Shirika
la afya duniani WHO, limesifia matokeo ya chanjo mpya ugonjwa wa Ebola, inatoa asilimia 100% ya kinga baada ya majaribio yake nchini
Guinea.
WHO linasema kuwa ulimwengu unakaribia zaidi kupata chanjo mpya dhidi ya ugonjwa huo hatari wa Ebola.Ijumaa, 31 Julai 2015
PROFESA MARK MWANDOSYA AFUNGUKA
Leo
ni siku inayofuatia jana, siku ambayo Ndugu yangu Edward Ngoyai Lowassa
aliacha rasmi uanachama wa CCM na kupewa kadi ya uanachama wa Chadema.
Si yeye tu bali alisindikizwa na mke wake mpendwa Mama Regina Lowassa.
Nilidhani
leo mitandao yote ingesheni habari hiyo kubwa. Kumbe nami nimekuwa
"staa" katika mitandao ya kijamii. Kuanzia asubuhi nimekuwa nikipokea na
kujibu simu mbalimbali nikiulizwa maoni yangu kuhusu tukio la jana,
kuhusu mchakato wa Dodoma uliomalizika hivi karibuni, na "habari" kubwa
imekuwa Mwandosya, Mwapachu na ole Medeye wahamia Chadema!
Kuhusu Ndugu Lowassa kuhamia Chadema nionavyo mimi ni jambo la kawaida sana katika demokrasia ya vyama vingi.
Wanachama
hutoka na kuingia karibu kila siku. Hivyo basi tukio la jana
lisingegonga vichwa vya habari kama isingekuwa kwa umaarufu wa mhusika.
Jambo la msingi kwa CCM ni kutafakari, bila ghadhabu, na kwa utulivu, ni
sababu zipi za msingi zilizofanya hili jambo litokee? Je tunaweza
kujifunza lolote katika hili ili kukiimarisha Chama? .
Tunaweza
kuboresha nini katika taratibu na kanuni zetu? Nimeulizwa pia kitendo
cha Ndugu Lowassa kuhamia Chadema kina athari gani kwa CCM? .
Pamoja
na kutotokuwa msemaji rasmi wa Chama, tukio hili lina maslahi ya umma
kwa ujumla hivyo kukwepa kujibu hakusaidii. Siasa ni takwimu, hasa
tunapoelekea Oktoba. Kwa mantiki hiyo mtu mmoja kukihama Chama kuna
maana kura moja iliyopungua.
Kwa
kuwa haiwezekani kuirudisha, basi changamoto ni kuwa na mkakati wa
kutafuta kura ya kufidia, kuzuia kupotea kwa kura nyingine, na kuongeza
idadi ya wanaoingia ili iwe kubwa kuliko ile ya wanaotoka.
Msaafu
wa dini unasema mchungaji bora ni yule anayeweza kuwaacha kondoo wake
tisini na tisa walio salama ili amtafute yule mmoja aliyepotea! Suala la
kujiuliza katika mazingira ya yaliyotokea ni je tulikuwa wachungaji
bora? .
Nadhani
moja ya mambo ya msingi CCM itabidi tulitafakari kuhusiana na mchakato
wa kumpata mgombea wetu kwa nafasi ya urais ni je tunamtafuta mwanachama
ambaye atakuwa Rais? Je tunamtafuta mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi na
Mwenyekiti wa Chama? Au tunamtafuta mtu atakayekuwa Rais na Waziri
Mkuu?
Vigezo
vya kumtafuta mtu huyo vinapishana kama ambavyo orodha wa wenye nia au
mifumo ya kumpata itapishana. Naamini tungelitafakari haya yote huenda
tusingefika hapa tulipo. Lakini Taifa ni kubwa kuliko sisi watu na uhai
wake ni mpaka "kiama cha wafu".
Tujadili
masuala haya na mengine muhimu, kwa ujasiri, uwazi na ukweli.
