuwaridhisha waisrael
na Marekani. Umoja huo unaundwa na UN, EU nchi ya Marekani na Urusi
Mwili wa Joseph Gabriel ukiwa barabarani kusubiri jeshi la polisi waje kuuondoa
Kijana Joseph Gabriel anayefanya vibarua mbalimbali vya kujiingizia
kipato amekutwa amekufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na
huku sehemu ya pua ikiwa imeondolewa sambamba na sehemu ya shavu lake la
kushoto.Mauaji haya ya
kutisha yametokea katika maeneo ya kata Karabagaine katika kijiji cha
Kitwe.Polisi pia walichelewa kufika eneo la tukio kutokana na kuwa
katika eneo jingine ambako pia kulikuwa na tukio jingine la kutisha kama
hili lilitokea siku moja kabla ya hili.Mwanamke mmoja
ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa kwa
kuchinjwa shingo na pua yake kuondolewa.Pua yake ilipatikana baadae
karibu na eneo la tukio.Mama huyu amekutwa na mauti katika mtaa wa
Kibeta kata ya Kibeta ambapo baadaye polisi waliweza kufika na kuchukua
mwili wa marehemu.
Usiku
wa kuamkia leo kulikuwa na kivumbi cha fainali ya Uefa ndogo, kwenye
mtanange ulioikutanisha Sevilla ya Hispania dhidi ya Dnipropetrovsk ya
Ukrain.
Katika mchezo huo uliopigwa mjini Warsaw nchini Poland,
Sevilla imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2, huku shukrani za dhati
zikienda mkolombia Carlos Bacca aliyetumbukiza kimiani mabao mawili kati
ya matatu yaliyoipa ushindi Sevilla.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa
timu hiyo kunyakua kombe hilo na kuweka rekodi ya kuchukua mara nyingi
zaidi taji hilo. Ukiachilia mbali ushindi huu walioupata jana, Sevilla
ilitawazwa kuwa mabingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2006, 2007 na 2014.
Mahakama nchini Kenya imeamuru hospitali maarufu kulipa faini ya dola zaidi ya elfu 48 kwa kushindwa kuzuia uzazi .
Jaji
alibaini kuwa mmoja wa wahudumu wa hospitali ya Aghakhan alizembea
katika kupachika mwilini dawa ya kuzuia utungwaji wa mimba
iliyochaguliwa na mwanamke kwenye mkono wake, licha ya kwamba mwanamke
huyo alifanyiwa upasuaji mdogo kwa ajili ya kuzuia uzazi. Mwandishi wetu
Anne Soy anarifu zaidi kuhusu uamuzi huo wa mahakama usio wa kawaida.
Maafisa
sita wa shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa katika hoteli moja
mjini Zurich, Switzerland. kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya
rushwa.
Watuhuhumiwa hao ambao wanasemekana kuwa ni pamoja na
makamu wa rais wa FIFA,wanashikiliwa wakisubiri kusafirishwa kwenda
Marekani.
Shutuma hizo zinahusisha rushwa ya takriban kiasi cha dola za Marekani milioni 100 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa kimataifa na naibu wake pamoja na Balozi mpya wa
Tanzania nchini Saudi Arabia katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar
es Salaam leo.
-Katibu
Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi Liberata
Mulamula akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
Katibu
Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Balozi Liberata
Mulamula akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan
Simba Yahya akila kiapo Mbele ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na
kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Balozi Hassan
Simba Yahya akipokea vitendea kazi kutoka kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na kukabidhiwa kanuni na miongozo ya kazi.
Balozi
mpya wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mh. Hemed Iddi Mgaza akila kiapo
mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya
kazi(picha na Freddy Maro)
Waziri wa maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu akimsikiliza waziri wa
Ardhi na Maendeleo vijijini, Celso Coreia jana mjini Maputo kabla ya
kusaini mkataba wa makubaliano ya kuhifadhi Pori la akiba la Selous
nchini Tanzania lililoungana na Hifadhi ya Nnyasa nchini Msumbiji ambapo
mbali na uhifadhi watashirikiana kupambana na ujangili , utaalamu na
vifaa.
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International
limelaumu majeshi ya Hamas huko Gaza kwa kuendesha vitendo vya kikatili
na utekaji nyara, mateso na mauaji kwa raia wa kipalestina kufuatia
mgogoro kati ya Israel na makundi ya wapiganaji wa Palestina katika
maeneo ya mpakani.
Mashambulio hayo yaliwalenga raia wakiwatuhumu kushirikana na Israel.
Amnesty
imesema kwamba hali ni mbaya wakati vikosi vya askari wa Israel wakiwa
katika harakati zao za mauaji ya kutisha na uharibifu kwa watu wa
Gaza,Hams inatumia fursa hiyo kujipanga kwa ushindi.
Ripoti hiyo
inabainisha kuwa harakati za chama cha Hamas ambacho kimekuwa
kikiaminiwa inaonyesha kuwa imekuwa ikitumia mashambulizi ya majeshi ya
Israel kulipiza kisasi dhidi ya maadui ndani ya chama hicho.
Dar/Mbeya. Ni dhahiri sasa kuwa
hatua ya vikao vya juu vya CCM kuwafungulia makada wake waliokuwa
wamefungiwa kwa kuanza kampeni mapema na kutangaza tarehe za kuanza
kuchukua fomu, vimechochea harakati za kusaka urais na kuongeza urefu wa
foleni ya wanaotaka kuelekea Ikulu kumrithi Rais Jakaya Kikwete. Hayo
yamejitokeza ndani ya siku nne baada ya uamuzi huo wa CCM kutangazwa
mjini Dodoma na kuwafanya makada wake, kuanza kujitokeza hadharani
wakiweka bayana tarehe za kutangaza nia hiyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa ya Singida na Shinyanga kuanzia jana,
Jumatatu, Mei 25, 2015.
Katika
uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Festo Luganda Kang’ombe kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na Ndugu Abdul Rashid Dachi kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kang’ombe alikuwa Mkurugenzi wa
Halmashuri ya Kibaha, Mkoa wa Pwani wakati Ndugu Dachi alikuwa Katibu
Tawala Msaidizi, Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi.
Ndugu Kang’ombe anachukua nafasi ya Ndugu Liana Hassan ambaye
amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria tokea Machi, mwaka huu,
na Ndugu Dachi anachukua nafasi ya DktAnselm Tarimo ambaye naye
alistaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria Januari 22, mwaka huu,
2015.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
26 Mei, 2015
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Mabalozi wa Tanzania
unaofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
unajadili kwa kina namna ya kutekeleza dira mpya ya Sera ya Mambo ya Nje
ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya Uchumi na Diplomasia Duniani
na kuleta tija nchini.