Nahitimisha kwa kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii
na watu wengi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mwandosya
kuhama kwenda Chadema.
Misingi
iliyojengwa na waasisi wa Chama, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume naendelea kuamini bado ni
sahihi. Ndiyo iliyotuletea heshima kubwa kama Taifa.
Kama
tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya
misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi Ilihali misingi ipo, na imara,
nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu
tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka
kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe! Prof.
Alhamisi, 30 Julai 2015
KENYA YAUA AL SHAABAB 3
Jeshi ya Kenya linasema limewaua magaidi watatu wa Al Shabab katika eneo la Lamu lililoko Pwani ya Kenya.
Wanajeshi watano walijeruhiwa katika shambulio hilo ,wakati gari la wanajeshi lilipogongwa kilipuzi na kulipuka.Msemaji wa jeshi la Kenya, Kanali David Obonyo amesema gari hilo la jeshi lilikuwa linafanya doria ya kawaida na ndipo likakanyaga kilipuzi kilichotegwa. Hivyo wanajeshi hao walianza mashambuzi na kufanikiwa kuwaua magaidi watatu na kuzipata bunduki mbili pamoja na risasi kumi na saba.
Eneo la Lamu limekumbwa na msururu wa mashambulizi kwa muda sasa. Mwezi Juni wapiganaji kumi na mmoja, akiwemo raia wa Uingereza, na wanajeshi wawili waliuawa , baada ya Al Shaabab kuvamia kambi ya jeshi eneo la Lamu.
Mwaka jana watu wasiopungua 60 waliuawa na AL Shababa katika shambulio eneo la Mpeketoni Lamu, siku mbili mfululizo. Na siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za magari ya abiria kuvamiwa na wanamgambo hao kwenye barabara ya Lamu, ingawa Polisi wamekanusha habari hiyo.
Hata hivyo msako Mkubwa unaendelea katika msitu wa Boni wanakodaiwa kujificha magaidi hao.
UKIKOJOA UKUTANI MKJO UTAKURUDIA
Onyo: Ukikojoa kwenye ukuta wowote wa mji wa San Francisco , huenda mkojo ukakurudia
Ajenti
wa wizara ya nguvu kazi mjini humo amesema kuwa wanajaribu aina ya
rangi ya ukuta inayorudisha mkojo katika maeneo ambayo ni maarufu kwa
watu kujisaidia ovyo ovyo.Mtu yeyote atakaye tumia ukuta uliopakwa rangi hiyo, mkojo wao utawarudia, hiyo ni kulinganana na msemaji wa mawakala hao.
Mkurugenzi wa mawakala hao alipata wazo hilo baada ya kupata maarifa kuhusu rangi hiyo akiwa katika sehemu moja ya burudani nchini Ujerumani.
MARADONA AMTUHUMU MKEWE KUMCHAPA HELA
Nguli
wa soka Duniani ,Diego Maradona amemtuhumu mke wake wa zamani Claudia
Villafañe kwamba kumuibia kiasi cha fedha zipatazo dola milioni tisa,
katika akaunti yake ya benki.
Akizungumza katika matangazo ya moja
kwa moja ya Luninga,Maradonna amesema Villafañe ambaye alikuwa mpenzi
wake wa zamani ni mwizi. Hata hivyo Villafañe amepinga vikali madai na
kudai kuwa yeye si mwizi na hakuiba fedha hizo.Wapenzi hao ambao walikutana katika mji uliokithiri kwa umasikini huko Buenos Aires kabla ya Maradonna kuwa maarufu na kuwa miongoni mwa wachezaji mahiri duniani katika historia ya soka,waliachana kimapenzi kutokana na kutofautiana.
Watoto wao wawili Dalma and Giannina,wamekaririwa kwenye mtandao wa twitter wakimtetea mama yao wazi wazi na kwamba hahusiki na upotevu huo wa fedha za baba yao.
Jumatano, 29 Julai 2015
KOCHA MIGUEL AFURUTWA KAZI
Kocha kutoka Mexico, Miguel Herrera amefukuzwa kazi baada ya kumshambulia mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha luninga.
Hatua
hii ya kufukuzwa kazi kwa kocha huyo kunakuja ikiwa ni mbili tu baada
ya kuongoza kikosi hicho kwenye kombe la saba la medali ya dhahabu
nchini Marekani.Miguel Herrera mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akiiongoza timu hiyo ya Mexico kwa miaka16 hadi sasa. katika utetezi wake Herrera amesema kuwa alifanyiwa fujo ndo maana akafikia hatua hiyo
Jumatatu, 27 Julai 2015
ZIARA YA RAIS OBAMA KENYA YAKAMILIKA
RAIS WA MAREKANI
BARRACK OBAMA AMEKAMILISHA ZIARA YAKE YA SIKU TATU NCHINI KENYA AMBAPO
ALIFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA AKAWAHUTUBIA WAKENYA KATIKA UWANJA WA
KASARANI NA BAADAYE KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA KIJAMII
KATIKA CHUO KIKUU CHA KENYATTA
MWANE WHITNEY AITWAYE BOBBI KRISTINA AFARIKI DUNIA
Bobbi
Kristina Brown, mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji
wa muziki wa R&B, amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda
wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu, tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.
Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 Januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado. Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitiliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufariki dunia.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.
OBAMA AIONYA ETHIOPIA KUHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BANADAMU
Rais
Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia
amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za
kibinaadamu pamoja na uongozi bora.
Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.
Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yaliyoafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo.
ABIRIA ATEMBEZA KISU NDANI YA DALADALA NAYE AUAWA
Mmoja wa abiria aliyejeruhiwa kwa kisu
Mtu mmoja
aliyekuwa abiria ndani ya daladala lililokuwa likitoka mjini kuelekea
Makumbusho amewashambulia kwa kisu abiria kadhaa ndani ya gari maeneo ya
Magomeni na kuwasababishia majeraha makubwa
Majeruhi wote wamekimbizwa
hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala.
Mshambuliaji huyo ameuawa na wananchi wenye hasira.
Hadi
sasa haijafahamika nini lililkuwa lengo la mshambuliaji huyo.
Wananchi wanaendelea kukumbushwa juu ya kutojichukulia sheria mkononi
MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU KUTOKA MAREKANI ATUA NCHINI, KUFANYA KONGAMANO LA WATOTO NA WAZAZI JIJINI DAR ES SALAAM
King Nahh
MTOTO
mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri wa kujijengea uwezo wa
kujiamini anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani, Lonnie Hudson
maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua jijini Dar es Salaam.
King
Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson ambapo wapo nchini
kwa mwaliko wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
Leo
mtoto huyo atafanya kongamano kubwa la watoto na wazazi katika
Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za watu
ambao wamekata tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini
katika maamuzi.
RAIS KIKWETE AKIMUAPISHA MKURUGENZI MPYA WA UCHAGUZI IKULU JIJINI DAR
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akimuapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi
Ikulu jijini Dar es salaam jioni Julai 25, 2015.
MADAKTARI WA DIASPORA KUTOKA MAREKANI WATOA HUDUMA ZANZIBAR
Madaktari wa kujitolea toka Marekani ambao wamepeletwa Tanzania na
Jumuiya ya Watanzania DMV wakiratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa chini ya kitengo cha Diaspora leo siku ya
Jumamosi July 25, 2015 walitembelea chuo cha elimu ya Afya na kutoa
elimu ya afya ikiwemo Sratani ya Matiti.
Madaktari wa kujitolea toka Marekani ambao wamepeletwa Tanzania na
Jumuiya ya Watanzania DMV wakiratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa chini ya kitengo cha Diaspora siku ya
Jumamosi July 25, 2015 wakitoa elimu ya afya katika chuo cha elimu ya
afya Zanzibar mapema.
Jumatatu, 20 Julai 2015
JAMAA AVAMIA MKUTANO WA SEPP BLATTER NA KUMFANYIA DHIHAKA
Wakati
Shirikisho la soka Duniani, FIFA likitangaza leo kwamba Februari 26
mwakani ndio siku ya uchaguzi mkuu wa Rais, limetokea tukio la aina yake
katika mkutano wa Sepp Blatter na Waandishi wa habari.
Sepp Blatter ambaye alitangaza kujiuzulu wadhifa wa Urais wa FIFA ametupiwa pesa na mtu aliyevamia mkutano wake.
Mvamizi
huyo aliyetambuliwa kwa jina la Lee Nelson, raia wa Uingereza
aliondolewa ukumbini humo mara moja na maafisa wa usalama wa FIFA.
ARSENAL WACHUKUA KOMBE LA BACLAYS ASIA TROPHY
Arsenal wakishangilia ushindi wa Barclays Asia Trophy 2015
Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutwaa taji la Barclays Asia Trophy kwa kuifunga klabu ya Everton kwa jumla ya magoli 3-1.
Ijumaa, 10 Julai 2015
BREAKING NEWS: CCM YATANGAZA WAGOMBEA WATANO WA URAIS
Kikao cha KAMATI KUU (CC) kimekamilika na kufanikiwa kuwateua wagombea wake 5 ambao ni: 1) Bernard Membe 2) John Magufuli 3) Asha Rose Migiro 4) January Makamba 5) Amina S. Ali. Hatua inayofuata ni majina ya wagombea hawa kukabidhiwa kwa HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) ili kupata majina matatu (3) yatakayopigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu asubuhi.
SANAMU KUBWA YA BILL COSBY YAONDOSHWA DISNEY
Sanamu
ya mwigizaji Bill Cosby imetolewa katika bustani ya Disney kutokana na
kesi inayoendelea kortini ambapo kumetokezea ushahidi kuwa Cosby alikiri
kumpatia mwanamke dawa za kulevya kabla ashiriki naye ngono.
Sanamu hii ni moja ya maonyesho katika bustani ya Disney Hollywood, mjini Florida ya kuwatambua waigizaji maarufu .Nyaraka zilizofichuliwa kortini zinaonyesha kuwa Cosby alitoa ushahidi 2005 kuwa alinunua dawa aina ya Quaaludes kwa madhumuni ya kuwapa wanawake aliotaka kushiriki nao ngono
Alhamisi, 9 Julai 2015
MICROSOFT KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 800
Moja ya kampuni kubwa zaidi duniani ya teknolojia, Microsoft, imetangaza awamu nyingine ya kupunguza wafanyakazi wake.
Kampuni
hiyo ya Microsoft imesema itawapunguza kazi wafanyakazi mia nane, wengi
wao kutoka kwa kampuni ya simu iliyonunua mwaka uliopita ya Nokia.Microsoft imesema kitengo hicho hakitaendelea kuwa biashara inayojisimamia, lakini sasa imejumuishwa ndani ya kampuni kubwa ili kukuza soko kwa mfumo wake wa compyuta unaoitwa Windows.
Aidha kampuni hiyo imepunguza dhamana ya kitengo hicho kilichonunuliwa kwa zaidi ya dola bilioni saba.
Simu za mkononi za Microsoft zinazotumia Windows, zimekuwa zikijaribu kushindana na simu zinazotumia mfumo wa Android na Iphone.
Jumatano, 8 Julai 2015
NOMOPHOBIA
Wengi
wetu tumejikuta katika kizungumkuti hiki, ni ushindani wa kila siku
kuhakikisha kwamba simu ya mkononi ina moto wa kutosha na tunakerwa kila
betri inapopungua nguvu.
Zamani hali ilikuwa tofauti, simu zilitumika kwa mazungumzo tu na ilikuwa rahisi kwa betri kusalia na nguvu kwa muda mrefu.Huenda simu zilikuwa nzito wakati huo mithili ya tofali lakini ni kweli pia kuwa nguvu za betri zilikuwa zinaweza kumudu kwa siku tatu hadi wiki moja.
Lakini sasa imekuwa mtihani wakati tunaona watu waking'ang'ana kufikia soketi za umeme ili kuongeza nguvu simu zao kila wanapoziona.
GAVANA WA BENKI KUU YA KENYA AKATAA MAISHA YA STAREHE
Gavana wa Benki kuu ya Kenya Patrick Njoroge amekataa jumba la kifahari baada ya kuteuliwa kuchukua wadhifa huo.
Suala
hilo limezua mjadala miongoni mwa wakenya kutokana na uamuzi huo wa
bwana Njoroge, kapera mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni mfuasi wa dini
ya katoliki wa kundi linalojulikana kama Opus Dei.HILI NDO JOKA KUBWA KULIKO YOTE DUNIANI LILILOUAWA MISRI
HIVI NI VIWANGO VIPYA VYA FIFA…BRAZIL YAPOROMOKA, ARGENTINA YAPANDA…WALES YA GARETH BALE YAINGIA TOP 10 KWA MARA YA KWANZA
Wales kwa
mara ya kwanza imefikia nafasi bora kuliko zote kwenye historia ya soka
la nchi yao. Kutoka nafasi ya 22 hadi namba 10 hivi sasa. Kupanda kwa
nafasi 12 kumetokana na ushindi mzuri wa mechi ya ku-qualify kwenye EURO
2016 dhidi ya Belgium. Miaka 4 iliyopita Wales ilikuwa namba 117 lakini
hivi sasa wameingia 10 bora.
Kwa upande
mwingine Brazil ambayo ilikuwa namba 5 hivi sasa imeshuka nafasi moja
imedondoka hadi namba 6. Argentina ilikuwa ni namba 3 na hivi sasa
imefika namba 1.
Huu ndio msimamo mpya wa top 10 ya FIFA World Ranking.
PRESHA INAPANDA PRESHA INASHUKA LEO DODOMA
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kuwa miongoni mwa mambo yanayoleta hofu na
kusababisha presha kuongezeka kila kukicha ni woga wa kufanya makosa
katika uteuzi wa ndani, hali inayoweza kukigharimu chama hapo baadaye
hasa kutokana na kuongezeka nguvu ya upinzani.
RWANDA YARUDISHA SIMBA WAKE
Rwanda imewarudisha simba katika mbuga yake ya Kitaifa ya Akagera kutoka
nchini Afrika Kusini baada ya Simba wa mwisho kuonekana katika mbuga
hiyo mwaka 2006.
Rwanda pia ina mipango ya kuongeza faru katika mbuga yake katika kipindi
cha mwaka mmoja wakati nchi hiyo ikijaribu kuwavutia watalii zaidi.
Kwa mujibu wa afisa mmoja katika mbuga hiyo shughuli za kuwatembeza watalii katika kile kinachoitwa safari ni biashara maarufu zaidi katika eneo la Afrika Mashariki na wanyama watano wakubwa wenye umaarufu barani Afrika ambao wanajumuisha Simba na Faru ndio kivutio kikubwa kwa watalii wanaokwenda katika Safari.
Kwa mujibu wa afisa mmoja katika mbuga hiyo shughuli za kuwatembeza watalii katika kile kinachoitwa safari ni biashara maarufu zaidi katika eneo la Afrika Mashariki na wanyama watano wakubwa wenye umaarufu barani Afrika ambao wanajumuisha Simba na Faru ndio kivutio kikubwa kwa watalii wanaokwenda katika Safari.
MAYWEATHER APOKWA TAJI
Bondia
Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Floyd Mayweather amepokonywa ukanda
alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei.
Mmarekani
huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la
ndondi la WBO ada ya dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa
aliyopewa ya tarehe 3 Julai.Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.
RAIS KIKWETE ASHUHUDIA KUSIMIKWA CHIFU KINGALU WA 15 KIJIJINI KINOLE.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia kusimikwa kwa Kiongozi mpya wa kabila
la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 katika kijijini Kinole mkoani Morogoro kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki Jumatano ya tarehe 1 Julai jijini Dar es salaam na kuzikwa Alhamisi Julai 3, 2015 kijijini hapo.
BREAKING NEWZZZ.....MBUNGE JOSHUA NASSARI ( CHADEMA) ANUSURIKA AJALI YA HELIKOPTA
Mbunge amekimbizwa ktk Hosptal ya Selian na kwa mujibu wa Katibu wa
mbunge hajaumia sana ila abiria wawili mmoja anajulikana kwa jina la Eve
ambaye ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA jimboni kaumia mbavu na mwingine
kavunjika mguu.
Tupo jimboni na tunawatoa hofu wananchi wote waliopata taharuki jimboni kuwa Mbunge ni mzima amepatwa na majeraha kidogo!
Mbunge Joshua Nassari (CHADEMA) amepata ajali baada ya Helikopta aliyokuwa akiitumia kukumbwa na dhoruba
- Yeye ni mzima lakini aliokuwa nao wamejeruhiwa kiasi
Tupo jimboni na tunawatoa hofu wananchi wote waliopata taharuki jimboni kuwa Mbunge ni mzima amepatwa na majeraha kidogo!
Mbunge Joshua Nassari (CHADEMA) amepata ajali baada ya Helikopta aliyokuwa akiitumia kukumbwa na dhoruba
- Yeye ni mzima lakini aliokuwa nao wamejeruhiwa kiasi
Jumatano, 1 Julai 2015
WANAOJIUNGA NA KIDATO CHA TANO HAWA HAPA
OWM-TAMISEMI
inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha
Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015. Wanafunzi waliochaguliwa ni
kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya
wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati ya
wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana
18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana
13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na
Biashara.
Wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula
wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa na fursa ya mabadiliko
yoyote ya shule.
Wanafunzi
wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo
mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya
mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine
aliyekosa nafasi.
Orodha ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya Ufundi
mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
=========================================================================
=========================================================================
REGIONAL ADMINISTRATION & LOCAL GOVERNMENT - PMORALG
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER'S OFFICE
BASI LAGONGA TRENI LAUA WATANO MOROGORO
Watu
wanne wamefariki dunia na 21 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Isuzu
kugonga treni ya abiria iendayo bara katika kilomita 276/0 kati ya
Stesheni za Kimamba na Kilosa mkoani Morogoro saa 11:25 asubuhi leo
Julai 01, 2015. Wahanga walipakiwa katika treni hiyo na kukimbizwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
MISRI YAUA WAPIGANAJI WA IS
Wapiganaji
wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa kuuawa katika
mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na kikundi hicho
katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano yalidumu kwa
saa kadhaa kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali kupeleka ndege na
helikopta za kivita.
Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha.Habari kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya Rais Abdel-Fattah el-Sisi.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la kuzitawala nchi hizo.
AFANYA UKAHABA KWA ROBO KARNE
Brenda Myers-Powell alikuwa mtoto wakati alipoanza kufanya ukahaba
katika miaka ya sabini. Alizaliwa eneo la Chicago, Marekani na mamake
mzazi alifariki dunia akiwa na miezi sita pakee.
Hapo ilimlazimu
kusalia na bibi yake. Aligundua baadaye kwamba mamake alikufa kutokana
na ulevi wa kupindukia.Kwa sababu bibi yake alikuwa mfanyakazi wa ndani
ilimlazimu Brenda kujipeleka shule na kurejea nyumbani mwenyewe licha ya
kwamba alikuwa kwenye chekechea.Baadhi ya watu walimdhulumu kingono mtoto huyo wakati alipokuwa akitoka chekechea.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)